Ikulu yaandaa habari kuchafua wabunge wa CHADEMA

Ndiyo maana mimi nawashangaa na nitaendelea kuwashangaa wote wale wanaoendelea kuweka matumaini yao kwa hiki chama, CCM. Jamani Watanzania hata kama ni upofu wa kutoona mbali lakini hii hali sasa inatisha, serikali hii si ya wananchi tena na taifa limetekwa nyara na genge la wahuni. Samahani ndugu zangu lakini hakuna namna ya kuweza kuuita huu utawala chini ya Kikwete zaidi ya utawala haramu unaodumu kiujanjaujanja bila kujali sheria wala kutoa haki kwa raia.

Kinachonisikitisha kuliko yote ni kuwa kama hata humu kwenye jamvi la JF wanapatikana watu wanaoishabikia, sasa hali ikoje huko kwingineko ambako habari hazifiki - kweli mtaji wa CCM ni ujinga, umasikini na maradhi ya wananchi ! Hii ndio sababu kwa sasa serikali ya CCM iko tayari kupiga na hata kuua mradi wanabaki madarakani hata kama taifa linateketea. Hata hivyo imekula kwao kwani mbinu wanazozitumia zinawasaliti kwa sababu kama ilivyotegemewa, zinapangwa kijinga.
 
Vipi na ile mikopo waliochukuwa wabunge wa Chadema, benki wakadhaminiwa na ofisi ya Katibu ya bunge Mbowe na Zitto ndio walikuwa wa kwanza
 
naona bonge la title kwenye gazeti uhuru 'SAKATA LA POSHO,UNAFIKI WA CHADEMA WADHIHIRIKA' Lol
 
Naona kweli hii habari ni ukweli na ndio maana hata listi ya mahudhurio ya wabunge ambayo huwa inakaa ofisi za Bunge sasa imewekwa kwenye FB na katibu wa UVCCM Mkoa wa Da Es Salaam .

Naona kuwa sasa mapambano yanaenda vizuri sana , wanajenga hoja eti wabunge wa CDM walisaini kwani ni lini waliwahi kusema kuwa hawatasaini?

Hoja hapa ni kuwa sitting allowances ziondolewe kwenye mfumo wetu wa malipo , sasa kama hata katibu wa Bunge anashiriki kupeleka taarifa ya mahudhurio ya wabunge CCM basi hapa kuna haja ya wabunge wa CDM kujenga hoja juu ya ofisi ya katibu wa bunge kwa kutumia ile sheria ya haki ,kinga n.k ya wabunge na haswa kipengele cha privacy kwani kupeleka nyaraka za bunge ccm ni kulifanya bunge kuwa la hovyo hovyo .
 
wapeleke magazeti ya shigongo ndiyo yanayouza zaidi ya yote..... huku kwingine tumeshawasaidia ndugu zetu wanasubiri feedbakc zetu huko vijijini wajue wafanye nini so hizi news haziuzi tena

Kumbukeni magazeti yanafikia less and less people especially yakiwa yanapinga upinzani
 
Nilikuwa naangali kipindi cha "Daladala" leo jioni ITV, Hoja mojawapo ilikuwa posho ya vikao za wabunge. Mwanamke mwendeshaji mwenza wa kipindi hicho amesema watu wengi alioongea au kukutana nao wanasema 'maandamano mengi yaliyoandaliwa na Chadema hawajashiriki lakini kuandamana dhidi ya posho hizi wote wataandamana. Hurray CDM kuwafungua macho wananchi.

Naye Dr. Bana wa UDSM jana akiongea nadhani kupitia MlimaniTV amesema "seating Allowances" zinazopingwa na Chadema zinawashangaza wengi. Anasema hazipo popote isipokuwa tanzania. Anaendelea kusema kama wabunge watakutana siku za mapumziko au kukaa vikao nje ya saa za kazi,hapo itakuwa sahihi kulipwa "seating Allowances". Vinginevyo sio ustaarabu.
 
Nimeiona hiyo Orodha kwenye Facebook Page! Sasa sijui wataihisishaje Orodha ya Mahudhurio na Kuchukua Posho maana wengine tumehudhuria Mikutano Kibao tukajorodhesha lakini hakukuwa na Posho
 
Tayari hiyo orodha inasambaa FB. Ukiweza kufika hapa Log In | FacebookLog In | Facebook utaipata

duh!! mkuu, haya mambo haya!!
Hizi siasa za kuwajaza wananchi ujinga na kuwapotosha na ukweli na mantiki, siku moja tutachapana live.

Mantiki: Tuondoe posho zisizo na tija bungeni na serikalini, na kwa kufanya hoovyo tutapata about 0.9trillion Tsh (Bajeti ya Upinzani)

What is wrong with these bogaheads from CCM? kama serikali imekataa si waseme tu kwamba posho are there to stay. Sio kusema hatufutii posho na nyie CHADEMA msichukue posho.

Je, CHADEMA wamesema Misamaha ya kodi kwenye madini ifutwe, Serikali imesema hapana, Je, CHADEMA waende kuchukua hiyo kodi kwa wachimba madini???

Nina hasira sana.
 
Sotori iko hivi ,

Mbowe, mkewe Slaa
wachukua posho Bunge

*Wabunge wao wagawanyika, 28 wasaini posho-
*Ubunge wa Zitto Kabwe sasa wawekwa rehani
*Ziara majimboni, maandamano yao katika hatihati

Na Mwandishi Wetu.
 
Sotori iko hivi ,

Mbowe, mkewe Slaa
wachukua posho Bunge

*Wabunge wao wagawanyika, 28 wasaini posho-
*Ubunge wa Zitto Kabwe sasa wawekwa rehani
*Ziara majimboni, maandamano yao katika hatihati

Na Mwandishi Wetu.

Ha ha haaaaaa Hii Inaitwa Pre Emptive Measure
 
nimeisoma attachment............ kama kweli ikulu inatumia mbinu hii kudhani itawagawa wananchi, basi imekwisha na rais ajaye needs an overhaul

wabunge wa chadema wana edge kwenye hili na watunze hizo pesa ziwe harambee ya maendeleo na mageuzi ya kweli

hard work pays
 
Ikulu wameomba orodha ya Nini? You cant be serious
TUNAOMBA DAFTARI ANALOSAINI KIKWETE TAFADHALI! WANANCHI WANATAKA KUONA, SI NDY WAAJIRI WAKE AU!
 
Hiyo ni orodha ya mahudhurio. Msimamo ni kwamba wanapinga posho hizo" seating Allowances" wameandika barua kuonesha kusudio lao. Kuhudhuria na kusaini mahudhurio sio kwamba wanazitaka posho hizo. WAMECHEMSHA! CCM ZII KABISA!
 
Back
Top Bottom