Ikulu ya Tz yaenda Afrika ya kusini...

Kibunango

Platinum Member
Aug 29, 2006
8,416
2,264
TIMU ya taifa ya netiboli Tanzania ‘Ikulu Netball Team’ imeondoka nchini jana kwenda Afrika Kusini kushiriki mashindano ya kusaka viwango kwa timu zitakazoshiriki mashindano ya Kombe la Dunia la 2010.

Akizungumza Dar es Salaam jana muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda huko, mkufunzi mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Kibira, alisema kuwa mashindano hayo yanayoanza leo yatafikia kilele Septemba 21 na yanashirikisha nchi saba.

Alizitaja nchi zitakazoshiriki mashindano hayo kuwa ni wenyeji Afrika Kusini, Uganda, Malawi, New Zealand, Jamaica, Botswana na Tanzania.

Mkufunzi alisema kuwa wachezaji wameahidi kupigana kufa au kupona ili kuweza kufikia viwango vilivyowekwa na Shirikisho la Netiboli la Kimataifa (IFNA), na kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia.

Timu hiyo iliondoka saa 4:00 asubuhi ikiwa na wachezaji 10 na viongozi watatu.

Wachezaji walioondoka ni Monica Aloyce, Elizabeth Fussi, Monica Kessy, Sophia Komba, Grace Daudi ‘Sister’, Theresia Mwakipanga, Helena Siboka, Christina Moses na Mwadawa Twalibu, huku viongozi ni Marry Protas ‘Super Coach’, (Kocha), Michael Wela (Meneja wa timu), na Anna Kibira (Mwamuzi).

Kibira alisema kuwa timu hiyo inatarajiwa kurejea nchini Septemba 22, siku moja baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.

Source: Tanzania Daima
 
Ni IKULU NETBALL TEAM au NATIONAL NETBALL TEAM? Kama wanasema walichomaanisha basi huo ni another type of ufisadi as mission ni kusaka timu ya kushiriki KOMBE LA DUNIA 2010
 
Ni IKULU NETBALL TEAM au NATIONAL NETBALL TEAM? Kama wanasema walichomaanisha basi huo ni another type of ufisadi as mission ni kusaka timu ya kushiriki KOMBE LA DUNIA 2010
Sijui ni nani aliwapa hilo jina, zamani walijulikana Tz Queens.. Sasa hilo la Ikulu sijui wana maana gani...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom