Ijue Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 - 2015

Kupanua mafunzo ya VETA yaweze kuchukua vijana wengi zaidi
wanaofuzu elimu ya msingi ili waandaliwe kujiajiri wenyewe.

hapa hakuna kipaumbele kwa wali waliofeli form 4 ambao hawana pa kwenda na hakuna kipaumbele cha kuhakikisha wanaomaliza primaryschool waende secondary ??????????????*****##@$:A S-confused1:
 
Kuendelea kutekeleza mpango wa kujenga maabara ya Sayansi na
ya Lugha katika kila Shule ya Sekondari ili kuboresha ufundishaji.

Shule nyingi za secondary ziko vijijini walimu watatushule nzima ya seconda, umeme hakuna Je hizo maabara zitaendeshwaje ikiwa hata lab technician hawapo?

Langu jicho
 
Kufufua vyuo 4 vya watu wenye ulemavu na kuvipatia rasilimali
watu na fedha.

Vilikufaje?? na je serikali hii ikichaguliwa na ikifa si itaviua tena
 
Shukrani sana kasimba123 kwa unavyochambua, hivi ndivyo inatakiwa unachukua kifungu na kukitolea uchambuzi na si kusifia au kuponda Ilani nzima, big up nazidi kujifunza.
 
Usawa wa Jinsia
18. Kwa kuzingatia Imani ya CCM juu ya usawa wa binadamu na wito wa kimataifa
juu ya usawa wa jinsia, Serikali chini ya uongozi wa CCM imeweza kutekeleza
yafuatayo:-
(a) Kuongeza ushiriki wa wanawake katika Bunge, Baraza la Wawakilishi na
Madiwani kutoka asilimia 30 hadi 40. Aidha, ushiriki wa wanawake
umeongezeka pia katika nafasi mbalimbali za uongozi na utendaji
Serikalini na katika Taasisi za Umma.
(b) Kuanzisha Benki ya Wanawake.
(c) Kupitisha Sheria ya Mtoto.

Hii benki ilishaanzishwa sasa wataanzisha ipi 2010-2015??
 
Kuimarisha usindikaji wa mazao mbalimbali katika ngazi ya kaya ili
kuongeza thamani na muda wa matumizi na upatikanaji wa chakula kwa
ujumla.

Hapa sijui kama hili linawezekana nilitegemea kitu kama kuwapa elimu ya usindikaji huyu mtu wa kaya atasindikaje kama hajui kusindika na je kama wanasema hawana pesa kila siku je watawezaje kulipia hizo gharama au elimu ya kusindika ?????????//
 
(q) Kuandaa programu ya kupunguza matumizi ya umeme hususan viwandani
na majumbani.
(r) Kufufua na kupanua mitambo ya TPDC ya kusafishia mafuta na
kuhakikisha kwamba mitambo hiyo inafanya kazi wakati wote.

(s) Kuwa na mpango wa kuhimiza matumizi ya nishati mbadala ya jua, upepo
na fungamotaka (biogas).

Ilikufaje???? si serikali hii hii ya CCM ndio iliyoua hii mitambo?
 
(j) Kupunguza Msongamano wa Magari katika Jiji la Dar es Salaam kwa
kufanya yafuatayo:
(i) Kujenga barabara za juu (fly overs) kwenye makutano ya barabara
maeneo ya Ubungo na TAZARA,

Mradi wa DART bado utachukua muda mrefu sana na labda hayo magari yapae Hata kabla ya kujenga flyovers Je mmeshindwa kufikiria kuwa watu wote wanaotoka Tegeta na mbezi beach kwanini wasitumie boat hadi Bandarini Posta na wanaotoka mbezi luisi hadi ubungo kwanini wasitumie treni kutoka ubungo hadi stesheni. watokao mbagala gongolamboto vile vile wanaweza kutumia treni kwa reli zilizopo bila hata kujenga reli kama temporary solution sijui watu hawafikirii au ni kuangalia mianya ya kuchota fedha?
 
(v) Kuendelea kutekeleza Programu ya kufundishia na kujifunzia kwa
kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Shule za
Sekondari.

Hivi lengo hili litafikiwaje wakati hakuna umeme wa kuaminika vijijini na hata kama upo lakini si wa uhakika nafikiri menginne yanawekwa kupamba tu
 
Ilani hiyo sijaisoma kwa kina kwa sababu najua imejaa uwongo mwingi sana. Kwa mfano, ukurasa wa tano unadai kuwa Serikali imekuza uchumi kutoka 4.5% mwak 2005 hadi 6.7% mwaka 2010. Hata hivyo kwenye ilani ya mwaka 2005 ukurasa wa sita walidai kuwa kipindi cha miaka kumi ya Mkapa kilikuza uchumi kutoka 3.6% hadi 6.7%. Wameshawazowea wanajua kuwa watanzania huwa hatuchambui maneno wanayotuambia viongozi wa CCM.

attachment.php

=================================================================================
2005-10.JPG 2010-15.JPG
attachment.php
 
Unajua Kichuguu nchi yetu haina wachambuzi wa mambo ya kitaifa hata waandishi wa habari wanakimbilia kuandika matukio ya siku hiyo. Kama ulivyosema ukiangalia kweli kwenye
ilani ya 2005-2010 uchumi ulikuwa hadi asilimia 6.7
ilani ya 2010-2015 uchumi unatarajiwa kukua kutoka 4.5% hadi 6.7% inamaana kama 2010 ulikuwa 6.7% na 2015 utakuwa 6.7% kwa hiyo tusitegemee uchumi kukua au ile asilimia ya 2010 walikuwa wanatudanganya. Sasa tuchukue lipi uchumi wetu ulikuwa asilimia ngapi mwaka 2010 4.5? au 6.7? ilani ipi nasema ukweli. Angalia tena hii mazingaombwe

48. Katika kipindi cha miaka 2005-2010, Sekta ya viwanda ilitarajiwa kukua kufikia
asilimia 15. Ukuaji halisi uliongezeka kutoka asilimia 8.5 mwaka 2005/2006 hadi asilimia 9.9 mwaka 2008/2009.

49. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010 – 2015, Chama Cha Mapinduzi kitaitaka Serikali iikuze sekta ya viwanda kutoka asilimia 9.9 ya sasa hadi asilimia 15 mwaka 2015

Hii maana yake nini, ni kuwa lengo la 15% lililowekwa na ilani ya mwaka 2005-2010 halikufikiwa sasa lengo hilo hilo la 15% limewekwa tena na ilani ya 2010-2015 na hata hivyo hawana uhakika kama mwaka 2015 litafikiwa, kwa maana hiyo inawezekana ilani ya 2015-2020 ikarudia tena lengo hilo hilo hadi lifikwe mwaka 2020 na kuendelea.

Ndiyo maana kuna wakati Mkapa alikiri kuwa Ilani ya CCM haitekelezeki ni mazingaombwe. I come to a conclution that ushindi huwa hauletwi na uzuri wa ilani is how campaign is organized.

Finally, Tanzania hatuna wadadisi wa mambo tuna wadadisi wa matumbo mradi waonekane TBC 1, vile vile hatuna waandishi wa habari tuna ma reporter wa matukio kitu ambacho hata mtoto wangu wa miaka mitano huwa anakifanya kwa sababu kila nikirudi kazini angalau huniambia tukio moja lililotokea, leo majirani wetu walikuwa wanapigana. Uandishi huanzia pale unapoletewa tukio na sio kutubandikia picha ya tukio gazetini na kuiita habari.
 
Wakuu,
Ilani imejaa vichkesho na maswali mengi zaidi ya majibu.
Nina mifano michache tu kutoka ilani hiyo:
[9] c: Kufanya mapinduzi ya viwanda.
Mapinduzi yapi wakati Mwl aliacha viwanda 450 na sasa vimekufa.
Hivi ni kwanini Mutex,Mwatex,Tanganyika Packager, etc vimekufa ili hali kila
resource inapatikana hapa nchini. Hivi mapinduzi gani yatafanikiwa ikiwa
tumeshindwa kuendesha shirika la reli na Tazara ambazo hazina ushindani
Mapinduzi gani kama hatuwezi kusindika hata machungwa eti mpaka yaende nje.
Mapinduzi gani wakati General tyre inakufa kwa kuagiza mitumba ya tairi.
Kabla ya kutueleza mapinduzi ya viwanda watueleze vilivyokuwepo vilikufaje!

