ifike wakati sheria iseme watoto wote wa viongozi wasome shule za umma na watibiwe hospitali zetu

ndevu mzazi

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
687
237
naomba yeyote mwenye maoni ya kujenga achangie.
kumbuka kwamba watoto wao wapo shaaban robert,mzizima,laureate,ist nk.
wanafunzi 1.jpg wanafunzi.jpg
 
Ethiopia wamejaribu hilo na nasikia wanaenda vizuri. Hii itasaidia maana uongozi ni hiari lakini ikiwekwa wazi kuwa watoto wa viongozi ni lazima wasome shule za serikali ila pale palipo na sababu za msingi itatulazimisha hata tukipata madaraka kuzipa hizi shule kipaumbele.
 
Kulikuwa na wakati (wakati huo niko sekondari early 90s) watoto wa viongozi (mawaziri, mabalozi) walikuwa wanapendelewa (baadhi) kusoma shule za serikali. nakumbuka Tambaza na baadae Minaki nilisoma na watoto wengi tu wa mawaziri na mabalozi ambao walikuwa wanaingia kinyemela nyemela tu.....lakini sasa hivi hata mlala hoi hasiye na elimu anajitahidi mwanae hasiende shule hizo, aende private.......where did the public school system went wrong?! Mbona watu tena hawashobokei Ilboru na Mzumbe...wanalipa mamilioni kwenda seminary na private schools!

Walimu wote wale wazuri waliotamba wakati huo hawako tena shule za serikali...wako private au wameacha kabisa ualimu!
 
umeiweka vizuri mkuu.
Ukiangalia hizo siku unazozisema hata heshima ya utawala ilikuwa afadhali. Kwa hiyo tunachohitaji sio kuwa hili ni wazo jipya bali ni restoration ya kitu kizuri tulichowahi kuwa nacho.
Sababu za kufanya hivyo ni nyingi lakini kubwa ni kuwa huu mfumo tulioamua kwenda nao umeshaonyesha wazi kuwa umeshindwa na hata wanaofanya hivyo wanaona na wanalijua vyema

Hivi mnaziongelea shule hizi ndio akasome mtoto wa kiongozi mfano Rais, Waziri Mkuu, Kawambwa, Mulugo.

rasa-la-tatu-na-la-nne-katika-shule-ya-msingi-Kidugalo-kata-ya-Rwinga-Namtumbo-mjini-mkoani-Ruvu.jpg

View attachment 60466

wanafunzi-mkapa-school.jpg

Wanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Selous wilayani Namtumbo wakiwa darasani.jpg

Na hizo Hospitali mnazoziaongelea ambazo mnataka Rais, Waziri Mkuu, hussein Mwinyi akatibiwe ndio mnamaanishi Hospitali kama hizi hapa:

WAGONJWA_ZAHANATI_KISAKI[1]_.JPG

Wajawazito_Temeke_Hospital.jpg

Yaani sijawaelewa kabisa, naomba mnielimishe mna maana gani hasa!!!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
tatizo ni linabidi lianze kwa kutunga sheria ambayo itaweka viwango maalum vya ada za shule na gharama za hospitali ili washindwe kupora walimu bora na madaktari bora.kwa mfano feza schools ada ni milioni 4.utashindana nae vp kwenye uajiri?kingine viongozi wasimiliki shule ambazo gharama zake ni juu.nknilivyokua mdogo mtu akivaa nguo ya azania unamtamani lakini leo hii unamuonea huruma.
 
Mbona WAMA wanasema mtoto wa mwenzio ni wako pia sijui kama ipo applicable kihivo maana mmmmh huku kwetu Katavi kazi kweli kweli
 
ha hii ikipita naona hospital za walalahoi kama sisi zitakuwa na vifaa vyakutosha na hatutamia bajaji kubeba wagonjwa tena ...
 
Business as usual! Very serious problems are normally given very simple answers by our leaders!
 
Aisee kweli kabisa kama kwenye kifungu cha katiba kingeshikilia kuwa watoto wote wa viongozi wa nchi wasome shule za serikali kweli kungekuwa na mabadiliko kielim,
 
duh nimevutiwa na hii thread.wac wac wangu ni hiki kinachoitwa TERRORISM .hv mtoto wamzee wa magogoni (34ml per month)asome public.ebu fikirien vizuri isije ikawa
easy say than done
 
Back
Top Bottom