MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,748
- 48,371
- Thread starter
- #41
Wengi mnaosema vita vya nyuklia vina mshindi, nadhani mtakua hamjui kwa nini Marekani na Urusi waliingia kwenye mkataba wa "Mutual assured destruction - MAD", huu mkataba unatambua kwamba
- Nchi husika, hata ikipigwa na nyuklia ya kwanza, ina uwezo wa kulipiza kisasi na kwa uzito pia
- Nchi husika, zina silaha za maafa makubwa na vita baina yao itasambaratisha dunia
- Kwamba kila nchi ina nyambizi zilizowekwa maeneo tofauti na zimejihami kwa silaha za nyuklia
Kwa kifupi, MAD ndio imezuia vita baina ya nchi zenye silaha za nyuklia, maana kwa mfano Mrusi akapeperusha mzinga dhidi ya Marekani, naye ajiandae maana muda usio mrefu kitu cha maafa makubwa kitatua kwake, na hapo itakua hakuna kuachia "ceasefire", pande zote mbili wataingia kwenye wenda wazimu wa kuachia mizinga kupepea hewani.
Washirika wao wenye mizinga kama hiyo hawatasazwa, itawabidi kuhusika pia, sisi na Afrika yetu itakua macho lakini kiaina tutaburuzwa tu.