Ifahamu VSLa (Village Saving and Loan Association) / VICOBA

Mkuu ni kweli kwa sasa vikundi vya hisa vinaweza kuendeshwa kupitia M pesa au Tigo pesa, na hii inasaidia kikundi kisiwe kinakutana kila wiki, so kinaweza kutana kwa mwezi mara moja.

2. Mkuu kuhusu faida na hasara kwa kweli hasara sijui ila hivi vikundi ni mkombozi hasa kwa wenye kipato cha chini. Kwa vikundi vinavyo kuwa siriasi hujikuta mwisho wa mwaka vimetengeneza faida ya kubwa ya hadi 200%za hivyo ni mkombozi hasa kwenye ishu ya mitaji.
Kuhusu kutumia simu kwa kweli hasara ni kukatwa unapo fanya miamala basi ila faida zake ni kubwa kwa sababu kikundi kinaweza hata toa mikopo kwa wanachama wake kupitia simu.
 
Asante kwa maelezo ya kina mkuu. Lakini nahisi ssomething is missing here. Kwa jinsi ninavyofahamu mimi (niliwahi hudhuria mafunzo kwa wiki tatu) vikundi hivi vinalelewa na taasisi inayoitwa UYAKODE? (spelling zinanitatiza). Hawa wanakuwa responsible kuwatafutia ufadhili wa miradi (na hapo ndipo yanaingia yale mashirika uliyoyataja). Nakumbuka nikiwa kwenye semina ilitolewa taarifa kuwa amepatikana mfadhili aliyetayali kutoa boti za uvuvi nne kama kikundi kitaridhia kufanya mradi huo. Wanachama wakakataa kwamba hawataweza kuzisimamia.

Pia kulikuwa na suala la kufungua akaunti. KIA MWANA KIKUNDI NI AZIMA AWE NA AKAUNTI TWIGA BANKCORP. Bank hii ndio yenye kibali cha kuoperate akaunti za VICOBA, hivyo kuna ushiriki wa serikali directly. Pia akaunti ya kikundi inafunguliwa huko, hivyo VICOBA haifi, tofauti na maelezo yako. Mwishoni mwa mwaka mnapiga mahesabu na kugawana faida. Kila mtaji unapokua ndio miradi mikubwa hufunguliwa. VICOBA ya kwanza kabisa Dar inamiliki jengo la ghorofa nne. Hisa za VICOBA hurithiwa na ndio maana mojawapo ya mambo muhimu kabisa katika documents za mwanachama ni jina la mrithi! Pia kuthibitisha haya, jaribu kutafuta vikundi ambavyo vina miaka mingi, ni vigumu sana kujiunga hata kama member mmoja atakuwa anajitoa, kwa sababu ya ada kubwa sana ya kiingilio (wamewekeza kwa muda mrefu mno and you have to march them!).

Again thank you so much for such a useful post.

UYAKODE wanasimamia vikundi vya Ukonga wilaya ya Ilala,hata hivyo si vyote,Ukienda Temeke kuna shirika linaitwa POVERTY FIGHTING TANZANI kwa kifupi PFT,uki-google utawapata,nao wanavikundi eanavyoviratibu,wao vikundi vyao vyote vina account bank,wanatumia current account,pia utawapata kupitia face book.wanachama wa vicoba ,vkundi vinavyoratibiwa na pft eamrgawanyika ktk makundi matatu ya shghuli zao ambazo ni wazalishaji eadogo,watoa huduma na wachuuzi,ki msingi ni mfumo mzuri sana ila tu tatizo ni serikali hawana sheria inayotumika kuviratibu vikundi hivi,na wala hakujawa na juhudi za makusudi wa kuvi-link na other financial institution ili vikundi vipate seed capital na vingine matching loan,lkn pia kuna tatizo la kuvijengea uwezo kwa kutoa skills training na technology development kwa wanaofanya shughuli za ualishaji,eg wasindikaji wa vyakula,watengenexa sabuni nk.
 
kuna tofauti kubwa sana kati ya sacco and vsla, kwa mfanyo vsla- wanachama wana say kubwa sana kwenye mwongozo wa kikundi na sacco ni wachache tu ambao wanao say mwenendo wa kikundi
 
Big up mkuu, somehow umejitahid kutoa information ambazo ni valid japo opetation ya VICOBA inaweza ktofautiana kati ya eneo 1 na lingine. Research yang y 1st degree mwaka huu nimefanya kwenye VICOBA,,,kifupi vinasaidia lakin vinahitaj mtu uwe na shughuli inayokuzalishia kwa 7bbu kukopa ni lazima kwa kila mwanachama ,so kama hauna cha kufanya ukikopa kwa ajili ya kula inakuwa mzigo kurudisha mkopo,,,halafu pia wanatoza Riba kubwa mno kuliko hata commercial banks!
 
Big up mkuu, somehow umejitahid kutoa information ambazo ni valid japo opetation ya VICOBA inaweza ktofautiana kati ya eneo 1 na lingine. Research yang y 1st degree mwaka huu nimefanya kwenye VICOBA,,,kifupi vinasaidia lakin vinahitaj mtu uwe na shughuli inayokuzalishia kwa 7bbu kukopa ni lazima kwa kila mwanachama ,so kama hauna cha kufanya ukikopa kwa ajili ya kula inakuwa mzigo kurudisha mkopo,,,halafu pia wanatoza Riba kubwa mno kuliko hata commercial banks!


then this is not VSLA i know off. i have worked on vsla for the last 3 years as a suppervisor nd kutokana na uzoefu nionao ni kuwa liba mara nyingi haizidi10% and yes sometime member huwa na tamaa ya kuona pesa zao zinawazalishia faida kubwa hivyo hupandisha liba hadi 20 - 30% na hii malanyingi huzua watu kukopa, however for VSLA to be really help to the community has to be accompaned with other additional training like financial literacy, Enterprise Activity selection, Planning & Management (SPM). Community business skills. Then you will have helped the member to borrow with a purpose not conscription
this is a little i know about VSLA
 
Wakuu "Sam Bilgate" na "Ngamba". Kwa kuwa ninatumia simu ya mkononi, sitaandika mengi. Riba za mikopo inayotozwa na Vikundi vya HISA hazipo kama ajari. Zinapangwa, zinajadiliwa , kukubaliwa na W/chama wa Kikundi husika kisha kuwekwa katika Katiba yao. Kiwango hicho cha Riba kinatakiwa kuwa chini ya wastani wa viwango vinavyotozwa na Mabenki na Taasisi nyingine za Fedha na isiwe ndogo sana kwa sababu kadhaa ikiwemo ukuaji wa Mtaji wa Kikundi, uwezo wa W/chama kulipa na mwisho wa mwaka W/chama kupata faida kutokana na Akiba zao. Kwa misingi hiyo INASHAURIWA Riba iwe kati ya 5%-10%. Kama Kikundi kikiendeshwa vizuri kwa maana ya uwekaji wa Akiba mzuri, ukopaji na urejeshaji mzuri, n.k., basi inatarajiwa kuwa "faida" itakayokuwa imepatikana mwishoni mwa "Mzunguko" iwe kati ya 30%-40%. Tuendelee kueleweshana!
 
Mkuu Nyenyere, inawezekana kabisa ulielewa vizuri kilichoelezwa kwenye Darasa hilo, tena sana. Tafadhali fahamu kuwa, kutokana na ukweli kuwa Mfumo wa HISA (VICOBA/VSLA) umeonyesha mafanikio ya juu sana kwenye Malengo yake ya Msingi hasa lile Lengo la kupeleka na kumfikishia Mwananchi huduma za kifedha mahali ambapo huduma hizo zinazotolewa na Mabenki na Taasisi mbalimbali za kifedha (Micro Finance Institutions) haziwezi kumfikia, "Makanjanja" wameuingilia, wameubaka, wameuchakachua Mfumo huu kwa manufaa binafsi wenyewe. Hili linakuwa rahisi kwa kuwa uendeshaji wa Mfumo wa HISA "sio rasmi" - Hakuna Sera yoyote rasmi ya Serikali inayovisimamia, na wahanga ni Wananchi wasionacho, wenye elimu duni, shida kibao na ambao ni rahisi kutapeliwa na kudhurumiwa.

Hivyo, kwa ufahamu wangu, hakuna Benki yeyote iliyoteuliwa "kusimamia Vikundi vya HISA" na UYAKODE hawana dhamana ya kusimamia Vikundi vya HISA hapa Nchini. Huenda wakawa wanasimamia Vikundi ambavyo ni Wanachama wao, hilo haliwahalalishi wao kusimamia Vikundi vilivyo katika Mfumo huo. Huenda Masomo mliyopewa ilikuwa ni sehemu ya Benki hiyo kwa kushirikiana na UYAKODE, kujitafutia Wateja, na kwa mantiki hiyo Somo lao lililenga kuwarubuni hivyo.

Ninaomba nigeukie suala la Mwanachama na Kikundi cha HISA kulazimishwa kuwa na Akaunti ya Binafsi na ya Kikundi Benki. Moja ya Malengo ya Msingi ya Mfumo wa HISA ni kupeleka huduma za kifedha kwa Watu ambao Huduma za Benki na zile zinatolewa na Taasisi nyingine za Fedha, zikiwemo MFIs, haziwezi kuwafikia. Hapa tunaongelea watu ambao uwezo wao wa kujiwekea Akiba ni mdogo na au haupo kabisa, wanaoishi Vijijini na Mijini, Watu ambao hawana dhamana inayowawezesha kupata Mikopo Benki na kwenye Taasisi nyingine za Kifedha na Watu ambao ni gharama kubwa sana kwa Taasisi hizo za kifedha kuwafikishia huduma za Kifedha.

Chukulia kwa mfano, Mtu anakiji-mghahawa chake kijijini umbali wa Kilomita 20 kutoka Mjini kwenye huduma za kifedha. Akiba anayoweza kujiwekea Benki kutokana na biashara yake ni Sh. 500/= kwa siku baada ya kutoa gharama za uendeshaji wa mghahawa wake na maisha yake binafsi. Nauli ya kwenda na kurudi mjini ili kuhifadhi hiyo akiba yake ni Sh. 2,000/=. Ili asafiri kwenda Benki Mjini, atalazimika kufunga Mgahawa wake kwa masaa kadhaa na inawezekana siku nzima. Akifika Benki atalazimika kujaza karatasi, kujipanga foleni na, pengine, kuvumilia "unyanyapaa" wa Wafanyakazi wa Benki hasa kwa Mtu anayetaka kuweka kiasi kidogo cha Fedha.

Hivyo kwa Mfano huu mdogo sana, Mfumo rasmi wa Benki na Taasisi nyingine za Fedha hazipo kukidhi mahitaji ya Masikini huyu.

Hapa ndipo Mfumo wa HISA unapata nafasi ya kuziba hilo pendo. Kwa maana ya kumwezesha Mtu huyu kwenye Mfano huo, kuweka akiba yake kwenye Kikundi chake cha HISA, na kutumia Akiba hiyo kama Dhamana ya Mkopo kwa ajili ya kuendeleza shughuli yake na au kukidhi mahitaji yake ya msingi. Kumbuka, kama ilivyoelezwa na Wachangiaji hapo kabla, Kikundi cha HISA kinaundwa na Wanachama wanaofahamiana na wanaokubaliana kwa hiari yao binafsi kuunda Kikundi hicho. Hivyo Akiba ya Wanachama, na kwa kiasi kidogo mapato mengine madogomadogo kama faini za Kikundi zinazotozwa kwa Mwanachama anayevunja Kanuni na Taratibu za Kikundi, ndiyo inyotengeneza Mtaji ambao unatumiwa na Kikundi kukopesha Wanachama wake. Kiasi cha Mkopo unaotolewa na Kikundi, kwa Mwnachama wake, kina uhusiano wa moja kwa moja na kiasi cha Akiba alicho nacho Mwanachama kwenye Kikundi. Hivyo inashauriwa, Kiasi cha Mkopo kisizidi mara tatu ya jumla ya Akiba (HISA) aliyonayo Mwanachama kwenye Kikundi. Hapa kuna maelezo zaidi.

Riba inayopatikana kwenye Mikopo inarudishwa na kutumika kutunisha Mtaji wa Kikundi kwa ajili ya kutoa Mikopo zaidi kwa Wanachama wake. Mwisho wa Kipindi ambacho Kikundi kinakuwa kimekubaliana wakati wa kuanzisha Kikundi, Kipindi ambacho huitwa "Mzunguko" na ambacho inashauriwa iwe miezi 9 - 12, madeni yote hurejeshwa, hesabu hu[pingwa ili kujua Kikundi kimetengeza "faida" kiasi gani, na faida hiyo hugawanywa kwa Wanachama kwa kuzingati ukubwa au udogo wa Akiba aliyenayo Mwanachama katika Kikundi. Hivyo "aliyepanda Kingi kama Akiba, anavuna kikubwa kama Faida, na aliyepanda kidogo kama Akiba/HISA, anavuna kidogo kama faida".

Nimeandika hayo yote kwa sababu mimi ni mnufaika wa miaka kadhaa wa Mfumo wa HISA, ninaumia kuona "makanjanja" wakiwemo Mabenki, Taasisi na Makampuni ya Biashara yanachakachua Mfumo huu wa akili ya kutengeza faida kwa migongo ya fukara na masikini na kwa ajili ya kuchokoza Mada ili Wataalamu wenye Ujuzi uliobobea katika Mfumo huu wajitokeze kutuelemisha.

Wasipojitokeza, nitaendelea kuandika ninachokifahamu ambacho kinaweza kuwa sio sahihi sana kutokana na mabadiliko na maboresho makubwa yanayoendelea kila kukicha katika Mfumo wa HISA!
 
Ili kuendelea kuchokoza Wataalamu wa Mfumo wa HISA/VSLA na kadhalika ili waje hapa kutupatia Elimu juu ya HISA ili tunufaike, ninaomba nikamilishe siku kwa kuweka hadharani "fomula" inayotumika kukokotoa Mahesabu ya Mwanachama anayeacha Uanachama katika Kikundi cha HISA kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake, kwa mfano kifo cha Mwanachama, kuhama makazi kutokana uhamisho wa kikazi, n.k.:

Hatua ya 1: Kukokotoa ili kupata Thamani halisi ya HISA moja kwa wakati hupo. Kwa mfano, kama thamani ya HISA moja iliyopangwa na Kikundi ni Sh. 1,000/=, thamani halisi ya HISA hiyo haitabaki hvyo, itabadilika kwa sababu HISA zilizokusanywa zimetumika kwa ajili ya Mikopo kwa Wanachama ambayo imekuwa inarejeshwa pamoja na Riba. Hivyo Thamani ya HISA haitabaki kuwa Sh. 1,000/= bali itakuwa imeongezeka (au imepungua kama Kikundi kimetengenza hasara). Hivyo, ili kukokotoa thamani halisi ya Kikundi katika muda huo, "fomula" ifuatayo inaweza kutumika:

(Fedha zilizopo + Mikopo - Madeni ya Kikundi) / Jumla ya HISA za Wanachama


Hatua ya II - Kukokotoa ili kupata Malipo ya Mwanachama anayeacha Uanachama:


(Jumla ya HISA za Mwanachama Husika X Thamani Halisi ya Thamani Moja) - Madeni na Salio la Mkopo wa Mwanachama Husika


Hatua ya III: Malipo kwa Mwanachama Husika.


