Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Status
Not open for further replies.
That is what happens when a bunch of misfits are given such power.I bet they are confusing the act running a nation with running a bar.Even drug cartels have a better communication system than this good-for-nothing government.
 
Serikali ifute kabisa huu mfumo wa posho. Wajumlishe kila kitu kwenye mshahara. Hivyo mbunge au mwingine yoyote akichukuwa mshahara wake ajue kabisa fungu la mboga, bia, warsha etc liko humo. Vinginevyo kila siku tutakuwa tunaongelea posho.
 
Well hapo sasa ndio tunajua nchi hii watu wapo makini kiasi gani kuokoa ngozi zao wenyewe lakini matokeo yake ni kama wanajikaanga kwa mafuta yao wenyewe.

Sasa hiyo taarifa ya Ikulu mbona inalenga zaidi kumuaibisha Rais na Utawala wake mbovu. Kweli watu wanatoa taarifa kama hiyo na kusema kwamba ni taarifa toka ofisi muhimu kuliko zote nchini? Ina maana hakuna mawasiliano kati ya Waziri Mkuu na Rais na Spika wa bunge? Ikiwa ni hivyo tunaelekea wapi kama nchi?

Dah inauma sana hii. Kuzaliwa Mtanzania sio laana ni baraka sasa kwa nini tuwaache wachache wachezee baraka tulizopewa na mwenyezi Mungu katika hii nchi yake?

Usishangae ndugu yangu. Hii ni reaction over nguvu ya umma. Madaktari wamegoma, watu wanakufa, umetishia kuwafukuza madaktari ambao hata hawatoshi nk, hali ni tete lazima Raisi aokoe jahazi. Unaongeza posho ya laki mbili kwa wabunge wakati umekataa kulipa posho ndogo tu ya madaktari! Wacha Raisi akane hata kama ni kujichanganya. Ndiyo response tuliyokuwa tunataka wala si vinginevyo. Tumtie moyo Kikwete hayo ya kujichanganya na W/Mkuu hayatusaidii sisi ili mradi wabunge wasiongezewe posho na madaktari wasikilizwe warudi kazini.

Pinda ana-act kama hatakuwepo kesho, hajali lawama hata kama ndugu zetu wanakufa Mahospitalini. Yoweee!
 
badala ya kutolea kauli la madaktari kugoma hili wamejibu haraka...hii ndio TZ ya JK

madaktari wauaji kuwatolea kauli ipi, kumbuka daktari wa machael Jakson kafungwa na kufutiwa leseni kwa kutoa dawa iliyomuua Machael jaribu kugoma kwa wenzetu na kuua.
 
Hapo pekundu means PINDA NA MAKINDA hawana Busara wala Hekima, yaani ni washenzi mana wamefanya maamuzi kishenzishenzi. Hapo c ndipo pa kuwataka wajiuzuru kwa kulidanganya Taifa???Walafi na wabinafsi, Manyang'au hao
Hawawezi kujiuzulu hao..
 
wewe mbona kutuambii posho unayopokea kwa kumshambulia JK acha longolongo hapa Jf

Tunahoji kauli za viongozi wetu zisizokuwa na mashiko kwa nini na wao wamekuwa wapiga kelele wakati ndio wenye maamuzi ya mwisho
 
Rais legelege anayeongoza serikali legelege. Siasa za nini? Kuoneana haya kwa nini?

Hakuna alichojibu hapa. Empty statement
Woote hawa (bunge na ikulu)lazima waoneane haya kwasababu woote tatizo lao moja......ubinafsi...hamna wa kumuhukumu mwenzake.....kwa kifupi...manyang'au na mafisi at work.........
 
Hivi kwa nini asiseme tu kuwa hakubaliani nalo hilo jambo?

Halafu yeye malipo yake ni shi'ngapi?

Bunge sio mhimili wa utawala/serikali kama ilivyo kwa afya upande wa madaktari ndio maana imekuwa rahisi kukataa ya madaktari kwa sababu iko chini ya serikali lakini bunge haliko chini ya serikali.
 
Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili.

Tuanzie hapo kwenye blue: Rais anakubali posho kwa wabunge ziongezwe au la? simple yes or no.
Wabunge wameshangalia upya posho zao na wakaja na figure 200,000 extra! Na ili waweze kulipwa ni lazima (kwa taratibu za sasa) rais atie sign.

Uongozi hana mamlaka juu ya e lazima ufanye maamuzi na uwe tayari kutetea maamuzi yako hata kama wengi watakasirika. Sasa ame-sign au haja-sign? Kama haja-sign kwa nini? Na kama ame-sign kwa nini? Hizi open-ended statement hazitoi mwongozo hata kidogo sana sana zinaonena dalili ya kukwepa kufanya maamuzi.

Rais hana mamlaka juu ya bunge kuwa makini kidogo tu. Jk yuko mhimili mwingine kama kuna jambo linaleta mvutano kati ya mihimili mazungumzo ndio njia mwafaka na ndio maana rais hana madaraka ya kumfuta kazi spika au jaji mkuu.
 
UNAFIKI UNAVYOENDELEA KUITAFUNA SERIKALI YA CCM SINA HAMU!!

Mkuu Ritz, Rekebisha usemi; kati ya Pinda na Kikwete nani kachanganyikiwa hapa?

Na kwa dozi hii ya DOUBLE STANDARDS huko Magogoni nakuambia kitendo alichokifanya Rais kuwadhalilisha Waziri Mkuu wake, Spika pamoja na Wabunge wa CCM kuonekana walafi kule Dodoma, nakuhakikishia kwamba maafisa waandamizi serikalini sasa wataanza kumgwaya huyu ROLE MODEL wako kama ukoma.

Nasema kwa mtaji huu wa mamuzi ya 'nenda-mbele-rudi-nyuma-kanyaga-watu' hivi sasa IMANI ITAKUA IMEWATOKA hata wasaidizi wa karibu wa Rais Kikwete kwa kuwa anaonyesha wazi udhaifu wake mitaani wa a person of a clouded mind and weak in decision making if notirrational in many instances!

Ritz tafadhali kamshauri huyu shujaa wako akajiuzulu mapema kwani mawimbi mazito ya nyumbani na kimataifa hatoyaweza kamwe; bora aondoke mapema kabla ya kudhalilika zaidi hapa!!

Habari ndio hiyo mkuu.


Pinda, kachanganyikiwa na migomo ya madaktari.
 
Huu ni Ushindi kwa Zitto Kabwe kwa kuwa aliwaambia ukweli kuhusu posho kutosainiwa wakabishi na kumzomea sasa hivi wanazomewa wao. wabunge wote waliozomea Hovyoooooooooooo!!

Tamaa ya pesa hufanya watu wawe viziwi na hivyo kutosikia vilio vya haki....Sasa itabidi mtu awajibishwe kutokana na ufidhuli huu.
 
madaktari wauaji kuwatolea kauli ipi, kumbuka daktari wa machael Jakson kafungwa na kufutiwa leseni kwa kutoa dawa iliyomuua Machael jaribu kugoma kwa wenzetu na kuua.

Madai ya madaktari ni ya muhimu kuliko posho za wabunge.
 
Watu walafi Rais anawaambia watumie busara hiyo ndiyo busara waliyotumia ya kuhalalisha posho, kwanini Rais asiwe na ujasiri wa kuwaambia anapinga ongezeko la posho hizo biashara iishie hapo.
 
Serikali ifute kabisa huu mfumo wa posho. Wajumlishe kila kitu kwenye mshahara. Hivyo mbunge au mwingine yoyote akichukuwa mshahara wake ajue kabisa fungu la mboga, bia, warsha etc liko humo. Vinginevyo kila siku tutakuwa tunaongelea posho.

FJM hiyo ndiyo tiba ya ugonjwa wa posho. Lakini hawa waheshimiwa hawatakubaliana na wewe kwa sababu ushauri huu ni kuwanyang'anya tonge mdomoni. Wabunge wetu hawataki hata kujifunza kutoka kwenye sekta binafsi (kama mabenki) hulipaje senior staff wao. Ni wizi mtupu.
 
Hivi hawa wako boti moja au ni mbili tofauti? Waziri mkuu anasema hivi..Raisi anakuja na kukana!
 
Jamani kwani hamjamuelewa JK, this is how he operates!! Anapenda kukimbia lawama! Yeye haoni shida ya kutolewa kwa statement tofauti tofauti< hili kwake si shida, ali-muradi akirudi atakuja na jinsi ya kutafuta sympathy kwa umma kuwa watu wanamhujumu; anahitaji kuwin watu wamuonee huruma!

JK ni mtu cheap sana! Asiye na ujasiri wa kufanya wala kuamua lolote, hayuko tayari kulaumiwa kwa maamuzi yeyote yale! EL alipojiuzuru ndo tukapata nafasi ya kumjua Jk alivyo, ni mtu anayeendekeza majungu, uzandiki, na mipasho!! Mimi kwa kweli sishangai...

Subirini tu, akirudi na kupumzika vizuri, ataishia kuongea na wazee, hapo ndo utakapojua u.kwere wake... just wair=t and see...

Rev. pole sana nakushauri boot tu, maana hautamaliza ku-download!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom