Ifikapo 2015 wasomi tusiogope kugombea ubunge kupitia CHADEMA

kkitabu

Senior Member
Dec 27, 2011
140
47
Mwaka elfu 2010 vijana wa chadema (Mnyika, Wenje, Mdee, Zitto n.k) waligombea nafasi ya kuwania ubunge kupitia Chadema na kufanikiwa kuwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, nashauri vijana chipukizi wanaomaliza Vyuo kuwaiga vijana tajwa hapo juu kwani wametuonyesha njia. Tuchangamke inawezekana kuwabwaga wazee wa ccm. John Heche, Dr. Kitila Mkumbo, Deus Kibamba msituangushe changamkeni.
 
Hatujasoma kwaajili ya ubunge siye unataka na fani yangu ya Civil nikawekwe waziri wa elimu. Wacha tubaki washauri wasomi ndio uchumi wa nchi tatizo waTZ hamjui ndo maana Mbunge analipwa ten times ya Muhandisi Mkuu sasa Majengo yataacha kuwadondokea hovyo?
 
ile miposho naweza mi nataka jimbo la selasini maana jamaa aliniboa kwenye ishu ya posho...kwani lazima niwe mchaga kugombea rombo?
 
Napiga jaramba huku nikimvutia kasi huyu jambazi Rweikiza
 
Vijana wote wana haki ya kugombea sio wasomi tu,na mnaposema wasomi mnaamanisha nini? maana hata aliyemaliza la saba kasoma naye ni msomi pia. cha muhimu wale waliobobea katika fani mbali mbali wabaki kuwa washauri na watendaji katika wizara na sekta mbali mbali,hapo tutasonga mbele. HUO NI MTAZAMO WANGU
 
nadhan ni muda muafaka wa kuwa na vigezo maalum ili kuwa na viongozi wenye maadili na kujua umuhim wa uongozi na dhamana yao!sio mtu yeyote kujisikia tu na ilkumbukwe kazi ya kiongozi wa kweli ni kubwa kuliko unavodhan, achilia hawa wa sasa wanaojiita viongozi hali ni watawala!
 
wasomi ni nani,siasa,usomi na uongozi wa umma ni vitu viwili tofauti usione una kidgree kimoja viwili ukaona unajua kiongozi anazaliwa si nyie mnaenda kutafuta ugali kwa gia ya mmesoma.maprofessor wangapi wameshidwa uongozi
 
Hoja za sasa zinanishangaze sana, ila angalieni tu wenzetu hawa wamekuja lini hapa ndio uaona tatizi nini?
 
Mwaka elfu 2010 vijana wa chadema (Mnyika, Wenje, Mdee, Zitto n.k) waligombea nafasi ya kuwania ubunge kupitia Chadema na kufanikiwa kuwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, nashauri vijana chipukizi wanaomaliza Vyuo kuwaiga vijana tajwa hapo juu kwani wametuonyesha njia. Tuchangamke inawezekana kuwabwaga wazee wa ccm. John Heche, Dr. Kitila Mkumbo, Deus Kibamba msituangushe changamkeni.
Mkuu kkitabu umenena! hata kama sio ushabiki wa vyama! niambieni Zamadamu Wahasira ana lipi jipya amejaa kutu ubongo umekufa! Bi kiroboto Aka watoto wa ndege: wenyewe tunaona jinsi Bunge linavyoendeshwa! Pinda pinda etc! Jamani vijana Aibu. Nipo kwa Kibaki wajamaa wametupiga bao zamani?!!
 
mimi natafuta mtu makini nikamwuze singida kaskazini.
sifa awe mwenyeji wa jimbo husika.

awe anajua shida na matatizo ya wanyaturu wa huko.

awe hajawahi kuwa fisadi wala kuhusishwa nao.

awe anajua matatizo ya mbunge aliyepo.
 
Back
Top Bottom