IGP Mwema na wenzake wanajifunza nini kuhusu kufungwa jela kwa mkuu wa polisi wa China?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa, vimetoa taarifa ya kufungwa jela, kwa miaka 15, kwa aliyekuwa mkuu wa polisi, wa jimbo la Chongquing, nchini China, Kwa makosa kadhaa, likiwemo la kutumia vibaya madaraka yake, kwa lengo la kumlinda mtuhumiwa wa mauaji. Mkasa wenyewe uko hivi, mwaka jana, mwezi Novemba, mwaka jana,mfanyibiashara mmoja, anayeitwa Neil Heywood, alifariki kwenye hoteli moja, kwenye jiji la Chongquing, nchini China, katika mazingira ya kutatanisha. Akalazimika mkuu wa polisi wa jimbo hilo, Wang Lijun, aunde Tume ya kipolisi, kuchunguza kifo hicho.

Matokeo ya uchunguzi wa kifo hicho yalipotoka, yakaeleza kuwa mtu huyo alikufa kutokana na kunywa pombe kupita kiasi. Hata hivyo, ukweli wa mambo ni kuwa mtu huyo, aliwekewa sumu, na mfanyakazi wa ndani, wa kiongozi mmoja wa juu kabisa wa chama cha kikomunisti nchini humo, Bo Xilai, kwa maelekezo ya mke wa huyo wa Kigogo, aliyetambulika kwa jina la Gu Kailai, Habari hizo alizitoa mkuu wa polisi mwenyewe, Wang Lijuan, baada ya kutokea kutoelewana, kati yake na huyo mwanasiasa kigogo, wa jimbo hilo la Chongquing. Alieleza kuwa njama hizo za mke wa kigogo wa chama cha kikomunisti wa nchi hiyo, zilifanywa kutokana, na mtoto wa kigogo huyo, ambaye ni mshirika kibiashana na huyo Neil Heywood, kutofautiana katika mambo ya biashara zao. Kutokana na taarifa hizo toka China, tunaweza kufananisha na matokeo ya mauaji mengi ya kutatanisha ambayo yamekuwa yakitokea nchini mwetu, na kuishia uundwaji wa Tume za kipolisi, ambazo mara nyingi, hutuletea matokeo ya marehemu aliuawa na kitu kizito, ambacho hakijajulikana, kililurushwa na nani! Lakini kama imetokea China kwa mkuu wa polisi kujisalimisha ubalozini, na kueleza kinagaubaga kuhusu kigogo wa chama cha kikomunisti, alivyohusika katika kuamrisha mauaji, na kumuelekeza kigogo wa polisi, alifukiefukie hilo jambo, lisijulikane, hadi pale kigogo huyo wa polisi, alipoamua kupasua jipu.

Naamini, hata hapa TZ, hawa maaskari wetu wa vyeo vya chini, wanaopokea maelekezo ya kuua raia wasio na hatia toka kwa mabosi wao, akina Mwema, Chagonja, Kamuhanda, Shilogile na wengine, ipo siku maaskari hao wa vyeo vya chini, wataamua kufunguka na kueleza ukweli wote. Hapo ndipo tutakaposhudia kigogo mmoja baada ya mwingine, wakipandishwa kizimbani, na hatimaye,kuhukumiwa kwenda jela kwa miaka kadhaa! kipindi hicho kimekaribia sana nchini mwetu, maana damu za wanyonge wengi, zimemwagika bila sababu ya msingi, kwa ajili tu ya kulinda maslahi ya wakubwa!!!!
 
Ndio maana kuna discipline China sasa Kamuhanda anahojiwa na vyombo vya habari anasema hawezi jiuzuru bse alikuwa anTimiza wajibu wake kisheria which means polisi apart from kulinda raia wana pia wajibu wa kuua
 
Enzi za Nyerere kuna RPC alifungwa jela na waziri wa mambo ya ndani alijiuzulu tokana na kashfa ya mauaji bila hatia mikoa ya kaskazini. Sikumbuki jina la RPC lakini waziri aliyejiuzulu alikuwa ni Alhaji Ally Hassan Mwinyi. Hayo yalitokea kipindi kile cha Nyerere na sijui kama yataweza kutokea tena na hasa kipindi hiki CCM feki iko madarakani.
 
Amri jeshi mkuu wa Tanzania ndio amewaweka Polisi wa Tanzania kuwa juu ya sheria kwake yeye ni ua ,tesa basi
 
China ni nchi inayoongozwa kwa mujibu wa sheria, Tanzania ni nchi inayoongozwa na amri na matamko ya viongozi, kitendo cha kamuhunda kusema kuwalikuwa anatimiza wajibu wake ni kuonyesha wazi kuwa hajui anachozungumza zaidi ya kutoa amri.
 
Ritz 1, majebere na wale ma pro ccm mmeyasikia haya mambo......binafsi nazipenda sana siasa/sheria za china hakuna longolongo.. Umeiba unawajibishwa, hakuna kuleanaleana, mtu ni mwizi wa mabilioni eti raisi anatoa amri ya kurudishwa , are we real serious????, mwizi wa simu anauliwa....lakini yanawmisho haya,
 
Said Mwema ajiandae, la sivyo 2015 akimbie mapema mkono wa sheria utamfuata na vibaraka wake wote
 
Binafsi nakerwa sana na hawa ccm hasa hawa wa awamu za 2,3 na 4 kuwa ndo vinara wa kuvunja sheria, halafu wanawataka wengine watii sheria bila shuruti. hii inasikitisha sana. tuilitegemea viongozi ndo kwanza watii sheria kwa vitendo halafu sisi waongozwa ndo tuige mfano. Viongozi ni waongo, halafu wanataka sisi waongozwa tuwe wakweli, viongozi ni mafisadi, halafu wanataka sisi waongozwa tuwe wazalendo, viongozi ni wauaji, halafu wanataka sisi waongozwa tuwe watetea haki, yaani viongozi ni waovu wa wa kupindukia bado wanataka sie waongozwa tukae kimya tu huku wao wakiharibu wanavyotaka. chanzo cha sekta ya umma kujaa rushwa na kutokuwajibika kwa namna kutisha ni matokeo ya viongozi wabovu wasiojua kusimamia sheria. halafu wanajigamba wao ndo wa kuongoza milele, wahat a crazy nation???
 
Mkuu thanx kwa waraka mzuri kwa hao watawala

Hii ni meseji tosha kwa watawala kuwa, ingawa wao ndiyo wanaowavimbisha vichwa kina Kamuhanda na Shilogile, waendelee kukalia nyadhifa zao, wakati ushahidi upo wazi kuwa wao ndiyo walioamrisha mauaji ya Raia wasio na hatia. kupitia askari wa ngazi za chini. Naamini damu za akina Ally Zona na Daudi Mwangosi, zitaendelea kuwalilia, naamini pia ipo siku ambayo hatuijui, miongoni mwa askari hao watajitokeza na kueleza namna wanavyotumika kutekelaza amri za ovyo za kuua Raia wasio na hatia, kwa sababu moja tu kubwa kuhakikisha utawala huu dhalimu wa mafisadi, unaendelea kuwepo hata kama wananchi wote watakuwa wamechoshwa nao na kuamua kuung'oa kwa sanduku la kura!!
 
Back
Top Bottom