IGP - Mtandao huu ni hatari - Part I

sinauhakika na mtoa mada nikupe simu ya igp said mwema au ya dci manumba mimi mwenyewe nipo kwenye system kama nikweli na ushahidi unao mimi naweza kusaidia

Ikiwa upo kwenye system, ni wakati wako huu umeshapewa taarifa fuatilia kisha utuletee majibu katika forum hii. na siyo kumwambia mtoa mada kuwa umpe namba ya IGP, na kumbe nawe ni mmoja wao.

Au unaelewa hili jambo?? POLISI tunakosa imani na nyie, ACHENI HIZOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
mkuu off point
hiyo!! Kazi ya polisi ni taaluma co siasa!!!!

Kama kazi ni Taaluma na siyo siasa mbona mnashindwa kuitumia vizuri taaluma yenu???? ina maana mnadhalilisha taaluma.

JIREKEBISHENIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
kwa staili hii kila mwenye mkasi mkononi anajifunzia kunyoa kwa mwenye nywele yeyote anaeonekana.
 
Habari hii ni kweli kabisa. Wiki tatu nyuma walivamia kiwanja Mbezi beach maeneo ya Five Star na kuzungusha ukuta na kuleta walinzi. Nina habari mwenye kiwanja hakupata ushirikiano kabisa na polisi ya Wazo zilipo ofisi za OCD hivyo kwa msaada wa ofisi ya mwanasheria wake waliweza kupata amri ya kusimamisha ujenzi iliyotolewa na mahakama ya Ardhi na kesi itaanza karibuni. Katika uvamizi huo walitumia risasi za moto kumtisha the legal owner na majirani na hata baada ya ku report polisi hawakuchukua hatua yeyote. Habari ni kuwa tapeli mmoja papaa mfadhili wa bendi ndie kiongozi wa kundi lakini anawatumia wasaidizi wake kuongoza uhalifu huu kwa kuwa ameshaonywa karibuni na baadhi ya viongozi wa Polisi na hajatii alichoonywa. Naomba ifahamike kabisa hutapata msaada polisi hawa jamaa wakivamia kiwanja chako na hii ni kwa sababu ya wanalindwa na baadhi ya viongozi wa polisi. Nadhani huu ni uonevu uliokithiri na swala hili lingefuatiliwa na usalama wa Taifa kwani linakua kwa kasi. Nawakilisha wakuu
Nafikiri huku mitaani kuna viongozi kuanzia wajumbe,madiwani,wabunge nk je hizi dhuruma hawana habari nazo ,na pia mi nafikiri kuna haja Usalama wa Taifa ofisi zao ziwe wazi kwa wananchi,sasa kama jeshi la polisi liko mfukoni mwa matapeli ,wananchi wa kawaida waende wapi,tatizo hata mahakama nazo zimejaa matapeli.Pia kwa hili suala wabunge na mkuu wa mkoa waingilie kati kwani si Kova yupo chini ya mkuu wa mkoa au?
 
sasa ushahidi si msearch hayo majina. Hebu nenda kwenye google usearch papa msofe au kama humfahamu kwa sura bofya hapa the eastafrica: Papaa msofe atuhumiwa kuvamia kiwanja mbezi beach!

pia papa msofe akamtapeli mama mjane na itv walimuhoji kamanda kenyela rpc wa kinondoni na huyo tapeli na kenyela akamtetea na kusema msofe sio tapeli ni mfanyabiashara. Baadae jamii forum na itv wakaripoti kwamba huyu papa msofe ambaye rpc amemtetea kwenye vyombo vya habari ni tapeli na kwamba wanaharakati wakiongozwa na mpiganaji mama ananelia nkya walilisimamia kidedea mpaka waziri mkuu akingilia kati na kuamuru swala hili lishughulikiwe mara moja. Cha ajabu kuona hivyo tunaambiwa polisi walimpa huyu tapeli siku saba kurudisha kiwanja na tapeli huyu hakuchukuliwa hatua yoyote. Nadhani ukisearch papa msofe au papaa msofe utapata skendo lukuki za huyu jamaa. Tunaambia polisi wanalipwa mshahara na huyu jamaa.

Mwingine ni mr mushi ambaye alikuwa ardhi. Naye ni hatari na anatetewa na maafisa wa ardhi na polisi.

Nasikia kweli ukienda polisi ukataja jina la mtu wanayemfahamu na kusema amevamia kiwanja chako ndio umewaletea mtaji, kwanza wanakwambia hawahusiki nenda kapigane nae mwenyewe au nenda mahakamani na baada ya hapo wanampigia simu huyo jamaa wanamwambia mkubwa naona umefanya kazi lete pesa yakulinda huku na jamaa fasta anawafikishia fungu lao.

huu ni ukweli sion majungu. Hakuna mtu tanzania anaweza kumdhulumu mtu ardhi bila kushirikiana na polisi - hakuna!
HAPO KWENYE RED.....
si kweli, nakataaa kabisa. Tuwe wakweli, polisi anahusika vipi na mchakato wa ugawaji ardhi kisheria? Tusiingize chuki binafsi dhidi ya polisi kwa mambo yasiyowahusu.
 
