Ikulu imechemka ilivyoandika pongezi kwa Papa Benedict XVI kwenda Vatican

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Kwanza niwashukuru walioleta thread ya Ikulu ikionyesha barua iliyoandikwa kwenda Vatican kumpongeza Pope Benedict kwa kile Ikulu yetu ilichokiita {Inauguration of the Pontificate of His Holiness Pope John Paul II}.

Thread yenyewe iko humu kwenye link hii:{Homily for Inauguration of Pontificate, John Paul II, 22 October 1978}.

Ilikuwa nichangie kwenye thread ileile lakini kama ukisoma utaona tayari imeshafika page ya pili na hakuna hadi sasa ambaye ameshaona technical mistake na hivyo uchangiaji umejikita kana kwamba kila kitu kiko sawa. Na kwa kweli asiyejua anaweza kuna ni sawa.

Lakini kwa tunaojua binafsi kwanza nimeshtushwa na headline. Baada ya kushtushwa na headline nikashawishika nisome details zaidi nikiamini nilichokiona nitakuta kimerekebishwa ndani ya maelezo, ukizingatia juzi tu kuna Waziri kachemka na thead yake inaendelea alipoutangazia ulimwengu kwamba Tanzania ni muungano wa Zimbabwe na Pemba.

Tuachane na kosa hilo la Waziri sasa tujikite kwenye kosa la Ikulu yetu.

Narudia, baada ya kusoma barua yote kwenda vatican kwa Papa, nikaridhika kabisa haya ni makosa yanayostahili kurekebishwa, na JF kumejaa wataalamu wa kuona makosa na kurekebisha. Je, kosa ni nini hapa kwenye barua hii?

Kulijua kosa inabidi kwanza tunanze kujua terms za Kanisa Katoliki. neno Pontificate linatumika kwa mambo yanayofanyw ana askofu lakini liktajwa peke yake basi linamaanisha Askofu wa Roma yaani Papa.

Hivyo "Pontificate" ni utawala wa Papa. Kwa kiingereza tungesema ni "reign". Pontificate ni kipindi chote cha huyo mtu kuwa Papa yaani tangu siku aliposimikwa kuwa Askofu wa Roma hadi atakapofariki au ku-resign.

Tunajua kwamba Papa huchaguliwa na mkutano wa makardinali uitwao "Conclave". Lakini Papa kama askofu wa jimbo lolote haishii kuchaguliwa tu, bali siku yake ya kwanza ya uaskofu wa askofu au upapa wa Papa (Pontificate) ni siku ile anapokaa kwenye kile kiti cha askofu kwenye Kanisa kuu liitwalo "Cathedral".

Narudia hii ni kwa kila askofu wa Kanisa Katoliki duniani akiwemo Papa. Hivyo "Pontificate" yaani siku ya kwanza ya utawala wa Papa yoyote huanza siku hii.

Narudi kwenye mshangao wangu, ni kwamba niliposoma ungedhani kuwa kuna Papa mpya ambaye upapa wake umeanza (Pontificate) na hivyo Ikulu yetu imetuma salamu za pongezi kwa kuanza upapa huo yaani {Inauguration of the Pontificate}.

Kibaya zaidi pametamkwa {Inauguration of the Pontificate of His Holiness Pope John Paul II}, ambapo kwa kiswahili sahihi ni {kuanza kwa Upapa wa John Paul II}.

Haikutakiwa kuandikwa hivi. Je, kilitakiwa ni nini?

Kilichotakiwa ni kuchunguza kwanza ni nini kinaendelea kabla ya kuandika. Kinachoendelea ni kumbukumbu ya kilichotokea miaka 34 yaani Jumapili, October 22, 1978.

Hii ndiyo siku John Paul II alipouanza upapa wake kwa kuendesha misa na kukali kile kiti {Cathedral} kilichomo kwenye Kanisa Kuu lake ambalo linaitwa {Archbasilica of St. John Lateran}. Najua baadhi, na ikibidi wengi wanaishia kulijua lile {St. Peter's Basilica}.

Lakini Kanisa hasa la upapa ni hili {St. Peter's Basilica} kama pale D'Salaam lilivyo kanisa la St. Joseph}.

Sasa, kilichotokea wiki hii pale Vatican, kinahusiana na mchakato wa kumtangaza John Paul II awe mtakatifu kwani yeye sasa tayari kikanis ayuko hatua kubwa zaidi kuliko ilivyo kwa Julius Nyerere kwa mchakato huohuo. John Paul II sasa yeye anaitwa "Beata" yaani "Mwenyeheri". Amebakiza ngazi moja tu kutangazwa mtakatifu.

Kutangazwa mtakatifu au mwenyeheri ni hatua moja inayoambatana na kuwekwa kwa siku maalumu ya kumkumbuka mtakatifu huyo. Watakatifu wengi hasa mashahidi wa dini siku yao huwekwa kuwa ni ile waliyokufa kama wale mashahidi wa Uganda. Lakini baadhi si lazima iwe siku hiyo.