[13] a: Uchumi umekuwa 6.7, 2010 ukilinganisha na 4.5, 2005
Kwanini nchi imeendelea kuwa na bajeti tegemezi 40% ?
Kwanini urari wa mapato na matumizi umeongezeka [fiscal deficit]

b: Mapato ya ndani yameongezeka 177 Billion /Month 2005 hadi 390/month 2010
Kwanini bajeti ni tegemezi 40% kama tume double tax collection!!!
Je thamani ya shilingi dhidi ya sarafu nyingine imebaki pale pale? Kama 2005
exchange rate ilikuwa 1000/dollar leo ni 1500/dollar utawezaje kusema
umekusanya zaidi? hapa nitatoa mfano, kama 2005 serikali ilikusanya Sh bilion
1 kwa mwezi hii ni sawa na dollar million 1. Leo Kama serikali inakusanya sh Bil
1.5 kwa mwezi ni sawa na dollar milion 1. Hapa kuna ongezeko kweli?

[18] Kuongeza ushiriki wa wanawke kutoka 30-40% bungeni na nafasi za utendaji
Hivi tatizo la mtanzania ni jinsia au umasikini!! kama kuna wanawake wanaweza
kuna tatizo gani wakiwa wote katika wizara moja, as long as they can deliver!!!.
Je kuchagua wanawake au wanaume kwa kuzingatia jinsia kunamuondolea vipi
dhiki na adha yule mzazi anayejifungulia sakafuni. Je kuna data gani zinazoonye
sha kuwa usawa wa jinisia unaleta maendeleo.
Nafasi za ubunge na udiwani zimesaidia vipi kutatua tatizo la mimba mashuleni.
Tutawezaje kuwa na uwakilishi sawa endapo watoto wa kike wanaozwa wakiwa
mashuleni. Je si kweli kuwa nafasi hizi zimekuwa zikitumiwa na watu waliomo
ndani ya sytem kupenyeza watoto na wake zao kwa kisingizio cha usawa wa
jinisia.!!!
Tujiulize,mbona kule India,marekani, Uk, ambako kuna wanawake wamekwenda
shule hasa,mbona hawajafikia usawa wa jinsia hata baada ya miaka zaidi ya 100
ya kujitawala, vipi sisi leo ambao hata kuzuia mimba za mashuleni na ndoa za
za mkeka tumeshindwa, tuanze na jinsia.
Kwanini mtu asichaguliwe kwa uwezo ni hadi tuangalie matiti au vipara!!

Ahasnteni

Mapato ya ndani yameongezeka 177 Billion /Month 2005 hadi 390/month 2010
Kwanini bajeti ni tegemezi 40% kama tume double tax collection!!!
Je thamani ya shilingi dhidi ya sarafu nyingine imebaki pale pale? Kama 2005
exchange rate ilikuwa 1000/dollar leo ni 1500/dollar utawezaje kusema
umekusanya zaidi? hapa nitatoa mfano, kama 2005 serikali ilikusanya Sh bilion
1 kwa mwezi hii ni sawa na dollar million 1. Leo Kama serikali inakusanya sh Bil
1.5 kwa mwezi ni sawa na dollar milion 1. Hapa kuna ongezeko kweli?
Kula tano
[18] Kuongeza ushiriki wa wanawke kutoka 30-40% bungeni na nafasi za utendaji
Hivi tatizo la mtanzania ni jinsia au umasikini!! kama kuna wanawake wanaweza
kuna tatizo gani wakiwa wote katika wizara moja, as long as they can deliver!!!.
Je kuchagua wanawake au wanaume kwa kuzingatia jinsia kunamuondolea vipi
dhiki na adha yule mzazi anayejifungulia sakafuni. Je kuna data gani zinazoonye
sha kuwa usawa wa jinisia unaleta maendeleo.
Kula tano zaidi
 
(q) Kuandaa programu ya kupunguza matumizi ya umeme hususan viwandani
na majumbani.
(r) Kufufua na kupanua mitambo ya TPDC ya kusafishia mafuta na
kuhakikisha kwamba mitambo hiyo inafanya kazi wakati wote.

(s) Kuwa na mpango wa kuhimiza matumizi ya nishati mbadala ya jua, upepo
na fungamotaka (biogas).

Ilikufaje???? si serikali hii hii ya CCM ndio iliyoua hii mitambo?

Pale Ruvu JKT mwanzoni mwa miaka ya themanini enzi za Colonel Makame (wakati huo kabla hajapanda hadi kuwa mkuu wa JKT) tulikuwa na grupu la maafande (green kwanja) wakatili kweli kweli. Wakati wa kwenda kula kule usawa wa Mess, walikuwa wakitupeleka kwa ngarambe ngarambe sana ila tunapokaribia usawa wa guduria na kuanza kutelemsha appetite zetu, jamaa wale walizowea kutugeuka na kudai eti "tumeanza kutembea kiraia" na hivyo kurudishwa tena usawa wa kombania kwa ngaramabe ngarambe kali ili tukaanze tena safari upya. Hadi inapofikia ukaruhusiwa kuchungulia kwenye lile pipa la ugali wa dona, unakuwa hata ile hamu ya kula chakule kile imekwisha kabisa.

