Ijue Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 - 2015

Naomba kujuzwa juu ya ilani ya CCM 2010. inasehemu inagusia juu ya Mahakama ya Kadhi? Kama sio, je 2005 ilikuwa ni danganya toto kwa ajili ya kupata kura? je, Waislamu wanaluchukuliaje hili?
 
Nilivyoiangalia kwa haraka haraka icho kitu kama hakipo
Na watakuwa wameiondoa bse wanajua ni issue
 
kwa sasa suala hilo halipo kwenye ilani...!

waislam wameruhusiwa kuanzisha mahakama ya kadhi kwani ni ibada yao.

kila la heri waislam.
 
Ilani ya Uchaguzi 2010-2015 inazungumzia mambo ya maana yanayowagusa Watz wote, sio ibada ya baadhi ya watu!
 
Ilani ya Uchaguzi 2010-2015 inazungumzia mambo ya maana yanayowagusa Watz wote, sio ibada ya baadhi ya watu!

Kumbe ile ya 2005 - 2010 ilikuwa ni ulaghai na wizi kwa Waislamu? Kwa nini wakubali kutumika?
 
Kumbe ile ya 2005 - 2010 ilikuwa ni ulaghai na wizi kwa Waislamu? Kwa nini wakubali kutumika?

Mbona Waislamu walishaambiwa kuanzisha Ibada yao (mahakama za kadhi) au wanasubiri Serikali iingie misikitini kuanzisha Ibada zao?
 
Naomba kujuzwa juu ya ilani ya CCM 2010. inasehemu inagusia juu ya Mahakama ya Kadhi? Kama sio, je 2005 ilikuwa ni danganya toto kwa ajili ya kupata kura? je, Waislamu wanaluchukuliaje hili?

katika kila kipindi cha uchanguzi kuna kuwa issue maalum as wakati ule mlishuhudia makanisa kumpamba JK kuwa chaguo la Mungu waislam wao walikaa kando kuangalia tija katika wakati ule ndio wazee wa propaganda wakaona hawa tukiwaambia sisi tutaleta mahakama ya kadhi lazima wajae kwenye kumi na nane yetu.....

Ilani huwa inapitishwa na watu ndani ya chama na kwa kusema ukweli mapadri, maaskofu na makasisi waliosema JK chaguo la Mungu waliikubali ilani ile pamoja na makada walioipitisha wakiwamo wakristo na wasio na dini. Lakini kilichotokea baada ya hapo mnakijua....wale waliosema Jk changuo la Mungu walikuwa wakwanza kupinga kipengele hicho wakisema nchi itaingia kwenye matatizo na kutilia mkazo serikali haina dini blah blah blah.......as if hawakuwa aware... huo unaitwa UNAFIKI ni mbaya sana kwa kiongozi uwe wa kaya, wa dini au wa jadi akiwa mnafiki hii hali ya unafiki ni mbaya zaidi na inaweza kuleta matatizo makubwa kuliko hata udini.

Issue ya pili ilikuwa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu....

Nakumbuka JK alihakikisha wanafunzi wanapata support ya fees, accommodation and meal allowances kwa 100% na kwa kauli yake siku ile alipokutana na wanafunzi Diamond jubelee alisema na naomba nimnukuu " hakuna mtoto wa masikini/mkulima atakaekosa kusoma kwa kushindwa kulipia gharama za masomo" mwisho wa kunukuu. wote mnajua kilichofuatia mwaka wa fedha 2006/2007 wanafunzi waliambiwa sheria ilipitishwa na bunge ya bodi ya mikopo inasema kuna kitu kinaitwa "sharing cost" 70% serikali na 30% mwanafunzi.... hakukuwa na budi walioweza welihakikisha wanauza viji ngo'mbe vyao mahindi na mtama wakalipia wakajikongoja mpaka wakamaliza elimu yao. kwa wenzangu na mimi vyuo viliwashinda wakarudi vijiweni sina uhakika pengine wengine walipatwa na wazimu kwa sababu ya msongo wa maisha na wengine kuingia kwenye mambo ya madawa ya kulevya.

Chukua tahadhani.

This time mmeona wafanyakazi wameongezewa salio kinyemela sijui hii kitu ipo kisheria au la nina wasiwasi yasije yakawafika yaliyowafika wanafunzi wa elimu ya juu Kalaga baho.
 
Mbona Waislamu walishaambiwa kuanzisha Ibada yao (mahakama za kadhi) au wanasubiri Serikali iingie misikitini kuanzisha Ibada zao?