Ikumbukwe kuwa "fomula" hiyo inayowezesha Mwanachama kulipwa Akiba/HISA zake pamoja na faida ni kwa Mwanachama anayeacha Uanachama kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake. Mwanachama anayeacha kwa Uanachama kwa ridhaa yake na anayefukuzwa Uanachama, huyo atalipwa HISA zake tu bila faida baada ya kuwa madeni na mkopo wa Kikundi vimelipwa.

Ninasubiri Wataalamu waje kunielewesha zaidi!
 
very
useful thread in deed.

big up kwa Chasha na wengine waliotoa ujuzi wao.

naomba kuuliza utaratibu gani hutumika kugawana fedha mwisho wa mwaka
ukizingatia hisa za wanachama zinatofautiana?

je utaratibu gani unatumika kukopesha, haiwezekani kufikia mahali
mwanachama akahitaji mkopo na kiasi kikubwa cha fedha kikawa kiko
mikononi mwa wakopaji wa awali? (kanuni na vigezo vya kukopesha ni vipi,
ili kuzuia malalamiko na upendeleo kwa baadhi ya wanachama)
 
Last edited by a moderator:
very
useful thread in deed.

big up kwa Chasha na wengine waliotoa ujuzi wao.

naomba kuuliza utaratibu gani hutumika kugawana fedha mwisho wa mwaka
ukizingatia hisa za wanachama zinatofautiana?

je utaratibu gani unatumika kukopesha, haiwezekani kufikia mahali
mwanachama akahitaji mkopo na kiasi kikubwa cha fedha kikawa kiko
mikononi mwa wakopaji wa awali? (kanuni na vigezo vya kukopesha ni vipi,
ili kuzuia malalamiko na upendeleo kwa baadhi ya wanachama)

VIKUNDI VYA HISA.
- Historia yake- Historia yake ilianzia Africa katika nchi ya Niger miaka ya 1994, ndo mfumo huu ulianza, na kwaBongo uliingia mwaka 2001 Kule Zanzibar so unaweza tambua ni kwa nini mfumo ulianzia Niger na ni kwa nini kwa Tanzania ulianzia Zanzibar.

Kwa sasa Mashirika yanayo endesha huu mfumo yako mengi sana Duniani kuyataja machache.

1. CARE INTERNATIONAL- Mwanzilishi wa mfumo wa hisa Duniani

2. OXFARM INTERNATIONAL

3. WORLD VISION INTERNATIONAL

4. PLAN INTERNATIONAL

5. CRS INTERNATIONAL

6. AGAKHANI FOUNDATION

7. PATHIFINDER INTERNATIONAL

8. OGUTU- VICOBA-

yako mengi sana hayo ni machache tu. Na kila shirika linaedesha linvyo jua yaani wanazidi kumodify

UNUNUZI WA HISA
-Kikundi hupanga chenyewe thamani ya hisa moja na kuna vikundi utakuta vina kuwana hisa moja Tsh 500-50,000 kutegemerana na uwezo

MIKUTANO
- Ni kila wiki lazima vikundi vikutane but kwa sasa kutokana na kukua kwa teknolojia kikundi kinaweza kikawa kinakutana kwa mezi mara moja na kila wiki watu wakawa wananunua hisa zao kupitia M-PESA, TIGO PESA,AIRTELL MONEY NA KAZALIKA.
Kwa sasa vikundi vinaweza kuwa vina operate kwa kutumia MPESA.

