IKULU Ubia upo, tuwajue wabia -Jenerali

Naona GT tayari ame-hit palipotakiwa, kupotosha hoja. Sasa hakuna kujadili hoja tena bali tunajadili maandiko na comments za GT.

Tiba

Tiba,
.......please.......vitu vingine kama huvielewi tuachie tunaomjua huyu jamaa .........please
 
Wakuu zangu,
Mimi napingana kihoja na Ulimwengu ktk hili.. rais anaweza kutokuwa mbia na mtu mwingine kama ilivyo ktk mashirka...Hao wote alowataja wanaweza kuwa waajiriwa wa rais kama alivyoelezea na ajira zao zinaweza ota majani anytime akipenda..utaratibu kama huu haupo ktk Ubia.
Na tukubali kwamba wote kina Mkapa na JK walipozungumzia Ubia hawakuwa na maana zaidi ya kwamba kazi waliyopewa hawana mshirika ambaye anaweza kuwa na nguvu sawa ama zaidi yao..wao ndio Alfa na Umega - The buck stop there!
Madaraka makubwa tulompa rais wa nchi ni makosa yetu kwani katiba hutungwa na sisi sio rais...Anaweza kuizuia au kuichelewesha lakini hawezi kufuta kabisa matakwa yetu..Mkapa na hata JK wote hawa wamezikuta hizo sheria kabla hata hawajachukua kiti cha Ikulu hivyo tusiweke visingizio kuwa wao ndio sababu.. Ni makosa yetu sisi sote kusubiuri hadi kiongozi anapoingia IKulu ndipo tunataka mabadiliko ya Katiba.. Tulikuwa na nafasi hiyo kipindi cha mwisho cha Mwinyi na pia wakati Mkapa anamalizia ngwe yake kubadilisha sheria au katiba..

Ni wakati ambao nchi inasubiri rais mpya hivyo ni rahisi kwa wabunge wetu kubadilisha katiba kuliko kusubiri mtu akisha ingia zizini ndipo unataka kupunguza nguvu ya rais..Kinachouma zaidi ni kujua kwamba rais ndiye Alfa na Omega kisha tunasubiri hadi kaingia Ikulu ndipo tunapoanza mashamsham ya kubadilisha katiba.. huyu ndiye mwenye kila nguvu kuliko hata chama CCM akisha kalia kiti cha Ikulu..

Mbali na kuwachagua viongozi wa serikali, rais ana nguvu kubwa hata ktk NEC anaweza kubadilisha mfumo wa uchaguzi na madaraka ndani ya chama.. tumeina sekretariet zikibalishwa na hata uchguzi wa CCM - Vijana tumeona nguvu ya rais..Tabia hii ipo hata ktk vyama vya Upinzani, tumeona Mrema akimfukuza mpiunzani wake, Malecela akitolewa nje ya wagombea, Salim akiondolewa ktk mchakacho wa pili badala ya kurudiwa mara ya tatu..

Ni utamaduni wa Mwafirka, baba kula nyama za paja na firigisi, hakifanyiki kitu bila mari yake na ndiye Alfa na Omega ndani ya nyumba, anaweza hata kumfukuza mwanaye na mke asifanye kitu.. mkesiii Mbia wala hana senti ndani ya mavuno ya bwana..Majukumu ya baba ni makubwa wakati kazi anazozifanya ni ndogo sana ukilinganisha na mke ktk malezi ya watoto.. but in reality mke hana Ubia inapofikia maswala ya utawala au finance.

Kifupi ni kwamba binafsi nilielewa walichokisema Mkapa na JK kuwa hawana mshirika ktk UTAWALA wala FINANCE.. hivyo wanaweza mfukuza mtu yeyote wanapojisikia kumwondoa..
Kama sikosei aliyasema haya JK kuhusiana na swala la Lowassa na kweli alimwondoa! Na tunaposema Kikwete au Mkapa bila shaka unazungumzia CCM, kkama vile tunaposemw Bill gates tuna maana ya Microsoft, sidhani kama kuna ubaia ubia kati yao..

Huwezi kutenganisha Mkapa au JK na CCM ndiye alowatenganeza..Huwezi kumwondoa CCM ukabakia na JK au Mkapa, lakini unaweza kumwondoa JK au Mkapa na ukabakia na CCM ikiendesha kazi zake za utawala kama kawaida..Na ukija tazama ktk Ubia, inawezekana kabisa mbia mmoja kuondoka asiathiri utawala au mbia akanunuliwa na mbia mwingine na kupoteza nguvu ya utawala..
Kwa hiyo sijui yawezekana mimi ndio sikuelewa vizuri kile alichotaka kuzungumza Ulimwengu au tunatazama picha mbili tofauti..
 
Last edited:
Kazi kweli tunayo mpaka huyu MNYARWANDA leo anakuwa na ubavu wa kutukosoa...kazi kweli kwelo...i wonder who will be next katika hilo kundi lao la ma INTERAHAMWE!

Kwa kuwa Jenerali jina lake ni TWAHA basi umeamua kutafuta unyarwanda na intrahamwe ili kuonyesha kuwa anayosema kuhusu ndugu yetu MRISHO ni chuki tu...

Kaka acha UDINI, fungu macho, kuwa objective

omarilyas
 
Mkandara,

Mimi nakubaliana na ulimwengu. Anachotuambia ni kuwa rais hana ubia ulio halali au ambao umewekwa kisheria na kikatiba. Rais ni all powerful person na anaweza kufanya chochote na katiba inamruhusu. Mwalimu aliwahi kusema hivyo na Kikwete vile vile ameshalizungumzia hilo.

Mi nilivyoelewa makala ya Ulimwengu ni kuwa ubia anaouzungumzia si ule uliowekwa kisheria. Kutokana na urais kuwa na nguvu sana ni vigumu sana vile vile kuwa mtu mmoja anaweza akapigana peke yake hadi kufikia huko kwenye urais. Matokeo yake ubia usiokuwa halali unajitokeza kwani haiwezekani kuifikia ngazi ile kwa nguvu yako mwenyewe. Huu ubia usiokuwa wazi ndo kitu anachokuzungumzia hasa Ulimwengu!

Mtu anaingia tukidhani hana ubia na sheria inasema hivyo. Lakini ukweli ni kuwa unahitaji nguvu ya ziada ili kufikia pale, na hili huwalazimisha kuunda ubia usiokuwa wazi, ubia ambao utakuja kuuona kivitendo zaidi kuliko kisheria. Hapa ubia anaouzungumzia na ambao naamini hajautaja wazi ni huu wa JK na RA. Unaweza ukaona jinsi kesi za EPA zinavyowakwepa baadhi ya SACRED COWS. Na serikali kupitia veiled statements imekuwa ikionesha wazi kuwa wahusika si watu wa kawaida. Kuwa ni watu wenye nguvu kweli kweli ambao huwezi kuwagusa bila kuitikisa serikali.

Sasa kwa wale tunaoelewa jinsi katiba yetu, watu ambao huwezi kuwagusa bila kuitikisa serikali ni watu wenye nguvu sawa au inayokaribiana na mheshimiwa rais. Sasa la kujiuliza ni hawa hizi nguvu wamepewa na nani? Mbona katiba haiwapi hizo nguvu ambazo serikali serikali inaziona. Bila shaka hizi nguvu wanazipata kutokana na ubia walio nao huko ikulu. Na huuu si ubia halali, ingawa ni ubia official. Ni official kwa sababu serikali inauona na inau honour.

Ndo maana Ulimwengu anasema kwa kuwa tumeshindwa kuweka mambo ya ubia wazi, tunalazimika kuangukia kwenye ubia usio wazi!
 
Sheria zimevunjwa na serikali inakiri sheria zimevunjwa na waliovunja wanaonekana. Lakini hawa watu wana nguvu sana na serikali imeshakiri kuwakamata ni ama haiwezekeani au itawezekana kwa gharama ya kutikiswa kwa serikali.

Sasa ikiwa sisi tumempa rais nguvu zote lakini inaonekana nguvu hizo zinamwelemea anaamua kuzigawa kwa watu wengine kwa siri, kwa nini tusiamue kuzigawa wazi kabisa ili tumpe rais nguvu inayolingana na uwezo wake?

