Ifikapo 2015 wasomi tusiogope kugombea ubunge kupitia CHADEMA

wasomi ni nani,siasa,usomi na uongozi wa umma ni vitu viwili tofauti usione una kidgree kimoja viwili ukaona unajua kiongozi anazaliwa si nyie mnaenda kutafuta ugali kwa gia ya mmesoma.maprofessor wangapi wameshidwa uongozi
Kushindwa kwa wasomi wachache kwenye nafasi mbali mbali za uongozi, sio justification ya kuongozwa wa watu wasioenda shule. Taifa lolote lililoendelea, ni matokeo ya matumizi ya taaluma flan katika ngazi mbali mbali za kufanya maamuzi. Hivyo kama tunapenda uongozi mimi nadhani tupambane tu kurudi shule kwani naimani kubwa kuwa katiba ijayo itatabanaisha level ya elimu inayotakiwa kwa diwani, wabunge mawaziri n.k. Katiba hii ya sasa ndiyo iliyotufikisha hapa. Inaeleza tu kwa ujumla kuwa ni mtanzania anayejua kusoma na kuandika. Yaan hata akiwa haelewi anachokisoma na kukiandika sio mbaya ilimradi tu ajue kusoma na kuandika. Hii ni weakness tu, hatuwezi kufika tuendako kwa kutohusisha elimu katika ngazi za kufanya maamuzi ya taifa hili.
 
Hatujasoma kwaajili ya ubunge siye unataka na fani yangu ya Civil nikawekwe waziri wa elimu. Wacha tubaki washauri wasomi ndio uchumi wa nchi tatizo waTZ hamjui ndo maana Mbunge analipwa ten times ya Muhandisi Mkuu sasa Majengo yataacha kuwadondokea hovyo?

Na daktari ataacha kumpasua mtu kichwa badala ya mguu!
 
Naunga mkono hoja kwani hawa wazee wanaojifanya wana hekima na busara ndo kabisa wanaturudisha nyuma zaidi ya miaka 50. Hebu tufikirie tu wenyewe shule ya serikali inakosa madawati wakati misitu tunayo ya kutosha kabisa hapa Tz lakini magogo yanpakiwa kwenye meli kupelekewa wazungu as if ni wa maana sana kuliko watz; wizi mtupu.

Hata zile chache zenye madawati yanachangwa (kama hela) na wazazi wa wanafunzi kwa kila mwanafunzi anayeingia shule, hata dawati lenyewe halinunuliwi kwani waliotangulia wakati shule inaanza waliacha madawati yao, wizi mtupu kwani akimaliza harudishiwi dawati lake na kila atakaeingia atachangishwa kama kawa.

Swala la rushwa na ubadhirifu (ufisadi) imekuwa ni nomo praktisi, inafanywa wazi wazi bil hata uficho na bahati mbaya ikigundulika aliyehisika ataambiwa arudishe kwa hiari na hata asiporudisha hachukuliwi hatua yoyote, wizi mtupu.
 
Tusipokubali mabadiliko, tusipochukua juhudi za kufanya mabadiliko tukawaachia wazee waendelee kushika hatamu tutegemee kuendelea kusindikiza nchi nyingine.
 
Yeyote mwenye kuhitaji kugombea nafasi yoyote kupitia CHADEMA, dawa ni kuanza sasa hivi kufanya kazi kwa karibu zaidi na wananchi pamoja na uongozi wetu huko huko mashinani.

Kwa mantiki hiyo ni kwamba wala usipoteze muda kuwapikia wengine majungu kwa uongozi wa juu taifa maana jibu la nani atakua mgombea wetu uko hapo hapo ulipo mashinani.

Samahani Chadema hatuna shina bali tuna msingi (yaani ngazi ya chini kabisa katika chama ni shina)

Samahni
 
Matunda ya kupost thread hii yameanza kuonekana kwani vijana wameanza kujitokeza mf. Ronald Baraka Shelukindo
 
Bado nakumbusha wasomi hatupaswi kuwa waoga wakugombea ubunge. Angalia Arumeru Nassari ni mwenzetu 2015 vijana wasomi tuchangamke
 
Wazo la vijana kujitokeza majimboni wala si la kupuuzwa. Vijana wengi wameonesha kuthubutu kutenda na kusawiri matamanio ya jamii pana. Ni tofauti na wazee maana walio wengi wamebaki kuuchapa usingizi tu bungeni au kujiapiza kuangamiza wapinzani kana kwamba wao ni citizens daraja la chini! Dawa imebaki moja tu. Kujitokeza majimboni na kuwachapa bakora kupitia sanduku la kura!!!:smile-big:
 
tabora mjini huko jiandaeni sasa niko njiani CUF ndo jahazi langu, Change we have to believe, wana tabora ya leo na maendeleo ya kileo yaja kijana wenu makini nipo
 
Ni rai nzuri maana kama ikitokea bunge likawa divided na kukawa na ulazima wa serikali ya muungano kama Kenya basi angalau watakaopata wizara wasiwe kudadadadadadeki!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom