Elections 2010 Ikiwa zimebaki siku 15 umejiuliza hili swali?

Nyange

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
3,516
1,865
Zikiwa zimebaki siku 15 tu kupiga kura Jibu swali hili? Tunakwenda wapi WATANZANIA? ( VISION)
Mi mara ya kwanza kumiriki gari ilikuwa 2004. Nilikuwa nanunua bei ya Petroli Tsh. 360 kwa lita!!!!!. Kwa sasa kwa mafuta hay ohayo ambapo TZ ilikuwa inanunua product hiyo nje, baada ya miaka 6, bei hiyo yamafuta kwa sasa ni Tsh, 1800!!!!!.

HAPA WATANZANIA TUNAFANYA MAAMUZI NA SI MZAHA WA KUPEWA TISHETI NA KOFIA KUCHAGUA VIONGOZI.

Maisha ya nchi hii yako mikononi mwangu na wewe. Vizazi vyetu vitatuhukumu kwa kura za tar 31/10/2010. Tuache ushabiki, hapa ni kazi tu. All the best wanaJF na weekend njema.
 
Mbaya zaidi Zambia na Malawi mafuta ni cheap kuliko Tz wakati yanapita via Tunduma highway.
Tz bwana yaani kila angle ni upupu wa rushwa na ufisadi
 
Mbaya zaidi Zambia na Malawi mafuta ni cheap kuliko Tz wakati yanapita via Tunduma highway.
Tz bwana yaani kila angle ni upupu wa rushwa na ufisadi

Hapo hujaweka uchakachuaji na kikwete gari ishazimika!, na BBC wamesha publish utafiti mpya wa Chuo kikuu cha Mlimani upande wa Economics. Tumeanza kusherehekea make huu utakuwa ni ushindi wa Kiuchumi.
 
huu ndio utafiti unaongalia maslahi ya nchi kwanini mafuta yawe rahisi zambia, rwanda au burundi, ug au kenya wakati hali ni kama sawa, i.e cost of transportation? labda Salima/Mirojo?Rikikwete
 
Kaka usiende malawi nenda rwanda mafuta aina ya petrol ni half price ya tanzania wakati yanapita hapa kwetu kwenda huko...

Mimi nimeshafanya maamuzi sahihi kabisa na naomba watanzania wote tuwafikirie watanzania zaiti ya milioni 40 maskini wa kutupwa....

Tufanye mabadiliko.....
 
Mbunge,waziri,ikulu lt 1 tsh 2500 kwa mwezi lt 700 kwa kila vx,v8 = 1750000 service $ 3000 Naomba hesabu waungwana kwa calc yangu ndo imfika mwisho wanajf...
 
Hapo umegusa product moja ambayo product zingine zote zianaitegemea (wese) so likipanda na vingine vyote vinapanda....... bado hujagusa shilingi inavyozidi kushuka thamani dhidi ya fedha za kigeni.....na mishahara ndo hii hii ya kuzugia mjini.....

Sure kaka....sidhani kama hili swali unahitaji kujiuliza...ni swala la kuona na kuamua....koz petrol station zote hata za kitaa zimedisplay bei....Ona/Tazama/ Angalia........Chukua hatua tar.31 Usiusumbue ubongo kwa saaaaaaana......
 
Mods mbona mnaiminya hii nawashangaa, is it true that is the place just we dear to talk openly?
 
Thats it mkuu, inabidi tufanye uamuzi wa busara sana ambao utaleta manufaa si ya ki maslahi, bali yale yanayojali mustakabali wa taifa zima la sasa na la vizazi vya baadaye.
"Wanajamii wote tushiriki kikamilifu tarehe 31, octoba na kufanya uamuzi sahihi, usipopiga kura inabidi ujitoe kabisa kwenye hii forum b'se we need people with vission 4 u'r nation, while u don't"
 
"Kura yako ndio uhai wako" Liko tangazo moja linatoka kuhamasisha wapiga kura. Sasa la msingi hapa ni kuchagua kiongozi bora na si bora Kiongozi. Kwani hawa waliotufikisha hapa ni bora viongozi tubadilike wananchi tuendako hakuna nuru chini ya madereva hawa.
 
Back
Top Bottom