Igunga: Sikubali matokeo

ukubali usikubali, CCM inasonga mbele. Wewe utabaki na upuuzi wako.
 
Uchambuzi mzuri! Hii inchi inasikitisha kwakweli; yaani wameona watz wote ni wajinga au hawana kitu wanachoweza fanya!
 
Aisee you must be genious? hilo nalo neno linahitaji tafukuri kwa mgombea wa CUF?


Mkuu hakuna cha mungu yupo hama hayupo mungu siku zote yupo,kubali kushindwa cha msindi cdm jipange vyema l
kisera mbele ya wananchi na si kulalamika hovyo bila sababu za msingi
 
Salama2015, You have proved that you are really a great thinker. Kwa uchambuzi uliouweka, ni yule tu ambaye Mungu wake ni tumbo, na akili zake ziko tumboni, anayewaza kula na kushiba tu, ndiye atakayepinga uchambuzi wako.

Asante, you have said it all.
 
sasa hlkpa igunga basi mtazisikia kwenye tv tu watu wamesha chukua vyao mapema sasa wanapanga mipango na matumizi
 
CDM, CCM hata CUF wanaweza kukubali matokeo, ni mtazamo wa nia zao. Ila Mimi kama Mtanzania wa nchi inayodai ni huru tena ya kidemokrasia.. SIKUBALI WALA KUAFIKI Matokeo ya Uchaguzi wa jimbo la Igunga kwa sababu hakukuwa na uchaguzi bali UCHAFUZI. nasema haya kwa sababu kuu tatu.

Sababu ya Kwanza:

igunga3.jpg


Tume ya Uchaguzi IGUNGA, kwa kitendo ambacho wanakiri wazi kwamba waliwatumia wajumbe wa nyumba kumi, kuorodhesha majina ya wananchi wao wenye shahada za kupigia kura, kitendo ambacho kiliendana na kaulimbiu yao ya kujua idadi halisi ya wapigakura ili kujiepusha na mamluki, na wajumbe wa nyumba kumi, maskini ya mungu wasiojua lolote wakatekeleza agizo kwa bidii, na mbaya zaidi wakaelekezwa kuainisha wapigakura wa CHADEMA na CUF, na wakafanya kazi yao barabara. Kisha wenyeviti wa vijiji na sekretariat zao, wakachukua jukumu la kufanya dislocations kwa wapigakura ili wawapangie vituo vya mbali washindwe kwenda huko kwa visingizio kwamba wamehamia vijiji vingine. na mchezo huo ilifanyika sana maeneo ya vijijini, takriban wapigakura 16,000 wameathirika na kadhia hii. kuna mifano ya vijiji vingi na wapigakura wengi wamepata kadhia hii. mfano kata ya Nkinga..

Mpiga kura wa kijiji cha Mwazumbi kwenye kata hiyo, ambaye siku zote amekuwa akipigia kura kwenye kituo kilicho katika shule ya msingi Mwazumbi, leo anaambiwa Jina lake liko kituo cha shule ya msingi Njiapanda ambacho ni kijiji kingine, na kutoka hapo alipo kwenda huko ni mwendo wa masaa matano kwa mguu.. maskini wale hata baiskeli hawana, vyombo vyao vya usafiri ni kama unavyoona baiskeli hiyo ya miti. mwenye baiskeli ya mchina ni tajiri sana kijijini, sasa kwa mantik hii unategemea atatoawapi moyo wa kwenda kupiga kura huko masafa marefu, ambapo pia hana uhakika kama jina lake ataliona, ni uonevu wa hali ya JUU.. nauliza nani atakubali??

Sio najitetea bali hata dhamira yako inakubaliana na hili?? Tusishabikie vyama tu, embu tuwe na UTU.


Sababu ya Pili:

udini3.jpg

Uchaguzi umegubikwa na karata ya Udini ambayo imedhoofisha Demokrasia inayoanzia kwa mtu. Ni Chama na wanachama wa chama Fulani ndio wanaoweza kuwahamasisha wananchi wasikiunge mkono chama fulani na badala yake wakiunge mkono chao kwa sababu kadha wa kadha. Lakini Dini, Makampuni, Serikali, sekta za watu binafsi, Vikundi vya kijamii NGO, CBO, FBO na vinginevyo, Mashule na Vyuo, Lazima visiwe upande wowote.