Habari hii ni kweli kabisa. Wiki tatu nyuma walivamia kiwanja Mbezi beach maeneo ya Five Star na kuzungusha ukuta na kuleta walinzi. Nina habari mwenye kiwanja hakupata ushirikiano kabisa na polisi ya Wazo zilipo ofisi za OCD hivyo kwa msaada wa ofisi ya mwanasheria wake waliweza kupata amri ya kusimamisha ujenzi iliyotolewa na mahakama ya Ardhi na kesi itaanza karibuni. Katika uvamizi huo walitumia risasi za moto kumtisha the legal owner na majirani na hata baada ya ku report polisi hawakuchukua hatua yeyote. Habari ni kuwa tapeli mmoja papaa mfadhili wa bendi ndie kiongozi wa kundi lakini anawatumia wasaidizi wake kuongoza uhalifu huu kwa kuwa ameshaonywa karibuni na baadhi ya viongozi wa Polisi na hajatii alichoonywa. Naomba ifahamike kabisa hutapata msaada polisi hawa jamaa wakivamia kiwanja chako na hii ni kwa sababu ya wanalindwa na baadhi ya viongozi wa polisi. Nadhani huu ni uonevu uliokithiri na swala hili lingefuatiliwa na usalama wa Taifa kwani linakua kwa kasi. Nawakilisha wakuu

Mkuu hapo kwenye red ni tatizo zaidi. Nchi hii hakuna watu vinyonga kama hao TISS. Wanakula kote kote. Muulize mzee wa kusaga na kukoboa unga mwilini kwake atakwambia. Mimi nilipoteza imani na polisi tokea nikiwa na miaka 9.
Nilitapeliwa madaftari yangu ya shule pale kariakoo sokoni na nikaenda kuchukua polisi pale msimbazi. Nikapewa askari anisindikize mpaka eneo la tukio na wale vijana nikawaona. Nikamuonyesha askari niliyepewa alivyokuwa chizi akaniambia kwa ukali '' wewe dogo hao hawawezi kuwa matapeli utakuwa umechanganyikiwa tu''. FROM THAT DAY nawaonaga polisi kama komando yosso au black mamba.

Anyway hii nchi imeshauzwa na kila mwenye ubavu anautumia kuibia wanyonge. Kila siku natamani tupate TAHRIR SQUARE yetu kama Egypt. Wanaotakiwa kutulinda ndo wanatuibia na kutuua. Refer enzi za IGP Ma...heater na Zombie wake.
 
naomba unisamehe, let me call you mpuuzi, yani ni bora kupuuzwa, waliofanya hivyo either hawapo tena au kama wapo, basi hawatafanya tena hiyo jitihada

ukiona mtu kaleta hapa kwa namna hiyo ujue hizo jitihada nyingine ameshafanya

Mkuu MTN, ni sahihi unachosema. Kesi ninayoiona hapo ni KUTISHIA KUUA KWA BASTOLA/BUNDUKI kama kweli wamefanya hivyo. Lakini subject matter ya post hii ni UNYANG'ANYI WA VIWANJA.

Jeshi la polisi limeanzishwa kwa mjibu wa sheria, na linafanya kazi kwa matakwa ya sheria. Afisa wa polisi anapopelekewa suala hilo la kunyang'anywa kiwanja, hana kifungu chochote cha sheria kufungua kesi na kuifanyia kazi. hana mamlaka kisheria kulifanyia kazi.

Kesi za viwanja zinaingia kwenye kesi za madai ambazo haziwahusu POLICE, isipokuwa kuna mamlaka zimeanzishwa kisheria kudili na kesi hizo. Hivyo mleta mada angeeleweka kama alishafika ofisi za aridhi kulalamika, au mahakamani ili atafutwe mmliki wa aridhi inayozungumziwa.

Ninachofahamu kuhusu POLICE, IGP Mwema alikuja na dhana ya POLISI JAMII na ULINZI SHIRIKISHI. Dhana hii, inajikita katika kutatua migogoro inayochangia kuwepo kwa uhalifu. Mfano katika madai ya mleta post, hakuna uhalifu/JINAI, ila lisipo fanyiwa kazi JINAI inaweza kutokea kwa kutukana, kupigana, kuua, na mengine yanayofanana na hayo.

Dhana ya POLISI JAMII, ni wachache wanaofahamu inataka nini. Kwani ni imani yangu kuwa, OCD/OC CID na viongozi wengine, kama sehemu ya kuzuia jinai kutokea, wangeitumia dhana hiyo kuonana na mamlaka husika na kuangalia namna ya kutatua tatizo lilopo. Lakini ni kwa mtu anayejua kazi yake vizuri ni nini kwa jamii.

Kama hajui, ataendelea kusubiri jinai ifanyike ndo aonekane yuko kazini. Tabu kweilkweli.

Katika matoleo kadhaa ya POLISI JAMII niliyoyapitia, IGP anawataka askari wote na maafisa wote kuwa PRO ACTIVE na sio RE-ACTIVE. Wachache wamemwelewa na wanafanya hivyo, wengine wanataka uasikari wa mahita wa maguvu kupita kiasi
 
HAPO KWENYE RED.....
si kweli, nakataaa kabisa. Tuwe wakweli, polisi anahusika vipi na mchakato wa ugawaji ardhi kisheria? Tusiingize chuki binafsi dhidi ya polisi kwa mambo yasiyowahusu.

Inatakiwa watu tuanze kujielimisha maana ya JINAI na nani anahusika nayo na maana ya MADAI na nani wahusika. hapa ndipo penye utata, na kwa vile polisi ni taasisi ya kulaumiwa kila siku, wanaingizwa kwenye lawama zinazowapasa mamlaka nyingine kama mahakama na idara ya aridhi/uhamiaji
 
sinauhakika na mtoa mada nikupe simu ya igp said mwema au ya dci manumba mimi mwenyewe nipo kwenye system kama nikweli na ushahidi unao mimi naweza kusaidia

Nyie mlio kwenye system ndo kabisa hamuaminiki. system yenu huwa inawalinda wenye hela tu. wakina kayumba hamuhusiki nao.
 
Sishangai izo ni common FEATURES za serikali legelege ie kuibuka kwa Miungu watu!
 
polisi wapewe kipaumbele bajeti ijayo, hawa madaktari wanaweza kufikiriwa bajeti ya 2013/14, napendekeza mishahara ya polisi kima cha chini kiwe 700,000/= labda itaondoa tatizo kama si kupunguza maana matendo yao kwakweli mh.. inafika kipindi mtu kabla ya kwenda kituoni unapitia kwanza bank au kwenda kukopa kwa jamaa

haaaah haaaah haaaah mkuu nimecheka ila ulichosema kina mantiki sana!
 
Mkuu MTN, ni sahihi unachosema. Kesi ninayoiona hapo ni KUTISHIA KUUA KWA BASTOLA/BUNDUKI kama kweli wamefanya hivyo. Lakini subject matter ya post hii ni UNYANG'ANYI WA VIWANJA.

Jeshi la polisi limeanzishwa kwa mjibu wa sheria, na linafanya kazi kwa matakwa ya sheria. Afisa wa polisi anapopelekewa suala hilo la kunyang'anywa kiwanja, hana kifungu chochote cha sheria kufungua kesi na kuifanyia kazi. hana mamlaka kisheria kulifanyia kazi.

Kesi za viwanja zinaingia kwenye kesi za madai ambazo haziwahusu POLICE, isipokuwa kuna mamlaka zimeanzishwa kisheria kudili na kesi hizo. Hivyo mleta mada angeeleweka kama alishafika ofisi za aridhi kulalamika, au mahakamani ili atafutwe mmliki wa aridhi inayozungumziwa.

Ninachofahamu kuhusu POLICE, IGP Mwema alikuja na dhana ya POLISI JAMII na ULINZI SHIRIKISHI. Dhana hii, inajikita katika kutatua migogoro inayochangia kuwepo kwa uhalifu. Mfano katika madai ya mleta post, hakuna uhalifu/JINAI, ila lisipo fanyiwa kazi JINAI inaweza kutokea kwa kutukana, kupigana, kuua, na mengine yanayofanana na hayo.

Dhana ya POLISI JAMII, ni wachache wanaofahamu inataka nini. Kwani ni imani yangu kuwa, OCD/OC CID na viongozi wengine, kama sehemu ya kuzuia jinai kutokea, wangeitumia dhana hiyo kuonana na mamlaka husika na kuangalia namna ya kutatua tatizo lilopo. Lakini ni kwa mtu anayejua kazi yake vizuri ni nini kwa jamii.

Kama hajui, ataendelea kusubiri jinai ifanyike ndo aonekane yuko kazini. Tabu kweilkweli.

