IGP Said Mwema na hadaa ya uwepo wa amani nchini

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,906
6,909
Wadau salamuni.

Tarehe 14.11.2011, IJP Mwema aliongea na vyombo vya habari na kutoa alichokiita PRESS RELEASE kama tahadhari lakini pia katika kuutumikia umma wa watanzania kama kazi yake ilivyo. Waraka huu, sijauona hapa JF pamoja na kuwa ulitolewa kwa wanahabari, labda wengi hawahudhurii humu ndani au wameuupuuza.

Nimefanikiwa kuupata waraka huu, ambao pia unapatikana katika web ya jeshi la polisi ili tuweze kuujadili. Kwani malengo ya afande ni kuusambaza waraka huu hadi ngazi ya vijiji ili wananchi wafundishwe kuendelea kuvumilia na wajiepushe katika michakato ya kutafuta haki mbalimbali.

Tunapoelekea katika mchakato wa kudai katiba mpya ambayo pia tutahakikisha inamwajibisha hata yeye mwenyewe kwa umma na sio kwa serikali kama ilivyo sasa.

Nawasilisha taarifa hiyo kwa kuijadili.

IJP MWEMA said:

TAARIFA YA INSPEKTA JENERALI WA POLISI SAID A. MWEMA ALIYOTOA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 14 NOVEMBA, 2011, KUHUSU VITENDO VYA VURUGU NA FUJO VILIVYOJITOKEZA KATIKA MAENEO MBALIMBALI HAPA NCHINI

Ndugu Wananchi,

1. Nimelazimika nizungumze nanyi kuhusu matukio ya vurugu na fujo yaliyojitokeza katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Matukio haya ya wananchi kushindwa kupata suluhu ya matatizo yao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu yamejitokeza katika mikoa ya Arusha, Mbeya, na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Matukio haya yamesababisha hasara kubwa kwa raia wema na hata kurudisha nyuma juhudi za maendeleo ya nchi. Naomba nitumie fursa hii ili kuwasiliana na wananchi wenzangu katika kuhakikisha kwamba amani, usalama na utulivu vinadumishwa hapa nchini.

2. Kama mnavyofahamu, moja ya jukumu la Polisi popote duniani ni kuhakikisha usalama na amani pamoja na kulinda maisha ya raia na mali zao. Ili Jeshi la Polisi lifanikishe jukumu lake hili ni muhimu sana kwa raia /wananchi kuenzi amani na usalama uliopo nchini. Sababu ya msingi ya raia kuenzi amani, usalama na utulivu uliopo nchini ni rahisi kuona kwani; Amani ya nchi ikiharibika ni kama mfano wa chombo kinachozama baharini, hakuna anayepona wote wanakwenda na maji. Ikiwepo bahati ni wachache tu wanaonusurika. Kwa mantiki hiyo, fujo na vurugu zilizojitokeza hivi karibuni katika baadhi ya maeneo hapa nchini si dalili nzuri na zinaashiria uvunjifu wa amani na utulivu ambazo ni nyenzo muhimu katika kuleta maendeleo nchini. Fujo, vurugu na vitendo vingine vya ukiukwaji wa sheria visipodhibitiwa haraka vinaweza kufikisha nchi pabaya.

3. Ili tusifike huko, na wakati tukisubiri matokeo ya uchunguzi wa matukio hayo, nimeona nizungumzie mustakabali wa amani na usalama wa nchi yetu kwa kutazama baadhi ya mambo yafuatayo:-
(i) Kuhamasisha kufanya fujo, vurugu kama vile kwenda kubomoa Benki, kuvamia na kuharibu vituo vya polisi, kuharibu mali za watu na kuharibu miundombinu mbalimbali iliyojengwa kwa kodi ya umma kwa kisingizio cha siasa ama jazba; ni kuvunja sheria. Kwa sasa yako mazoea ya kutaka huruma itokane na shinikizo la kisiasa. Ikumbukwe Tanzania ni yetu wote na sote lazima tuheshimu sheria tulizojiwekea. Itakuwa sio hekima kwa nchi yetu kuona sheria inavunjwa na watu wachache kwa kisingizio cha siasa ama jazba bila kuchukuliwa hatua. Shughuli za siasa ni kitu kimoja na fujo ama vurugu za jazba ni kitu kingine. Upo umuhimu wa kutenganisha mambo hayo mawili na hapana budi mamlaka za kisheria ziheshimiwe na watu wote bila kujali itikadi zao kisiasa au kijamii.
(ii) Waheshimiwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walipitisha sheria ya Vyama Vya Siasa na Sheria ya Jeshi la Polisi, sheria hizo zimeweka utaratibu na miongozo ya kufuata katika kuratibu mikusanyiko mbalimbali ikiwemo maandamano na mikutano ya hadhara. Haki na utaratibu wa kufuatwa na Vyama Vya Siasa pamoja na Jeshi la Polisi kupewa taarifa ya mikusanyiko imefafanuliwa pia katika sheria hizo. Kwa hali hiyo ifahamike wazi kwamba Jeshi la Polisi halina nia mbaya ya kuzuia mikusanyiko ama maandamano. Hata hivyo, katika utekelezaji wa sheria na kanuni hizo, pale Jeshi la Polisi linapopata taarifa ya mkusanyiko au maandamano, hulazimika kuzingatia mambo mengine muhimu kabla ya kuruhusu mkusanyiko ama maandamano kama vile: haki ya raia wengine ambao hawatahusika na mikusanyiko hiyo kwa mfano njia ya kupita na mahala pa mkutano, kuepusha migongano, kusaidia watu wengine kuendelea na shughuli zingine za kujitafutia maisha, watoto kwenda shule, au wagonjwa kwenda hospitali. Kwa hiyo ikitokea Polisi kuzuia mkusanyiko isihesabike kwamba wanaonea wanasiasa ama kundi fulani la watu. Sheria tajwa zinatoa pia fursa ya kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na hata kwenda Mahakamani ikibidi kudai haki iliyozuiwa. Vilevile hakuna kipengele cha sheria kinaruhusu kufanya fujo na kujichukulia sheria mkononi kwa sababu za zuio la Polisi. Taratibu hizi ziko pia katika nchi nyingine nyingi zilizokomaa kidemokrasia kwa miaka mingi kama vile Marekani, Uingereza na Ujerumani.
(iii) Katika kutekeleza jukumu la kuhakikisha amani na usalama unakuwepo wakati wote nchini, Polisi wanawajibika kisheria kudhibiti vitendo vyote vya uvunjifu wa amani. Wakati mwingine, kulingana na mazingira ya vurugu na fujo, polisi hulazimika kutumia nguvu za kiasi kulinda maisha na mali za raia pamoja na kukamata wahalifu. Wakati wa matumizi ya nguvu za kadri polisi hufanya mchakato ili kupima ni nguvu za aina gani zitumike kulingana na changamoto zilizopo kwa wakati huo. Kutoa tafsiri ya fikra ya nguvu kubwa ni nini na nguvu ndogo ni nini na ni matukio gani yaliyokuwa yanatendeka wakati nguvu inatumika, matendo na mazingira ya mapambano ndio yanayolazimisha Polisi kutumia nguvu kumkabili yule anayelazimisha nguvu itumike ili kumzuia mtu ama kikundi cha watu wanaovunja sheria.
(iv) Ndugu wananchi, mbali na vurugu hizo za kisiasa na kijamii, nchi yetu inakabiliwa pia na matishio mengine ya kiusalama kama vile: Ugaidi, Uharamia, Uhamiaji haramu, Ujambazi, Mapigano na vurugu zinazoendelea katika nchi za jirani. Naomba kutumia fursa hii kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kuhusu wale wote wanaowashuku kuhusika na uhalifu wa aina yoyote ili kudumisha amani na utulivu nchini hususan katika kipindi hiki tunachoelekea mwisho wa mwaka na maadhimisho ya miaka hamsini tangu tupate uhuru wetu.
(v) Pia, navishukuru vyombo vya habari kwani nyinyi ni sehemu ya Watanzania. Naamini kwa taaluma zenu mnayo fursa kubwa ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya fujo kwa maana vurugu zitawagusa na nyinyi pia. Usalama ni bidhaa muhimu na adimu ambayo inahitajiwa na kila mtu. Usalama ninaozungumzia hapa sio wa chama tawala au vyama vya upinzani tu, ni usalama wa Watanzania wote (watoto, vijana, wazee, wanawake kwa wanaume). Kwa hiyo ni lazima sote tushiriki kuhakikisha hakuna mtu anayepata nafasi ya kuvunja amani na utulivu wa nchi yetu. Ni muhimu kila mtu atii sheria bila shuruti, kwa wale wanaokaidi hatuna budi kuwashurutisha watii sheria, jambo ambalo limekuwa na gharama kubwa kwa kodi za wananchi. Polisi kama chombo cha dola hatutakuwa na ajizi kwa yeyote atakayevunja sheria za nchi na kila mtu atawajibika peke yake kwa kosa alilolitenda.
(vi) Natoa rai kwa watanzania wote kuelewa kuwa Polisi ni Jeshi lao; askari ni watoto wenu ama ndugu zenu. Pia ni watumishi wenu mliowaajiri kulinda usalama. Tutafakari ni kwanini mtu mwenye busara au kikundi cha watu wanaotakiwa kutii sheria wanamua kufanya fujo, vurugu na hata kupigana na Polisi, ni kwa nini tulazimishe nguvu itumike? Historia inaonyesha fujo na vurugu haziwezi kutatua kero na malalamiko yoyote bali zinarudisha nyuma maendeleo kiusalama, kiuchumi, kijamii na kidemokrasia (Kisiasa). Nawasihi wananchi kufuata taratibu katika kuwasilisha kero kwa mamlaka husika. Pia, nawashukuru wananchi wote ambao wamekuwa wakitupa ushirikiano kwa kutii sheria bila kushurutishwa. Niwaombe waendelea kuwa watulivu kwa kutokukubali kushawishiwa na mtu yeyote au kikundi cha watu wanojihusisha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa maisha ya raia na mali zao.


AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA

 
Wadau salamuni.

Tarehe 14.11.2011, IJP Mwema aliongea na vyombo vya habari na kutoa alichokiita PRESS RELEASE kama tahadhari lakini pia katika kuutumikia umma wa watanzania kama kazi yake ilivyo. Waraka huu, sijauona hapa JF pamoja na kuwa ulitolewa kwa wanahabari, labda wengi hawahudhurii humu ndani au wameuupuuza.

Nimefanikiwa kuupata waraka huu, ambao pia unapatikana katika web ya jeshi la polisi ili tuweze kuujadili. Kwani malengo ya afande ni kuusambaza waraka huu hadi ngazi ya vijiji ili wananchi wafundishwe kuendelea kuvumilia na wajiepushe katika michakato ya kutafuta haki mbalimbali.

Tunapoelekea katika mchakato wa kudai katiba mpya ambayo pia tutahakikisha inamwajibisha hata yeye mwenyewe kwa umma na sio kwa serikali kama ilivyo sasa.

Nawasilisha taarifa hiyo kwa kuijadili.

Hofu yangu ni kuwa, mwema ataharibu mchakato mzima wa wananchi kudai katiba mpya kwa kuruhusu askari kutumia risasi na mabomu kama alivyowahi kusema mbunge mmoja wa CCM mjengoni kuwa wananua vifaa hivyo ili kuwadhibiti wanaopinga serikali ya CCM. Nimesahau alikuwa wa wapi
 
Awape polisi kila mmoja awe na nakala yake mimi sihitaji, mbona haongelei ukatili na mauaji ya raia unaofanywa na jeshi la polisi, mfano polisi kuiba maiti motuary na kuzitupa barabarani.
 
Awape polisi kila mmoja awe na nakala yake mimi sihitaji, mbona haongelei ukatili na mauaji ya raia unaofanywa na jeshi la polisi, mfano polisi kuiba maiti motuary na kuzitupa barabarani.

hata haya yapo? ilitokea wapi mkuu seal team
 
kati ya wakuu wa Polisi wote waliopita Mwema namsifu sana kwa utendaji kazi wake. Ila serikali iliyopo madarakani ni ya ubabaishaji sana, nawaambia kama mwema angetii yoote aambiwayo tusingekuwa hapa leo.
Nguvu hii mwema inayoanza huwa haizimishwi kwa lolote bali ni mabadiriko yanayotakiwa na umma. Mimi niliyelala njaaa juzi, jana na leo sina uhakika wa kula, watoto hawana uhakika wa kwenda shule utanituliza kwa mabomu ya machozi???

Uliangalie hilo kaka tunapoenda ni pabaya.
 
huyu bwana niliwahi kusikia kutoka kwa watu waliokuwa naye interpol, wanasema alikuwa na uwezo mkubwa sana kiutendaji.
Lakini wanasema kwa mfumo wa kitanzania (na hasa wateule wa ccm) inakuwa vigumu kufanya kazi.

Binafsi sikuwahi kuamini kama ndiye alisema "ukikamata KAGODA nchi itawaka moto"!

Ni kweli kwa dunia ya leo ni vigumu kuzuia huu mkondo wa mabadiliko. Chukulia mfano wa majeshi yenye nidhamu kama Egypt (Misri), wamesalimu amri na kunusuru maafa makubwa ambayo yangeweza kutokea.
 
Tarime huko Mara!

walikuwa wanaficha nini? ohooo kumbe wale wajinga waliopora maiti ya wale wanancnhi wenye uchungu waliokuwa wanadai madini yao? nashukuru kunikumbusha mdau. Hivi ile kesi alifunguliwa Lissu waziri wetu wa katiba na sheria imefikia wapi!!!!!!!!!!!
 
kati ya wakuu wa Polisi wote waliopita Mwema namsifu sana kwa utendaji kazi wake. Ila serikali iliyopo madarakani ni ya ubabaishaji sana, nawaambia kama mwema angetii yoote aambiwayo tusingekuwa hapa leo.
Nguvu hii mwema inayoanza huwa haizimishwi kwa lolote bali ni mabadiriko yanayotakiwa na umma. Mimi niliyelala njaaa juzi, jana na leo sina uhakika wa kula, watoto hawana uhakika wa kwenda shule utanituliza kwa mabomu ya machozi???

Uliangalie hilo kaka tunapoenda ni pabaya.

Ni sahihi kabisa uliyoyazungumza. Mwema alikuja na falsafa ya POLIS JAMII NA ULINZI SHIRIKISHI, kwa kiasi kikubwa, alitaka kujikita kwenye vyavyo vya matatizo vinavyopelekea watu wagome, waandamane, na wajichukulie sheria mikononi.

Mwema alikuwa na nia nzuri, tatizo linakuja kwa aliyemteua, anayemalazimisha kufanya kazi si kwa kufuata sheria wala kuangalia vyanzo vya matatizo katika jamii, bali kupambana na matokeo ya matatizo hayo kwa kuwapiga watu risasi, mabomu na mengineyo mengi ya kukiuka haki za binadamu.

Mwema kwa kadri siku zinavyokwenda, hazingatii tena sheria, bali anachokifanya ni kuhakikisha CCM hawabugudhuwi, ameaacha kujikita katika matatizo yanayowasibu watanzania.
 
Mwema kwa hakika ni mwema kama jina lake na wanamchafua kwa matendo ya CCM

Kama anashinikizwa kufanya vitu nje ya utaratibu, si ajiuzulu? kwani lazima kuwa IJP? kwa umri wake, yuko safi kiuchumi, sidhani kama ni njaa, au labda anabanwa na waraka kwa maofisa wa serikali/watumishi wa umma ambao nitauambatanisha hapa chini.


VIONGOZI WA SERIKALI NA MAMLAKA MBALIMBALI ZA SERIKALI VIONGOZI HAO LAZIMA WASAINI NA KUKUBALIANA NA MKATABA HUU.




THE GOVERNMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


DECLARATION REGARDING RESPONSIBILITY UNDER THE OFFICIAL SECRET ORDINANCE AND REGARDING MEMBERSHIP OF POLITICAL ASSOCIATION.


APENDEX Q/11 (SEE GENERAL ORDERS Q:22 AND Q.2.1.

1. My attention has been drawn to the provisions of the Official Secrets Ordinance. Cap.45 of the laws whichi are set out on reverse of this form and I am fully aware of the serious consequences which may follow any breach of such provisions.

2. Understand also that these processions apply not only during the time of employment but also after employment with the government of the united republic has ceased. I understand also that, all information which I acquire pr to which I have access owing to my official secrets official secrets ordanance and that it would be a contravention of the ordinance for me after I have left the service of the United Republic.a) To public without authority any such information in any form. Whether orally or in any document articles, books, lay, film or otherwise in this country or abroad, OR (b) To communicate without lawful authority any such information to any other person whether or not in service of the Republic.

3. I further undertake on leaving the service of of the republic to surrender any sketch, plan, model, article, note or document made or acquired by me in course of my official duties.

4. I have been made aware that CIVIL SERVANT who are eligible may become members of the Tanganyika African National Union (TANU) and the Afro-Shiraz Party (ASP) {now CHAMA CHA MAPINDUZI-CCM} and not of any other political organization.

5. I here by sole my declare that I am not a member of any other political organization at present and shall refrain from associating myself in any way the activities of such organsation so long as I remain in service of the United Republic.

Station…………………………………………………………………………….. Signature……………………………………………….
.................................................. .......................


