Elections 2010 Igunga: Mbunge kunywa sumu CCM ikishindwa

Sasa ndugu zangu CCM huyu mbunge anaongeza kura za CCM au anapunguza?jiulize anawambia hivyo watu wa uelewa gani...!kwa akili zangu ndogo tena sie watu wa vijijini tunajiju, mtu akisema kitu fulani kikitokea atafanya hv, kwa desturi zetu sie wenye uelewa mdogo ndio tunafanya hivyo ili tuone atakunywa sumu kweli au..???CCM inahitaji watu makini kwa mwendo huu haaa sijuii

Source:Tanzania daima.

Ukiwa na mbunge mwenye akili kama hizi unategemea nini? Nimegundua bora mara mia Mzee Malecela,kwa hakika hapa Mtera mmeruka mkojo mkakanyaga mavi....
 
Huyu ni kilaza mkubwa na hili ndio tatizo lake kubwa,elimu yake kaishia la nne tu ndio maana hajui kujenga hoja kazi yake ni kupayuka
 
Si ameshapewa taarifa ya kiasi cha vitambulisho vya mpiga kura vilivyonunuliwa mpaka sasa na vilivyoorodheshwa na wenyewe kutishwa mkiwapigia upinzani tutajua namba zenu tunazo.
sasa hukounakotaka kufika kwa hisia potofu ndipokunako watisha watanzania na kutokupigia kura chama chenye vitisho na ubabe ubabe.​
 
Jamani Living stone Lusinde Babo ana fikra za zamani..!

KAMPENI za uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga, zimezidi kupamba moto baada ya Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), kujiapiza mbele ya wananchi kuwa atakunywa sumu iwapo chama hicho kitashindwa kwenye uchaguzi huo.

Akizungumza na wanakijiji wa Ugaka kwenye kata ya Nkinga wilayani hapa wakati akimwombea kura mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu, Lusinde alisema kutokana na mwenendo mzuri wa kampeni za CCM na jinsi wanavyowafikia wananchi, haoni sababu za kushindwa kwenye uchaguzi huo.

“Hapa nimewaona waandishi wa gazeti la Mbowe (Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA); nataka mkaandike kwa namna ambavyo tumezunguka, CCM tukishindwa nakunywa sumu,” alisema na kuongeza:

“Nataka tuwaambie, tutawapiga bao la mbali kabisa na huyo Dk. Slaa sisi tunammudu ndiyo maana tukamwambia Mzee Kikwete, endelea kuongoza nchi atuache vijana tumkabe koo maana yule mzee ni mnafiki mkubwa,” alisema Lusinde.

“Kale kazee kagonjwa kale, ndiyo maana nimekuja kuwaambia inawezekana viongozi wa CHADEMA wanavuta bangi, zile bangi zile, haiwezekani unatembea nchi nzima unahamasisha vurugu, unatangaza vita,” alisema Lusinde Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.

Kwa upande wake mratibu wa kampeni hizo, Mwigulu Mchemba, aliwataka wananchi hao kumchagua Dk. Kafumu na kusema wanasiasa wa upinzani wanasema tangu uhuru serikali ya CCM haijafanya kitu kabisa, Igunga haijapata maendeleo wakati si kweli.

“Wenzetu wanapandikiza chuki kwa vijana wa vyuo vikuu nao wanakubali kupotoshwa na wanasema serikali ya CCM haijafanya kitu si kweli. Kwanza idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu imeongezeka halafu wanasema Rais huyu hajafanya kitu, kama si kulaaniwa ni nini?” alihoji.

Alisema wapinzani wanatumia umaskini wa wananchi kama mtaji wa kisiasa, wamelalamikia kupandishwa kwa bei ya pamba ili watu wakasirike na kutoichagua CCM.

“Wacha niwaambie wakati wa ukame serikali ya CCM iligawa chakula jimbo lilipokuwa wazi wakasema tusigawe chakula eti hiyo ni rushwa sasa tusipogawa chakula mtatuchagua? Hivi njaa ina likizo? Kwa nini serikali ipeleke chakula mpaka Somalia lakini Igunga ibaki na njaa hivi mtapiga kura mkiwa na njaa?” alihoji Mwigulu.

Nahisi harufu ya uchaguzi mdogo Mtera.
 
Hapo angekuwa ni wa CDM katoa kashfa kama hizo angekamatwa na kuwekwa ndani,lakini kwa kuwa ni CCM lazima apongezwe na kupewa donge nono,HUO NDIO UONGOZI WA CCM ULIVYO.
 
Wana Mtera wamekula hasara kwa kweli...afadhali wangebaki na Mzee Chigweyemisi!
 
Tumuombee huyu dogo ibilisi wa kifo aliyempanda aondoke ili asife kweli. Hata hivyo kilichomfikisha katika miropoko hiyo ni msongamano wa mambo mengi, elimu yake ndogo, cheo kikubwa cha ubunge alichopata, nafasi ya ujumbe wa NEC aliyotunukiwa na kubwa zaidi kuwa na uwezo wa kupata fedha nyingi kupita mahitaji yake bila kutegemea. Amezuzuka huyo, tumuombee apate busara.
 
Eti nae huyu ni kiongozi wa umma. Kweli sasa kama taifa tunaelekea kubaya. Huu ni urithi mkweli kama kiongozi? Hapa bwana sasa siasa imeingiliwa na makanjanja. Huwezi pata uongozi bora kwa kutegemea vijana kama hawa. Hapa tusubiri tu kupata bora viongozi. Nimeshangazwa sana kwa kumsikia huyu kijana akiropoka pumba kama hizo tena isitoshe kwenye ummati wa wananchi.

Tumekwisha kabisa kama chama na taifa kwa ujumla. Jamani tuchukue hatua!
 
TAREHE 3/10/2011;
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinapanga kumsimamisha Kamanda Chakaza kuwania kiti cha ubunge Mtera kilicho achwa wazi na Marehemu Lusinde (RIP) aliyejitoa uhai wake kwa kunywa sumu isiyofahamika kutokana na ushindi wa Bw Kashinde ktk uchaguzi mdogo wa Igunga. Marehemu Lusinde alikunywa sumu hiyo kutimiza ahadi yake ya dhati aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi Igunga wiki chache zilizopita.
Wananchi wengi wamempongeza Marehemu kwa kuonyesha mfano bora wa kiongozi kutimiza ahadi zake anazozitoa kwa wananchi. Gazeti hili nalo linampongeza kwa dhati marehemu.

Source; Gazeti la Uhuru
 
Unajua wakuu mmekuwa mkisingizia sana eti mtu akiropoka pumba basi anaambiwa elimu yake ni ndogo. Naomba kuuliza hivi kila mwenye elimu kubwa huwa anaongea na kutenda mambo ya maana?

Hapa mnafanya dhambi ya ubaguzi na sichelei kuwaita asilimia kubwa ya wana JF ni makaburu. Kwa nini tusimhukumu mtu kwa uwezo wake tu wa kufikiri na si kusema eti tatizo ni elimu ndogo. Unajua elimu si tu ile ya kuhudhuria madarasani na kupandishwa vidato.

Mtu waweza kuelimika kwa busara zako tu mungu alizo kujaalia. Jamani acheni ubaguzi kwani hamtutendei haki wengi wetu kwa kuwa tu eti hatujasoma. Mbona hata waliosoma wanaropoka tu mambo ya ovyo?

Kuna hata maprof, madakt, na hata mainjinia. Au mnabisha hakuna wasomi wanaoropoka? Au ndio kunya anye kuku akinya bata ameharisha. Acheni hizo bwana huyu Mh Livingstone ni ulevi wake tu ndio unamfanya aropoke hivyo kwa kuwa anakumbatiwa na CCM.
 
...KAMPENI za uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga, zimezidi kupamba moto baada ya Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), kujiapiza mbele ya wananchi kuwa atakunywa sumu iwapo chama hicho kitashindwa kwenye uchaguzi huo.

Akizungumza na wanakijiji wa Ugaka kwenye kata ya Nkinga wilayani hapa wakati akimwombea kura mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu, Lusinde alisema kutokana na mwenendo mzuri wa kampeni za CCM na jinsi wanavyowafikia wananchi, haoni sababu za kushindwa kwenye uchaguzi huo.
Sasa kama anaamini CCM itashinda, anaomba kura za nini?
 
Jaman naomba mnijuze. Huyu lusinde si ndo alisema alipata zero na Wenje akamtolea mfano bungen kwa waliofelishwa na ccm au?
 
Naomba Lusinde akapimwe akili, nahisi Mtera wanaongozwa na Mwehu.
 
Tangia nimeanza kumsikia huyu jamaa, sijaona siku ametumia kichwa kufikiri. Ni Mimasaburi tuuuu Masaburi tuuu! Hivi huko ugogoni hakuna mtu mwenye akili kuwakomboa wenzie maana Malecela ndo Mafisadi wameshamdhibiti. Hili ni zaidi ya Litakataka.
 
Sasa ndugu zangu CCM huyu mbunge anaongeza kura za CCM au anapunguza?jiulize anawambia hivyo watu wa uelewa gani...!kwa akili zangu ndogo tena sie watu wa vijijini tunajiju, mtu akisema kitu fulani kikitokea atafanya hv, kwa desturi zetu sie wenye uelewa mdogo ndio tunafanya hivyo ili tuone atakunywa sumu kweli au..???CCM inahitaji watu makini kwa mwendo huu haaa sijuii

Source:Tanzania daima.

Malalamiko kila mdomo, viongozi, wanachama, wafuasi na gazeti. Chadema kazeni buti kulialia hakuzalishi kura!
 
To commit suicide or attempt to commint suicide ni kosa la jinai. Je Polisi wako wapi kumtia mbaroni huyu Lusinde aliyetishia kujitoa roho yake.Nafikiri wananchi wa Igunga sasa mmepata sababu tosha ya kuichangua CDM, ili tuone kama huyo Lusinde atatimiza ahadi yake ya kujiua.
 
Zamani kuna Watu walikuwa wanawekeana dhamana kwenye mpira hususan washabiki wa Simba na Yanga, kwamba kama mtu timu yake ikifungwa atatoa "Masaburi" kwaMpinzani wake. Huenda huyu kijana alitoa ahadi hiyo kwa Wasira ili apate nafasi ya kwenda Igunga kwamba wakishindwa atampa Masaburi. Sasa hali aliyoikuta huko imemkatisha tamaa kwa hiyo anaona ni bora afe wakishindwa kuliko kukutana na dhahama ya "Mzee Pono" ambaye hata dhana za China zilizorudishwa na South Africa kwamba ni ndogo kwa "Mzee wa kuuchapa usingizi" ni Chamtoto. Sasa anawaza atammudu vipi! Anajutia ahadi yake ya awali. Hizi tamaa za pesa za kwenda Igunga ndizo zinazomtesa dogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom