Ifahamu VSLa (Village Saving and Loan Association) / VICOBA

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,912
IFAHAMU VSLa(VillageSaving and Loan Association)/VICOBA

- Watu wengi wamekuwawakisikia hili neon na kuna wanao fahamu, VSLa ni Vikundi vya Hisa ambavyo kwajina jingine wanaita VICOBA, hivi ni vikunndi vinavyo undwa na wakina Baba,wakina mama, na hata vijana,

- MASHILIKA YENYE KUTOA HII HUDAMA HAPA TANZANIA,

Vikundi vyahisa ni kitu ambacho ni hot sanakwa sasa na kuna mashirika kibao yanatoa hii service na mengi ya hayo ni yakutoka nje ya nchi yaani Intetnational Organization

a. CareInternational- hawa ndo waanzilishi wa VICOBA
b. Planinternatinali
c. Oxfarm USA
d. CRS
e. AGAKHANFOUNDATION
f. VICOBA
g. Fhi
h. TASAF

- Hayo ni moja ya mashirika machache yanayo toa hiihuduma hapa Tanzaniaingawayako mengi sana

HISTORIA YA VICOBA/VSLa

- Huu mfumo ulianziahuko NIGER mwaka 1994 na ulibuniwa na Care Internatinal, Care wana operatekaribia Dunia nzima, Nigerndipo huu mfumo wa VICOBA/VSLa ulipo asisiwa

- Kwa nini NIGER?

- Kule Niger wanawakewalikuwa wananyanyaswa sana na waume zao, na ukiingatia NIGER ni nchi yaKisilamu, so huo unyanyasaji ndo ulifanya Care wakabuni kitu cha kuwa saidiahawa wakina Mama, ndo wakabuni VSLa ambapo wakina mama walikuwa wakiundavikundi vayao na wanakuwa wanachangiana kwa kununua hisa na kukopeshana

-

TANZANIA
- Huu mfumo kwa Tanzaniauliletwana Care na ulianzia Zanzibarkwamara ya kwanza and then uka sambaa hadi Bara
- Kwa Care pekee yake kunazaidi ya VIKUNDI 40,000 50,000 vya hisa Tanzaniakote na unafanya kazi katika Mikoa kama Arusha, Tanga, Manyara, Kilimanjaro,Singida, Dodoma,Morogoro, Pwani, Mwanza,Shinyanga, Kigoma, Dar, naZanzibar

JINSI MFUMO WAVICOBA/VSLa UNAVYO FANYA KAZI

1. Kwanza kuna kuwa na kikundi cha watu 15- 30
2. Wanakutana kila Wiki
3. Wanaluwa na vioongozi waowatano, Mwenyekiti,Katibu, mweka hazina na wahesabu fedha wawili
4. Wanakuwa na katiba yao
5. Wanakuwa na sanduku lakufungwa kwa kufuli Tatu
6. Hili sanduku linatunzwa namweka hazina wao
7. Ila anaye Tunza sandukuhawezi kulifungua make kuna watu wengine wa tatu wanao tunza Funguo za sanduku
8. Kikundi kinapanga thamani yahisa
9. Wanakuwa na mfuko wa jamii
10. wanakuwa wanatoa mikopo kwa wanachama wake
11. Mwisho wa mwaka wanagawana fedha zote

HIVI VIKUNDI VYA HUSA, VSLa/ VICOBA
- Kikundi kinaweza pangathamani ya hisa yake moja kuna baadhi ya vikundi vinatumia thamani kubwa navingine thamani ndogo
a. 500
b. 1000
c. 2000
d. 3000
e. 5000
f. 10,000
g. 15.000
h. 20,000
- Inategemeana na uwezo wa wanakikundi husika, Hapani kwamba kila wiki mtakuwa mkinunua hisa Tanzo so kama limit ya wiki ni hisaTano maana yake kamahisa moja ni Tsh 20,000 kwawiki utatoa Tsh 100,000 kununua hisa Tano
- Na si razima ziwe hisaTano unaweza nunua Moja, au Mbili au Tatu ila haitakiwi kuvuka Tano

- MIKOPO KWENY HUU MFUMO WA VICOBA/VSLa

- Mikopo yake inatolewakwa members peke yake, na mwana kikundi ana uwezo wa KUKOPA MPAKA MARA TATU YATHAMANI YA HISA ZAKE, kamasiku ya Mkopo wewe hisa zako zina thamani ya Tsh 500000 basi utakopa Tsh1,500,000 limiti
- Hii ni ili kudhibitiwatu wasio nunua hisa nyingi kukopa pesa nyingi
- Mikopo inatolewa kilabaada ya wiki nne