(Name to be written in block capital letters in full here)





Date……………………………………Designation………………………………
Countersigned………………………………………………………
Principal secretary/Head of Department
Regional Administrative Secretary.
 
huyu bwana niliwahi kusikia kutoka kwa watu waliokuwa naye interpol, wanasema alikuwa na uwezo mkubwa sana kiutendaji.
Lakini wanasema kwa mfumo wa kitanzania (na hasa wateule wa ccm) inakuwa vigumu kufanya kazi.

Binafsi sikuwahi kuamini kama ndiye alisema "ukikamata KAGODA nchi itawaka moto"!

Ni kweli kwa dunia ya leo ni vigumu kuzuia huu mkondo wa mabadiliko. Chukulia mfano wa majeshi yenye nidhamu kama Egypt (Misri), wamesalimu amri na kunusuru maafa makubwa ambayo yangeweza kutokea.

Ni sahihi kabisa kuwa, Mwema yuko tofauti na viongozi wengine wa polisi waliopita.
1. Kwanza kielimu yeye ndo anaongoza kwa kuwa na elimu ya juu, LL.M
2. Anawajali askari wake kwani alipoingia, alihakikisha ntu halipwi kwa cheo/rank yake balli analipwa kwa elimu aliyonayo. Viongozi wengine walitukuza vyeo,na walihakikisha wasomi hawapati vyeo, hasa huyu mahita ambaye tunaambiwa ni STD 7.
3. K wa mara ya kwanza nchini, Mwema, alibadilisha hadhi ya jeshi kutoka kuwa kimbilio la waliofeli mitihani mbalimbali na kuajiri wasomi. Amekuwa akiajiri graduate wa fani mbalimbali. Naamini hawa siku wakiwa viongozi watafanya maajabu sana.
 
Mwema kinachomwangusha kwa upande mwingine, ni kama watu akina kova ambao wala shule kichwani haku. Kama angekuwa na viongozi ka Sirro ndo wakawa washauri wake wa karibu, nadhani haya mauaji ya kila siku tusingeyasikia labda kwa majambazi tu
 
Inahitaji maandalizi ya kutosha ki-psychology kumaliza kuisoma hii taarifa!!!

Ni sahihi Rzan bt kama ukiisoma kuna mazuri yake ambayo tunatakiwa kuyafahamu siye wanaharakati, lakini pia tujipange kwani WARAKA HUO tayari umewafikia viongozi hadi wa serikali za kijiji. Tusipoujadili hata support ya kudai katiba mpya kutoka kwa wanavijiji wenye uelewa wa kadri itakuwa ngumu kiongozi Ezan
 
Nakuunga mkono 100% utendaji wa mwema ni mzuri sana ila anaendeshwa sana kisiasa asimamie miguu yake.

Ni nini mwarobaini wa viongozi kutofanya kazi kwa matakwa ya kisiasa? Katiba mpya ingejibu hili lakini hali ilivyo, CCM wameihodhi. kazi ipo
 
mwema acha unafiki, toa kwanza boriti ktk jicho lako ndipo utaona kibanzi cha mwenzio, mbona unashindwa kutetea matatizo ya polisi wako? unadhani hatujui ni haki ngapi wanazulumiwa, hapo kweli kwa akili yako unadhani kuna uzalendo, tatizo mnawanyanyasa sana askari polisi wa ngazi za chini ndomaana nao kwasasa wamo kwenye vikindi hivyohivyo, hii ni pamoja na maafisa usalama wa taifa na wanajeshi, msipokaa sawa kuimalisha haki zao wao ndo watakaopindua nchi hii kwa kushirikiana na raia wanaoandamana kila kukicha. shauriana na Othumani na Mwamnyange.
 
This man is talking total nonsense. Mwaka huu peke police wameshaua raia wapatao 70 na ushee, raia wasio na hatia. Hakuna uchunguzi wowote umefanyika, sana sana ni police kuita raia panya. Sasa leo anatokeza kuhubiri hizi ngonjera kwa manufaa ya nani? Said Mwema alikuwa Mbeya wakati wa mkasa wa mahabusu kufa mikononi wa polisi. Anakumbuka alifanya nini na sasa anafanya nini? Yale maadali aliyokuwa anafuata wakati ni RPC Mbeya yameenda wapi au siku police nii ruhusa kuuwa? Lakini nina hakika anamjua vema alikuwa mkuu wa police Kenya - Ali, Sasa hivi ana keso the Hague na huko ndiko Mwema anaelekea.
 
Back
Top Bottom