IGP Mwema, 'mob justice' na kuuawa kwa polisi

Tutaona mabadiliko au yatakuwa ni yale yale?

=============================

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua
nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.

Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence)katika Jeshi hilo la Polisi.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).

Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni...Mwema alijitahidi sana katika kipindi chake ila alizungukwa na akina chagonja, feleshi, hosea na wateule wengine waliokuwa wanapokea amri kutoka kwa akina Nchimbi na Mwigulu ...
 
angeachia madaraka kama aliona anaburuzwa..je unakumbuka sakata la jan 5.1.2011 nani alibaka sheria juu ya maandamano ya chadema.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni...Mwema alijitahidi sana katika kipindi chake ila alizungukwa na akina chagonja, feleshi, hosea na wateule wengine waliokuwa wanapokea amri kutoka kwa akina Nchimbi na Mwigulu ...

Mwema hakufanikiwa sehemu yoyote katika core functions za kazi yake. Kesi upelelezi haukamiliki kwa asilimia zaidi ya 90, kwa vile tu hakuna kufuatilia but kuna idadi kubwa Sana ya unsolved murder cases, upelelezi duni na finyu unaochukua muda mrefu. Kuna rushwa ya wazi wazi, hata Leo nikiamua kuvunja sheria makusudi na kutumia hela hakuna WA kunigusa. Polisi wanabambikia watu kesi, polisi wanaiba vidhibiti, na kila aina ya uozo. Kwa kifupi Said Mwema alikuwa janga la kidunia.

Alichofanikiwa Ni kuanza kuboresha makazi ya askari polisi, which is NOT a core function of IGP post
 
Mwema Pumpzika. kula bata kwa raha zako...

AMANI YA NCHI IPO. AMANI YA MTU MMOJA MMOJA IPO. WIZI WA KWENYE MABASI UMEKWISHA. NARUDI NYUMBANI SINA WASIWASI WA KUVAMIWA NA MAJAMBAZI USIKU. NATEMBEA BARABARANI KIFUA MBELE. TRAFIC WAPO NA WANAFANYA KAZI KISAWASAWA NA MUDA WOTE....

WEWE SI MALAIKA......LAKINI TUNASHUKURU......
 
Mkuu endelea kupumzika huko kwenye nchi uliyopo huku ukiota ndoto kuwa Tanzania kuna Amani ya Nchi. Haipiti wiki siku siku hizi lazima Wakulima na Wafugaji wachinjane kwa kugombea ardhi, wewe na Mbulumundu wenzio mnajidanganya kuwa kuna Amani ya Nchi. Amani ya nchi ni mfumo, wale waliochinjana JUZI kule Malinyi - Ulanga walivuka mipaka na kuvamia kituo cha polisi kutaka kukisambaratisha kwa kuwa uwepo wa polisi kwenye eneo lao hauwasaidii. Mikoa ya Morogoro, Pwani, Iringa, Tanga na Rukwa kwa uchache imeripoti kuwepo mauaji na uvunjifu wa amani kati ya wakulima na wafugaji, cha ajabu nyie watawala hamjui maana ya amani ya Nchi
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni...Mwema alijitahidi sana katika kipindi chake ila alizungukwa na akina chagonja, feleshi, hosea na wateule wengine waliokuwa wanapokea amri kutoka kwa akina Nchimbi na Mwigulu ...

ndo maana ile kitu ya dhahabu ilipotea?
 
Back
Top Bottom