Naona sasa serikali hii ya CCM sasa imekuwa nayo inatuongoza kama hao maafande wa Green Kwanja. Wanatupeleka kwa ngarameb ngarame kwenda usawa wa maendeleo kwa kukoseshwa mahitaji ya muhimu kusudi serikali ifanye jambo fulani, jambo hilo likikaribia tu kukamilka wanawarudhsiaha nyuma tukaanze tena upya. Kibaya zaidi ni kuwa angalau wale maafande walikuwa wakiturudisha nyuma bila kuhamisha chakula, hata kama tungecheleweshwa vipi bado tulikuwa tunakikuta chakula kile kile. Hawa CCM wanaturudisha nyuma, na kuwapa "Wawekezaji" kile chakula tulichohenyea, halafu baadaye wanataka tuanze tena safari nyingine kutafuta chakula kingine wakati hatuna uhakika kama kweli chakula kitapatikana.
 
Wakuu,
Ilani imejaa vichkesho na maswali mengi zaidi ya majibu.
Nina mifano michache tu kutoka ilani hiyo:
[9] c: Kufanya mapinduzi ya viwanda.
Mapinduzi yapi wakati Mwl aliacha viwanda 450 na sasa vimekufa.
Hivi ni kwanini Mutex,Mwatex,Tanganyika Packager, etc vimekufa ili hali kila
resource inapatikana hapa nchini. Hivi mapinduzi gani yatafanikiwa ikiwa
tumeshindwa kuendesha shirika la reli na Tazara ambazo hazina ushindani
Mapinduzi gani kama hatuwezi kusindika hata machungwa eti mpaka yaende nje.
Mapinduzi gani wakati General tyre inakufa kwa kuagiza mitumba ya tairi.
Kabla ya kutueleza mapinduzi ya viwanda watueleze vilivyokuwepo vilikufaje!

[13] a: Uchumi umekuwa 6.7, 2010 ukilinganisha na 4.5, 2005
Kwanini nchi imeendelea kuwa na bajeti tegemezi 40% ?
Kwanini urari wa mapato na matumizi umeongezeka [fiscal deficit]

b: Mapato ya ndani yameongezeka 177 Billion /Month 2005 hadi 390/month 2010
Kwanini bajeti ni tegemezi 40% kama tume double tax collection!!!
Je thamani ya shilingi dhidi ya sarafu nyingine imebaki pale pale? Kama 2005
exchange rate ilikuwa 1000/dollar leo ni 1500/dollar utawezaje kusema
umekusanya zaidi? hapa nitatoa mfano, kama 2005 serikali ilikusanya Sh bilion
1 kwa mwezi hii ni sawa na dollar million 1. Leo Kama serikali inakusanya sh Bil
1.5 kwa mwezi ni sawa na dollar milion 1. Hapa kuna ongezeko kweli?

[18] Kuongeza ushiriki wa wanawke kutoka 30-40% bungeni na nafasi za utendaji
Hivi tatizo la mtanzania ni jinsia au umasikini!! kama kuna wanawake wanaweza
kuna tatizo gani wakiwa wote katika wizara moja, as long as they can deliver!!!.
Je kuchagua wanawake au wanaume kwa kuzingatia jinsia kunamuondolea vipi
dhiki na adha yule mzazi anayejifungulia sakafuni. Je kuna data gani zinazoonye
sha kuwa usawa wa jinisia unaleta maendeleo.
Nafasi za ubunge na udiwani zimesaidia vipi kutatua tatizo la mimba mashuleni.
Tutawezaje kuwa na uwakilishi sawa endapo watoto wa kike wanaozwa wakiwa
mashuleni. Je si kweli kuwa nafasi hizi zimekuwa zikitumiwa na watu waliomo
ndani ya sytem kupenyeza watoto na wake zao kwa kisingizio cha usawa wa
jinisia.!!!
Tujiulize,mbona kule India,marekani, Uk, ambako kuna wanawake wamekwenda
shule hasa,mbona hawajafikia usawa wa jinsia hata baada ya miaka zaidi ya 100
ya kujitawala, vipi sisi leo ambao hata kuzuia mimba za mashuleni na ndoa za
za mkeka tumeshindwa, tuanze na jinsia.
Kwanini mtu asichaguliwe kwa uwezo ni hadi tuangalie matiti au vipara!!

Ahasnteni

Mkuu nakuvulia kofia. Unaona mbali.
"Tujiulize,mbona kule India,marekani, Uk, ambako kuna wanawake wamekwenda
shule hasa,mbona hawajafikia usawa wa jinsia hata baada ya miaka zaidi ya 100
ya kujitawala, vipi sisi leo ambao hata kuzuia mimba za mashuleni na ndoa za
za mkeka tumeshindwa, tuanze na jinsia.
Kwanini mtu asichaguliwe kwa uwezo ni hadi tuangalie matiti au vipara!!"

Jambo hili ndilo limemchukiza Mwanahalisi hadi kuandika ile makala yenye utata kuhusu SS
 
Unajua Kichuguu nchi yetu haina wachambuzi wa mambo ya kitaifa hata waandishi wa habari wanakimbilia kuandika matukio ya siku hiyo. Kama ulivyosema ukiangalia kweli kwenye
ilani ya 2005-2010 uchumi ulikuwa hadi asilimia 6.7
ilani ya 2010-2015 uchumi unatarajiwa kukua kutoka 4.5% hadi 6.7% inamaana kama 2010 ulikuwa 6.7% na 2015 utakuwa 6.7% kwa hiyo tusitegemee uchumi kukua au ile asilimia ya 2010 walikuwa wanatudanganya. Sasa tuchukue lipi uchumi wetu ulikuwa asilimia ngapi mwaka 2010 4.5? au 6.7? ilani ipi nasema ukweli. Angalia tena hii mazingaombwe

Hii maana yake nini, ni kuwa lengo la 15% lililowekwa na ilani ya mwaka 2005-2010 halikufikiwa sasa lengo hilo hilo la 15% limewekwa tena na ilani ya 2010-2015 na hata hivyo hawana uhakika kama mwaka 2015 litafikiwa, kwa maana hiyo inawezekana ilani ya 2015-2020 ikarudia tena lengo hilo hilo hadi lifikwe mwaka 2020 na kuendelea.

Ndiyo maana kuna wakati Mkapa alikiri kuwa Ilani ya CCM haitekelezeki ni mazingaombwe. I come to a conclution that ushindi huwa hauletwi na uzuri wa ilani is how campaign is organized.

Finally, Tanzania hatuna wadadisi wa mambo tuna wadadisi wa matumbo mradi waonekane TBC 1, vile vile hatuna waandishi wa habari tuna ma reporter wa matukio kitu ambacho hata mtoto wangu wa miaka mitano huwa anakifanya kwa sababu kila nikirudi kazini angalau huniambia tukio moja lililotokea, leo majirani wetu walikuwa wanapigana. Uandishi huanzia pale unapoletewa tukio na sio kutubandikia picha ya tukio gazetini na kuiita habari.

Ndugu zangu Hivi kwanini tusiamini Kuwa CCM wana copy na kupest hizi ilani...Haiwezekani Jamani tunadanganywa tuuuu kila kukicha...SAFARI HII HATUDANGANYIKI yani nakupa big up Luteni haya ndo mambo yakuzungumzia siyo siasa za ushabiki lets work on reality
 
katika aya ya mwisho number 226 kuna haya " Inawezekana kujenga Maisha Bora kwa kila Mtanzania na
Tanzania yenye Neema Tele kama Uongozi wa sasa wa Chama utabadilika kiutendaji, kimsimamo na kimtazamo."

Kwa ufupi ni kwamba uongozi wa sasa sasa wa Chama (Mwenyekiti Kikwete na team yake) unatiliwa mashaka kama unaweza kubadilika kiutendaji. Maisha Bora kwa kila Mtanzania na Tanzania yenye Neema Tele tanzania hayawezekani kwani kuna utata na viongozi wa sasa wa ccm kuweza kubadilika kama ilani ilivyojieleza...:becky:
 
Leo nimeamua kupitia zote ya 2005-10 alafu 2010-15 kwa haraka haraka zote hazina YALIYOMO wala TAMATI na wameshindwa hata kuilembesha na bendera ya chama pale front page.
CCM nchi imewashinda ata uandishi nao tabu KHAAAAAA
Sijui kilichomo ndani kitakuwaje?Ngoja niichambue pamoja na ya CHADEMA
 
Back
Top Bottom