Ijue IP kiundani

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
423
115
Wakuu katika kuhakikisha mambo yanakuwa sawa,timu nzima ya AfroIT itakuwa inakuletea mafunzo ya Networking kwa maandishi na Video,Hivyo kaa mkao wa kura.Maoni na ushauri unahitajika katika kuhakikisha tunafika lengo la kujenga jamii imara na yenge maarifa.
Tembelea AfroIT Elimu,hapa ndio uwanja wa kujiunoa kwenye ICT na mambo mengine mbalimbali ya teknolojia kwa mada mbalimbali.

Ijeu IP kwa undani

IP, au Internet Protocol,ni kitambulisho cha kifaa kwenye ulimwngu wa Internet.Siku hizi karibuni kila kifaa kuanzia kompyuta,modems,majokofu,AC,routers,simu za mkononi,simu za mezani,printers nk zote zina IP address.IP vilevile ni kitu cha kawaida kwenye ulimwengu wa tovuti kwani kila tovuti lazima iwe na IP.IP ni kitu cha muhimu mno kwenye ulimwengu wa teknohama kwani bila IP maisha yengekuwa ni magumu mno kwakuwa ingekuwa ngumu kwetu kuwasiliana na kutofautisha vifaa tunavyomiliki kwenye ulimwengu wa teknohama.

IP katika Uhalisia wake

Ingawa nimeshaelezea IP ni nini, lakini ni wengi wetu bado watakuwa wanafikiria na kujiuliza je hii IP inafanana na kitu gani haswa? IP ifananaishe na anuani yako ya posta,kwa mfano mimi anuani yangu ni "Kilongwe,Mtaa wa AfroIT,Plot No.1565,P.o Box 104648 DSM".Sasa kama utaangalia hiyo anuani hapo juu.Chukua mfano mtu yupo Ujiji Kigoma,na anataka kuniandikia mimi barua kunitaarifu kuhusu umuhimu wangu wa kupiga kura. Basi huyu mtu ataandika anuani yangu kamili kwenye bahasha na kuitumbukiza kwenye sanduku la posta.Yeye bila kujua nini kitatokea,anachotaka ni kusikia kuwa "NIMEPATA BARUA YAKO".Hajali imetumwa vipi.Sasa kwenye ulimwengu wa teknohama,mfumo wa ufanyaji kazi unalingana sana na posta,kwani posta kitu cha kwanza itaangalia je huo mtaa wa AfroIT upo wapi? tayari mtumaji ameshaandika kuwa upo Dar es Salaam,basi posta ya ujiji utatuma moja kwa moja hiyo barua kwenda Dar es Salaam,ikishafika DSM,jamaa wataanza kuangalia hiyo p.o box 104648 je ipo upande upi? ukweli ni kuwa kila p.o box huwa ni moja tu,hivyo basi wao wataipeleka moja kwa moja kwenye hiyo p.o box,sasa chukua mfano Bw Kilongwe amejisajili kwenye huduma ya kufikisha hadi mlangoni,basi posta watakuwa na mtu ambaye atafungua hilo box la 104648 na kupeleka barua barua hadi plot 1565.Sasa kwa malekezo ya hapo juu hiyo P.o Box ndio IP kwenye teknohama na hiyo Plot No.1565 ndiyo MAC(tutakuja kuiona siku za usoni).Tofauti ya posta na teknohama ni kuwa,kwenye posta kuna uwezekano kukawa na P.o box mbili zinazofanana,ila zipo miji tofauti.Kwenye tekknohama hii kitu ipo,ila hizi address zinatakiwa kutumiwakwa matumizi ya ndani tu(Private IP),Pindi unapowasiliana na watu wa nje,hutakiwi kutumia hizi address na unatakiwa kutumia IP za uma(Public IP) .
Aina za IP.

katika ulimwengu wa teknohama wa leo,IP zimegawanyika katikamakundi wamili
1.Static IP
2.Private IP