Katika matoleo kadhaa ya POLISI JAMII niliyoyapitia, IGP anawataka askari wote na maafisa wote kuwa PRO ACTIVE na sio RE-ACTIVE. Wachache wamemwelewa na wanafanya hivyo, wengine wanataka uasikari wa mahita wa maguvu kupita kiasi
Elimu nzuri kabisa hii Mkuu. Nadhani hao walalamishi wamekuelewa.
 
ndoleha Unaweza kukutana na mimi kesho njoo makumbusho unipe data naweza kufanyia kazi kama kweli unayoyasema na ushahidi unao sitaki mambo ya udaku au umepata viroba

Kama kweli upo police jamii fatilia eneo lililotajwa na Ndohela kuliko kumtaka aje hapo uliposema, kwa sababu za kiusalama. Simshauri Ndohela aonane na wewe. Unanipa mashaka, Au nawe ni kati yao?
 
Kama unafahamu haki zako huwezi lalamika, namba ya simu ya huyo IGP ipo mpigie mweleze na ushahidi uwe nao
Utakaporudi na hiyo part 2 uje na majina ya hao wahalifu pamoja na hao makamanda

polisi akisha pewa jambo ni kufuatilia na sio kukaa na kusubiri ushahidi kutoka kwa mtoa taarifa

ushauri wangu ni kwmba haina haja ya kuwasiliana na polisi, cha msingi tumesha elewa kuwa polisi hawana msaada tena kwa raia wasio na pesa,so tunachotakiwa kufanya ni mapambano tu kati ya hilo genge na wanamasikini,pindi genge hilo litakapo fika eneo husika kufanya umafia huo basi wananchi kwa umoja wetu kwa kila aina ya slaha kupambana nao hadi kieleweke,naimani nguvu ya umma ndio sululisho,kwani polisi hakuna msaada tena
 
Dada Jane nakupa pole kama unataka kufanyia kazi huu mtandao umeshachelewa kwani hawa wanakula na maboss wako hasa wasaidizi wa mwema kwani ndio wanajua usalama wao jaribu kuongea na wale askari wanaotembea na yale magari yenu watakwambia kwani huwa wanajitahidi kupambana ila wanakutana na vikwazo kutoka kwa maboss wenu. Na watu hawataamini ila kamanda mstaafu Tibaigana anawajua vizuri sana hawa wahalifu

Yaani huyu ndo ana miaka 18 tu asikuhangaishe! Mwache aende f5 kama atapata na div3 yake. Sometimes we have to be serious. Jane please acha jokes wakati watu wanaongelea masuala ya hatari.
 
Sasa ushahidi si msearch hayo majina. Hebu nenda kwenye google usearch papa msofe au kama humfahamu kwa sura bofya hapa the eastafrica: PAPAA MSOFE ATUHUMIWA KUVAMIA KIWANJA MBEZI BEACH!

Pia Papa Msofe akamtapeli Mama Mjane na ITV walimuhoji Kamanda Kenyela RPC wa Kinondoni na huyo Tapeli na Kenyela akamtetea na kusema msofe sio tapeli ni mfanyabiashara. Baadae jamii forum na ITV wakaripoti kwamba huyu Papa Msofe ambaye RPC amemtetea kwenye vyombo vya habari ni tapeli na kwamba Wanaharakati wakiongozwa na mpiganaji Mama Ananelia Nkya walilisimamia kidedea mpaka Waziri Mkuu akingilia kati na kuamuru swala hili lishughulikiwe mara moja. Cha ajabu kuona hivyo tunaambiwa Polisi walimpa huyu tapeli siku saba kurudisha kiwanja na tapeli huyu hakuchukuliwa hatua yoyote. Nadhani ukisearch papa msofe au papaa msofe utapata skendo lukuki za huyu jamaa. Tunaambia polisi wanalipwa mshahara na huyu jamaa.

Mwingine ni Mr Mushi ambaye alikuwa ardhi. Naye ni hatari na anatetewa na maafisa wa Ardhi na Polisi.

Nasikia kweli ukienda Polisi ukataja jina la mtu wanayemfahamu na kusema amevamia kiwanja chako ndio umewaletea mtaji, kwanza wanakwambia hawahusiki nenda kapigane nae mwenyewe au nenda mahakamani na baada ya hapo wanampigia simu huyo jamaa wanamwambia Mkubwa naona umefanya kazi lete pesa yakulinda huku na jamaa fasta anawafikishia fungu lao.

HUU NI UKWELI SION MAJUNGU. hakuna mtu Tanzania anaweza kumdhulumu mtu Ardhi bila kushirikiana na Polisi - HAKUNA!

Jamani tumekuwa wapole sana juu ya hawa kina Msofe,mbona wezi wanachomwa moto?
 
Wakati Mwakyembe linamkuta ulisema haikuhusu na hata sasa watanzania tutasema haituhusu, hivi kwanini isifike mahali tuwe wazalendo? Tukubaliane nini cha kufanya.
 
Back
Top Bottom