Ijue Epoxy Metallic floor, style ya kisasa ya floor!

Powder

JF-Expert Member
Jan 6, 2016
4,417
5,441
Wakuu katika kucheki kwangu fulsa mtandaoni nikakutana na hiyo kitu tajwa hapo juu, as a Professional painting artist, nilipendezwa Sana na kazi za Sanaa zinazofanywa ndani yake, ikapelekea niwe registered kwenye madarasa tofauti online na hatimaye kuhitimu, Epoxy Metallic floor color Ni mchanganyiko Maalumu wa rangi special kwa ajiri ya floor, ambapo rangi huchanganywa na Chemicals mbalimbali kuhakikisha inakua strong kwa muda wote, Kuna hatua 3 mpaka 4 za Ku apply Epoxy floor mpaka kazi kukamilika, pia Epoxy imegawanyika kulingana na matumizi, Ipo Epoxy kwa ajiri ya Garages, Sitting rooms, Bed rooms n.k, Epoxy huleta muonekano usio kifani na mng'aro wa ajabu, ambapo baada ya Ku apply primer, then Epoxy basement color, baada ya hapo unaweza Ku apply style yoyote ya painting unayotaka, then mng'ao unaletwa na epoxy Metallic iwe Ni natural ama colored, Maelezo Ni mengi Wadau, tupeane hizo kazi tupendezeshe floor za majumbani mwenu Wakuu! Karibu kuuliza chochote na ukiwa interesting usisite kuni inbox.

NB:Unawenza kutengeneza popote hii floor, Hotel, Night Club, Majumbani, Garages... Sehemu ambapo jua halifiki, zipo Epoxy automatically uki apply inatengeneza Urembo mbalimbali, Ni pia ukipenda Una apply mwenyewe michoro.
wp_ss_20160426_0014.png
wp_ss_20160426_0020.png
wp_ss_20160426_0022.png
wp_ss_20160426_0024.png
wp_ss_20160426_0025.png
wp_ss_20160426_0026.png
wp_ss_20160426_0027.png
wp_ss_20160426_0028.png
wp_ss_20160426_0029.png
wp_ss_20160426_0018.png
 

Attachments

  • wp_ss_20160426_0015.png
    wp_ss_20160426_0015.png
    202.1 KB · Views: 179
Hayo ndo maajabu ya Epoxy ambako huko Duniani, watu hawaangaiki tena na tiles! Hapa Bongo imefanyika sehemu chache hasa kwenye Mahotel makubwa, ambapo Wataalam walitoka nje ya nchi!
 
Mkuu inakuwaje hii, hebu idadavue zaidi...
Ubora wake, uimara na gharama yake vikoje ukilinganisha na tiles
Mkuu kuhusu ubora ina ubora wa kutosha kabisa, hii Una apply baada ya kuweka floor ya kawaida ikiwa imepigwa Niru, baada ya hapo unaanza na Primer, Primer yake Ni very strong ambayo inatengeneza uhusiano Kati yake na floor ya Cement, actually ina gharama kuliko tiles, nikitulia ntaweka hapa cost zake!
 
Nipe email yako mkuu ama namba yako ya simu, sehemu naweza kukupata nk
 
Mkuuu tunasubiiri gharama zake
Samahani kwa kuchelewa kuweka gharama hapa, Ni kutokana Na pilika za maisha, sasa nipo tayari, nataka nitumie lugha Na hesabu nyepesi kabisa Ili nipate kueleweka.....
Tuchukulie may be Sebure yako Ina ukubwa wa 120 square foot, ambapo Ni ukubwa wa wastani wa sebure nyingi, Materials cost itakua wastani wa 500,000
huku gharama za ufundi zikiwa wastani wa 700,000.

Hivyo ndo tuseme gharama zote kwa 1 Square foot Ni sawa Na 10,000.....kama ukubwa wa kazi yako unazidi Square foot 300 labda 500 ama 1,000 pia ntakupunguzia Na gharama kwa maana itakua chini ya 10,000 kwa square foot.


Kama sehemu yako inahitaji michoro tunaita broadcasting basi itategemea Na mchoro unaotaka, Kama Ni logo ya kampuni, hotel ama media house Na unataka ionekane kwenye floor pale mtu anapoingia Tu ndani, hivyo vyote Ni makubaliano, ama Ni michoro flani unataka ionekane kwenye floor za Lounge ama Night club au hata Sebureni vyote Ni kuelewana coz inategemea Na mchoro ama painting style unataka...

siwezi kumchora Mungu Tu vile sijawahi muona otherwise chochote unachotaka tunakifanya kwenye floor! Naimani mtakua mmepata picha, karibuni kwa maswali!
 
Nipe email yako mkuu ama namba yako ya simu, sehemu naweza kukupata nk
Mkuu niandikie kwa email hii..
trechian@gmail.com
au Nipigie kwa 0714417641 pia Whatsapp
utanipata kwa namba hiyo, hata kwa ushauri kuhusu Wall painting style mnakaribishwa. Coz Mimi nimebobea upande wa rangi, iwe Ni wall painting, paintings artwork Na sasa Epoxy Metallic floor painting! Na hata kufanya decorations mbalimbali, Karibu!
 
Mkuu Bill nimeweka tayari
Mkuu inakuwaje hii, hebu idadavue zaidi...
Ubora wake, uimara na gharama yake vikoje ukilinganisha na tiles
gharama zake hapo juu post #12, kama utakua na swali lolote usisite kuuliza!
 
Wakuu toka nimeweka bandiko hili nimepokea simu nyingi Sana toka kwa wadau ambao wamekua interesting na hii Epoxy Metallic floor designing, wakiuliza maswali mbalimbali, SI vibaya Niki share yale ya muhimu ambayo sikupata nafasi ya kuyaainisha pale juu.

Kwanza floor ambayo inatakiwa kuwekwa hii Epoxy Ni lazima iwe katika quality iwe strong iwe level, na muhimu lazima nije site kukagua kuona kama inafaa Ku apply hii Epoxy, kumbuka Epoxy inakua separated kwa Materials aina mbili, then yanatakiwa yawe mixed 15-20 mins kabla ya matumizi, yanapokua mixed ndo yanapotengeneza ule u strong ambao unaizidi Cement, sasa kama floor ya Niru haipo strong, floor ambayo inaweza kutobolewa na Sisimizi, then uka aaply hii Epoxy, kwa ile nguvu ambayo iko nayo baada muda inabandua Niru, Niru inauumuka, so make sure Floor yako Ni strong enough kuweza kuhimiri hii Epoxy!
 
Pia niliulizwa inawezekana Ku apply Epoxy kwenye flloor ambayo Ina Tiles? Jibu Ni Ndiyo, unaweza Ku apply Epoxy juu ya tiles, isipokua Kuna maandalizi yanafanyika ikiwemo kuondoa ule u smooth juu ya tiles na kuziba nyufa na matundu yote kabla ya Ku apply Epoxy!
 
Pia wadau waliuliza kama kunaweza kuwa na unafuu wa bei, tatizo mpaka sasa, Tanzania hakuna Kampuni ya rangi inayotengeneza hii Epoxy Metallic Materials, naagiza nje South Africa ambapo kuna kampuni nyingi zinatengeneza, na Kenya ambapo kuna kampuni moja tu, so gharama za kununua Materials haya na shipping cost yake inakua kubwa, ndo maana bei yake inakua juu kidogo!

Kama utakua na swali usisite kuuliza, iwe kupitia hapa au kwa namba ambazo nimeweka hapo juu ama email! Karibuni.
 
Back
Top Bottom