Hilo swala kaka ni vere sensitivu usijaribu kudhihaki imani za wenzako I can read between the lines unachuki na huo usilamu tu maana hauna cha kuongea hapa kinazungumzwa ilani na jinsi ilivyotekelezwa sasa kama hujui nini maana ya ilani na inakuwaje hiyo ilani sema watu waanzishe mjadala upate kuelimika.

Yaliyowakuta waislam yanweza kuwakuta wafanyakazi na kwenye kundi hilo hakuna cha mwislamu wala mpagani. Sisi kama watanzania tuwe wamoja msiendekeze propaganda za watu walioishiwa hoja kama eti ohhh unajua bwana hii serikali yetu haina dini! whaaaaaaaaat? hivi leo waislamu wakisimama waseme kuwa wakristo ndio mnaudini na mnashikilia serikali mtakataa? ilhali nchi hii ukombozi wake ulianzishwa na kuasisiwa na waislam Mungu awalaze mahali pema peponi kina Sheikh Takadir, Abdulwahid sykes na bibi titi mohamed.

Wewe fikiria ikiingia tarehe kumi natano december ofisi zote za serikali zinapewa fungu la kununua mauwa ya christmass na vimulimuli ( na wengine wanapatia kuweka cha juu kwenye manunuzi)

Kama serikali haina dini kwanini kwenye wimbo wataifa wanamtaja Mungu?
Kwanini wansali wanapoanza mkutano wa bunge?
Huyu Mungu wa Serikali ni Mungu gani? na serikali haina dini?

Mkuu rudi kwenye mada usichokonoe mambo!
 
Kama wananchi waliahidiwa maisha bora na wakaachwa wamefulia, itakuwa ishu ya kikundi cha dini?

Acheni hizo bwana!!

Acheni kujadili dini.

Muulizeni Sheikh Makamba na Sheikh Kikwete. Siyo kutusumbua sisi.
 
Sasa tujadili jinsi yakuchagua viongozi bora
 
Iko siku watawapa waislamu mahakama ya kadhi bila kuombwa kama sasa...

Siku hiyo inafika hata ikibidi kwa nguvu...iwe leo iwe kizazi cha watoto wetu nk...

Naamini iko siku hata kama watu kama wewe mtachukia hadi kufa...haitasaidia

Sasa tunamshughulikia yule hakimu aliyemfunga muislamu eti kavaa kofia! baada ya siku tatu na sio saba walimwachia..

iko siku tutawapa siku mbili wataanzisha kile kilicho haki yetu msingi..

na wewe na watoto wafuasi wako wakiona huku wamechukia kama huyu hakimu alivyomuona jamaa katolewa huku anachukia aibu! chuki ni ugonjwa wa wakristo.

Wewe madrassa imeharibu sana kichwa chako, waislamu wameambiwa waanzishe mahakama zao, hawataki mpaka Serikali iwaanzishie! Mbona Wakristo wana "mahakama" zao (eg Roman Catholic mahakama zao zina hierarchy inayoishia Vatican) na zinafanya kazi bila kuingiliwa na Serikali? Kama unafikiri kwamba kuwaambia Waislamu waanzishe Ibada zao na kuziendesha wenyewe ni "chuki kwa Waislamu" then you got it wrong!
 
Hilo swala kaka ni vere sensitivu usijaribu kudhihaki imani za wenzako I can read between the lines unachuki na huo usilamu tu maana hauna cha kuongea hapa kinazungumzwa ilani na jinsi ilivyotekelezwa sasa kama hujui nini maana ya ilani na inakuwaje hiyo ilani sema watu waanzishe mjadala upate kuelimika.

Yaliyowakuta waislam yanweza kuwakuta wafanyakazi na kwenye kundi hilo hakuna cha mwislamu wala mpagani. Sisi kama watanzania tuwe wamoja msiendekeze propaganda za watu walioishiwa hoja kama eti ohhh unajua bwana hii serikali yetu haina dini! whaaaaaaaaat? hivi leo waislamu wakisimama waseme kuwa wakristo ndio mnaudini na mnashikilia serikali mtakataa? ilhali nchi hii ukombozi wake ulianzishwa na kuasisiwa na waislam Mungu awalaze mahali pema peponi kina Sheikh Takadir, Abdulwahid sykes na bibi titi mohamed.

Wewe fikiria ikiingia tarehe kumi natano december ofisi zote za serikali zinapewa fungu la kununua mauwa ya christmass na vimulimuli ( na wengine wanapatia kuweka cha juu kwenye manunuzi)

Kama serikali haina dini kwanini kwenye wimbo wataifa wanamtaja Mungu?
Kwanini wansali wanapoanza mkutano wa bunge?
Huyu Mungu wa Serikali ni Mungu gani? na serikali haina dini?