MFUMO MZIMA
.

vsla-members-in-kisarawe-demonstrating-to-the-plan-ceo-nigel-chapman-how-the-vsla-box-is-opened-and-organised



1. Mwenyeki wa kikundi-Huyu anasimamia mikutano na nizamu ndani ya kikundi

2. Katibu w akikundi- Huyu anatunza au kuandik kumbukumbu za kikundi kama maheabu na kazalika.

3. Mweka hazina-Huyu anatunza sanduku la kikundi pekee yeye anatakiwa kutunza anduku la kikundi lenye pesa n vifaa vingine vya kutumia

4. MWEKA HAZINA A KWANZA

5.MWKA HAZINA WA PILI- Hawa ni kuhesabu fedha za kikundi

Hapa utaona kuna uwazi wa hari ya juu kabisa kwa sababu kuu tano

1. Mwenyekitu wa kikundi haruhusiwa kujishughulisha na pesa za kikundi yeye ni kutunza nidhamu pekee.

2. Katibu wa kikundi- Haruhusiwi kushika pesa ya kikundi yeye ni kuandika tu.

3. MWEKA HAZINA WA KIKUNDI- Haruhisiwi kushika pesa ya kikundi yeye ni kutunza sanduku likiwa limeisha fungwa.

4. WAHESABU FEDHA- Hawa ndo pekee wanahesabu fedha za kikundi ila hawawezi kuzitunza, anaye tunza ni mwingine



MIKOPO
- Mikopo hutolewa kila Mwezi hivyo kwa wiki tatu huwa ni makusanyo tu/kununua hisa na wiki ya nne ni Mkopo
MAREJEHO.
- Ni kila mwezi, hivyo utaona siku ya kutoa mkopo kabla ya mkopo ni lazima kwanza kikundi kukusanye marejesho kutokakwa walio kopa siku za nyuma.

RIBA/ZIADA.
-Hapa ni kwamba kikundi hupanga chenyewe Ziada ya mkopo wake na vingi huwa ni 5%-10%

ZIADA- Vikundi vya hisa havitumii Riba bali huitwa Ziada ya mkopo na kuna sabau za kwa nini inaitwa ZIADA YA MKOPO BADALA YA RIBA

KUGAWANA

- Baada ya majuma 52 kikundi hugawana pea zao zote na kunaza upya, Vikundi vya hisa huwa havitumii kalenda huwa vinenda kwa mikutano, hivyo kikundi kikianza Tarehe 25/5/2012, si kwamba Tarehe 25/5/2013 kitagawana au kumaliza mwaka.
Tunatumia mikutano walio kaa inatakiwa mikutano ifikie 52, ukitumia kalenda kun wakati hua hawakutanikutokana na sababu mbali mbali kama misiba na kazalika.

MAHESABU YA MGAO

-Yatapigwa kwa kutumia kanununi hii.

1. Jumla ye fedha zote za kikundi- Madeni kikundi kinadaiwa/Kwa jumla ye hisa zote.

MFANO: jumala ya fedha za kikundi ni Tsh 7,000,000 na jumla ya hisa zote ni 5000
7000000/5000
Hapo utapata hisa mpya ambayo itatumika kuzidisha na kila hisa zakila mtu.

VIKUNDI HUWA HAVIGAWANI SAWA KWA SAW, HUWA MWENYE HISA NYINGI NDO ATAPATA PESANYINGI KULIKO MWENYE HISA CHACHE
 
Nimeipenda mada.....je, huu mfumo wa M-pesa uliokuwa kwenye majaribio ushathibitishwa? Kwa sasa inawezekana kikundi kuitumia hiyo huduma ya M-pesa? Mitandao mingine inao utaratibu kama wa M-pesa? Asanteni wadau.
 
wakuu hongereni kwa huu uzi, ni wa zamani lakini una faida sana...ila hapa kuna kitu sijaelewa kwa mtoa mada na wenginewe...naona kama VSLa na VICOBA mmefanya kuwa kama kitu kimoja, je inamaana hamna utoafauti wa hivyo vitu? kama hamna utofauti kwanini vina majina tofauti....VSLa waanzilishi ni care internationa je VICOBA waanzilishi ni kina nani?
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom