Ikulu kuwafutia posho Wabunge!

mluga

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
676
215
Mwandishi Wetu - Raia Mwema


  • Matanuzi yao sasa kutegemea mshahara
  • Upembuzi wa athari wafanyika
  • Siku nne tu za ‘wikiendi' walilipwa milioni 129/-

SAKATA la nyongeza ya posho kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeingia katika sura mpya, na sasa uchunguzi wa Raia Mwema, umebaini kuwa si tu Rais Jakaya Kikwete hatasaini nyongeza hiyo mpya kama tulivyoripoti wiki iliyopita, bali posho hizo za ‘kukaa kitako' (sitting allowance) zitatangazwa kufutwa rasmi wakati wowote.

Vyanzo vya habari vya gazeti hili ndani ya Ikulu vimethibitisha ya kuwa Rais Kikwete amepewa ushauri wa kufuta posho hizo kutoka kwa baadhi ya watalaamu wake na uamuzi unaweza kufanyika na kutangazwa wakati wowote.

Inaelezwa kuwa upembuzi wa kina wa athari za kufuta posho hizo kwa wabunge na hasa kujua kama zitaathiri majukumu yao umekwishakufanyika na kukamilika na taarifa zinasema kati ya waliowasilisha takwimu za ‘kihasibu' Ikulu, ni pamoja na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila.

"Suala lililopo mezani kwa Rais si kusaini au kutosaini waraka wa mapendekezo ya nyongeza ya posho, bali ni kufuta sitting allowance zote kwa wabunge. Huo ndio ushauri wa kitaalamu unaohusisha hesabu za wahasibu na ambao, Rais ameukubali na unatarajiwa kutangazwa karibuni.

"Kama akitangaza kufuta posho hizi maana yake, masuala mengine ya wabunge yanaweza kufanyiwa marekebisho katika mshahara, ambayo nchi itanufaika kwa kukata kodi pia, unajua walikuwa hawakatwi kodi kwenye posho.

"Wabunge hawastahili malipo ya sitting allowance, kwa sababu wanakuwa wanatekeleza wajibu wao na stahili yao ni kulipwa mishahara tu," alisema mtoa habari wetu.

Lakini wakati hayo ya Ikulu yakiwa hivyo, uchunguzi wa Raia Mwema umebaini ya kuwa wakati wa jaribio la kutaka nyongeza ya posho mpya, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alizungumza tu na Rais Jakaya Kikwete akiamini kuwa angeridhia wito wa wabunge na hivyo, mchakato wa malipo ya posho mpya ukianza si tatizo.

Mbali na Spika kuzungumza tu na Rais Kikwete bila kufikia muafaka, inaelezwa kuwa akishirikiana na Tume ya Bunge, walimshinikiza Katibu, Dk. Kashilila, kulipa posho mpya, naye akagoma.

Taarifa zaidi zinasema hata Spika Makinda mwenyewe aliwekwa katika shinikizo kubwa la wabunge wakitaka posho mpya na kama angeshindwa, walimtisha kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye na hivyo, kumng'oa madarakani.

Taarifa za uchunguzi zilizotufikia zinaeleza kuwa wabunge karibu wote waliunga mkono posho mpya na kupitia Tume ya Bunge, azimio la nyongeza likapitishwa kutoka Sh 70,000 hadi 200,000.

Kutokana na azimio hilo kupitishwa, wajumbe wa Tume hiyo kwa kushirikiana na Spika, walimtaka Katibu Dk. Kashilila kuanza kuwalipa katika mkutano uliopita wa Bunge.

Lakini, kwa mujibu wa taarifa hizo, akikariri mchakato unaofutwa katika malipo ya aina hiyo ambayo yanahitaji mamlaka husika iridhie, na katika suala hili mamlaka hao ni Rais Kikwete ambaye alikuwa hajaridhia, Dk. Kashilila aligoma kuwalipa akisema bado mamlaka husika (Rais) hajaidhinisha kwa vile hakuna instrument ama waraka idhinishi kwa ajili hiyo ambao lazima usainiwe na Rais kabla ya kwenda Hazina kuomba fungu.

"Katibu alishinikizwa sana, alipowaeleza hana instrument Spika akamwambia yeye ameongea na Rais na amekubali, lakini Katibu anajua kukubali kwa Rais si kwa maneno bali ni kutia saini waraka.

"Kwa hiyo, naye Katibu akamwambia Spika, kama Rais amekubali naomba niandikie rasmi kwa maandishi ili nifanye malipo...hapo Spika hakuandika.

"Lakini pamoja na Spika kutoandika, alisisitiza kwamba amekwishakuzungumza na Rais, na pia Tume ya Bunge iliweka shinikizo kali dhidi ya Katibu alipe posho mpya.

"Alichofanya Katibu hakulipa posho isipokuwa amelipa malipo ya wabunge kwa siku walizofanya kazi mwishoni mwa wiki, kuanzia kwenye kamati na vikao vya Bunge, si wabunge wote waliopata malipo hayo," kinaeleza chanzo chetu cha habari.

Raia Mwema
ilizungumza na Katibu wa Bunge, Dk. Kashilila kujua kama alishinikizwa lakini katika majibu yake akasisitiza akisema; "Sikulipa mbunge yeyote posho mpya, mimi ndiye mlipaji...nasema sijalipa.

"Nilicholipa ni malipo wanayostahili waheshimiwa wabunge waliofanya kazi siku za mwisho wa wiki, wengine kwenye vikao vya kamati na wengine vikao vya Bunge Dodoma.

"Tunaandaa taarifa za mchanganuo na kuwatumia wahusika wote, halafu mkawaulize nilichowalipa ni ongezeko la posho au nini?" alisema Dk. Kashilila.

Hata hivyo, gazeti hili limebaini kuwa malipo yanayotajwa kufanyika kwa wabunge kama anavyoeleza Katibu wa Bunge, yamefanywa kwa wabunge 307, kila mmoja akilipwa Sh. 420,000 zinazohusisha siku nne za mwisho wa wiki walizofanya kazi, wakati wa mkutano wa Bunge uliopita na baadhi ya vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge, kabla ya kuanza kwa mkutano huo uliofanyika Novemba, mwaka huu.

Taarifa zinaonyesha kuwa jumla ya Sh. 128,940,000 (takriban milioni 129) ndizo zilizolipwa kama fungu la ziada ambalo limesababisha wabunge kuhisi ongezeko kwenye akaunti zao.

Takwimu hizo zinapingana moja kwa moja na kauli ya Spika kuwa wabunge walilipwa posho mpya tangu mkutano uliopita.

Utata kuhusu kauli ya Spika

Uchunguzi zaidi wa gazeti hili umebaini kuwa kauli ya Spika kuwa posho zimelipwa haina ukweli isipokuwa kilichofanyika kwa wakati huo ni agizo alilotoa (Spika) kutaka hesabu za malipo ya posho mpya ziandaliwe na kama Rais angesaini, basi walipwe kwa kuongezea juu ya posho za Sh 70,000 kwa siku walizolipwa mkutano uliopita wa Bunge.

"Spika kule bungeni aliagiza hesabu za malipo ya posho kwa viwango vipya zifanyike. Kwa hiyo, wabunge wangelipwa hizo Sh.70,000 lakini baada ya Rais kusaini, wangeongezewa (kufidiwa) ili ifikie Sh 200,000. ndiyo maana alisema wabunge wameanza kulipwa mkutano uliopita, kilichopo ni kwamba waliamini Rais angesaini tu kiurahisi," anasema mtoa habari wetu.

Juhudi za gazeti hili kumpata Spika kuzungumzia suala hilo zimegonga mwamba kwa siku kadhaa sasa, ikiwa ni pamoja na kumpigia kwa simu yake ya mkononi iliyokuwa ikiita bila majibu.

Njama kumng'oa Katibu zasukwa

Kutokana na suala hili kuonekana kuibua mvutano wa kiutawala ndani ya Bunge, sasa kuna taarifa kwamba mkakati maalumu umeanza kusukwa ili kumng'oa Dk. Kashilila.

Mpango huo ambao Raia Mwema imeunasa, unatajwa kuhusisha baadhi ya viongozi wa Bunge, wakiwamo baadhi ya wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge.
Wenyeviti hao (majina yanahifadhiwa) wanadaiwa kuchukizwa na uamuzi wa Katibu wa Bunge, wakiamini ni kati ya wasiotaka wabunge kuongezewa posho na kwa hiyo, wanadhani ni kikwazo kwa mafanikio ya Spika Makinda.

Raia Mwema
imetajiwa baadhi ya wenyeviti hao akiwamo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mahesabu ya Serikali Kuu, Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Momose Cheyo ambaye alikataa kuzungumzia jambo hilo alipoombwa aeleze maoni yake wiki hii na mwandishi wetu.

Cheyo, ama maarufu kama Bwana Mapesa, alisema ya kuwa kama ana mawazo yake kuhusu posho anajua sehemu sahihi pa kuyawasilisha.

Kikwete awajibu kupitia CCM

Wachambuzi wa mambo wanasema ya kuwa taarifa ya Rais Kikwete ya kuukataa mpango huo wa posho kwa wabunge imejieleza wazi katika hatua ya wiki hii ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutangaza kwamba hakiafiki posho hizo ziendelee kulipwa na kwamba ni busara suala hili liachwe kwa sasa.

CCM kupitia kwa Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa tamko ikisema: "Tunaamini busara itatumika kuachana na jambo hili, kwani kuendelea nalo kunaweza kutafsiriwa ni kuwasaliti watendaji katika sekta nyingine, wakiwamo askari, walimu na madaktari.

"Kwa kuongeza kiwango hicho cha posho kwa wabunge ni kuongeza pengo la tofauti ya kipato kati ya wenye nacho na wasionacho katika jamii yetu hasa kwa kuegemea baadhi ya makundi.

"Swali kubwa hapa linakuwa je, maisha yanapanda Dodoma peke yake na kwa wabunge tu? Kuongoza ni kuonyesha njia hivyo si sahihi kwa wabunge kuonyesha njia kwa kujiongezea posho peke yao kwa kisingizio cha ugumu wa maisha."

Kauli ya Zitto Kabwe

Miongoni mwa wabunge, Ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, pekee mwenye msimamo wa wazi kupinga si tu ongezeko la posho za sasa, bali hata posho nyingine zinazolipwa kwa wabunge kwa kutimiza majukumu yao ya kawaida, ambayo kipato halali kwa mujibu wa tasiri ya Kabwe ni mshahara.

Alipoulizwa na gazeti hili kuhusu tafsiri yake kutokana na tofauti ya msimamo na kauli kati ya Spika Makinda na Katibu wa Bunge, Dk. Kashilila, Zitto alisema Spika amewekwa katika shinikizo na wabunge.

"Speaker is under pressure (anashinikizwa), wabunge wamemtisha ili ahakikishe kunakuwapo posho mpya na asipofanya hivyo kuna vitisho kwamba anaweza kupigiwa vote of no confidence (kura ya kutokuwa na imani), ushauri wangu hapa ni kwamba Spika anatakiwa awe bold enough (imara), akatae shinikizo na aseme hakuna posho mpya.

"Najua amewekwa kwenye pressure na Tume ya Bunge na wabunge wengine, lakini kama kibali cha Rais hakuna aseme, awe jasiri," alisema Zitto.

Waziri Mkuu achukizwa

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kati ya viongozi walioshitushwa na kauli ya Spika Makinda kuhusu ongezeko la posho kwa kuzingatia ugumu wa maisha Dodoma, ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Pinda ananukuliwa akisema; "Hili suala bado lilikuwa katika mchakato ambao uamuzi wa mwisho hautokani na Bunge, sasa kwa nini amekwenda (Spika) kueleza kabla ya kujua majibu ya mwisho?

Kuhoji huko kwa Pinda kumetafsiriwa na baadhi ya viongozi kuwa, Spika alichofanya ni kucheza mchezo wa kisiasa kwa kujivua pressure iliyokuwa ikielekezwa kwake na wabunge na kutua mzigo huo kwa Ikulu, na hususan Rais Kikwete, ambaye naye sasa amecheza ‘siasa' kwa kutumia CCM.

Inaelezwa kuwa Spika Makinda amekuwa akishinikizwa na baadhi ya wabunge ambao wanamzongazonga wakihoji kwa nyakati tofauti; "Mbona Sitta (Samuel, Spika aliyepita) aliweza, wewe unashindwa nini?"
 
Kwa kweli sometime nashindwa kumponda au kusmfia JK. Hii leadership na management style yake ya kichonganishi kuuma na kupuliza haijawai kutokea.
 
Duh hii kali jamani...mnamshangaa nape anapokanushaga habari za ccm kama kujivua gamba haya jk nae kakubali leo anamgeuka makinda...shamba la bibi hilo ngoma inogile
 
Niko hapa nasubiri na bango langu kwa hawa WABUNGE MAPOSHO; siambiliki wala sielewi kitu kuchezea kodi zetu hivi.
 
Mimi sioni kama wananchi tuna cha kushangilia hapo. What I know ni kwamba itafutwa sitting allowance na the same amount itaingizwa sehemu nyingine. Kama mtu ana mshahara wa Tsh 1000 na posho Tshs 200, leo hii tukiambiwa anafutiwa posho yake ya tshs 200 na kuongezewa mshahara kufikia 1,400 kuna nini cha kushangilia hapo?

Shangilieni nyinyi msioijua CCM na serikali yake.
 
Sitegemei kitu kama hicho toka kwa serikali ya magamba kwani wamekuwa ni watu wakulipana fadhila
 
Pole yetu walimu. Mara ooh madai yameanza kulipwa mara mwezi ujao. Ee Mungu tukumbuke maana hata hao wabunge tumewafundisha lkn vigeu geu hawatuhurumii. Ama kweli there's somebody gas!!!!
 
Mimi sioni kama wananchi tuna cha kushangilia hapo. What I know ni kwamba itafutwa sitting allowance na the same amount itaingizwa sehemu nyingine. Kama mtu ana mshahara wa Tsh 1000 na posho Tshs 200, leo hii tukiambiwa anafutiwa posho yake ya tshs 200 na kuongezewa mshahara kufikia 1,400 kuna nini cha kushangilia hapo?

Shangilieni nyinyi msioijua CCM na serikali yake.
Bora walipwe kutumia system inayojulikana (mshahara) ambayo inaweza kutozwa kodi kuliko kuwa kwenye posho ambayo haitozwi kodi na malipo yake hayajulikani vizuri mara form zake ziletwe asubuhi mara jioni kutegemea mapenzi ya mtu mmoja, kumbuka siku CDM walipotoka bungeni form zikaletwa jioni ili tu wabunge wa CDM wakose.
 
Ni jambo ambalo litapokelewa vzr na wengi mm mmjawapo.Hiyo ni hatua ktk kufikia mageuz saf.Kumbuka tajir kuonja pepo ni ngumu!
 
Inachekesha! ndiyo maana CCM waliukuwa wachangamfu kwenye kupitisha katiba wakijua watamfurahisha Mh.rais ili naye aje awalipe fadhila kwenye posho, KAWATOSA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!
Nitafurahi sana posho zikifutwa ili watu waache kurogana kwa ajili ya ubunge(=POSHO) Ili wanaoingia bungeni wawe ni wenye mapenzi mema na siasa na siyo wapenda posho na kutafuta utajiri wa uzeeni na haraka.
 
Mimi sioni kama wananchi tuna cha kushangilia hapo. What I know ni kwamba itafutwa sitting allowance na the same amount itaingizwa sehemu nyingine. Kama mtu ana mshahara wa Tsh 1000 na posho Tshs 200, leo hii tukiambiwa anafutiwa posho yake ya tshs 200 na kuongezewa mshahara kufikia 1,400 kuna nini cha kushangilia hapo?

Shangilieni nyinyi msioijua CCM na serikali yake.

Mkuu, ebu tusaidie kufahamu haya masuala ya posho kwani vyama vya upinzani wabunge wao wanachukuwa kiasi gani?
 
Inachekesha! ndiyo maana CCM waliukuwa wachangamfu kwenye kupitisha katiba wakijua watamfurahisha Mh.rais ili naye aje awalipe fadhila kwenye posho, KAWATOSA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!
Nitafurahi sana posho zikifutwa ili watu waache kurogana kwa ajili ya ubunge(=POSHO) Ili wanaoingia bungeni wawe ni wenye mapenzi mema na siasa na siyo wapenda posho na kutafuta utajiri wa uzeeni na haraka.
Posho zikifutwa angalau JK atakuwa amesaidia kutibu moja ya magonjwa tuliyonayo kwenye siasa na labda wataalam wetu watatulia kwenye fani zao, kina Mwakyembe watarudi kwenye idara zao.
 
Mkuu, ebu tusaidie kufahamu haya masuala ya posho kwani vyama vya upinzani wabunge wao wanachukuwa kiasi gani?
Kinachojadiliwa hapa ni posho ya wabunge wote si posho ya wabunge wa chama fulani, jaribu kutofautisha masuala ya kitaifa na vyama, hata role model wenu Nape mliyemponza kasema kwenye suala la posho anatanguliza taifa kwanza, sasa wewe unaleta mambo ya upinzani ya nini ili upate cha kubishana, kama huna cha kuchangia unaweza kusoma comments za wenzako.
 
Kinachojadiliwa hapa ni posho ya wabunge wote si posho ya wabunge wa chama fulani, jaribu kutofautisha masuala ya kitaifa na vyama, hata role model wenu Nape mliyemponza kasema kwenye suala la posho anatanguliza taifa kwanza, sasa wewe unaleta mambo ya upinzani ya nini ili upate cha kubishana, kama huna cha kuchangia unaweza kusoma comments za wenzako.

Usipende kurukia pipe kwa mbele angalia nimemjibu nani...halafu wewe uwezi kunipangia cha kusema humu JF..

JF sio ya Chadema ni Forums huru wala sio ya mzee wako..

Kama unataka kupangia watu humu cha kusema nakushauri fungua Forum yako mkuu..

Maneno mengi tu changia basi hata JF isonge mbele porojo tu..
 
Kwenye ukurasa wake wa fb rais Kikwete amekemea matumizi ya posho kwenye taasis za umma,ametolea mfano TANAPA
 
Ukisikia mambo ya msingi unaenda kuongelea kwenye vijiwe vya gahawa ndo haya sasa.
 
Back
Top Bottom