Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,444
*YAACHANA NA MERCEDES BENZI
Na Ramadhan Semtawa
Source: Mwananchi
My take
Haya sasa ooh serikali haina pesa ooh nchi yetu maskini.
Mambo hayo magari haya tayari yamesha igharimu serikali si chini ya Bilioni 1.
Bado msafara wa Pinda,Shein,KArume na wengineo.
Na Ramadhan Semtawa
AWAMU ya nne ya Serikali ya Jakaya Kikwete, imeamua kuachana na magari iliyotumia kwa muda mrefu ya Marcedes Benz na sasa inatumia magari mengine ya kifahari ya BMW kwa ajili ya msafara wa rais.
Mercedes Benz, gari ya kifahari inayotengenezwa nchini Ujerumani, imekuwa ikitumiwa na serikali zote tatu zilizopita zilizoongozwa na Mwalimu Julius K. Nyerere, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa. Gari iliyotumika mwanzoni mara baada ya kupata uhuru ilikuwa Rolls Royce.
Lakini kwa sasa, msafara wa Rais Kikwete unapambwa na magari matano ya BMW, mawili yakiwa ni X 5, ambayo ni mithili ya Toyota VX kwa ukubwa na matatu yakiwa Series Seven, Mwananchi imeshuhudia.
Hatua hiyo ya Ikulu imekuja wakati mpango wa wataalamu wa kutaka kupunguza magari ya kifahari ya serikali ukiwa umekwama katika meza ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.
Wakati Luhanjo akiwa na ripoti ya mpango huo ambao unaonyesha serikali ina magari 40, 000 ya kifahari maarufu kama mashangingi Vx na Gx, yakiwa ni 15,000, Ikulu imeibuka na magari hayo mengine ambayo bei yake ni kati ya Sh200 milioni hadi Sh500 milioni.
Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa gari hizo ziliingizwa nchini kwa ndege kutoka Afrika Kusini na kwamba, lengo la kuhama Mercedes Benz ni kuimarisha zaidi usalama wa rais na msafara wake.
Lakini Katibu Mkuu Kiongozi, Luhanjo alipoulizwa sababu za Ikulu kuhamia BMW, hakutaka kueleza lolote.
Luhanjo alisema kwa kifupi: "Ahaa, bwana ee...!"
Wakati Luhanjo akiwa bubu, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rais, Salva Rweyemamu, naye aliamua kuwa kimya.
Salva alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi hakuipokea, lakini baadaye akiwa nje ya nchi kwenye msafara, ndipo alipotuma ujumbe mfupi wa simu (sms).
Mkurugenzi huyo, ambaye aliwahi kuwa mwandishi mahiri na mchambuzi mzuri wa sera za serikali, alituma ujumbe huo mfupi akisema: "Niko nje, siko nchini."
Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu ambayo ndiyo yenye dhamana ya ununuzi wa magari ya serikali, Omar Chambo, akionyesha ushirikiano kwa mwandishi, alisema kwa uwazi kwamba, hakuwa na taarifa na mpango huo.
Chambo, ambaye ni mtendaji na mmoja wa wateule wa rais mwenye uhusiano mzuri na vyombo vya habari, alisema: " kwa kweli kabisa sina taarifa kwani si mpango wa wizara, uliza Ikulu kama kuna kitu kama hicho maana mimi sijakisikia."
Mercedese Benz ndizo gari ambazo zimekuwa zikitumiwa na marais katika misafara yao.
Katika uchunguzi huo, Mwananchi imebaini kwamba uamuzi wa kuhama Mercedes Benz unatokana na ushauri wa timu ya usalama wa rais.
Pamoja na gari hizo kuwa na bei kati ya Sh200 milioni na Sh500 milioni, gari ambazo huagizwa kwa maelekezo maalum kutokana na mahitaji ya mteja (specifications) huwa na bei tofauti na zile zinazouzwa sokoni.
Kwa ujerumani, bei ya BMW ndogo ya 730d ni kati ya Euro 69,500 na euro 70,000, wakati kubwa kabisa, BMW 750Li ni Euro 94,000 kwa magari ambayo hayajaagizwa, au yale yaliyo sokoni.
Hata hivyo, magari hayo mawili-Merceds Benz na BMW hayana tofauti kubwa ya bei, ingawa Mercedes imekuwa ikionekana kuwa imara na inayodumu kwa muda mrefu.
Inaelezwa kuwa baada ya kuwasilishwa kwa mpango wa kuhama Mercedes, Rais Kikwete alipinga wazo hilo, lakini timu ya usalama ikashauri na kusisitiza kuwa gari hizo ni muhimu kwa sasa.
Ingawa inaonekana gari hizo ni za gharama, lakini timu hiyo ilisisitiza kwamba usalama wa rais ni jambo muhimu zaidi.
Hata hivyo, Rais Kikwete bado anatumia gari aina ya Mercedes Benz kwenye misafara yake na alitumia msafara wa Mercedes wakati alipokuwa Dodoma kuongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM.
Akiwa Dodoma, Rais Kikwete alitumia Mercedes Benz kubwa ya milango sita, ambayo ilimchukua kutoka Uwanja wa Taifa mara baada ya kukabidhiwa nchi na rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
Source: Mwananchi
My take
Haya sasa ooh serikali haina pesa ooh nchi yetu maskini.
Mambo hayo magari haya tayari yamesha igharimu serikali si chini ya Bilioni 1.
Bado msafara wa Pinda,Shein,KArume na wengineo.