Kitendo cha sisi kutoa nguvu zisizomithirika kwa rais ina maana tunawatwisha hawa watu mzigo wasioweza kuubeba. Ndo maana wanawagawia wengine sehemu ya mzigo huo. Sasa tunabaki kujiuliza; kwa nini rais hapa hafanyi hiki na kile? Ukweli ni kuwa nguvu yake kawapa wengine na yapo mambo ambayo rais anashindwa kuyashughulikia kwa sababu hana uwezo wa kuyashughulikia. Hana uwezo kwa sababu amegawa madaraka yake kwa wabia wake!!!
 
Kwa kuwa Jenerali jina lake ni TWAHA basi umeamua kutafuta unyarwanda na intrahamwe ili kuonyesha kuwa anayosema kuhusu ndugu yetu MRISHO ni chuki tu...

Kaka acha UDINI, fungu macho, kuwa objective

omarilyas

Kaka Omar, huo udini dini gani? naona alichokosea GT si udini ila ungeweza kujadili labda maslahi tu yanayomgusa. Ninachoweza kuona kwamba GT kateleza ama kwa bahati mbaya ama kwa makusudi (huwa anafanya sana) kuhusu Jenerali akiwa na malengo ya kuchokoza mjadala apate faida. Soma mada zote za GT anatetea sana Waislamu na ni yeye aliyweka MOU ya Kanisa na Serikali iliyosainiwa na Lowassa.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/32562-mou-kati-ya-serikali-na-kanisa.html
 
Last edited:
Ili tuweze kuachana na uongozi mbovu ambao chanzo chake ni ubia wa Mwalimu inatubidi sasa tutizame elsewhere kutafuta uongozi mzuri ambao hautakuwa na uhusiao wa kiubia na Mwalimu.Tuachane na chama cha CCM cha ubia wa Mwalimu.
Kama akipatikana mtu ambae hajawahi kukamata kadi ya CCM huyo ndie atakuwa hakuwa na ubia na Mwalimu lakini hawa wengine wote wakiukwaa huo Urais wataendeleza yale yale MFANO, Familia ya Mbowe ni wale wale waliotoka kule kule CCM, Maalim Sharif wale wale alikuwa waziri kiongozi enzi zile zile za Mwalimu, Mrema yeye ndio funga kazi na kadi ya CCM bado anamiliki,sasa yupi ni bora kama wote hawa walikuwa watawala enzi za mwalimu kama sio wao wazazi wao, tufanye nini tusimpate mtu aliyekuwa mbia wa Mwalimu?
 
Kila siku najiuliza Nyerere angekuwa hai Rostam, Lowassa, Kingunge, Jeetu, Omar Mahita na wengine wangekuwa wapi. Sipati jibu, Lowassa at least ndiye anayeweza kujaribu kujibu swali hili. Lakini saa hizi haa watu wanpeta tu na ulinzi juu. Kweli kulia kunaonesha furaha na majonzi. machozi ya kifo cha mwalimu yalikuwa na yote mawili.

- Mkuu Bongolander, heshima yako bros hivi kwa nini mnapenda kupindisha ukweli, yaani unataka kusema hawa viongozi uliowasema wana umri wa miaka 24? Is that so kwamba wamezaliwa baada ya Mwalimu kungátuka?

- Acheni hizi jamani, hawa walikuwa ni viongozi Mwalimu akiwepo na guess what walikuwa mafisadi pia na Mwalimu alikuwa akiwaita Ikulu kuwaonya badala ya kuwapeleka kwenye sheria, ili kutusaidia taifa la leo sasa matokeo ni kwamba wamekuwa mafisadi papa, sasa na wewe mtu makini badala ya kukubali ukweli kwamba hii ni moja ya mapungufu makubwa ya Mwalimu as a nation we are paying for, wewe unajaribu kupindisha ukweli ili tu Mwalimu awe malaika halafu you wonder kwa nini tumekwama na wanapewa ulinzi, Mungu alisaidie taifa hili siku moja liamke huu usingizi mzito sana mwe!

Respect and Out.

Kamanda FMEs.
 
Topic ilikuwa ya kumhusu Kikwete ila naona imegeuzwa kuwa ya kumhusu Mwalimu.

Kazi kweli kweli
 
Mbia = shareholder?
Nani anashare power na Kikwete = Shein

Sasa kusema hakuna mbia sio sawa kwa hiyo argument ya kwanza tu. Tukiendelea kwenda huko chini tutapata wabia wengine (Proof by Induction)
 
Yaani Kikwete mwenyewe aliona ana project independence na positive incorrigibility kumbe anachemsha.

Lazima tuwe humble.

Bluray si kwamba anayoona tu no ndivyo anavyoact wala si utani. Kuna siku anahutubia Bunge akanukuu kwamba yeye ni rais anao uwezo wa kusema Dr. Slaa akamatwa aweke ndani na akawekwa ndani bila maswali. Sasa hii ni nini jamani? Issue hapa ni nini? Yaani kwake madaraka/udikiteta ni kwake muhimu kuliko kudeliver.
 
Ili tuweze kuachana na uongozi mbovu ambao chanzo chake ni ubia wa Mwalimu inatubidi sasa tutizame elsewhere kutafuta uongozi mzuri ambao hautakuwa na uhusiao wa kiubia na Mwalimu.Tuachane na chama cha CCM cha ubia wa Mwalimu.

Duuuh!
Itawezekana kweli kuachana na chama hiki?

Maana asilimia kubwa hawajui na wala hawataki kujiuliza juu ya mambo haya.Na ndio hao hao wanaokipa kura chama.
 
Bluray si kwamba anayoona tu no ndivyo anavyoact wala si utani. Kuna siku anahutubia Bunge akanukuu kwamba yeye ni rais anao uwezo wa kusema Dr. Slaa akamatwa aweke ndani na akawekwa ndani bila maswali. Sasa hii ni nini jamani? Issue hapa ni nini? Yaani kwake madaraka/udikiteta ni kwake muhimu kuliko kudeliver.


Nukuu zingine, mmmh!!
 
ndio Ni MNYARWANDA huyu kwani uwongo?

woga wenu ni nini kukubali kama huyu ni Mtusi na ni Mnyarwanda au basi tuu ?


the same applies to Salva naye si mtanzania

iko wapi ile thread ya Salva si Mtanzania?



Kuitwa raia ama si raia inategemea upo upande gani .... Kama haupo upande wao, basi wewe "si raia" ... kama upo upande wao hata kama "si raia", basi utaendelea kuwa raia hadi hapo utakapotofautiana nao.

The same applies here ...
 
- Mkuu Bongolander, heshima yako bros hivi kwa nini mnapenda kupindisha ukweli, yaani unataka kusema hawa viongozi uliowasema wana umri wa miaka 24? Is that so kwamba wamezaliwa baada ya Mwalimu kungátuka?

- Acheni hizi jamani, hawa walikuwa ni viongozi Mwalimu akiwepo na guess what walikuwa mafisadi pia na Mwalimu alikuwa akiwaita Ikulu kuwaonya badala ya kuwapeleka kwenye sheria, ili kutusaidia taifa la leo sasa matokeo ni kwamba wamekuwa mafisadi papa, sasa na wewe mtu makini badala ya kukubali ukweli kwamba hii ni moja ya mapungufu makubwa ya Mwalimu as a nation we are paying for, wewe unajaribu kupindisha ukweli ili tu Mwalimu awe malaika halafu you wonder kwa nini tumekwama na wanapewa ulinzi, Mungu alisaidie taifa hili siku moja liamke huu usingizi mzito sana mwe!

Respect and Out.

Kamanda FMEs.

Mkuu nakupata. Kama utakuwa umepitia nyuzi moja inazungumzia Kingunge akitahadharisha kuhusu waraka uliotolewa na kanisa katoliki, kuna member mmoja ametamka kuwa "haka kazee kaliishi kinafiki sana, baada ya mwalimu kufa kamekuwa kafisadi kwelikweli na kateteaji ka mafisadi". Wote hao mwalimu alifanya nao kazi kwa namna moja au nyingine, tatizo ni kuwa walikuwa wanafiki sana. Labda ningekuwa wazi kuwa kama haya yangewekwa wazi wakati mwali akiwa hai sijui ingekuwaje. Nakumbuka ni Lowassa tu ndiye aliyemtoa nishai hadharani. Mwalimu was no saint, ana lundo la upungufu kiutendaji, lakini bado naweza kusema la ufisadi hata alipokuwa mzee mpaka alikuwa anasema "kanchi kananuka rushwa", atleast alikuwa anakemea na sio kulinda kama sasa, kama unavyosikia wengine wanasema wazi kabsa kuwa wanaogopa kuwakamata watu wa EPA.
 
Kwa wale wasiojua au waliosahau:
Ikumbukwe ingawa J. Ulimwengu ana asili ya kitusi, lakini stahili yake apate. Ikumbukwe kuwa ni mtu wa kwanza kama mbunge (CCM-vijana) kutamka bungeni juu ya serikali kujaa uozo. Enzi hizo alikuwa pia ni mkuu wa wilaya (nadhani ni mojawapo ya wilaya za dar) na Malecela akiwa Waziri Mkuu. Huo ndio mwanzo wa yeye kutengwa na mafisadi wa serikali iliyokuwa chini ya mzee Mwinyi/Malecela.

Tujitahidi kutosahawa historia fupi kama hii.
 
Kazi kweli tunayo mpaka huyu MNYARWANDA leo anakuwa na ubavu wa kutukosoa...kazi kweli kwelo...i wonder who will be next katika hilo kundi lao la ma INTERAHAMWE!

Mkuu GT,
Kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, Jenerali Twaha Ulimwengu NI RAIA wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
KipimaPembe,
Mi nilivyoelewa makala ya Ulimwengu ni kuwa ubia anaouzungumzia si ule uliowekwa kisheria. Kutokana na urais kuwa na nguvu sana ni vigumu sana vile vile kuwa mtu mmoja anaweza akapigana peke yake hadi kufikia huko kwenye urais. Matokeo yake ubia usiokuwa halali unajitokeza kwani haiwezekani kuifikia ngazi ile kwa nguvu yako mwenyewe. Huu ubia usiokuwa wazi ndo kitu anachokuzungumzia hasa Ulimwengu!
Mkuu wangu kama maneno ya Ulimwengu yalikuwa na maana hiyo basi inaonyesha wazi Ulimwengu ana mashaka na hii kitu Demokrasia.. Kwa sababu hakuna rais duniani ambaye kaweza kupanda hadi darini kwa nguvu zake.Hata hao tunaowaita madikteta walikuwa na watu nyuma yao..Kihs basi waliyemchagua ni sisi wananchi hivo kuna Ubia kati ya wananchi na JK au wapambe wake?..

Lakini muhimu tuelewe kwamba alichosema Kikwete na Mkapa ni kuhusiana na tuhuma za watu kwamba kuna watu - Untouchables ambao wao wamekula yamini kulindana..as shareholders... kweli wapo watu hawa ktk serikali yetu lakini sidhani kama ni kutokana na Ubia kwa rais ila chama CCM... hawa watu walikua Untouchables toka wakati wa Nyerere, Mwinyi hadi kesho (kina Chande)..na wale waliojitokeza kama Rostam na wengineo, mimi naamini kabisa kuwa hawa watu wamejizatiti ktk chama na sio rais.
Kati ya viongozi wote wa nchi hii, Mkapa (baada ya Nyerere kututoka) naweza kuamini kwamba hakuwa na mbia (kwa maana ya mshirika) ila alikula na watu, na alijua nguvu ya wadhifa alokabishiwa na akautumia.

Kikwete nina amshaka kama anajua nguvu alokuwa nayo, nina mashaka sana na uwezo wake kuwa rais kwa sababu mambo mengi anaweza kusema yakawa kesho yake lakini mara nyingi ameonyesha kuwa kiongozi mdhaifu kwa sababu hajui ama mwoga wa madaraka ambayo kayatokea jasho kwa maandalizi miaka 10..Hivyo hana Ubia isipokuwa nina hakika kabisa kwamba kuna vyombo ambavyo vina nguvu kumshinda..kifupi ni rais MWOGA na woga wake ndio unatupa wasiwasi ya kuwepo Ubia.....
 
Last edited:
Jenerali si mkweli na ana hofuu kama akina Kingunge na wenzao wa aina hiyoo..

Anajitahidi kujitenga kimawazo na wenzake ila uhalisia uko pale kwamba alishiriki kwa kiasi kikubwaa tuu kuubariki Ubia wa uongozi..

Awe mkweli, aongoke kwa dhati, jamii itamsamehee...hatuhitaji chuki, katika kujadili hoja. Ameumizwa nao alipotaka kuwa tofauti nao kimkakati..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom