Ikulu: Mkapa hawezi kupanda mahakamani; Hahusiki kesi ya Mahalu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
* Hahusiki kesi ya Mahalu

Na Mwandishi wetu (Gazeti la Uhuru)
Thursday, 28 April 2011

IKULU imekanusha habari kwamba imekuwa ikihaha kumsafisha Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, katika kesi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Reyemamu, alisema jana kuwa Ikulu haiwezi kufanya hivyo, kwani Mkapa hahusiki na kesi hiyo. Alisema habari hizo ni za uongo zinazolenga kumhukumu mtu bila hatia.

Rweyemamu alikuwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kufuatia gazeti la MwanaHalisi kuandika habari ikisema: 'Mkapa kutinga kortini' na kwamba 'Ikulu yahaha kumuokoa Kikwete'.

Gazeti hilo toleo namba 239 la Aprili 27 hadi Mei 4, mwaka huu, lilichapisha habari hiyo katika ukurasa wa mbele ikiwa na kichwa cha habari kisomekacho ‘Mkapa kutinga kortini'.

"Ikulu inakanusha taarifa zilizochapishwa na gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki kuwa imekuwa ikihaha kumsafisha Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa. "Na inasisitiza kamwe haiwezi kufanya hivyo, kwani yeye si mhusika katika kesi hiyo," alisema Rweyemamu na kuongeza kuwa kuandika habari hiyo huku kesi ikiendelea ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Rweyemamu alisisitiza Rais mstaafu Mkapa hahusiki katika kesi hiyo na kwamba badala yake anayehusika ni Profesa Mahalu, hivyo kuleta mijadala au kuingiza nje ya mahakama ni kuingilia mwendelezo wa kesi, jambo ambalo si busara.

Aidha, Rweyemamu amewataka waandishi wa habari kuwa makini na kuzingatia maadili ya taaluma hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoingilia masuala ambayo yako mahakamani.

Habari hiyo, ilidai katika hati ya kiapo cha Machi 31, mwaka 2011 chini ya sheria ya usajili wa nyaraka, Mkapa alitoa utetezi kuwa kila kitu kilichofanywa na Profesa Mahalu kilikuwa sahihi.
 
huu ni ujinga Mubarak watu wameandamana hadi anafikishwa mahakamani soon, huyu Mkapa ni nani?
thats why we need katiba mpya kuondoa kulindama kama hivi, hakuna mtu aliye juu ya sheria
 
Tehe tehe teheeee!
Kazi kwelikweli.
'Hawezi kutinga mahakamani' who is he!
 
nani mwenye uhakika na uraia wa Salvatory Reyemamu:frusty::frusty::frusty::frusty::frusty::frusty:
 
hivi ni banyamulenge au mhaya? au alirudia darasa la saba na kuvaa hilo jina la kihaya?

..HIMA EMRIRE SYNDICATE......................

......Huyu mke wake alijilipuwa London kama mkimbizi wa Rwanda.....

only possible in Tanzania.....
 
too bad jk amezunguukwa na meccenaries watupu and he cant see it na anawapuuzia watz wenzake.
 
hausiki kivipi?salva ni hakimu?huko ndiko kuingilia uhuru wa mahakama!HOSNI MUBARAK mwenyewe yupo jela sasa inashindikana mkapa kutoa ushahidi?
 
wana JF tusijadili sana suala la uraia wa reyemamu, hebu tulitazame kwa marefu na mapana suala la mstaafu Chinga kama nihaki afikishwe kizimbani au la; bado haijajulikana mbele ya sheria nani katoa melezo sahihi kati ya gazeti na Reyemam, naomba wanasheria mtufafanulie vizuri juu ya hili.:A S 39:
 
* Hahusiki kesi ya Mahalu

Na Mwandishi wetu (Gazeti la Uhuru)
Thursday, 28 April 2011

IKULU imekanusha habari kwamba imekuwa ikihaha kumsafisha Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, katika kesi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Reyemamu, alisema jana kuwa Ikulu haiwezi kufanya hivyo, kwani Mkapa hahusiki na kesi hiyo. Alisema habari hizo ni za uongo zinazolenga kumhukumu mtu bila hatia.

Rweyemamu alikuwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kufuatia gazeti la MwanaHalisi kuandika habari ikisema: 'Mkapa kutinga kortini' na kwamba 'Ikulu yahaha kumuokoa Kikwete'.

Gazeti hilo toleo namba 239 la Aprili 27 hadi Mei 4, mwaka huu, lilichapisha habari hiyo katika ukurasa wa mbele ikiwa na kichwa cha habari kisomekacho ‘Mkapa kutinga kortini’.

“Ikulu inakanusha taarifa zilizochapishwa na gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki kuwa imekuwa ikihaha kumsafisha Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa. “Na inasisitiza kamwe haiwezi kufanya hivyo, kwani yeye si mhusika katika kesi hiyo,” alisema Rweyemamu na kuongeza kuwa kuandika habari hiyo huku kesi ikiendelea ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Rweyemamu alisisitiza Rais mstaafu Mkapa hahusiki katika kesi hiyo na kwamba badala yake anayehusika ni Profesa Mahalu, hivyo kuleta mijadala au kuingiza nje ya mahakama ni kuingilia mwendelezo wa kesi, jambo ambalo si busara.

Aidha, Rweyemamu amewataka waandishi wa habari kuwa makini na kuzingatia maadili ya taaluma hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoingilia masuala ambayo yako mahakamani.

Habari hiyo, ilidai katika hati ya kiapo cha Machi 31, mwaka 2011 chini ya sheria ya usajili wa nyaraka, Mkapa alitoa utetezi kuwa kila kitu kilichofanywa na Profesa Mahalu kilikuwa sahihi.

Hakuna marefu yasiyo na mwisho kama yalivyo na ncha.Sijaelewa unaposema hawezi kutinga mahakamani?kwakuwa hana makosa au? kwani hati yake aliyoisaini ipo wazi na sheria ikifuatwa mwisho wake anatakiwa kutoa ushahidi.Rweyemamu kwanini mnapenda kutufanya sote wajinga katika sheria?

Ndani ya makosa ya jinai president anakinga gani?iko katika ibara gani ya katiba?

kwa mantiki hiyo Mkapa anaweza na iko siku atapanda kizimbani whether he likes it or not.watanzania wanaopanda vizimbani ni wanadamu pia.Huu ni uonevu mkubwa kwani sheria zinapindishwa kupita maelezo hakuna kitu uhuru wa mahakama.Ndiyo maana tunadai katiba mpya.Time will tell.
 
Mbona hajakanusha hati ya kiapo iliyowekwa gazetini inayo onyesha ushahid wa mkapa akiutoa mbele ya mwanasheria?
 
ishu hapa ni hati inayo onyesha Mr clean kaapa na sio huyo Banyamlenge anavyo tetea Ikulu.
Kwanza ni mgeni na shughuli za Ikulu na mala nyingi amekuwa anajibu majibu mengi kwa ufahamu wake na si IKulu
kutokana na kuto jua maadili ya TIS na kazi zao.
Hana jipya zaidi ya kusoma magazeti na kukurupuka na majibu ya mizaha. Any way fadhila za uwana mtandao hizo.
 
* Hahusiki kesi ya Mahalu

Na Mwandishi wetu (Gazeti la Uhuru)
Thursday, 28 April 2011

IKULU imekanusha habari kwamba imekuwa ikihaha kumsafisha Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, katika kesi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Reyemamu, alisema jana kuwa Ikulu haiwezi kufanya hivyo, kwani Mkapa hahusiki na kesi hiyo. Alisema habari hizo ni za uongo zinazolenga kumhukumu mtu bila hatia.

Rweyemamu alikuwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kufuatia gazeti la MwanaHalisi kuandika habari ikisema: 'Mkapa kutinga kortini' na kwamba 'Ikulu yahaha kumuokoa Kikwete'.

Gazeti hilo toleo namba 239 la Aprili 27 hadi Mei 4, mwaka huu, lilichapisha habari hiyo katika ukurasa wa mbele ikiwa na kichwa cha habari kisomekacho ‘Mkapa kutinga kortini’.

“Ikulu inakanusha taarifa zilizochapishwa na gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki kuwa imekuwa ikihaha kumsafisha Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa. “Na inasisitiza kamwe haiwezi kufanya hivyo, kwani yeye si mhusika katika kesi hiyo,” alisema Rweyemamu na kuongeza kuwa kuandika habari hiyo huku kesi ikiendelea ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Rweyemamu alisisitiza Rais mstaafu Mkapa hahusiki katika kesi hiyo na kwamba badala yake anayehusika ni Profesa Mahalu, hivyo kuleta mijadala au kuingiza nje ya mahakama ni kuingilia mwendelezo wa kesi, jambo ambalo si busara.

Aidha, Rweyemamu amewataka waandishi wa habari kuwa makini na kuzingatia maadili ya taaluma hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoingilia masuala ambayo yako mahakamani.

Habari hiyo, ilidai katika hati ya kiapo cha Machi 31, mwaka 2011 chini ya sheria ya usajili wa nyaraka, Mkapa alitoa utetezi kuwa kila kitu kilichofanywa na Profesa Mahalu kilikuwa sahihi.
Kama gazeti limingilia huru wa mahakama kwa kuandika ya kua 'Mkapa kutinga korti'Je Ikulu au Salva Rweyemamu amefanya nini kwa kutamka ya kua 'Mkapa hausiki na kesi hiyo'Ameutoa wapi ujasili wa kutamka hivyo?Au kuna Watu ambao mahakama au mkondo wa sheria sio mahala pao.Ki-mantiki kunauwezekano wa Mkapa kutinga mahakamani kwani alikua bosi wa Mahalu.Kauli ya Ikulu inathibitisha ni jinsi gani ufisadi ni falsafa ya CCM.Kauli zao tumezizoea" hakuna mpasuko ndani ya chama"Hakuna mafisadi"n.k.And then..."Tume ya mwinyi kuondoa mpasuko katika chama""kujivua magamba"n.k.OMUKAMA TA RWEYEMAMU NOTUGWISA!!!!!!!!!!
 
Ndiyo sababu tunataka katiba mpya hiyo kinga ya kikatiba ya Rais iondolewe,ili waende mahakamani wakifanya madudu ikulu,tunataka ya Zambia yatokee hapa kwetu ili wakome kukimbilia Ikulu tena wakome kabisa kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Tutaanza na mzee ruksa kwa kumilikisha loliondo kwa waarabu,Chinga kwa kufanya biashara ikulu,ufisadi wa kujimilikisha kiwira nk na ****** ana kesi ktk IPTL akiwa waziri kuna dili kubwa alicheza hapo na Mahalu anawajua wote waliohusika nae akiwemo boss wake wa mambo ya nje wkt huo.Wote hawa lazima wapande kizimbani kujibu mashtaka yanayowakabidhi.Kapanda Chiluba wa Zambia, waziri mkuu wa Italia nae kapanda sasa kwani Mkapa kawa nani asipande wajamini? Tungekuwa wazi kama nchi za wenzetu kusingekuwa na tuhuma kubwa za ufisadi kama sasa.Katiba mpya muhimu na lazima kinga ya viongozi tuitoe.Aluta Continue.Wanaogopa kulishtaki mwanahalisi kwani litaanika zaidi uozo wao ndio maana wamekanusha bila kusema liombe radhi.
 
Back
Top Bottom