Pope JOhn II alitangazwa mwaka jana kuwa "Beata", na hivyo kukawa na debate kuwa je, siku yake iwe lini. Ndipo kabla ya kumtangaza Vatican ikaamua kwamba siku yake iwe ni siku alipouanza upapa wake yaani October 22.

Hivyo, October 22, ni maalum kwa Beata John Paul II kama ilivyo siku ya mtakatifu au mwenyeheri yoyote unayemjua.

Hivyo, kilichofanyia juzi, zutio wake wa kwanza kabisa ni makanisa duniani kuadhimisha kwa mara ya pili siku ya Mwenyeheri John Paul II.

Lakini tukio hili limegongana na mambo kadhaa ambako maaskofu wengi akiwemo Polycarp Pengo wako Vatican kwa shughuli iliyoanza wiki mbili zilizopita iitwayo Synod. Hivyo, hilo limeongeza populality ya jambo hili kuonekana ni special kwa kiasi fulani.

Haishangazi kuwepo kwa meseji ionyeshayo {Inauguration of the Pontificate}. Lakini kama umeshasoma hadi hapa utakuwa umeelewa ni kwamba Vatican haina mpango wa kusherehekea siku ya Papa ambaye tayari ameshakua lakini cha msingi dunia kukumbushwa siku ya "Uenyeheri" wake na ikitokea akatangazwa utakatifu itakuwa ni siku ya "Utakatifu" wake kuadhimishwa makanisani.

Sasa, barua ya Ikulu ambayo imetolewa na Wizara ya mambo ya nje inaonyesha kama kwamba ni uzinduzi wa Upapa, tena wa Papa aliyekwisha kufa.

Nafahamu Salva Rweyemam ni mkatoliki lakini nafahamu Bernard Membe si tu kwamba ni mkatoliki tu bali alipita seminari na meseji kama hii angeweza kugundua hiki ninachoeleza.

Nawatakia usomaji mwema.
 
Viongozi wetu hawana mda wa kusoma, wako busy kuuwaza urais na watachowafanyia wabaya wao siku wakipata uongozi!
 
On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, and on my own behalf, it gives me great pleasure to congratulate you most sincerely on the occasion of the Inauguration of the Pontificate of His Holiness Pope John Paul II.......

Mie pia niliiona hii ikanitatiza sana, nikafikiri labda kuna kitu katika protocol za Vatican kama vile Papa anachukua upapa wa papa aliyemuacha na anaweza kupongezwa kwa niaba yake :)

1. Why congratulate Pope Benedict XVI now for something that happened 34 years ago (and not as a commemoration either)?
2. Why call this "the occasion of the inauguration of the Pontificate of .." while it is a commemoration and not the actual inauguration?

The only way one could explain this is if the word occasion is meant as in commemoration. Then the congratulatory note is congratulating the Vatican on this commemorative day just as the Vatican can congratulate Tanzania on some commemorative day, say Nyerere's inauguration as president, depending on how we commemorate such days.

Salva alishawahi ku mangle a two sentence statement, sitashangaa hapa akitumia lugha tata bila ulazima. Ikulu haina hata proofreaders, worse still haijui hata kutumia spellcheckers.
 
To be fair, as pointed out before, there is such a thing as interpreting the word "occasion" in the commemorative sense.

As in Q: "What is the occassion?" A: "It is the boy's fourth birthday". The occasion commemorates the birthday which took place four years ago on the same calendar day as well as the fourth anniversary of that birthday.

Similarly, this message congratulates the current pope on the occasion (commemoration) of the inauguration of the Pontificate of His Holiness Pope John Paul II.

In that sense, there is nothing wrong with the message. Although in most cases, to eliminate confusion, if "on the occasion" is used, the writer would elaborate as in "on the occasion of the 34th anniversary of the inauguration of the pontificate of His Holiness Pope John Paul II" to distinguish the commemorative anniversary occasion (fourth birthday, 34th anniversary) from the original occasion (inaugural pontification, day of birth).

Sadly the distinction does not appear on the Ikulu message, fueling further confusion.
 
Nikupateje

Shida yote nafasi zinatolewa kwa undugunization ungepewa mtu kama wewe ungeisaidia Ikulu yetu kila dini inawatalaam wake
 
Last edited by a moderator:
Mimi mwenyewe barua ya ikulu ilinitatiza sana nikashindwa kuelewa Pope atakuwa amepata message ya aina gani!
 
Ikulu yetu haina wataalamu wa lugha na kwa ujumla lugha sanifu ni janga la kitaifa.

Ningekuwa mimi Kikwete ningemtumia kwa karibu sana BW Mkapa kunisaidia mambo ya lugha manake yuko sawasawa. Vinginevyo nakuunga mkono Lugha Ikulu ni janga la kitaifa
 
Ningekuwa mimi Kikwete ningemtumia kwa karibu sana bwn,Nkapa kunisaidia mambo ya lugha manake yuko sawasawa.Vinginevyo nakuunga mkono Lugha Ikulu ni janga la kitaifa.
 
Back
Top Bottom