Mkuu rudi kwenye mada usichokonoe mambo!

Hatuna woga wa kusema ukweli eti kwa sababu issue ni "sensitive!" Mimi sidhihaki imani ya Kiislamu ila nawakumbusha kwamba Serikali ilishawaambia ianzishe Mahakama zao za Kadhi na wasisubiri mpaka Serikali iwaanzishie! Sasa hiyo ni dhihaka au unataka watu tuwe na heshima ya woga tukiogopa kuwa watu watalipua balozi mbalimbali kama walivyofanya wakati katuni ya mtu aliyekufa karne tano zilizopita ilipochorwa? Hizo heshima za woga zimepitwa na wakati sasa!

Na hiyo unayodai Serikali imetoa mafungu ya kununulia maua ya Krismasi ni uwongo na uzushi mbaya sana!
 
Buchanan,
Mkuu unaweza kunambia haswa maana ya sura hii yenye signature yako?..
Neither is there salvation in any other: for there is none other name under heaven (except the name of Jesus Christ of Nazareth) given among men, whereby we must be saved!" (Acts 4:12).
 
Niambie hujaelewa nini hasa kuhusu Signature ili nikujulishe! Hujui kiingereza au namna gani ili niiweke kwa Kiswahili?
 
Ni muhimu kuzisoma hizi Ilani kwa makini kwa ndio check list ya kuwapima walio madarakani mwisho wa siku. Tuachane na ushabiki zaidi, nadhani utashi na ukomavu wa kisiasa ni muhimu zaidi.
 
Wanajamii kama kuna mwenye ilani ya uchaguzi ya CCM naomba anisaidie kuiweka hapa janvini,
ninawasiwasi sana juu ya ahadi anazotoa wakati huu wa kampeni na sioni wa kumuuliza hata zile za 2005 ametekereza ngapi? ninachohisi anachofanya ni kudanganya tena kwa ahadi zake mara viwanja vya ndege mara meli? je vipo kwenye ilani ya CCM maana anajua kabisa kama atafaulu this time hizo ahadi anajua hatatekereza na hatakuwa yeye wakujibu...
 
Ilani ya Uchaguzi 2010-2015
(vi) Mapato ya Serikali kutokana na uchimbaji mkubwa yameongezeka
kutoka Sh. 457.4 bilioni mwaka 2005 hadi Sh. 840.0 bilioni mwaka
2008.
(vii) Thamani ya madini yanayouzwa nje imeongezeka kutoka dola za
Marekani 727.45 milioni mwaka 2005 hadi dola 1,075.9 milioni
mwaka 2008.

Kwanini (vi) isomeke hivi ili iwiane kimantiki na (vii) ?
(vi) Mapato ya Serikali kutokana na uchimbaji mkubwa yameongezeka
kutoka dola 304.93 milioni mwaka 2005 hadi dola 560.0 milioni mwaka
2008.

Exchange rate: 1US$ = 1500 Tsh.

Nini kinafichwa kwenye hizo figures hasa currencies?
 
