IGP Mwema na mkakati wa kuwa na polisi 'weledi'! Kumbe maadili yazidi kuwa mabovu!

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,304
431
Wakuu;

Tumekuwa tukimsikia IGP Mwema akiimba 'wimbo bora' wa kujenga 'Jeshi lenye 'Weledi'' na askari wa kisasa..! Je, mwenendo huu unaojitokeza kila kukicha kutokana na polisi kuzidi kuwa na maadili mabovu na kuhusika katika matukia yanayokera na kudhoofisha usalama wa wananchi na mali zao ni ishara ya kufanikiwa kwa IGP Mwema au ndio kushindwa kabisa! Hawa watendaji 'wamejaa siasa' kama kawaida, kudhani bado wananchi wanapokea maneneo wakati matendo yanazidi kuashiria kushindwa kazi kwa Idara ya Polisi?
Matendo ya wananchi kujiamulia wenyewe na kutokujali tena kuwa Polisi wanaweza kuwasaidia lolote kiusalama ni pigo la kitaifa! Tutafakari wakuu!

Kwa sababu "tunajenga Jeshi lenye weledi" Katika Matukio machache ya hivi karibuni, yanatuthibitishia picha halisi kuwa Uongozi mzima wa Polisi, Mambo ya Ndani na Watendaji wake kazi ya kuongea na kutenda ni tofauti na utendaji umewashinda!
  • "Polisi atinga ndani ya Baa Mjini Moshi na SMG yenye risasi 30 akitaka kumwangamiza mgomvi wake!" - Source: Magazeti na Capital FM
  • "Polisi wawili wahusishwa na wizi wa Gari la Mwanadada maarufu jijini, ktk maeneo ya bwawa la kuogelea ndani ya Chuo kikuu, wampigia simu kumwambia wakutane baa iliyo Sinza awape Milioni 3 wamrudishie gari, akawaahidi Mil 2 na nusu, kweli wakaenda eneo tajwa kwa lengo la kupokea hela, ila wakanaswa kwa mtego uliowekwa" Source: Capital FM
  • "Polisi katika Mji mdogo wa Tarakea-Rombo wasababisha kifo cha Mfanyabiashara, Ndg Shayo, kwa kumpora mzigo wa Magunia ya Maharage zaidi ya gunia 20 ya thamani ya zaidi ya Milioni 4 na kuuza wakishirikiana na Mtendaji wa Kijiji , huku wakamweka kifichoni Mmiliki wa mzigo kusikojulikana toka asubuhi akiteswa hadi aliporejea jioni akiwa hoi, na kufariki muda si mrefu" - Source:Capital FM
  • "Polisi katika Maeneo ya Lupa Tinga Tinga wasababisha kifo cha Mwanafunzi aliyeiba simu na kusababisha wananchi kukasirika na kuchoma nyumba za polisi na ya mwenye simu" - Source: Magazeti
  • "DCI Manumba katoa taarifa ya Ugonjwa wa Mwakyembe kuwa ugonjwa wake hauhusiki na kuwekewa sumu, wakati Waziri wake Shamsi V Nahodha akana na kuhoji DCI Manumba kapata wapi taarifa hizo" - Source: Magazeti
  • Na memgineyo mengi tuongezee.............
  • .......................
  • .....................

Wakuu, haya ni masuala nyeti yanayoonyesha mwelekeo usiotabirika kwa jeshi letu la polisi hasa ukizingatia tatizo la msingi la maslahi, kama ilivyokuwa kwa Madaktari, Waalimu na watumishi wengine wa umma ni 'pilipili kali' ambayo serikali hii 'sikivu' haipendi kusikia!

Naomba kuwasilisha, tujadili wakuu!
 
Polisi wanapita kukusanya Pesa kwa wachezesha Kamari maeneo ya shule ya uhuru,soko la mchikichini na mwenye Kamari anatamba kwamba hata ukalalamike kokote unajisumbua
 
Wana JF,

Honestly the most worse Department in the Government sector in Tz ni Police Department imeoza kupita maelezo kabisa. Police imekuwa ndio gumzo hapa nchini ufani wa kazi zao ni zero kabisa, Na hili ni Chanzo cha Top Level ya Department hii kuburuzwa na viongozi wa Si ha sa police wakubwa kukubali kuwa vibaraka wa viongozi wa si ha sa ndiko kutaligawa taifa siku zijazo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom