Ikulu sasa ni BMW kwa kwenda mbele

Status
Not open for further replies.
Jamani,hapa JK tusimuonee.Haya magari wamepewa buree toka uarabuni.Tena hawa waarabu walileta mpaka mtaalamu wa haya magari toka Ujerumani kuja kuyafanyia service kabla hayaanza kutumiwa.Hata lile benzi alilotumia Mkapa wakati anamaliza muda wake nalo lilikuwa la chee toka hukohuko.

Asa gharama ambazo zinaonekana kuwa associated na hayo magari ni za nini kama wamepewa bure? ama za mafuta?
 
Jamani,hapa JK tusimuonee.Haya magari wamepewa buree toka uarabuni.Tena hawa waarabu walileta mpaka mtaalamu wa haya magari toka Ujerumani kuja kuyafanyia service kabla hayaanza kutumiwa.Hata lile benzi alilotumia Mkapa wakati anamaliza muda wake nalo lilikuwa la chee toka hukohuko.

Ukiona mtu anakupa msaada mkubwa kama wa magari ya mamilioni ujue hapo kuna kupeana fadhira in return sasa kama ni kweli waarabu wametoa hayo magari kuna kitu nasi tunawanufaisha hakuna urafiki usio kuwa na manufaa lazima mmoja aumie mwingine anufaike huu ndo urafiki wote mkitaka kunufaika basi mifalakano huanza.

...:D te he he, "kula uliwe!"
 
Jamani,hapa JK tusimuonee.Haya magari wamepewa buree toka uarabuni.Tena hawa waarabu walileta mpaka mtaalamu wa haya magari toka Ujerumani kuja kuyafanyia service kabla hayaanza kutumiwa.Hata lile benzi alilotumia Mkapa wakati anamaliza muda wake nalo lilikuwa la chee toka hukohuko.

Kumbukumbu zangu zinanikumbusha kuwa Muamar al Qudhafi aliwahi kutoa magari huko kipindi cha nyuma, sina hakika ni magari aina gani lakini ilikuwa kitambo kidogo..

Na nikizingatia nukuu ya hapo chini, na kukizingatiwa kujiumauma kwa Katibu Mkuu wa Rais ni wazi maelezo yako ni ya kutiliwa mashaka:

Masaki said:
Nawashangaa waandishi wetu wa habari kwa kuchelewa kuripoti habari hii. Mboan msafara wa JK umekuwa ukitumia BMW kwa zaidi ya miezi mitatu sasa!
 
Sasa hamtaki kukubali kuwa nchi yenu ni maskini? Waziri Mkuu kasema sisi ni "maskini sana" halafu mnakataa; mnataka Rais atumie usafiri gani kuendana na hadhi yake kama Amiri Jeshi Mkuu, na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi. Hawezi kusafiria Corolla!

Lengo la viongozi wengi wa Afrika kumng`oa mkoloni halikuwa kwa sababu walikuwa na uchungu wa kuboresha maisha ya wananchi wao bali walikuwa wamejaa hamu ya kuishi maisha ya mkoloni aliyokuwa akiishi Ikulu.

Hivyo waliwatimua magavana wa kikoloni ili wao wakalie zile ikulu walizokalia wakoloni,watembelee magari yenye hadhi na heshima waliyotembelea magavana hao na waishi maisha yaleyale ya kifahari kama mtawala wa kikoloni alivyoishi bila kujali wananchi walalahoi kama vile gavana mkoloni alivyokuwa hajali walalahoi.

Tofauti ya utawala wa kikoloni na wa kiafrika tofauti yake ni ngozi tu.Ikulu ya zamani alikuwepo mzungu mwenye nywele nyeupe wakati ikulu ya sasa yuko ngozi nyeusi.Lakini huwezi kuwatofautisha yupi mkoloni na yupi si mkoloni kwa kuangalia maisha yao,magari wanayotembelea,misafara inayowasindikiza na wanavyoshindwa kuwajali wananchi. Karibu wote wanafanana tu.

Labda Waziri mkuu Pinda ndiye yuko tofauti kidogo labda kwa kuwa anatoka kabila maskini dogo la wakonongo ndiyo maana hana makuu na anapenda kuwa karibu na watu wa hali ya chini na kujitambulisha nao na kusikiliza na kujali kero zao, tofauti na wenzie wengi ambao hupenda kujitambulisha kama sehemu ya matabaka ya watu wa juu waendesheo maisha KI-BMW na KI-BENZI kama alivyofanya gavana mkoloni waliyemtimua walipodai uhuru ili wakalie wao nao wafaidi kama yeye alivyofaidi.

Nchi nyingi za kiafrika haziendelei kwa sababu kilichobadilishwa ni rangi ya mtawala. Badala ya mtawala mkoloni mzungu sasa nchi za kiafrika zina watawala wakoloni weusi.Lakini vitendo vyao,staili za maisha yao ni zile zile hazina tofauti na za watawala wakoloni.Kodi zinazokusanywa lengo kuu kama ilivyokuwa wakati wa mkoloni ni kwa ajili ya kugharimia utawala ikiwemo mishahara,posho nono na magari ya kifahari ya watawala.Pia kazi ingine ni kujenga barabara nzuri ili magari yao ya kifahari yasiumie yakisafiri na kumrusha rusha mheshimiwa mtawala akajisikia vibaya.Masuala mengine ya maendeleo hilo si jukumu la serikali ni la mwananchi mwenyewe ajiletee maendeleo yake.Wakati wa mkoloni jukumu la kujiletea maendeleo lilikuwa ni la mwananchi mwenyewe na baada ya uhuru jukumu la kujiletea maendeleo ni la mwananchi mwenyewe.Hivyo hakuna tofauti ya mtawala kiutendaji kati ya mkoloni wa zamani na sasa.

Kazi ya mtawala iwe ni wa kikoloni au wa sasa kazi yake kubwa ni kuzunguka kwenye BMW na BENZ zake akiwapungia mikono wananchi waliochoka kwa umaskini na kukata tamaa waliojipanga barabarani kwa kulazimishwa na watawala wa maeneo kujipanga barabarani kwa masaa mengi kusubiri kushangilia misafara ya mtawala ya Mi- BMW na Mi-BENZ inayopita kwa kasi na mbwembwe nyingi za ving`ora,mikao ya kininja kama ya sinema ya wanausalama,ma-mabaunza n.k inapopita mbele yao ili mheshimiwa mtawala na waandishi wake wa propaganda waandike kuwa alishangiliwa kila alikoenda na misafara mirefu ya wananchi wanaompenda ambao walimgojea kwa hamu kwa masaa mengi ili wamshangilie mtawala wao mpendwa aliyekuwa kafichwa kwenye gari lenye usalama wa hali juu lililonunuliwa kwa mamilioni ili kuwazuia wenye wivu wanaomwonea gere mtawala anavyofaidi raha kuliko wao wasimshambulie kwa hasira za njaa yao na gere yao.

Nchi zetu bado ziko chini ya wakoloni.Kabla ya uhuru ilikuwa ni ukoloni PART ONE sasa hivi baada ya uhuru ni Ukoloni PART TWO. Ndiyo maana kiongozi bila kutembelea BMW,BENZ uongozi wake unakuwa haujakolea au kukamilika sawasawa.
 
Hatuna fedha (serikali) za kuwakopesha wanafunzi 100% vyuo vikuu!! Tulizo nazo ni za kuhakikisha tu usalama wa viongozi hivyo kununua BMW customized/special order bulletproof.

Ama kwa hakika usalama wa kiongozi is a function of what he does, what he decide, what he defend, what he is, how his image is perceived, how he makes decision, how he talks or make speech, how he keep close to the people. If all is well kiongozi can walk even in the mid night on foot in Manzese suburbs, 1200 noon at Kariakoo, or going to mosque/church at 0500am on foot at Magomeni. I do not mean the president must risk but security should not cost us too much over the interest of the citizens. Mbona viongozi wetu wa vijiji hawahofu security? BUT Yes we are unique and we LOVE our president and our country too! Outside the box we need to have very well organised team to set priorities and prioritize when it comes to matters of high financial coughs.

CREDIT to our hon. President kwa kukubali kwa kutokubaliana na uamuzi huo wa usalama kununua BMW wakati duniani Mercedes inakubalika na tunazo za kutosha. Haya watueleze hizo walizo nazo Benz watazipeleka wapi au ndio minada ya kishikaji kimya kimya? Hata mimi ningependa kununua Benz walizoendeshwa marais wangu Dar es Salaam. Tena bado zitakuwa mma kabisa kwani hazijavuka Dar es Salaam. Barabara ni mkeka kama Nyu Yoku vile. Cha kubadilisha ni matairi tu.

