Kichwa Ngumu
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 1,726
- 312
Kifo cha ccm kimefikia 50 per ce
<br />Kuna haja ya Pinda kujiuzulu ili kulinda heshima yake kama PM
<br /><b>Pinda is an accidental prime minister cheo kakipata kibahati na haikutokana na nguvu yoyote aliyo nayo ndani ya chama. Jairo inajulikana wazi ni mtu wa JK tokea zamani. Pinda kaukwa tu kwa vile EL alijiuzuru na serikali ilihitaji mtu asie na makundi wala nguvu kujaza nafasi. Huo ndiyo ukweli.</b>
IKULU INAMHITAJI ZAIDI JAIRO KULIKO PINDA
lol! Nnampa pole mtoto wa farmer.
Waziri Mkuu angejitengenezea mazingira mazuri sana na ya kuheshimika kama hapo ijumaa wakati wa hotuba yale ya kuhairisha bunge la kumi angetamka pia kwamba anajiuzulu rasmi nafasi yake ya uwaziri mkuu. Pengine atafanya hivyo, tusubiri.
Hii ilifahamika tangu mwanzo ya kua katika swala la kuwahonga wabunge ili wapitishe bajeti ya wizara ya nishati na madini ulikua ni mpango wa JK na serikali na ulipata baraka zote toka kwa JK na serikali kwa ujumla.Na hii imekua inafanyika kwa muda mrefu na hii ndio siri ya mikataba feki.Jairo alikua mtekelezaji tu.Kwa madai ya Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo ya kua wafanyakazi waliovujisha siri watachukuliwa hatua kimenishanagaza!Kama utaratibu huo ni halali kwanini uwe siri!Waziri Mkuu alisema kama angekuwa na mamlaka angemuwajibisha Katibu Mkuu Nishati na Madini siku ileile iliposomwa ile barua bungeni.
Baada ya ripoti ya CAG Katibu Mkuu Kiongozi Luhanjo anasema alichofanya Jairo ni utaratibu wa kawaida kabisa ...na kama Jairo ataweza kuwashtaki waliomdhalilisha ni yeye tu.
Nini implication ya haya kama sio kumdhalilisha na kumshusha Pinda na kumnyanyua Jairo ni nn?
Ndo maana mi nasema IKULU INAMHITAJI ZAIDI JAIRO KULIKO PINDA
Kwenye nyekundu hapo, hiyo ndiyo stahili ya Utawala ya JK, Yeye anawasha Moto halafu anakaa kimya pembeni akijifanya kama hajui lolote linaloendelea, kwamba yeye hausiki.Jamani Jairo ni rafiki sana wa JK na asingekubali rafiki yake adharirishwe na serikali yake pia iendelee kupata aibu hivyo ilikuwa ni lazima Jairo asafishwe kupitia kwa CAG. Pia JK aliona Pinda hafai kwa vile amezielewa vizuri ukweli wa tuhuma na alikuwa tayari kumwadhibisha Jairo. Hivyo aliona Luhanjo ambaye ni mdogo kwa ranking apewa kazi ya kusimamia kumsafisha jairo, mawaziri wa wizara hiyo na serikali yake, baada ya kutoa maelekezo kwa Luhanjo na CAG, JK kama kawaida akanyamaza kama vile yeye si Rais wa Jamhuri ya Tanzania.
Sasa kusafishwa kumekamilika vizuri sana, wabunge na Pinda wameonekana ni waongo na wapika majungu. Ama kweli Watanzania tumekuwa kuku wa kizungu bandani.