Ikiwa chungu tema Zitto.

Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,552
2,359
Nasikitika sintoweza kuweka sehemu yote ya shairi hili kwa sababu za zilizo ndani ya uwezo wangu ukizingatia hali ya mijadala ya kisiasa na upepo dhoruba ndani ya CHADEMA. Enjoy!!

Ikiwa chungu tema Zitto.

Natanguliza salamu, kwako kamaradi Zitto,
Natumai utimamu, wewe na mama mtoto,
Kitabu na majukumu, si haba ni kazi nzito,
Donge ulilolimeza, likiwa chungu uteme.

Likiwa chungu uteme, nduguyo nakushauri,
Watakuvika utume, sifa na umashuhuri,
Vyote hivyo uvipime, visije kupa kiburi,
Donge walilokunywesha, likiwa chungu uteme

Taifa lakuhitaji, kupinga hao fisadi,
Wasikufanye mtaji, siasa kwao mradi,
Wakufunike theluji, kukukinga na baridi,
Ukishindwa kulimeza, donge chungu uliteme.

Na pia uwe makini, na hao zako rafiki,
Wa nje na pia kundini, wapo pia wanafiki,
Watakuja kurubuni, kwa mbinu za kifataki
Usije jilazimisha, donge chungu uliteme.
Kwa njaa na zao shida, taifa wameliuza,
Wamechokonoa donda, madini kuya maliza,
Wajifanya wakupenda, gutuka wanakuchuza,
Usijitwishe machungu, kama hauwezi tema.
 
I can see mpwa you are back fulu mashairi.......
 
Ni jana tu nimetambua mchango wako katika mashairi,
Sina wasi wasi wewe kwenye hii fani ni mashuhuri,
Umekuwa kimya nikaingiwa na woga nini kinajiri?
Mungu si Athumani unatokeza kama nyota ya alfajiri.

Kuhusu shairi la Zito siwezi ku comment siasa kabisa
na aleji ha hio kitu kidogo mpwa Geoff machio anapapasa
 
Ni jana tu nimetambua mchango wako katika mashairi,
Sina wasi wasi wewe kwenye hii fani ni mashuhuri,
Umekuwa kimya nikaingiwa na woga nini kinajiri?
Mungu si Athumani unatokeza kama nyota ya alfajiri.

Nilipatwa masahibu,ya dunia kunipata,
Nashukuru jadidu, sa' dhoruba imepita,
Na leo nipo muhibu, yamekwisha yalopita,
Shukrani mpwa nguli, na wote wadau jamvi
 
Nilipatwa masahibu,ya dunia kunipata,
Nashukuru jadidu, sa' dhoruba imepita,
Na leo nipo muhibu, yamekwisha yalopita,
Shukrani mpwa nguli, na wote wadau jamvi

Dont forget Burn that i too remembered you...Could you do a bit of the stuff for me also!...lol!
 
Dont forget Burn that i too remembered you...Could you do a bit of the stuff for me also!...lol!

Siwezi kukusahau, wa ukweli pakajimi,
Wewe ndio mdau, unaokuza uchumi,
Ntawezaje kusahau, nikose milioni kumi,
Watu wote ntasahau, mpwa paka sithubutu
 
ndugu burn shukurani, kwa kujali yangu hali,
kamwe mimi sikudhani, kazi hii kumbe ghali,
donge lilitiwa hani, kuumia sikujali,
donge chungu sitamani, kulitema ndo siwezi.

mbwembwe walinipatia, ili nikubali donge,
mbali sikuangalia, litanifanya nikonde,
sasa ninaugulia, na wananipiga makonde,
donge chungu sitamani, kulitema ndo siwezi.

Nadhani wanielewa, napokata kulitema,
nyuma yangu wamekaa, wenye kutaka kugema,
wanasema bado saa, kinichoka tanitema,
donge chungu sitamani, kulitema ndo siwezi.
 
Dont forget Burn that i too remembered you...Could you do a bit of the stuff for me also!...lol!

pakajimy wachekesha,
tena wanifurahisha,
tenda wema nenda zako,
usitake vya wenzako,
akiona yakufaa,
takupa bila jinaa!
 
pakajimy wachekesha,
tena wanifurahisha,
tenda wema nenda zako,
usitake vya wenzako,
akiona yakufaa,
takupa bila jinaa!

Mkuu sikufahamu, nawe kumbe wamo,
Bado nina hamu, yakuelewa lako somo,
Radical e'nature wamfahamu, katoa changamoto,
Tushirikiane kutoa hii elimu, tena mashairi yasiyo ya kitoto.
 
eeh!
zitto AGAIN!
agrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrh!
 
Mkuu sikufahamu, nawe kumbe wamo,
Bado nina hamu, yakuelewa lako somo,
Radical e'nature wamfahamu, katoa changamoto,
Tushirikiane kutoa hii elimu, tena mashairi yasiyo ya kitoto.

ndugu nguli wasalaam, pote uliko zifike,
sidhani wanifahamu, wala kamwe usitake,
somo limekupa hamu, au wataka litoke?
na kama wataka somo, utalipata babake!

watch da space...
 
Back
Top Bottom