Ujengelele
JF-Expert Member
- Jan 14, 2008
- 1,253
- 22
Harakati za kujipatia ushindi wa kishindo zimeendelea leo baada ya mgombea urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi kumnadi mgombea ubunge huko igunga kwa tiketi ya ccm mh. Rostam Aziz, asema ni mtu safi anasingiziwa!
Lini Kikwete amekuwa hakimu mpaka aseme fisadi huyu anasingiziwa? kama alijua anasingiziwa mbona hakumfikisha mahakamani ili kujibu tuhuma dhidi yake na kuacha sheria ifuate mkondo wake? Mafisadi wote alikuwa anawaogopa akina Chenge, Yule aliyekuwa MD wa tanesco, Karamagi, Lowassa, Mkono na wengineo. Kama alikuwa anajua kuna ushahidi wa kuwaweza kushinda kesi zao basi angeruhusu wapandishwe kizimbani, vinginevyo kauli zake hazina mvuto wowote na zinathibitisha kwa mara nyingine kwamba Kikwete ni mtetezi wa mafisadi.