Mafanikio ya Kiuchumi:
13. Katika kipindi hiki Serikali imeweza kutekeleza mipango yake kwa ufanisi
mkubwa na kuleta mafanikio ya kiuchumi yafuatayo:-
(a) Ukuaji wa uchumi ulifikia wastani wa asilimia 6.7 mwaka 2010
ukilinganishwa na wastani wa 4.5 mwaka 2005.
(b) Mapato ya ndani ya Serikali yaliongezeka kutoka wastani wa Shilingi Bilioni
177 kwa mwezi mwaka 2005 hadi kufikia wastani wa Shilingi bilioni 390
sawa na ongezeko la zaidi ya mara mbili kwa mwezi mwaka 2010.
(c) Mfumko wa bei ulibaki katika tarakimu moja tangu mwaka 2000 hadi 2007
isipokuwa mwaka 2008 ambapo ulifikia kiwango cha 10.3 kutokana na
mtikisiko wa uchumi duniani.
(d) Bajeti ya Sekta ya Kilimo imeongezeka kutoka asilimia 4.5 mwaka 2005
hadi asilimia 7.9 mwaka 2010. Kutokana na umuhimu unaoongezeka
wa kilimo cha umwagiliaji nchini kama hatua ya uhakika ya kupambana na
njaa, Serikali imechukua hatua za kuimarisha mkakati wa umwagiliaji na
miundombinu yake, kwa kuendeleza hekta 289,245 za kilimo na kuweka
miundombinu ya umwagiliaji. Hatua hii imeongeza ufanisi wa matumizi ya
maji kwa umwagiliaji kutoka asilimia 12 iliyokuwepo kabla na kufikia
asilimia 30. Aidha, ufanisi huo umeongeza mavuno ya zao la mpunga
kutoka wastani wa tani 1.8 kwa hekta na kufikia tani 5 kwa hekta.
(e) Ukuaji wa Sekta ya Viwanda umeongezeka kutoka asilimia 8.4 mwaka
2005 hadi asilimia 9.9 mwaka 2008.
(f) Sekta ya Madini imekuwa na kuleta mafanikio yafuatayo:-
(i) Kukamilika kwa Sera ya Madini ya mwaka 2009.
(ii) Kuanzishwa kwa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania.
6
(iii) Kukamilisha ramani tatu za kijiolojia zinazoonyesha uwepo wa
madini Tanga, Nachigwea na Liganga.
(iv) Kutengwa kwa maeneo ya wachimbaji wadogo katika maeneo ya
Kilindi, Winzo, Mvomelo, Melela, Rwamagaza, Nyarugusu, Maganzo
na Mererani. Maeneo hayo yana jumla ya kilometa za mraba
5,876.5.
(v) Mchango wa Sekta ya Madini kwenye pato la Taifa umeongezeka
kutoka asilimia 2.4 mwaka 2005 hadi asilimia 2.6 mwaka 2008.
(vi) Mapato ya Serikali kutokana na uchimbaji mkubwa yameongezeka
kutoka Sh. 457.4 bilioni mwaka 2005 hadi Sh. 840.0 bilioni mwaka
2008.
(vii) Thamani ya madini yanayouzwa nje imeongezeka kutoka dola za
Marekani 727.45 milioni mwaka 2005 hadi dola 1,075.9 milioni
mwaka 2008.
(vii) Ajira katika uchimbaji mkubwa imeongezeka kutoka wafanyakazi
7,000 mpaka 13,000.
 
Ni muhimu kuzisoma hizi Ilani kwa makini kwa ndio check list ya kuwapima walio madarakani mwisho wa siku. Tuachane na ushabiki zaidi, nadhani utashi na ukomavu wa kisiasa ni muhimu zaidi.

Mushi, Umesema kweli kabisa, lakini swali kubwa ni je watanzania wengi wanajua kusoma kilichoandikwa between the lines?

Kwa mfano ukisoma SURA TISA ya ilani ya UCHAGUZI wa CCM (2010-2015), Kifungu namba 226, wanakiri wazi kuwa CCM ni chama cha mafisadi na kupata maendeleo chini ya CCM ni miujiza na hili pekee linatosha kuwafanya watanzania wakinyime kura hapo October 31, 2010:

Nanukuu kifungu hicho na kuongezea comments in red na penye mashaka in Blue

" 226. Kimsingi utekelezaji wa Ilani hii utafanikiwa kama (my take hawana uhakika) Chama kitatekeleza jukumu lake la kusimamia kwa kuhakikisha kuwa programu ya utekelezaji inaandaliwa na kusimamiwa ipasavyo. Inawezekana kujenga Maisha Bora kwa kila Mtanzania na Tanzania yenye Neema Tele kama Uongozi wa sasa wa Chama utabadilika kiutendaji, kimsimamo na kimtazamo (wanajua kuwa uongozi wa chama ni ule ule na ni vigumu mafisadi kubadili mtazamo, msimamo na utendaji kwani lengo lao ni kuchuma zaidi)."

Hitimisho lao lenye neno "KAMA" linaifanya Ilani hiyo kuwa ya majaribio zaidi na hata CCM hawana uhakika wa kuitekeleza ndiyo maana wamehitimisha kwa neno "KAMA"
 
Ndugu wanajamii,

Tunamshukuru huyu jamaa kututumia hizi ilani za chama cha CCM,

Langu swali ni moja je kiasi gani CCM wanatekeleza na kuisimamia ilani yao baada ya kushinda uchaguzi,uzoefu umeosha kuwa wakati wa kampeni wana CCM wanakuwa karibu na wananchi,na kuwashawishi tumefanya hili na lile kwenye makaratasi lakini mwenye macho haambiwi,tazama.
Ndugu mwananchi tumia kura yako vizuri,

Elisante Yona
 
Back
Top Bottom