LiverpoolFC
JF-Expert Member
- Apr 12, 2011
- 11,348
- 3,219
Kusainiwa au kutokusainiwa sio hoja, jua kuwa ni taarifa ya ukweli huwa sijawahi kuweka kitu cha kutunga ama hisia hapa jamvini
Nakuaminia Kamanda we2!
Kusainiwa au kutokusainiwa sio hoja, jua kuwa ni taarifa ya ukweli huwa sijawahi kuweka kitu cha kutunga ama hisia hapa jamvini
Hata haiingii akilini, kama maamuzi yalifanyika toka mwaka 2005 (chini ya Mkapa) imekuwaje bado wafungwa hao bado walikuwa wamefungwa hadi leo?..
Labda anadhani wanaharakati watapaza sauti amsamehe babu Seya na mwanae Nguza kwa kutumia mlango huo huo uliowasehe polisi hao wawili.Mimi naona kama kuna kitu kimejificha nyuma ya huo msamaha.....
Hapo kwenye RED.....Haya sasa kama kawaida ya wazee wa kiduku, wanajibu kama siyo serikali. Kama maamuzi yalifanywa kabla ya JK na kama yalifanywa na Ikulu hiyohiyo kwanini wasitoe ufafanuzi wa swala hilo kuliko kutoa statement fupi tu inayoacha maswali zaidi ?
Halafu mwandishi wa ile habari alijitahidi kweli kueleza mpaka kifungu kinachompa mamlaka rais kusamehe, sasa nashangaa Ikulu inaweweseka nini? Jamaa wamewahoji mpaka hao ex - wafungwa na jamaa kuelezea jinsi walivyoishi maisha ya jela hadi kuachiwa kwao. Mimi naamini gazeti la mwananchi si wazushi, ila kuna aina fulani ya kutaka kumis lead watu. Halafu kwa jinsi Ikulu ilivyojibu ndiyo itaibua maswali mengi kuliko ile taarifa ilivyotoka kwenye gazeti.Mkuu hilo ndo swali la msingi ambalo salva alitakiwa kulijibu. Lakini kila mmoja anashangaa jinsi taarifa hii ya ikulu ilivyo kuwa fupi na yenye kuacha maswali mengi yanayohitaji majibu.
utashangaa waunde tume ya uchunguzi hapo,lol
Ufafanuzi upo kwenye kashfa tu, mambo mengine yanapotezewa.Hapo kwenye RED.....
Kumbe na ww mkuu umeliona nilitaka kuandika hivyo hivyo, halafu mbona hata hiyo statement haieleweki? Haielezi nani anahusika, haisemi kama walipunguziwa adhabu kweli yaani haikani na wala haikiri,
Statement yote ndo hii hapa yale mengine ya juu ni maelezo kuhusiana na gazeti la Mwananchi...
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete hajawahi na hajapata kuhusika hata kidogo kutoa msamaha wa kirais kwa kupunguza adhabu ya wauaji hao wa Luteni Jenerali Kombe tokea kuingia madarakani.Masuala yote yanayohusu polisi hao waliohukumiwa kifo kwa mauaji ya Luteni Jenerali Kombe yalifanyiwa maamuzi kabla ya Rais Kikwete kuingia madarakani Desemba 21, 2005.
Ebu fikirieni huku ni kufafanua kweli? hii kurugenzi ya mawasiliano ikulu wanaumwa nin kiasi cha kuwa hata wavivu kueleza kitu kama hiki? Na ni kwanini wanaibuka kutoa maelezo kwenye issue ambazo sio za kitaifa wakiacha issues kubwa za kitaifa zikielea tu? Uchumi wetu una didimia hakua ufafanuzi, shilingi yetu inapoteza dhamani hakuna ufafanuzi, Kuna taarifa za serikali kupanga njama za mauaji kwa baadhi ya wabunge na mawaziri na raia wengine kurugenzi imekaa kimya... wengine tunaogopa BAN tu hapa lakini tunauwezo wa kufyatuka kwa maneno makali, Mungu apishe mbali!!!
Pambaf kabisa...