Mungu ibariki Tanzania!

Wataachiwa wakina salva.....
 
Mbona Tanzania tupo tayari kupokea pokea? Hao waarabua wametoa bure kwa sababu zipi,Kwani zile benzi zilikuwa zimechoka? Ni tabia hii ya kupokeapokea inatufanya tuonekane hovyo na inawalemaza viongozi wetu wanakuwa wavivu wakufikiri!
 
Jamani,hapa JK tusimuonee.Haya magari wamepewa buree toka uarabuni.Tena hawa waarabu walileta mpaka mtaalamu wa haya magari toka Ujerumani kuja kuyafanyia service kabla hayaanza kutumiwa.Hata lile benzi alilotumia Mkapa wakati anamaliza muda wake nalo lilikuwa la chee toka hukohuko.

Kama ni msaada kwanini uingie kimya kimya!? Je, Waarabu hao wamepewa nini toka nchini mwetu hadi wakatoa zawadi za magari hayo? Au ni wajomba zetu wa siku nyingi ambao walikuwa wametusahau na sasa wameamua kutukumbuka?
 
Mambo mengina hakuna hata haja ya kuyajadili, hivi kweli kuna sababu za kuhoji why Raisi wetu amebadilisha gari kwa ajili ya matumizi yake? tunapaswa huhoji anaendeshaje nchi yetu lakini hili ambalo watu walipo kwenye kamati ya usalama wa raisi wameona kuwa linafaa kulinda usalama wake halipaswi kujadiliwa na kulikosoa, na sitashangaa kuona watu wanakuja humu na kusema hizo pes azilizonunua magari wangewapa wanafunzi wa vyuo vikuu... hahaha some times JF makes me happy
 
This is all crap!
Nchi yetu kweli ni maskini ila watu wanaponunua magari ya kifahari ya ikulu kwani raisi ndiye anasema nataka nipande BMW?
Vitu vingine tunamlaumu huyu JK bure tuu!
 
Kama ni msaada kwanini uingie kimya kimya!? Je, Waarabu hao wamepewa nini toka nchini mwetu hadi wakatoa zawadi za magari hayo? Au ni wajomba zetu wa siku nyingi ambao walikuwa wametusahau na sasa wameamua kutukumbuka?

Usisahau wamemilikishwa kule Loliondo! Wanataka kupata vitalu zaidi kwa ajili ya kuwinda! Na labda Tanzania kuna mafuta wanataka wawekeze!
 
..Acha hasira...mi nasubiri watangaze mnada tu nijipatie angalau ka-benz nisafishe jina mjini hapa!!!!!!!!!!!!!

That will only happen in your daytime dreams..hizo benz zishagawanywa kitambo..

Hebu msikie huyu kwanza:

Luhanjo alisema kwa kifupi: "Ahaa, bwana ee...!"
... Kwa kukusaidia kutafasiri maanake wanene hawataki mainzi kwenye anga zao ..

teh teh teh..
 
acha kutudanganya bana, waarabu gani hao wanaoingia hadi kwenye usalama wa Rais? wewe umejuaje? isitoshe misaada huwa inatangazwa.

Kama wewe unakaa Dar,unafikiri yale mabenzi meusi wanayotumia foreign affairs kwa wageni,na lile jeusi alilotumia Mkapa mwishoni yalitoka wapi? Yalitoka kwa Ghaddafi.Haya ma BMW yametoka Saudi Arabia.Hawa watu walishapewa eneo kubwa tu la kujenga ubalozi wao,Masaki.Pia taarifa wanapewa eneo kubwa kujenga bandari.
Sasa wewe unaesema mimi mwongo basi njoo na risiti,au atleast bei ya hayo magari yamenunuliwa wapi,tusiitane waongo tu bila facts.Prove me wrong,lakini usiniite muongo.
 
Jamani;

Naomba muwe wapole. BMW ni za msaada. Huyu mwandishi alistahili kuchunguza kwanza kabla ya kuhitimisha na kutaja ma bei.

FP
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom