Ijue Ndege Aina Ya C-5 Galaxy

Mwazange

JF-Expert Member
Nov 16, 2007
1,056
81
Leo tutazungumzia ndege nyingine iitwayo C-5 Galaxy.

C-5 Galaxy ni ndege iliyoko katika hazina ya zana za kijeshi la jeshi la marekani. Ndege hii ilitengenezwa kwa ajili ya kusaidia kusafirisha vifaa vikubwa na vizito vya kijeshi kwa umbali mkubwa. Ndege hii imekuwa ikifanya kazi katika jeshi la marekani tokea mwaka 1969 na ni ndege kubwa ya kijeshi kuliko ndege nyingine yoyote duniani.

Mnamo mwaka 1961, makampuni mengi ya kutengeneza ndege marekani yalikuwa yakifanya utafiti jinsi ya kutengeneza ndege kubwa ya kusafirisha mizigo ambayo ingeweza kubadilisha na ndege za usafirishaji za wakati huo kama C-133 transport na C-141 Starlifter kwa ufanisi, kwani ndege hizo zilikuwa ndogo sana kwa ndani kukabiliana na muongezeko wa ukubwa wa vifaa vya kijeshi.
Utafiti ulipelekea kuundwa kwa ndege yenye mashine 6 iitwayo CX-4, lakini mwaka 1962 mpango huo ulikataliwa kutokana na kwamba, haukufanya mabadiliko makubwa sana yaliyotarajiwa kuzidi ndege aina ya C-141 ambayo ndio ilikuwa kubwa kuliko zote kwa wakati huo.
Mwishoni mwa mwaka 1963, kundi jingine la watafiti, wakaja na michoro mingine yenye mabadiliko makubwa, mojawapo ikiwa ni kupunguzwa kwa idadi ya mashine toka 6 hadi 4. Michoro hiyo mipya ikaonyesha ndege itakuwa na jumla ya uzito wa kilo 24,9000 ikiwa tupu, na kusafiri kwa mwendokasi wa kilometa 806 kwa saa. Sehemu ya mizigo ikiwa na mapana ya meta 5.2, marefu ya meta 30.5 kimo cha meta 4.11 pamoja na milango miwili, mbele na nyuma kwa ajili ya kupakia na kupakua mizigo yenye hadi uzito wa kilo 81,600.

Baada ya hatua zote za mwisho za mpango huu kukamilika, ushindani wa zabuni za kutengeneza ndege ulitolewa kwa makampuni mbalimbali kama Boeing, Douglas, General Dynamic, Lockheed na Martin Marietta; wakati ule wa zabuni za mashine na mitambo kutolewa kwa General Electric na Pratt and Whitney.

Mnamo mwaka 1965 washindi wa zabuni hii walitangazwa kuwa ni Lockheed kwa ndege na General Electric kwa mashine, hakukuwa na zengwe, ni ujuzi tu ndio uliotamba
Ndege ya kwanza ya C-5 Galaxy ilianzwa kutengenezwa mnamo tarehe 2 mwezi Machi mwaka 1968 katika mji wa Marietta jimbo la Georgia. Miezi mitatu baadae, ndege hiyo ikaanza majaribio yake, maarufu kwa jina la ‘eight three o three heavy' katika kambi mbalimbali za jeshi kama Altus Air Force Base jimbo la Oklahoma, Charleston Air Force Base jimbo la South Carolina. Hadi kufikia mwanzoni mwa miaka ya 70, C-5 Galaxy ikachukua taji la kuwa ndege kubwa ya mizigo ya kijeshi, ikisafirisha hadi ndege za kwenda mwezini "Space Shuttle" katika kituo chake cha Kennedy Space Center.

Ndege hii imefanyiwa ukarabati zaidi ili kuifanya iwe ndege ya kisasa zaidi kwa kuekewa computer system za kisasa, MADAR (Malfunctioning Detection Analysis and Recording) ambayo hugundua kama ndege inahitaji matengenezo kabla ya tatizo kuwa kubwa zaidi, na system maarufu kwa jina la FRED (Fucking Ridiculous Economic/Environmental Disaster) kutokana na kwamba hutumia mafuta mengi sana katika uendeshaji wake.

Kwa ujumla ndege hii imeisadia sana jeshi la marekani katika kampeni zake za kijeshi duniani, kwa kusafirisha vifaru, mizinga na helikopta kwenye mistari ya mbele ya kivita. Inabeba kikosi cha wanajeshi zaidi ya 100 wakiwa na vifaa vyao kamili vya kivita; kama alivyowahi kunukuliwa waziri wa ulinzi wa mwarekani mwaka 2004 bwana Donald Rumsfeld kuwa "ndege hii moja inaweza kwenda kuanzisha vita sehemu yoyote duniani kwa muda kadhaa kabla ya kuhitaji msaada" maana ya kwamba, inabeba wanajeshi, vifaa vyao vya kivita pamoja na chakula chao kwa muda.
 

Attachments

  • C5.jpg
    C5.jpg
    85.4 KB · Views: 175
Back
Top Bottom