Ikitokea kwako utafanyaje?

Mom

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
708
29
wewe ni mwanamke/mwanaume una rafiki ambae mlipatana sana na kuheshimiana. wewe umeoa/kuolewa nae pia ana mwenzi wake, sasa inatokea kwenye ndoa yako kuna migogoro mingi inayopelekea hata kuiona ndoa chungu. rafiki yako huyu humshirikisha katika maamuzi shida zake na ni mshauri wako mzuri.

inatokea cku moja unaenda kwake baada ya kukorofishana na mwenzi wako huko home na unamkuta mwenyewe katika ile kukupoza upunguze hasira mnajikuta mko katika step nyingine ambayo hukutarjia na at the end mnafanya kitendo ambacho kimekua majuto kwako mpaka leo hii hutamani kumwona huyo rafiki tena!
 
Pole sana mom, ilikuwaje tena ukaamua kufanya infidelity?? Anyway ni shetani alikupitia.

Sasa tubu dhambi zako na usirudie tena kutenda dhambi...............:lie::lie::lie:
 
Pole sana mom, ilikuwaje tena ukaamua kufanya infidelity?? Anyway ni shetani alikupitia.

Sasa tubu dhambi zako na usirudie tena kutenda dhambi...............:lie::lie::lie:

nitubu kwa nani? MR? au mke wa jamaa au?
 
Hivi kama huna amani moyoni hata wazo la kubanjuka juu linakuwepo ?

haya tuambie kwa nini hutaki kumuona rafiki/au mpenzi ?
 
sasa sijui ningefanyeje n ando nsha do na rafiki

is it possible to undo?
 
Hivi kama huna amani moyoni hata wazo la kubanjuka juu linakuwepo ?

haya tuambie kwa nini hutaki kumuona rafiki/au mpenzi ?

kwa kosa kama hilo ulilofanya si unakua umeshaharibu urafiki wenu! hapo kwenye red cjui kwa kweli lakini ni kweli imemtokea my very best frend, nami nilimshauri aije kumweleza mumewe kitu hicho
 
kwa kuanzia ...............i dont believe na marafiki wa karibu sana hivyo wa jinsia tofauti. U r either in a relationship na huyo rafiki yako au u stay away from each other.

hii dhana ya 'rafiki yangu tu' siielewi............hivi mwanamme unamruhusu vipi mkeo kuwa na rafiki wa karibu hivyo mwanamme mwenzio?
mimi kwa upande wangu mume wangu siwezi kumruhusu rafiki wa karibu hivyo wa kike...............ataniwia radhi
 
wa jinsia tofauti

Dah afadhali.nilitaka kuogopa sana.Hapo cha kufanya ni kama alivyosema Mtumishi wa Bwana Chrispin.Tubu dhambi zako kwa maana ni mwema sana.Zaburi ya 32:3-4 inasema hivi.....'3.Bwana kama wewe ungehesabu maovu EE Bwana nani angesimama?4.Lakini kwako kuna msamaha ili wewe uogopwe......
Na ukishatubu AMINI kuwa umeshasamehewa dhambi zako na Mungu hatazikumbuka tena hivyo na wewe usitende dhambi tena na usijihukumu tena.
Amen
 
kwa kosa kama hilo ulilofanya si unakua umeshaharibu urafiki wenu! hapo kwenye red cjui kwa kweli lakini ni kweli imemtokea my very best frend, nami nilimshauri aije kumweleza mumewe kitu hicho

uk-ido na rafiki yako mnaharibu au ndo mme-cement urafiki???

bht nawe unachekesha! sasa hapo nawish ingekua possible

nachekesha tena mamiii, nimeuliza....maana kama yakimwagika hayazoleki basi utafanyeje sasa??!!
 
Ajali huwakumba wanaochukua na wasiochukua tahadhari!! Ingawa kwa anayechukua tahadhari humjia katika madhingira ambayo hayakwepeki (mfano hayo ya kwako)

Hupaswi kujuta but ni funzo la kukuongezea umakini ili lisitokee tena.

Onana na mwenzio ili ujue moyoni mwake alidhamiria au ni ajali kama kwa upande wako.
 
chrispin ......hebu nikuulize kidogo................wewe huwa unamruhusu mkeo kuwa na rafiki wa karibu wa kumhadithia matatizo yake yooote mwanamme ?
 
kwa kuanzia ...............i dont believe na marafiki wa karibu sana hivyo wa jinsia tofauti. U r either in a relationship na huyo rafiki yako au u stay away from each other.

hii dhana ya 'rafiki yangu tu' siielewi............hivi mwanamme unamruhusu vipi mkeo kuwa na rafiki wa karibu hivyo mwanamme mwenzio?
mimi kwa upande wangu mume wangu siwezi kumruhusu rafiki wa karibu hivyo wa kike...............ataniwia radhi

kwan gaijin hujawahi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti b4 marriage na je kama alikuwa after marriage urafiki ulikufa?
 
chrispin ......hebu nikuulize kidogo................wewe huwa unamruhusu mkeo kuwa na rafiki wa karibu wa kumhadithia matatizo yake yooote mwanamme ?

Hebu rudia swali lako mama. Naona kama sijaliona vizuri............... Yaani mama watoto wangu awe na rafiki wa kiume ambaye anaenda kumwambia matatizo ya familia yangu? Yaani............. Sielewi bado.:mad:
 
mom ....kusema ukweli sikuwa na rafiki wa jinsia tofauti wa kihivyo.............rafiki close nnao lakini sio wa kwenda (a) kwake (b) sehemu private tuko na yeye tu.

juu ya hivyo, baada ya kuwa kwenye ndoa nimepunguza urafiki...................sitafutani nao kihivyo, na kuwatafuta kwangu ni kuwaalika kwangu for dinner or lunch na mimi na mume wangu...................mimi na yeye faragha hamna hata kidogo.

at the end now wamekuwa rafiki wa mume wangu kuliko mimi...................wanatafutana bila ya mimi kuwa na habari.

kwa ufupi urafiki umepungua...........status yangu haini ruhusu kuwa na marafiki wa kihivyo nafikiri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom