Igunga: CUF yaanza kuwalipa mawakala posho ya uchaguzi mkuu uliopita

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Aliyekuwa mgombea wa jimbo la Igunga kupitia tiketi ya CUF, Lucas Mahona, amesema wameanza kuwalipa posho mawakala wote 522 waliosimamia uchaguzi mkuu uliopita, amesema mawakala hao walikuwa wanawadai hivyo wameamua kuwalipa Sh4,000 kila mmoja hivi sasa na kwamba walichelewa kuwalipa kwa sababu hawakuwa na fedha.

"Ni kweli tunaendelea kuwalipa mawakala wetu na hiyo si rushwa kwa vile ni haki yao. Mafungu yalichelewa kutufikia ndio maana tunawapa posho zao na si kwa sababu ya uchaguzi mdogo, tunaomba mtuelewe," alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa Chadema, Mwikabe Mwita Waitara ambaye yuko Igunga, amedai CUF wamekuwa wakipita vijijini huku wakigawa fedha katika mazingira ya rushwa wakijidai kulipa madeni ya mawakala wao katika Uchaguzi Mkuu uliopita kiasa cha Sh5,000 na nyongeza ya Sh4,000 kama fidia na usumbufu.

Source: Mwananchi
 
Hao magamba B waache mambo hayo ya ajabu siku zote walikuwa wapi mpaka waje kuwalipa leo?
 
Kwa hiyo kusingekuwa na uchaguzi wasinge walipa hizo hela?ndo mana huwa wanapokea rushwa na kuuza matokeo,hiv chama kinashindwa kumlipa msimamizi sh 4000 tu?ruzuku inakazi gani?
 
Hawa magamba B wanafanya rafu isiyo na aibu,ivi walikuwa wapi kulipa izo posho? Kama isingekuwa huo uchaguzi unaokuja,ivi wangelipa izo posho kweli? Je huko si kuwahonga hao mawakala? Mi nadhani hao mawakala waelewe na wawe na machungu na muda mwingi waliopoteza bila kulipwa hizo posho zao timely! Mawakala msidanganyike kabisa kwa hiyo elfu4 ya usumbufu,maana hawa magamba B wamewalipa this time kwa kuhofia tu kutoswa in the comming election,vinginevyo msingelipwa this time!
 
hawa jamaa ni matapeli kabisa na hawafai kuongoza nchi kwani wanawaibia wananchi.
 
Hawa magamba B wanafanya rafu isiyo na aibu,ivi walikuwa wapi kulipa izo posho? Kama isingekuwa huo uchaguzi unaokuja,ivi wangelipa izo posho kweli? Je huko si kuwahonga hao mawakala? Mi nadhani hao mawakala waelewe na wawe na machungu na muda mwingi waliopoteza bila kulipwa hizo posho zao timely! Mawakala msidanganyike kabisa kwa hiyo elfu4 ya usumbufu,maana hawa magamba B wamewalipa this time kwa kuhofia tu kutoswa in the comming election,vinginevyo msingelipwa this time!

Definitely, hiyo ni rushwa. Kwanini Igunga tena wakati huu na siyo majimbo mengine? Hao CUF wanataka kutuambia majimbo mengine yote mawakala wameshalipwa isipokuwa Igunga? Na kama majimbo mengine bado ila wameamua kuanza na Igunga, kwa kigezo kipi? Sikutegemea, CUF, chama makini kinachoongozwa na Profesa makini kama Lipumba ku-apply mkakati wa kishenzi namna hii unless taarifa hizo siyo sahihi. Nilitegemea mbinu kama hizo zitoke kwa magamba walioishiwa technics.
 
ni malipo yao halali ila tu ya mechelewa, cuf ni chama cha wanainchi chenye mrengo wa kiliberali, si kama cdm mabepari.
 
kweli birds of the same feathers fly together-hata baba yake chama cha magamba hawana hela,ma dc na ma-rc hawajachaguliwa mpaka leo,bado mishahara NMB inawapa support-
 
TAKUKURU na MSAJILI wa vyama vya siasa waanzishe uchunguzi,kuna moshi wa rushwa
 
Chadema inatumia utaratibu gani kuteuwa wakurugenzi wake kama huyu bwana anayeitwa Mkurugenzi wa Sera na Utafiti alipatikane vipi? Nani anajuwa Wakuu anisahidie.

Hili la rushwa na nadhini ni la PCCB na wananchni wenyewe kama bado bado wanataka kutawaliwa kwa uonevu na kukosa uwakilishi imara bungeni kwa sababu ya Tsh.5,000 +Tsh.4,000 kwa miaka mitano! basi hao ni watu ambao bado wapo katika evolution stage ya nyuma kidogo.
 
CUF kwisha habari yao! Wtz wa sasa si wale wa itikadi mfu ya miaka ya nyuma.wanaele fika kilichopo.Nawashauri ]wana ,Posho zao chukueni kwa kuwa ni jasho ,kisha fanyeni kweli!!!!! chagueni kilicho bora!
 
Aliyekuwa mgombea wa jimbo la Igunga kupitia tiketi ya CUF, Lucas Mahona, amesema wameanza kuwalipa posho mawakala wote 522 waliosimamia uchaguzi mkuu uliopita, amesema mawakala hao walikuwa wanawadai hivyo wameamua kuwalipa Sh4,000 kila mmoja hivi sasa na kwamba walichelewa kuwalipa kwa sababu hawakuwa na fedha.

"Ni kweli tunaendelea kuwalipa mawakala wetu na hiyo si rushwa kwa vile ni haki yao. Mafungu yalichelewa kutufikia ndio maana tunawapa posho zao na si kwa sababu ya uchaguzi mdogo, tunaomba mtuelewe," alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa Chadema, Mwikabe Mwita Waitara ambaye yuko Igunga, amedai CUF wamekuwa wakipita vijijini huku wakigawa fedha katika mazingira ya rushwa wakijidai kulipa madeni ya mawakala wao katika Uchaguzi Mkuu uliopita kiasa cha Sh5,000 na nyongeza ya Sh4,000 kama fidia na usumbufu.

Source: Mwananchi
chama kinafeli kuwajali mawakala wake wenyewe halafu kinategemea kipate dhamana ya kuwajali watanzania wote including wa upinzani

hivi vyama vingine kama vina laana vile
 
chama kinafeli kuwajali mawakala wake wenyewe halafu kinategemea kipate dhamana ya kuwajali watanzania wote including wa upinzani

hivi vyama vingine kama vina laana vile

Hapo kwenye red; excellent point. Bado narudia tena, kwanini Igunga tena wakati huu? Eti hela zilichelewa ila za jimbo fulani (Igunga) tu zikapatikana ghafla baada ya jimbo husika kuwa wazi! Jamani mzaha huu. Ina maana kama jimbo lisingekuwa wazi mawakala ndio walishadhulumiwa hivyo halafu mnategemea uchaguzi mkuu ujao (mawakala) wawafanyie kazi nzuri! Halafu chama hicho hicho kinaomba ridhaa ya kuwaongoza watanzania kwa mizaha ya namna hii!

Ningekuwa CUF ningetafuta sababu nyingine ya kuwaangukia mawakala na naamini wangeelewa kuliko kujidhalilisha hivi. Kwa kweli kwa ujinga huu hata CCM wana haki ya kuvidharau baadhi ya vyama vya siasa ikiwemo CUF. Mnajidharaulisha wajameni.
 
Back
Top Bottom