Ni kweli kwamba followers wa kikundi, Dini au makampuni wanaweza kuwa na Upenzi binafsi wa Vyama Vyao. Sasa Viongozi Husika wanapotoa AMRI na maelekezo kwa followers wao, ni kukiuka misingi ya Demokrasia, Kukiuka misingi ya haki ya raia kuchagua anachokipenda, Unyanyasaji wa kiimani. Ni kweli wale wenye mtazamo na akili timamu hawatababaishwa na misimamo hiyo kwa sababu hata CHADEMA ina waislam wabunge zaidi ya kumi, sasa unapotoa tamko waislam waogopeni CHADEMA kama UKOMA, unamaanisha hata wale Wabunge walioko Ndani ya chama hicho wajiondoe?.. Then Chama kibaki na nani? Wakristo.. oke na wakristo walioko vyama vingine wahamie CDM, sasa itangazwe vyama vya kidini!! Watanzania hawako hivyo, wala kitu kama hiyo ni ngumu kutokea kwa sababu mkristo kamwoa muislam, na wanapendana na kuishi pamoja.. sasa kutoa matamko kama hayo ni hatari..

Kundi kubwa la watu limenyanyaswa, kuathirika na kukosa haki zao za mapenzi ya chama wanachokitaka kwa kuhofia wakienda kinyume na viongozi wao basi watasomewa Duwaa na hali zao zikawawia mbaya.. dini zina nguvu mtu asikatae.. sasa kwa mantik hii.. utaniambia wa Igunga ni Uchaguzi au Uchafuzi?. Ingepaswa Serikali isimamie Kuondoa kadhia hii lakini nayo imekaa kimya na kuruhusu uchaguzi ufanyike kwenye mazingira hayo. So na wao wamekubaliana na hili, tukisema walilipanga kwa hofu yao ILIYOPITILIZA ya kuhofia kulipoteza jimbo tutakuwa tunakosea?.


Sababu ya Tatu:

MAGUF.jpg

Na Mwisho, Kwa kuwa Serikali Inaongoza watumishi chini yake, watumishi wa serikali, taasisi na mashirika ya umma ambayo ni kama Injini ya Ujenzi wa taifa. Na humo kuna watu wa Vyama vyote, Dini zote na halikadhlika. Kwa hiyo Basi, na kiongozi wa serikali anatakiwa kuwa Muadilifu asiye egemea Upande mmoja na kudhoofisha upande mwingine. Chama hushika HATAMU ila SERIKALI INAONGOZA. Ndio maana Bunge lina matawi matatu, Wabunge (ambao ni wawakilishi wa wananchi kupitia vyama mbalimbali), Mawaziri (kama watendaji wa serikali walioajiriwa na wananchi) na Spika(kama mwenyekiti wa majadiliano kati ya wananchi (wabunge) wanaomuuliza waliyemwajiri (serikalikupitia mawaziri) ajieleze kuhusu kile wanachokitaka kupitia katiba yao) kwa maana hiyo, Kiongozi wa serikali hatakama anatokea chama fulani cha Upinzani, ila kwa madaraka aliyonayo yeye ni kiongozi wa wote sasa, hawezi hadharani akajitokeza kuonyesha upenzi na ukereketwa wake kwenye chama chake. Kitendo ch Mhe Magufuli, kama waziri mwenye dhamana ndani ya serikali, kutoa matamshi kwamba atakitumia kiti chake kama waziri, kumsaidia kiongozi wa chama chake atapochaguliwa ili awaletee maendeleo ni ubaguzi mbaya kabisa. Akaenda mbali zaidi na kutamka waziwazi kwamba msimchague kiongozi ambaye hawezi kufika ofisini kwangu moja kwa moja. Ni matamshi makali na mabaya kuwahi kutokea. Kwani yeye anaongoza serikali ya wana ccm au watanzania.?

Ndio maana kwa nafasi yake kama Waziri asingepaswa kujiingiza kwenye kampeni. Kikubwa zaidi Raisi mwenyewe kahusika kwenye kupiga kampeni.. katibu mkuu wa CCM Wilson Mukama pamoja na Wasira Stephen, kwenye mikutano yao hawakusema mwenyekiti wa Chama katutuma tumpigie Debe kafumu bali walitamka waziwazi RAIS ametutuma, na Rais mwenyewe hakukana.. Hakuna uchaguzi wa namna Hii.. ni Uchafuzi..
Mimi binafsi SIKUBALIANI NA MATOKEO nataka makosa haya yawekwe mezani, yarekebishwe yote na UCHAGUZI URUDIWE..

Kama mwananchi wa kawaida ila mzito sana serikalini naweka shilingi
Mkuu sababu ya kwanza siku zote ndo janja ya Magamba.
hata uchaguzi mkuu ilitumika hiyo kuwakatisha tamaa watu kwa kuhamishwa vituo na matokeo uliyaona.
toka 20mil mpaka 8mil ndo ilipiga kura.
na waliokomaa mpaka kikaeleweka nao waka wachakachua pia.
 
kazi Tuliyo nayo mbele yetu ni kubwa na nzito, tunawajibika kuikabili kunusuru kizazi chetu kitachofuata..
 
Back
Top Bottom