Ikulu yaandaa habari kuchafua wabunge wa CHADEMA

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
Leo majira ya mchana tukiwa News room kuna taarifa ambayo imeandikwa na imesambazwa kwa wahariri ikiwa na lengo la kuwachafua wabunge wa CHADEMA kesho kuhusiana na posho.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya Ikulu kulitaka Bunge liwapelekee mahudhurio ya wabunge wote waliosaini kwenye orodha ya mahudhurio na imetumika hiyo kwa kuangalia ni wabunge gani wa CHADEMA waliweza kushiriki kwenye vikao na hivyo kusema kuwa ni orodha ya kupokea posho.

posho.png


Habari hiyo itakuwa ndiyo front page kwenye magazeti mbalimbali kesho na lengo ni kuhakikisha kuwa walau wanapumua ili suala la posho wananchi waone kuwa limekigawa CHADEMA kati ya wabunge wake.

Naomba kuishia hapo kwa sasa kwani ndio tunakimbizana na deadline, ntarejea baadae kuwajuza na nikiweza nitaiscan taarifa hiyo na kuiweka hapa jamvini.
 
Huo upupu ndio unaowadhalilisha mafukara wa akili Ndani ya ccm, walishindwa kupumua wakati wa uchaguzi pamoja na porojo za kipropaganda zote .
Ccm wanacheza ngoma ya CDM, hawatapona.
 
hizi harakati za ikulu zinaonesha jinsi gani hoja hii ya kuondolewa kwa posho yaweza kutumiwa vizuri na upinzani kuendelea kuiondolea CCM kibali kwa wapigakura...nonetheless they are late!
 
Tunashukuru mkuu, just waiting for updates!

Utakatifu wa ikulu wote umekwisha...

eeeh! Mungu turudishie Nyerere siku moja tu ili aone wahuni wanavyoishi ikulu yake!
 
powa kabisa mkuu kwa kutupa alert, daaa naona wamegonga mwamba basi kama ni hivyo hahaha....hawana jipya hawa jamaaa.....tusubiri pumba zao kesho....
 
Kwa nini Ikulu inajiingiza kwenye issue ya posho za wabunge?
 
Speaker atamfukuza Zitto bungeni akigoma kusaini attendence register. Na ili wakombozi wetu waendeleze mapambano bungeni they've to sign it. They're being forced to accept allowances which could'd otherwise been allocated to other initiative and sustainable development projects.
 
Wahisha hii habari haraka ili tuanze nayo magazeti kesho washangae .Usilale bila kuweka hapa mkuu
 
Kama mimi ningekuja JK ningeondoa posho MARA MOJA angalau watanzania walalahoi wangenikumbuka kwa hlo.
 
Mbona hilo liko wazi na limeshasemwa na Mbowe kuwa ajenda hiyo ni ya chama orodha ya kusaini kutosaini haitasaidia kitu kuwagawa wapinzani.
 
Back
Top Bottom