Igunga: Jinsi wakala wa CHADEMA alivyouliwa...

Bakwata Igunga ilikuwa njaa tu lakini wengi walipigia CDM kama hukuwa unalijua hilo basi elewa hivyo
 
Pole san mkereketwa, hii ni picha mbaya sana kwa taifa lenye tafsiri ya Demokrasia.

Ni matumaini yetu kuwa Serikali italifanyia kazi suala hili na litasimama kama kipimo cha hawa wenye dhamana.

Binafsi nimehuzunika sana na taarifa hizi ambazo kwa kila sababu serikali haikua tayari lisikike kwenye vyombo vya habari.

Ni vyema tukakubali kuwa taswira ya Taifa letu inaelekea kubaya kutokana na hali kama hizi na yamkini viendo vyingi visivyofahamika. Ndani ya chama tawala kwa sasa si salama sana kutokana na makundi.

La msingi hapa ni kuhakikisha ya kuwa hawasambazi sumu za makundi na wala hatuzikubali propaganda zao iwapo zitaonesha kulikwaza Taifa letu.

Watanzania wengi tuna imani ya mabadiliko na tukubaliane na changamoto hizi katika kuifikia demokrasia ya kweli.

Ninachoamini pia wapo makada ndani ya chama tawala ambao kamwe nafsi zao hazitawatuma kukubaliana na misingi ya ukandamizaji na ubakaji wa demokrasia kwa walaghai wananchi pamoja na wazaledo wengine.

AMANI YA TANZANIA IPO MIKONONI MWETU SOTE WATANZANIA.
 
Kipindi cha kampeni Igunga ilitokea tafrani DC akavuliwa ushungi tu CCM+ BAKWATA wakatoa matamko mengi ikiwa pamoja na kusomwa kwa dua mbaya kama Chadema wasingeomba radhi.
Sasa hili ni zito tena sana la mauaji ya ndugu yetu Masoud Mbwana aliejitolea kwenda kulinda haki ya wana Igunga, mauaji ya kutisha na ya kinyama yaliyofanywa na watu wenye nia mbaya kwa taifa letu. Sasa na hapa napo tunataka tamko na ile DUA kama ni kweli hapa ndipo mahala pake ili wahalif wajulikane na hukumu ifanyike hapahapa.

Nakuhakikishia hautapata tamko lolote toka kwa watu hao, wao huwa wanaangalia issue ambazo zinaweza zikaleta mtafaruku ndo wanakomaa nazo.afterall huyo masoud ni wa Chadema
 
Hali inatisha,icho kikaratasi kinanikumbusha kile kilichosalimika baada ya banda la kuku la mwenyekiti wa CCM kuungua,RIP shujaa wa mageuzi,ukweli utajulikana.
 
Kwa hali kama hii tunapata uhakika kwamba jeshi la polisi pamoja na vyombo vyote vya ulinzi na usalama haviko kwa maslahi ya watanzania wote.

Na ndio maana kiongozi wa ccm anaweza kusimama jukwaani mbele ya vyombo vya habari na kutangaza kwamba nchi hii ina wenyewe, na wenyewe ni ccm na asichukuliwe hatua yoyote.

Hawa ccm wanajaribu kutugawa sana watanzania, nadhani kuna faida kubwa wanayoipata kwa kuleta mifarakano na ubaguzi miongoni mwa wananchi.

Wanatumia vyombo vya dola, asasi za kiraia, asasi za kidini, viongozi wa serikali pamoja na viongozi wa kidini kutugawa watanzania kwa nia yao ovu ya kuendelea kututawala bila ridhaa yetu.

Kama jeshi la polisi linataka liendelee kuaminiwa na wananchi ni lazima libadilike, lifanye kazi kitaalamu, liache kuinyenyekea ccm, litambue kwamba nchi hii ni yetu sote na kila mmoja anastahili haki yake ya kuishi na hakuna mtu awaye yeyote anaweza kuondoa uhai wa mwenzake kwa kisingizio chochote.

Hali hii ya watu kuuawawa kiholela na jeshi la polisi kutokuchukua hatua ikiendelea namna hii, tusishangae siku moja tukishikiana mapanga, mikuki na mishale kwa ajili ya kulipizana kisasi.

Sasa, ili tusifike huko ni wajibu wa jeshi la polisi kujitenga na wanasiasa hawa wa CCM wasiothamini uhai wa watu zaidi ya mali zao na tamaa zao za madaraka.
 
Kipindi cha kampeni Igunga ilitokea tafrani DC akavuliwa ushungi tu CCM+ BAKWATA wakatoa matamko mengi ikiwa pamoja na kusomwa kwa dua mbaya kama Chadema wasingeomba radhi.
Sasa hili ni zito tena sana la mauaji ya ndugu yetu Masoud Mbwana aliejitolea kwenda kulinda haki ya wana Igunga, mauaji ya kutisha na ya kinyama yaliyofanywa na watu wenye nia mbaya kwa taifa letu. Sasa na hapa napo tunataka tamko na ile DUA kama ni kweli hapa ndipo mahala pake ili wahalif wajulikane na hukumu ifanyike hapahapa.

BAKWATA hii uwa haitoi matamko kwa mambo ya msingi na yanayogusa kwa karibu maslahi ya Taifa.....matamko yake yanasubiri uharo na majitaka fulani hivi ndio watoe tamko........tusubiri tuone!!
 
Forget it mkuu. siasa uchwara za CCM zitafika mwisho wake hivi karibuni.
mwisho wake ni lazima tutachinjana kidogo tutiane akili!

Mungu ailaze roho ya Masoud mahali pema.
 
Hakuna tamko lolote litakalotolewa hapo, labda kama angekuwa wa CCM
 
mimi siamini kama ni Tanzania nilikuwa sijasikiliza habari siku kadhaa .inauma inauma viongozi wetu tunaomba mtuongoze kwa hili.
 
Jamani ukatili huu watupeleka wapi? Unyama huo unasaidia nini?

RABI mweza wa yote atawahukumu walotenda hayo, afanyaye hayo mbaya yatamkuta tu. Amani wahubiriyo i wapi? Au ndo hiyo ya raia wema kufa bila hatia!

Wale wasema udini kwa haya yalotekea wana jipya? Tuwape pole ndg wa marehemu, la zaidi wapenda amani ya kweli tumwachie Rabi yeye ndo mweza wa yote. AMINA.
 
Na hapa BAKWATA watoe tamko kwani aliyeuwawa kikatili ni muislam aliyekwenda kulinda haki huko Igunga.
Ile BAKWATA ya DC feki tu waislamu wafike mahali wasiwe wanatumiwa vibaya na CCM.

KIKWETE AMEWATUMIA VIZURI SANA, IGUNGA MNAENDELEA KUTUMIKA KIJINGA KABISA MBONA MASOUD KAUAWA BAKWATA IKO WAPI, MPAKA MHONGWE? ACHENI AIBU
 
Waganga njaa wa magamba kwa hil wapo kimya hawa wanyonya damu wa watu,kwan kwao utu nyuma dhuluma mbele ndo kaul mbio yao hiyo.
 
Kudadeki wameniharibia kabisa mood ya kufanya kazi. Hiki chama cha Magamba kimepoteza uhalali wa kuongoza hii nchi.

Tusubiri kwanza CDM watasema nini kuhusu mauaji haya, kimsingi damu ya Mtanzania mwenzetu isipotee bure...
 
Nafikiri kuna kitu kimechelewa au tunakichelewesha
I agree, sina uhakika ni kitu gani, lakini kuna ucheleweshwaji mkubwa wa mambo.....

Where is CHADEMA here?? Mwongozo tafadhali, vyombo vya habari vipo kwa nini mnakaa kimya?

Wanafamilia kwa nini wasiwe-supported kwenda kwenye vyombo vya habari na kuelezea ndugu yao alikuwaje na wanaamini nini kwa yaliyomkuta?

Pamoja na kwamba najua CHADEMA wanashughulikia mazishi and all that, najua very few people have knowledge of this barbaric act.
 
Waache wajidanganye kwamba hii nchi ni mali yao siku ya kusema sasa basi watajuta kuzaliwa manake uvumilivu nao hufika mwisho
 
Inauma sana hii, kijana Masoud kosa lake nini mpaka atendewe unyama huu!! Hakika damu ya mtafuta haki itazaa matunda ya mageuzi.

Nape alisema hili na limetokea kweli, Green Guards washatangaza vita na vijana wataka mabadiliko. Poa
 
Back
Top Bottom