Julius K. Nyerere: Ikulu ni pahali patakatifu, sio pango la wanyang'anyi

Nimeamini maneno Hayati Mwl.Nyerere kama kichwa cha habari kinavyosema,pia wana jf hii ndio habari yangu ya leo.

Nimemsikiliza Raisi hotuba yake, kwenye suala la siasa na usalama wa nchi natofautiana naye kwa asilimia mia moja,kwanza kabisa nadiriki kusema anajaribu kutisha wananchi waogope kuwa wawakilishi wao ati wanataka kuindoa serikali halali madarakani kitu hiki sijawahi kukisikia naona anaogopa kivuli chake,je suala la udini halipo tena?au ameona hiyo propaganda imefeli?na anakuja na mpya?

Siku zote serikali yenye matatizo huwa inaweweseka sana,maana hatma yake mbele ya safari haipo,na siku zote serikali inapoamua kwa makusudi kufinyanga haki za wananchi wake haiko salama hata kidogo,maana IKULU imegeuka mahakama,ukumbi wa disco kwa wachache waliodhamilia kuhujumu mali na rasilimali ya nchi yetu na ulanguzi.Ikulu haijali shida za watanzania wengi ambao ni masikini.Mikataba mibovu,bei za bidhaa muhimu kwa maisha ya binadamu kupanda hovyo hovyo,lakini Ikulu inaona ni sawa tu.

Je ni kwanini JK anailaumu chadema kwa kufanya maandamano nchi nzima wakieneza chuki dhidi ya serikali yake.Hali halisi ya serikali;serikali hii inamatatizo makubwa sana hasa ya kuwanyonya watanzania kwa kufanyakazi yenye ubinafsi,yaani kuwaneemesha wachache na gharama kuwabebesha masikini Ikulu ikiwa kimya na tena kutowatambua wamiliki wa hizo biashara je ni serikali gani duniani isiyotambua wabia wake wa biashara.

Kwa mtazamo wangu,kwanini CHADEMA inakwenda moja kwa moja kwa wananchi kwa kundaa maandamano na mikutano kuwaeleza moja kwa moja maovu ya Serikali,sababu iko moja kubwa,ni kufinyangwa kwa haki na sheria za nchi kuwanyima wawakilishi wa wananchi kuwashilisha matatizo yanayowakabili sehemu husika,asisahau vitendo vya spika Anne Makinda katika nguvu zake kuzuia hoja muhimu ambazo kama angeruhusu wasingekuwa na uwezo au nguvu za kuzizungumzia katika majukwaa.

Ukiruhusu Ikulu ikatumike kama pango la walanguzi ujue unaharibu maisha ya serikali, ni ajabu kwa kiongozi kulalamikia chama cha upinzani eti kinataka kupindua serikali yake,lakini anasahau jinsi serikali yake ilivyoshindwa kazi.kinachotakiwa aweke urafiki kando na kutoa adhabu stahiki kwa wakosefu na kuhakikisha serikali inasimamia vizuri raslimali za nchi kwa manufaa ya watanzania na si vinginevyo.

Chama chochote makini huindoa serikali legelege madarakani kwa hoja ambazo zinasababishwa na hiyo serikali,hivyo JK usilalamike imalisha serikali yako kuwa mkali uone matokeo la sivyo 2015 ni karibu wenzako wameanza kujenga msingi/mtaji wa 2015.
 
Wana JF
nimepata mkwaruzano wa hoja na mwana jf (Tumaini Letu) kuhusu ikulu kuwa ni mahali patakatifu!!!!!!!!!!!!
mimi nilimueleza kwamba ikulu sio mahali patakatifu kama mahali ila hiyo ni kauli kuweka msisitizo kwamba kwa Mwananchi yeyote hatakaye onyesha nia ya kwenda kufanya kazi IKULU basi hawa na hisia au awe tayari kuishi kama mbinguni kwa matendo yake pale ikulu.
na hiii sio katika misingi ya dini Nyerere alikuwa na maana ya matendo ya kiuungwana na wema.
lakini sio kwamba alikuwa na maana kwamba ikulu ni mahali patakatifu kama mahali

TUMANI LETU yeye anasema nanukuu
>>>>>>>>>>>> KAMA DK SLAA ANGEKUWA RAISI INAMAANA MCHUMBA WAKE AMBAE NIMJA MZITO SASA ANGEJIFUNGULIKA IKULU,HVYO MTOTO ANGEKUWA WA NJE YA NDOA NA PALE IKULU NIMAHALI PATAKATIFU
>>>>>>>>>>>>>>>

sasa sijui kwa mfumo wa utakatifu huo anaoudai mkuu kama kuna mtu angeweza kuishi pale?
has huyo aliyepo
sasa je Nyerere alikuwa na maana gani kusema ikulu ni patakatifu?
 
Kitu kikubwa ambacho Nyerere alimaanisha ni kuwa mtu yoyote anayetakiwa kuingia ikulu awe mwadilifu yaan mtu yaani atakayeongoza nchi kwa misingi ya utawala bora na asingie ikulu kwa njia ya rushwa na ndio maana alisisitiza kuwa ikulu sio pango la walanguzi. Kwa hiyo cha msingi hapo ni kuhusu mtu anayefuata mising ya uongozi, utakatifu aliomaanisha sio ule kwamba ikulu ni mahal patakatifu kama vile msikitin au kanisan hakuumaanisha hivyo.
 
Wazo la baba wa taifa, hayati Nyerere kuwa ikulu ni mahali patakatifu si kweli. Ni nadharia potofu inayodhihirishwa na hali halisi kuhusiana na ukweli kuwa sehemu hiyo ni makazi ya rais na si sehemu ya ibada. Tuachane na dhana hiyo tukijua kwamba ikulu itabaki kuwa ikulu, na kamwe haitakuwa mahali patakatifu labda pageuzwe kuwa sehemu ya ibada (msikiti au kanisa) jambo ambalo si rahisi kutokea. Hivyo, usitegemee mambo matakatifu kutokea ikulu, kwa kudhania eti ikulu ni mahali patakatifu, you'll be highly disappointed! Tuwaache watakatifu wabaki na utakatifu wao kwa mujibu wa imani zao, na ikulu ibaki kama ilivyo - just a State House.
 
Itieni mamlaka iliyopo duniani,utakatifu unaongelewa ni kuwa mwaminifu na siyo kuwa fisadi yaani kutumia madaraka uliyo pewa na wananchi kujinufaisha ndiyo maana ya mahali patakatifu. fikiri kabla ya kueleza jambo
NI ufafanuzi tu.
 
Utakatifu aliousema Baba wa Taifa ni kuhusu uaminifu katika kutumia madaraka ya Ikulu katika kuwajali watu wengine na sio utakatifu unaotokana na kuwepo kwa nyumba za ibada eneo hilo. Alikuwa anonyesha tabia ambayo mtu anayetaka kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania anatakiwa kuwa nazo.
 
Na tangu aondoke yeye hajatokea mtu wa aina hiyo katika ikulu ya nchi yetu. Labda tutegemee 2015.
 
hata kama si patakatifu lakini lowasa hata kaa aishi pale maisha yake, mmasai mwizi sana yule, nyerere alishatuonya, kama alikuwa raisi wa monduli akaiba hivyo akiwa rais wa tz si atatufi.... yule?
 
Nyerere alituonya sana juu ya Lowassa, na Malecela, na Kikwete akamwambia asubiri akue!
 
Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere alipata kusema, kwamba " Ikulu ni sehemu patakatifu" Yeyote anayekimbilia Ikulu muogopeni kama ukoma. Rais wetu, na genge lake la majambazi ambao hawalijali taifa wamepageuza Ikulu kuwa sehemu ya walanguzi na wafanya biashara chafu. Hata Majasusi wakubwa kama wa "symbion Paul na Joe wilson" ambao wasingekaribishwa nchi yoyote wamepata shamba la baba la Kuchuma.

Wafanyabiashara wachafu wote nchini wamepita Ikulu na Kubarikiwa na Rais, Waarabu wanaowauwa Wananchi loliondo wamepitia ikulu. Wanaoiba Migodini Wamepata Mibaraka Ya Kikwete. Ikulu yetu imekuwa sehemu chafu na si patakatifu TENA. Rais Kikwete Kwa Heshima ya Taifa la Tanzania Tunaomba ujiuzulu. Kwanza wewe siyo Rais. Wewe ni Mtalii anayezunguka Dunia. Tuachie nchi yetu tuisafishe. Ondoka, Fanya Ustaarabu Kama alivyofanya Rostam Aziz. Watanzania hawakutaki tena. Usiposikia basi aibu utakayoipata itakuwa kubwa Zaidi. Watanzania wamechoka
 
Dawa ya Kikwete ni nguvu ya umma
 
Ni lini Ikulu imekosa kuwa genge la Majambazi?.

Jamani tatizo sio JK bali ni CCM haya yote mnayaona ni ktk UCCM wenyewe kwa nini afanye nje ya dira ya chama. Toka Mwinyi hadi Mkapa hakuna wakati Ikulu imeheshimiwa kwani mikataba mibovu ndio ilizaliwa rasmi. Ukianza kuhesabu Mkapa namba moja, Kisha JK na Mwinyi na wote hawa walialika wageni wa ajabu ajabu kiasi kwamba alipokuja Bush aliiteka Ikulu nzima kwa siku nne.
 
Back
Top Bottom