Igunga: ITV na uchakachuaji wa habari

Hawa jamaa wanaripoti CCM tu Igunga harafu wananyamaza bila aibu. tena pale tu CCM wanapokuwa wanajitahidi kujibu hoja kwa kudanganya.
 
Ni siku ya pilli leo nashangaa ITV wanaonesha CCM tu hawaoneshi vyama vingine kuna nini? Mbona hapo nyuma kilikuwa kituo kizuri cha kutoa habari? Kuna nisilolijua?
Wataripoti kitu gani cha wamwagia watu tindikali na wapiga wakuu wa wilaya?
 
Ni siku ya pilli leo nashangaa ITV wanaonesha CCM tu hawaoneshi vyama vingine kuna nini? Mbona hapo nyuma kilikuwa kituo kizuri cha kutoa habari? Kuna nisilolijua?

I don' understand! ITV ya IPP Meadia au ITV UK?!
 
Nilimnukuu Alfrd Masako akiripoti matukio ya wiki nami nilishangaa. maana niliona picha video za Chadema zikionesha anayehutubia bila kuonesha wanaohutubiwa. Ilipofika kwa CCM ikawa tofauti na lugha ikawa ifuatavyo. '.... maelefu na mamia ya waIgunga walifika kuhudhuria ufunguzi wa cpeni za CCM Igunga'. Huyu mzee wa hii TV ni opportunist sana. Nachooombea ile kesi anayodaiwa senti moja imrudi kisawasawa.
 
Hamna taarifa ya jana usiku imeonyesha vyam vyote vitatu, labda uwe hujaangalia taarifa ya habar yote. Mi nimeangalia jana ambapo dr.Slaa alikuwa akikanusha barua walioshutumiwa na ccm kuandika ikiwatuhumu kwa taarifa za uongo.
 
Ni siku ya pilli leo nashangaa ITV wanaonesha CCM tu hawaoneshi vyama vingine kuna nini? Mbona hapo nyuma kilikuwa kituo kizuri cha kutoa habari? Kuna nisilolijua?
Juzi ITV walionyesha Chadema pekee yake, jana saa 2 usiku ilianza na CCM kupitia Wassira akijibu maswali magumu (aliripoti Novatus Makunga),ikafuata Chadema kupitia Dr Slaa na Kashindye (aliripoti Ufoo Saro), then CUF kupitia kwa Profesa Lipumba). Kwenye hili napingana na wewe Mkuu ITV wamejitahidi kuonyesha Chadema karibu kila siku isipokuwa leo asubuhi
 
Ni siku ya pilli leo nashangaa ITV wanaonesha CCM tu hawaoneshi vyama vingine kuna nini? Mbona hapo nyuma kilikuwa kituo kizuri cha kutoa habari? Kuna nisilolijua?

Acha uchonganishi,ITV haiko biased muda mrefu sasa, mimi siku hizi naangalia taarifa za ITV pekee hasa baada ya kuondolewa TIDO kule TBC.Baada ya kuangalia taarifa ya ITV huwa naangalia THE CITIZEN ya jirani zetu kenya kila saa 3.00 usiku. ITV na the CITIZEN ndizo pekee africa mashariki zenye habari non-biased.
 
Hivi una uhakika na unachokisema??umeangalia ITV jana saa 2 usiku ile taaifa ya habari?? TBC walichakachua kwa kuwaonyesha wanafunzi wanatoka shule kwenda kuhudhuria kampeni za CDM, nilitune ITV nikakuta nyomi ya watu wanamsikiliza Dk Slaa kwenye kampeni...sasa utasemaje siku hizi ITV wako biased?? Same juzi walionyesha!!

So thatz enough for them!! Na nakupa assigment, leo angalia taarifa ya habari mwanzo mwisho then njoo hapa!!
 
angalau ndugu yangu umeongea,na siyo itv tu mpaka tanesco wana njama hzo.Jana katika habari hyo akaanza kuongea mgombea wa ccm na pale tu ilipotakiwa aanze kuongea doctor slaa umeme ukakatika ukarudi tu baada ya slaa kumaliza na mwanachama wa cuf ndo anaongea.Leo asubuhi nimesubiria marudio nashangaa ile habari ikakatwa.Wameshanunuliwa wote hao lakini mwisho wao hauko mbali
 
mie jana nimemuona kamanda Slaa akimwaga ugali na mboga kwa pamoja itv,b keen guys
 
Ni siku ya pilli leo nashangaa ITV wanaonesha CCM tu hawaoneshi vyama vingine kuna nini? Mbona hapo nyuma kilikuwa kituo kizuri cha kutoa habari? Kuna nisilolijua?

Kwa sababu mmiliki wa ITV ni kada wa CCM na mdau mkubwa wa serikali iliyopo madarakani. Ni wakati wa CHADEMA au makada wake kuanzisha TV stations zitakazorusha kampeni zao kwa kadiri wanavyopenda.
 
Mbona jana walitangaza habari za vyama vitatu tena kwa ufasaha??
 
Kwa sababu mmiliki wa ITV ni kada wa CCM na mdau mkubwa wa serikali iliyopo madarakani. Ni wakati wa CHADEMA au makada wake kuanzisha TV stations zitakazorusha kampeni zao kwa kadiri wanavyopenda.

Hili ndio la muhimu..
 
Back
Top Bottom