Static IP

Static IP ni IP ambayo haibadiliki,kama jinalake linavyojieleza.Ingawa aina hii ya IP haitumiki kwa sana ila ina umuhimu mno.Kwa mfano,tovuti zinahitaji kuwa na static IP ili kuweza kuzipata bila ya kuzitafuta.Vilevile watumiaji wana uwezo wa kubookmark tofuti,unaweka tovuti unayoipenda kwenye orodha,ukija kwa siku za usoni basi unaweza kuipata bila utata.Vilevile static IP inahitajika kwa wale wanaotumia VPN(Virtual Private Networks),mfano mzuri wa VPN ni wale wafanyakazi ambao wapo site ila wanatumia zana toka main office yao.Vilevile kwenye mambo ya usalama na michezo ya online,kwa kutumia static IP unahakikisha kuwa utahifadhi kumbukumbu za mtumiaji kwa usalama zaidi.Ingawa siku hizi wengi hutumia cookies,ubaya unakuja kwakuwa cookies huweza kufutwa kiurahisi na mtumiaji lakini sio static IP.

Dynamic IP

Dynamic IP ni aina nyingine ya IP ambayo ni kinyume cha static IP,hii inamaanisha inabadilika. Wakati static IP huwa haibadiliki hadi mtumiaji anapofanya maombi ya kubadilisha kwa kujaza baadhi ya form na usumbufu kibao,dynamic IP yao huwa inabadilika pindi mtumiaji anapoingia kwenye internet au kuiwasha kompyuta yake,hivyo IP yako ya jana sio sawa na IP yako ya leo. Kwenye ulimwengu wa kompyuta networks,kuna vifaa vingi ambavyo vina kazi ya kugawa IP na kuweka rekodi ya nani ana IP gani,vifaa hivi ni kama Modems,DHCP servers nk.Umuhimu mkubwa wa dynamic IP unakuja pale unapomuwezesha mtumiaji kuweza kuingia kwenye internet bila usumbufu.HIvyo kwa mtindo huu huu,tunaweza kuhakikisha tunabudget idadi ya IP,kwani sasa sio lazima kila mtu awe na IP yake.Kumbuka kwa sasa tuna uhaba wa IP kwakuwa kila kifaa siku hizi kinataka kuwa na IP yake,binafsi nimewahi kuona vitanda vina IP,kwani vimeunganishwa na heating system,hivyo hutumia IP ili kuchunga jotoridi lake.

Private vs Public IP

Hapo juu niligusia aina hizi mbili za IP,aina hizi zinaweza kuangukia kwenye kundi la ststic au dynamic,haijalishi.Kama majina yake yanajieleza.hebu tunagalie kwa undani
Private IP(IP Binafsi).

Private IP ni aina mojawapo ya IP ambayo yao hutumia kwa matumizi ya ndani tu,aina hii ya IP hairuhusiwi kutoka nje ya eneo husika.Kwa mfano munaweza kutumia aina hi ndani ya kampuni yenu,ndani ya nyumba yenu au ndani ya shule yenu.Pindi unapotaka kutoka nje basi unahitaji kutumia public IP.
private%20ip.jpg

Matumizi:

Matumizi ya private IP ni mengi ila lililo kubwa ni pale unapotaka kuunganisha vifaa zaidi ya kimoja wakati wewe umenunua IP moja tu toka kwa kampuni husika.Kwa mfano mimi ni mmiliki wa internet cafe,nina kompyuta kama mia moja hivi.Sasa ninapoenda TTCL au VODA kununua Internet connection,wao hunipa IP moja tu.Ninachotakiwa kufanya ni kuzipa private IP kwa hizo kompyuta mia moja,halafu nitaseti NAT(Netmork Address Translation).Ambapo hutafsiri kila Private IP kwenda public IP hivyo nitaziwezesha hizo kompyuta moa moja kutumia private IP kibao wakati zote zikitegemea private IP moja tu.Mfano mzuri chukulia timu ya mpira,ingawa kwenye timu ya mpira kuna wachezaji kumi na moja lakini wote wanajulikana kwa jina moja tu,iwe yanga au simba au Azam,hehe.Sasa kila mchezaji anapotaka kwenda nje,basi timu husika itakuwa na utaratibu wa kumtambulisha huko nje kwa kutumia timu yake na sio jina husika tena.(Tutajifunza kwa undani kuhusu NAT siku za usoni na kuona ni jinsi gani tunavyoweza kuset NAT).Kumbuka private IP yoyote mwisho wake ni kwenye router.Ikifika hapo router huitupa kapuni na kuibadilisha na public.

Public IP

Hili nalo ni kundi kama lilivyo la Private,ila kwa hili ni kuwa IP ambazo ndizo zinatambulika kwenye ulimnwengu.Chukulia leo hii mcezaji wa simba akaenda fifa na kusema mimi ni fulani,FIFA hawatamtambua,ila akisema mimi ni fulani wa simba basi atatambulika.Sasa simba ndio Public IP,yaani inatambulika na kila mtu wakati huyo mchezaji ni private IP,anatambulika kwake tu.Public IP ndio zinazotumiwa katika kubadilishana address kati ya routers.

Inakuja karubuni-->1.Jinsi ya kuset IP address
2.IPv4 na IPv6
3.Localhost
4.JInsi ya kuset NAT kwenye IPv4 nk
Pia tembelea AfroIT Elimu kwa Video ya Mada hii hivi karibuni.
 
Ijeu IP kwa undani

IP, au Internet Protocol,ni kitambulisho cha kifaa kwenye ulimwngu wa Internet.Siku hizi karibuni kila kifaa kuanzia kompyuta,modems,majokofu,AC,routers,simu za mkononi,simu za mezani,printers nk zote zina IP address.IP vilevile ni kitu cha kawaida kwenye ulimwengu wa tovuti kwani kila tovuti lazima iwe na IP.IP ni kitu cha muhimu mno kwenye ulimwengu wa teknohama kwani bila IP maisha yengekuwa ni magumu mno kwakuwa ingekuwa ngumu kwetu kuwasiliana na kutofautisha vifaa tunavyomiliki kwenye ulimwengu wa teknohama.

Mkuu naomba nikusahihishe kidogo hapo kwenye red. Tovuti as such huwa haina IP yenyewe kama yenyewe, isipokuwa inakuwa nayo kutokana na Komputa inayo-host tovuti hiyo. Kwa mfano Gari Yako inaweza ikawa na IP fulani inapokuwa hosted na server iliyoko Tanzania, ila the same website IP yake itabadilika kama itakuwa hosted na server tuseme iliyoko Marekani. Tovuti huwa ina-acquire IP address kutoka kwenye server, lakini yeyewe kama yenyewe huwezi kui-assigh IP address. Una-assign IP address kwenye host server, halafu hiyo server ndiyo ita-determine IP address ya websites itakazozihost. However, thanks for your post
 
Shukrani kwa kuweka mambo sawa kaka, niliogopa kama utaanza kuchanganua jinsi gani Website inavyotumia IP ya Sehemu inayoishi (Server au kompyuta ya kawaida) ingekuwa ni somo lingine so nikaishia kuwa kila website lazima iwe na IP inayotambulisha. Lakini ni vyema ulivyorahisisha na hii ndiyo elimu, mmoja anaanza wengine wanaendeleza na kuboresha pale alipochanganya mpaka tunafika.

BTW; Hii makala ni ya zamani, duh watu wana search..
 
Uko sahihi, kila tovuti lazima iwe na IP address. Inapewa na wale ISP nayehost website hiyo. Sema tu ukibadilisha ISP na IP address ya website nayo pia inabadilika.
 
Mada kama hizi ndio zinadetermine aina ya raia tunaoishi nao

Ingekuwa umbea sasa ungekutana na comment buku
 
Back
Top Bottom