ijumaaa ooh Kanumba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
JackWalperwwww.jpg
Na Mwandishi Wetu
Msanii wa kiwango cha Kimataifa nchini, Steven Charles Kanumba anazidi kung’ang’aniwa na ‘skandali’ za kuwafaidi warembo anaocheza nao filamu mbalimbali za Kibongo, Ijumaa Wikienda linasasambua.

...Kanumba
‘Shutuma’ hizo zimemkuta nyota huyo kupitia mtandao mmoja wa Bongo ambapo wadau ‘wamemshambulia’ wakimuonya kwamba amekuwa na katabia ka kuwatumbukizia ‘denda’ wasanii anaocheza nao ‘muvi’.
Picha ambazo msanii huyo amepondwa ni zile alizoshiriki kuigiza tangazo moja la hoteli maarufu ya ufukweni na nyingine ni muvi ya This Is It ambayo msanii huyo ameicheza na Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’.

...Wema
Katika maoni yao, wadau walikuwa wakiponda kulingana na picha hizo zilivyo, ukitia ndani mapozi yao mbalimbali.
Kwa mujibu wa wadau hao, mbali na kudaiwa kufanya kweli katika denda, pia Kanumba ‘anashutumiwa’ kuwa, amekuwa akiweka mapozi ya kumaanisha na wasanii hao mazingira yanayotafsiriwa kwamba, huenda baada ya kumaliza ‘kazi’ hiyo kuna kinachoendelea zaidi.
Watoa maoni hao kwenye ‘neti’ waliendelea kumponda staa huyo kwamba, tabia anazozifanya, hata kama ni kuigiza, lakini yeye anapitiliza.

...Penina
Hapa tunazinukuu baadhi ya meseji hizo zilizotumwa na wadau baada ya mtandao huo kuweka picha hizo:
“Ndugu yangu Kanumba, najua uko so handsome kama vidosho wanvyojigamba, jana nimeangalia movie yako moja nikaona kama ya sita kwangu unanyonyana (ndimi) na mwanamke...najiuliza hata kama mnaigiza, hao mabinti hawaoni ulizoigiza ambazo unapigana kisi za midomo na wengine?”

...Nkiru
“Mmhhhh ...haya yote ni maigizo!!!!”
“Daaaah anafaidi kweli, acha nifanye juhudi nami niwe muigizaji.”
“Director yeye mwenyewe unategemea nini?”
“Nasikia kuna dada mmoja kwenye zile za ki-Nigeria, waigizaji wa kiume huwa wanamgombania awe mke kwa sababu yeye hutoa kabisa, siyo maigizo! Kanumba humalizia kama yule dada wa Nigeria anavyomalizia kabisa- mfano yeye na Wema Sepetu mpaka ukawa ugomvi baada ya kupata mwingine!”
“Mmmmmmmmh ! Haya”

...Monalisa
“Mmmh! Wasanii wa kiume wanafaidi!”
“Ndo maana hawaoi eeeee.”
“Ni picha yenye maudhui ya ‘X’ au?”
“Wakimaliza kuigiza hapa, wanaanza kufanya kweli, hivi hali kama hii, mke wako unaweza kumkubalia awe muigizaji?”
“Hiyo ya mwisho mh? Alikuwa anataka kumpaka sun lotion nini? upaja huooo! Huyu binti (Aunt Ezekiel) naye atakuja kuporomoka fasta, walikuwepo akina Nora, Sinta, Johari na wengine wa wapi bwana.”
“Kanumba hii ni muvi ya tano kama sikosei nakuona unaburudika kiukweli na vidosho…”

...Mecy
Hata hivyo, utafiti wetu umebaini kuwa, kama ni kweli msanii huyo ‘anafaidi’ mazingira ya kimalavedave na wasanii wa kike anaoigiza nao, basi nyuma yake anao kwa idadi ya karibu saba.
Ijumaa Wikienda linadiriki kuweka kifua mbele kwa kuwataja majina wasanii aliokwishacheza nao filamu kuwa ni, Irene Uwoya, Wema Sepetu, Jennifer Rymond ‘Penina’, Mercy Johnson (Mnaijeria huyu) na Jacqueline Wolper.

...Lisa
Wengine ni Lisa Jensen, Yvonne-Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’, Nkiru Sylvanus (Mnaijeria huyu), Nargis Mohamed na Shamsha Ford.
Baada ya hatua yote hii, Ijumaa Wikienda lilimtwangia simu Kanumba ambapo baada ya mwandishi kujitambulisha, alimwomba asubiri kidogo akakata simu.

Alipopigiwa baada ya dakika tano mbele, simu yake ilionesha kuzimwa kabisa.
Kwa upande wake, Aunt Ezekiel alipoulizwa kuhusu kufanya kweli na Kanumba kwenye filamu ya This Is It alikiri huku akisema kuwa, anachojua katika hali ya kuvaa uhalisia na ili ujumbe ufike inavyokusudiwa lazima kuwe na vitendo vya kweli.
Akasema, lakini kama Kanumba yeye anafikiria mbali ya hapo, basi hayo ni mawazo yake.

...Jack
“Ni kweli, lakini unajua ili uoneshe uhalisia na ujumbe ufike lazima tufanye kweli matukio kama yale, lakini tukimaliza filamu kila mmoja kivyake, sasa kama yeye mwenzangu atakuwa anafikiria mbali zaidi sijui mwenyewe,” alisema Aunt.
Msanii mwingine aliyeongea na gazeti hili ni Penina ambaye alisema kuwa, hajawahi kula denda na msanii yeyote zaidi ya kisi. “Na ukiona wasanii wanakula denda kiukweli basi wana yao,” alisema Penina.


View attachment 10879View attachment 10880View attachment 10881View attachment 10882View attachment 10883View attachment 10884View attachment 10885View attachment 10886
 
Back
Top Bottom