Mulama
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 3,018
- 1,791
Mkuu IGP, Kamanda Saidi Mwema,
Hebu Shuhudia!.
Hii ndio picha ya mwisho ya mwanahabari, mpiganaji Daudi Mwangosi aliyefia kwenye uwanja wa mapambano!,
1. Ukiangalia kwa makini, utashuhudia hapa, Daudi Mwangosi alikuwa amepigwa mpaka kuangushwa chini, askari hao 6 wenye uniform na mmoja plain clothes mwenye T-shirt ya blue na kofia nyeusi ameshika bastola kwa mkono wake wa kulia, walikuwa wanaendelea kumpigia nini ili hali hana silaha yoyote, haja resist arrest yoyote, why all this police brutality?.
2. Ukimwangalia Mwangosi, amejishika kiunoni kwa huyo OCD mwenye kifimbo, licha ya kipigo alichokipata, kamwe hakuacha zana zake za kazi, mkuno wake wa kulia bado umeshika kamera yake na baada ya kifo, begi lake la laptop ndogo lilikuwa pembeni yake!. Hivi hawa polisi wote sita, wanamshambulia mtu mmoja tena mwenye camera inaonekana wazi, huku kamanda wao akijitahidi kuwazuia kwa kumkinga, lakini bado wakaona haitoshi ndipo unamuona askari huyo akimuelekezea kabisa mtutu wa bomu la machozi!, whay all this police brutality, why?!.
3. Najua Mkuu Kamanda Mwema, inawezekana wewe hupati muda kupita humu jf kwa vile mtandao huu hauna jema la kuisifia serikali yako, na vile vile uko bize sana na shughuli za ulinzi wa raia na mali zao (japo wengine kwa kuwaua kwa makusudi mazima), lakini naamini vijana wako wanapita humu na watakuletea hizi salamu zetu,
tunakuomba sana sana sana, stop this police brutality, utakuja kumponza bure shemeji!.
4. Tanzania tuna uchache sana wa wanasheria, na waliopo wengi hufanya kazi kwa wenye nazo, hivyo tangu huu mlolongo wa mauaji ya polisi, hakuna mwanasheria, shirika, wanaharakati, au chama chochote cha siasa kimelifikisha jeshi la polisi mahakamani, simply because wanaokufa wote ni watu hohehahe, familia zao hazina uwezo wa hata tuu wa kujua haki zao za kudai fidia rasmi serikalini, bali uwezo wa kuajiri mwanasheria kuwatetea mbele ya haki kwa kulishitaki jeshi la polisi!.
5. System ilipoamua kumshuhulikia Imram Kombe kwa kutumia polisi wazembe, angalau familia ile ilikuwa na uwezo wa kuajiri wakili jeshi la polisi likashitakiwa na serikali ikalipa fidia ya kifuta machozi cha mamilioni, japo mlizuga kuwa askari wale walihukumiwa vifungo japo hawakuvitumia lakini familia ile angalau chochote kitu ilipata, milioni 300 kwa miaka hiyo, japo hailingani na uhai wa binadamu, lakini angalau ilikuwa sii haba!, hawa wengine wote, hawakuwa na wa kuwapigania lakini kwa Mwangosi, its a wrong button!.
6. This time, tunataka kuwaona vijana wako behind bars, the soonest posible wakati uchunguzi ukiendelea, hata kama utawashitaki wewe kwa negligence, sisi bado tutakushitaki wewe kwa kesi ya madai, ili familia ya Mwangosi angalau ipate pa kushikilia!.
7. Yote vijana wako waliyoyafanya, watu wamevumilia l;akini kwa hili la Daudi Mwangosi, uvumilivu umetufika mwisho maana ni kifo cha unyama wa ajabu kab isa kupata kushuhudiwa na binadamu alietendewa na binadamu mwingine kwa kisingizio cha line of duty!.
8. Nimekupa angalizo, kama usipochukua hatua madhubuti zenye genuinity kama sura yako inavyoonyesha, unaweza kushindwa kuamini kuwa hata 2015 inaweza kuwa mbali, angalia sana usije kujikuta unamponza shemeji, wewe na yeye na wenzenu, mnaweza kujishtukia mko njia moja kuelekea the Hague bila kuamini!.
9. Watanzania ni watu wapole, wavumilivu na wastahimilivu wa hali ya juu, lakini angalia usiwafikishe mahali, wakaishiwa upole, uvumilivu na usahilivu na kufikia kuamua liwalo na liwe, Hata Ghadafi alijua kuwa anapendwa hivi hivi anavyopendwa shemeji, hata Hosni Mubarak alijua anapendwa hivi hivi anavyopendwa shemeji, hata Wamisri nao walikuwa wapole, wastahimilivu na wavumilivu kama Watanzania, hata Walibya nao walikuwa vivyo hivyo, uvumilivu ulipofika mwisho, matokea sote tunayajua, yakitokea ya kutokea, usije kusema hatukukuonya kabla!.
10. Mwisho kiukweli, to be honest, Kamanda Mwema kama lilivyo jina lalo, unaonekana wewe ni mwema genuinely kwa maneno na matendo, na naamini alishataka kuwachukulia hatua vijana wako siku nyingi, ila ulizuiwa na aliyekuzuia tunamjua na sababu tunazijua!, nakushauri this time, usikubali!, mkatalie na uchukua hatua zile za dhamira yako inazokutuma, vinginevyo 2015, na wewe utajikuta unatafuta nchi ya kuhamia!.
RIP KAMANDA MPIGANAJI DAUDI MWANGOSI, DAMU YAKO HAIKUMWAGIKA BURE!, SOMEONE MUST PAY VERY DEARLY HAPA HAPA DUNIANI! KAMA NI NOMA NA IWE NOMA!, LIWALO NA LIWE!.
PASCO.
NB: Pasco wa JF ni mwanahabari wa kujitegemea aliyesomea fani ya sheria lakini anaendelea kuitumikia fani ya habari kutokana na mapenzi makubwa ya fani hii!. Kufuatia kifo cha Mwangosi kumgusa sana, sasa ameamua kumbe msaada mkubwa kwa Watanzania sio fani ya habari tena, anaanza taratibu za ku wind up, kuachana na ku fani ya habari, na kuelekeza majeshi kuitumikia rasmi fani ya sheria, to stand for the voiceless ambao can't affort to pay for an advocate!.
Mzee Pasco 2015 ni mbali mno! tunatakiwa ku act now and just now, sikumbuki vizuri ni nchi gani lakini kuna story ya kijana mmachinga aliyejipiga kiberiti kwa kupinga unyanyasaji wa askari waliokuwa wanawanyanyasa kama wafanyavyo mgambo wa manispaa za Tz, nakumbuka alivyoibuka kuwa vuguvugu la mapambano ya ana kwa ana yaliyoleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi wa nchi hiyo.
Daudi Mwangosi awe ni kichocheo cha mapambano ya vitendo dhidi ya polisi wadharimu wa nchi hii tupambane nao kwa vita ya kutoana roho kama wanavyotufanyia kwa kutumia siraha tulizonunua wenyewe tukawakabidhi wakazitumia kutumaliza! inawezekana raia kuwashinda polisi suala ni kuondoa woga tu.
Jamaa yangu msomi aliwahi kuniambia kuwa ubinafsi ndio ulisababisha mwarabu mmoja mwenye gobole kuongoza watumwa zaidi ya mia eti kwa sababu hakukuwa na wakujitoa muhanga kumkamata mwarabu kabla hajafyatua gobole lililohitaji nusu saa kushindilia baruti kwanza! kila mtumwa alikuwa anaogopa akijitokeza wa kwanza atauawa yeye japokuwa hilo lilikuwa halizuii kuuawa kwao.
Tangu tumewaogopa polisi hatujanusurika kuuawa lakini tunaogopa kuchukua hatua kwa kile tunachodai tutauawa kumbe tunadelay time tu kwani wao ni zilahir wanachukua wanayemtaka kwa wakati wanaotaka! Twaweza kupamabana na kupata haki ya uhuru wa kuishi.