- RIBA ZA HII MIKOPO

- Vikundi vingi vinatoza5% vingine 10% ila limiti ni 10% so hii inapigwa kwa mwezi, means marejeshoyanafanyika kila mwezi

-KUGAGAWANA FEDHA ZA KIKUNDI
- Inapo fikiamwisho wa mwaka au majuma 52 kikundi kitagawana fedha zake zote hapa kikundikilicho kuwa siriasi unakuta kina hadi MILIONI 100 AU MIA 50
- kikundihakitagawana kwa pasu no Kuna mahesabu yake na yule mwenye hisa nyingi ndoatakaye pata pesa nyingi kuliko wengine

- JE HIVI VIKUNDI NI KWA VIJIJINI TU?
- Jibu ni hapana KuleTanga nilitembelea kuna hadi wahindi kwenye hivi vikundi inategemeana tu nathamani ya hisa yenu moja
- Kuna watu wanamilikimagari na miradi mikubwa bado wako kwenye hivi vikundi,
- SO HIVI VIKUNDI VIKPHADI MIJINI TENA NDO VINAFANYA VIZURI

- JE NI KWA MASIKINI PEKEE?
- Jibu ni HAPANA ingawalengo la kubuniwa lilimanisha hivyo, ila kwa sasa hadi matajiri wamo na kunawanao nunua hisa moja Tsh LAKI MOJA

- JE NI LAZIMA KUKUTANA KILA WIKI?
- Jibu ni hapana, mnaweza kukutana kila mwezi, VODACOM wametoa mfumo wa kuoperate kwa M-PESA hatamkiwa mbali mbali mnaweza operate

-JE INAFANANA NA SACCOS?
Kuna mfananoFulani ila kuna vitu vichache vinatofautiana, SACCOS inaweza toa mikopo kwawasio members lakini VICOBA haiwezi, wanachama wa SACCOS wanaweza kuwa hata mialakini VICOBA/VSL ni 30 limit

KAMPUNIYA VODACOM(M-PESA) NA TIGO(TIGO PESA WATENGENEZA LAINI MPYA KWA AJILI YA HIVIVIKUNDI

-Wakuu hi indohabari njema kabisa, kwa sasa Kampuni ya VODACOM wametoa laini special kwaajili ya hivi vikundi vya HISA/VICOBA/VSL na inafanyiwa kazi katika mikoa yakanda ya Kaskazini
Vikundivinaoperate kupitia M-pesa, haina haja ya kukutana kila wiki,

WAKUU NITAWAPA MAELEZO ZAIDI NA ANAYE TAKA INFORMATION ZAIDI ANAWEZA KU NIPM

nitakutafuta unipe maelezo ya jinsi huu mfumo unavyo fanya kazi, napenda sana hii jambo, ningependa ufafanuzi kwenye, mikopo, huo mfumo wa M -PESA, na jinsi ya ku operate
 
nitakutafuta unipe maelezo ya jinsi huu mfumo unavyo fanya kazi, napenda sana hii jambo, ningependa ufafanuzi kwenye, mikopo, huo mfumo wa M -PESA, na jinsi ya ku operate

Mkuu kwenye swala la

1. MIKOPO- KIKUNDI HUWA KINATOA MIKOPO KWA WANACHAMA WAKE NA KAMA THAMANI YA HISA YENU NI KUBWA MTU ANAWEZA KUKOPA HADI MILION 10,
Mfano: wewe ukiwa na hisa zenye thamani ya Milioni 1 basi unaweza kopa hadi milioni 3

2. M-PESA- Huu nfumo unafanyiwa majaribia MIKOA ya arusha na Kilimanjaro na kuna watalamu kutoka benki ya Dunia waliwahi kuja kucheki huu mfumo ulivyo make haupo mahali popote pale Duniani na VODACOM wametengeneza laini special kwa ajili ya huu mfumo, hizi laini zina mfumo tofauti na tunazo zifahamu
- Hii itasaidi wana chama ku operate wakiwa hata mabali

3.
 
This is wonderful, helpful and will always make JF entrepreneurs think about VICOBA. Keep inspiring KOMANDOO. But kuna vitu sivioni hapa, hivyo nimeona ni busara kuviongezea

MTAJI
Sehemu kubwa ya mtaji wa VICOBA inatokana na michango ya wanachama kupitia hizo HISA alizosema KOMANDOO, hivyo hakuna external saving or crediting partner apart from the village bank members. Lakini external partners wanaweza wakasupport VICOBA kwa kutoa seed money kupitia donations, gifts, fundraising campaigns and sometimes soft loans that can be afforded by the group. (kama anavyofanya Mwenyekiti wa IPP)

MAFUNZO
Mfumo huu wa VICOBA (haswa vikundi vya watu walio na upeo mkubwa) huwa una package ya mafunzo ya ujasiriamali kwa wanachama wake, kwani miongoni mwa mambo yanayosababisha wengi wao kushindwa kurejesha mikopo na kukwamisha maendeleo ya kikundi ni ukosefu wa masoko na elimu ya ujasiriamali.

USHAURI
Hii ni njia sahii ya Watanzania kujikwamua kiuchumi kwani wanaweza kuwekeza kwa pamoja kile kidogo walichonacho, na kila mmoja kwa nafasi yake anaweza kuwekeza kutokana na Mkopo atakaoupata
 
MKUU

1.MTAJI- Ni kweli mtaji unatoka kwa wanachama na kila mwanachama hupambana kununu hisa za kutosha ili akope zaidi, na hii ni kupitia kununua hisa,
NJIA ZINGINE ZA MITAJI
- Hisa
- RIBA
- FINE
- ,MIRADI
1. RIBA- Kikundi hutengeneza pesa sana kupitia riba na faida ya hapa ni kwamba hizi RIBA hazitoki nje bali hubakia ndani ya kikundi

2. FINE- Fine nazo hutengeneza faida

3. miradi ya kikundi, kuna vikundi vinakuwa na MIRADI ya kikundi hii ni moja ya njia nzuri sana ya kukuza mitaji ya kikundi, kuna vikundi vinakuwa na MIRADI YA KUKU, MAGARI, MASHAMBA, MASHINE ZA KUSAGA NA KAZALIKA

2. MAFUNZO
KUNA MAFUNZO 8
1. Uuundwaji wa kikundi
2.kuweka kanununi mbalimbali
3. Katiba
4. Jinsi ya kuendesha mikutano
5. Jinsi ya kukunua hisa na mfuko wa jamii
6. Jinsi ya kukopa
7. Jinsi ya kurejesha
. Na jinsi ya kugawa
 
kuna tofauti ya vicoba na saccos?

Ya kuna vitu vinafanana na kuna vitu vinatofautiana

1. UFANANO
- Hisa, kote kuna kununua hisa
- Mikiopo kote kuna kutoa mikopo
- Miradi inakuwepo kwa sehemu zote SACCOS NA VSLa

2. UTAFAUTIONA
- VICOBA/VSL- haifuatiliwi na serikali kama ilivyo SACCOS
- Wanachana wa VSL ni wachache ukilinganisha wa SACCOS
- Uwazi- Vikundi vya hisa vinaendeshwa kwa uwazi wa hali ya juu ukilinganisha na SACCOS
- VIKUNDI VYA HISA VINATUMIA SANDUKU/BENKI/M-PESA- SACCOS HUTUMIA BENKI TU
- vikundi vya HISA hukutana kila wiki, SACCOS sio lazima
- Vikundi vya HISA kwa sasa vinaweza kuendeshwa kwa njia ya M-PESA
 
Asante kwa maelezo ya kina mkuu. Lakini nahisi ssomething is missing here. Kwa jinsi ninavyofahamu mimi (niliwahi hudhuria mafunzo kwa wiki tatu) vikundi hivi vinalelewa na taasisi inayoitwa UYAKODE? (spelling zinanitatiza). Hawa wanakuwa responsible kuwatafutia ufadhili wa miradi (na hapo ndipo yanaingia yale mashirika uliyoyataja). Nakumbuka nikiwa kwenye semina ilitolewa taarifa kuwa amepatikana mfadhili aliyetayali kutoa boti za uvuvi nne kama kikundi kitaridhia kufanya mradi huo. Wanachama wakakataa kwamba hawataweza kuzisimamia.

Pia kulikuwa na suala la kufungua akaunti. KIA MWANA KIKUNDI NI AZIMA AWE NA AKAUNTI TWIGA BANKCORP. Bank hii ndio yenye kibali cha kuoperate akaunti za VICOBA, hivyo kuna ushiriki wa serikali directly. Pia akaunti ya kikundi inafunguliwa huko, hivyo VICOBA haifi, tofauti na maelezo yako. Mwishoni mwa mwaka mnapiga mahesabu na kugawana faida. Kila mtaji unapokua ndio miradi mikubwa hufunguliwa. VICOBA ya kwanza kabisa Dar inamiliki jengo la ghorofa nne. Hisa za VICOBA hurithiwa na ndio maana mojawapo ya mambo muhimu kabisa katika documents za mwanachama ni jina la mrithi! Pia kuthibitisha haya, jaribu kutafuta vikundi ambavyo vina miaka mingi, ni vigumu sana kujiunga hata kama member mmoja atakuwa anajitoa, kwa sababu ya ada kubwa sana ya kiingilio (wamewekeza kwa muda mrefu mno and you have to march them!).

Again thank you so much for such a useful post.
 
Mkuu wewe ndo hujanielewa kabisa na Rudia kusoma Maelezo yangu hapo Juu utanielewa vizuri sana

Mkuu huu mfumo wa Hisa ni mpana sana na usizani kwamba unafanya kazi hapa Tanzania pekee, Labuda kwa kifupi baadhi ya Nchi za africa na Asia na Amerika kusini

KWA AFRICA
1. Niger
2.Ghana
3Tanzania
4.Kenya
5. Malawi
6. Uganda
7. South Africa
Na zingime nyingi

Asia kuna
1. India
2. Thailanda
3. Philipine
4. Bangaladeshi
5. China

Na zingine nyingi

So mkuu VICOBA ni shirika na huna mashirika mengi sana yanayo endesha hivi vikundi vya hisa na huwa wanafadhiliwa Mfano kuna Mradi wa Vikundi vya Hisa vya Shirika la care, huo mradi ulikuwa unafanya kazi katika Mikoa mi nne, Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara, na ilikuwa inafadhiliwa na Bill and Melinda Get Foundation,

Na kuna mifumo mingi sana ya ku oparate hivi vikundi vya hisa
 
Basi lile darasa nililopata kwa kuhudhuria lilikuwa la uongo. Kwani ilisemwa kuwa mfumo huo unasimamiwa na serikali through BANKCORP na si kila watu wanajiendeshea bila usajili (kama ie ya kuzungusha hela kwa wiki). Pia tulielezwa kuwa sserikali inassimamia VICOBA kupitia shirika liitwalo UYAKODE. HII NI KWA TANZANIA. Hizo nchi nyingine sina interest. Inawezekana sikuelewa vema.
 
nimeipenda sana hii maada coz niemjifunza mengi niliyo kuwa siyajui kabisa by the way unaweza kupitia huku Welcome — Social and Economic Development Initiative of Tanzania - SEDIT maana kuna vitu nimeviona katika pita pita yangu nimevikuta mnaweza pitia pia keep blesed
 
Basi lile darasa nililopata kwa kuhudhuria lilikuwa la uongo. Kwani ilisemwa kuwa mfumo huo unasimamiwa na serikali through BANKCORP na si kila watu wanajiendeshea bila usajili (kama ie ya kuzungusha hela kwa wiki). Pia tulielezwa kuwa sserikali inassimamia VICOBA kupitia shirika liitwalo UYAKODE. HII NI KWA TANZANIA. Hizo nchi nyingine sina interest. Inawezekana sikuelewa vema.

Hivi vikundi vinaendeshwa na Mashirika Binafisi hata hao VICOBA ni shirika wanajiita OGUTU, na hata wewe unaweza anzisha kikundi chako cha hisa au ukaanzisha vikundi vya hisa ni rahisi sana na huwa havina ghalama za uendeshaji kama ilivyo vikundi vingine kinacho takiwa huwa ni

1. Kikundi cha watu 15 mpka 30

2. Wawe na sanduku la kufungwa na kufuri tatu

3. Wawe wanakutana kila wiki ingawa hata kila mwezi inawezekana

3. Wawe na viongozi watano

4. Wawepo wahika funguo watatu ambao wao watakuwa wakitunza funguo za sanduku, so anaye tunza sanduku hana funguo za kufungulia na ili sanduku ifunguliwe ni lazima wawepo washika funguo waote wa tatu

5. Wawe na katiba

6. Wanapanga wenyewe thamani ya hisa moja

Hayo ni machache ila yako mengi sana

- Hivi vikundi mkiwa mnajuana ni vizuri sana na wengine mweisho wa mwaka hujikuta wana hadi milioni 60
 
Mkuu KOMANDO.
SACCOs zilipokuwa zinaanzishwa,lengo lilikuwa kutumia uwezo wa ndani katika working capital zao.
Lakini, kutokana na kuongezeka kwa wingi wa wanachama na wateja wao, wamekuwa wakichukua mikopo katika benk na vyanzo vengine vya kukopesha taasisi za fedha.
VICOBA nao wanaweza wakapata mikopo kutoka katika vyanzo vya kukopesha taasisi za fedha (kama OIKO CREDIT, CRDB, NMB, PPF, NSSF)?
 
Mkuu inawezekana kabisa kukopa Benki na vipo vingi sana vinavyo kopa benki, FAIDA ZA HIVI VIKUNDI

1. Vinawafanya/vinawajengea wanachama uwezo wa kuweza kukopa katika Mabenki kwa sababu tiyali wanakuwa wano uzoefu

2. Riba zainakuwa ni mali yao na hiztoki nje ya kikundi- Hapa ni wakiwa wanakopeshana wao kwa wao

3. Uwazi

OK BACK TO THE TOPIC

- Kuna jambo moja lazima mlijue, VIKUNDI HIVI VYA HISA WANATOZANA RIBA KUBWA KULIKO HATA MABENKI, Mfano kwenye Kikundi ukikopa 50,000 kwa riba ya 5% unatakiwa kurejesha huu mkopo ndani ya miezi miatatu na hii riba inapigwa kila mwezi,
MFANO
1. Nimekopa laki moja 100,000 riba ni 10% na natakiwa kuirudisha ndani ya miezi mitatu hivyo

- MWEZI WA KWANZA NAWEZA REJESHA 10,000/ pekee hapa nitabakiwa na Mkopo 100000 na nitapigiwa riba ya 10% tena kwa mwezi wa pili
- Mwezi wa pili nilileta 10,000 tena itabakiwa 100000 mkopo na nitapigiwa riba tena kwa mwezi wa mwisho hivyo

- Mwezi wa tatu nitatakiwa kuleta 110,000 nimalize mkopo

MFANO MWINGINE

- Nikikopa 100000 laki moja na riba ya 10%

1. Mwezi wa kwanza naweza rejesha 50,000/ Hapo katika 110, 000/ ninayo daiwa itakuwa imebakia 60,000 hivyo basi kwa mwezi wa pili nitapigiwa riba kwenye hiyo 50,000/ so 10% yake itakuwa sh 5000/

Hivi vikundi vinatumia reducing balance katika kukokotoa mikopo yao

So mkuu vikundi vingi sana vinakopa na si kukopa tu kuna vyenye miradi mikubwa sana na kuna vyenye pesa kuliko hata SACCOS na nitolee mfano vikundi fulani vilivyoko chini ya Shirika la Care International, hivi vikundi kuna ambavyo vimeunganishwa na huduma ya M-PESA NA kampuni ya VODACOM wametengeneza laini special kwa ajili ya hivi vikundi yaani hizo laini zina progaram tofauti na hizi laini zingine na ni special kwa hivyo vikundi vya Hisa,

-Na kuna baadhi ya Vikundi vimeunganishwa na Benki sitaki kuitaja jina, na vimeunganishwa na TIGO PESA vilevile so Kikundi kikikopa Benki kinachukua mkopa wake through TIGO PESA na kikundi kikifanya marejesho vilevile kinatumia TIGO PESA KUPELEKA MAREJESHO YAO BENKI, hakuna kwenda kupanga foleni Benki

- Na hii systeam ya vikundi vya hisa kutumia mfumo wa simu ni ya kwanza DUNIANI NA ina fanyiwa study huku Tanzania na WALISHA KUJA HADI WATALAAMU WA BENKI YA DUNIA KUSTADY HII KITU

SO MKUU MNAWEZA KOPA BENKI TENA VIKUNDI HIVI VINAKUWA TRASTED
KULIKO HATA SACCOS NA WANACHAMA WANAKUWA NA UZOEFU WA HALI YA JUU KATIKA MASWALA YA RIBA
 
mkuu nimekusoma.
Vipi kuhusu uendeshaji wa hivi vikundi? vinategemea zaidi msaada wa weledi kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali kama CARE international na mengine.
vinajengewaje uwezo wa kujiendesha venyewe ili vidumu zaidi ili misaada ya taasisi kama hizo za care international itakapositishwa, viwe na uwezo wa kujiongoza venyewe?
 
Mkuu, VSL ni vikundi ambavyo vinaweza kujiendesha vyenyewe bila misaada kutoka nje, Hata hayo mashirika niliyo yataja si kwamba wanatoa pesa kuendesha bali wanatoa elimu PEKEE, hivi vikundi vinajiendesha vyenyewe

1. KIKUNDI HUPANGA THAMANI YA HISA

2. KIWANGO CHA JUU CHA HISA ZA KUNUNUA KWA WIKI NI 5

3. MWANACHAMA ANAWEZA KUNUNUA HISA MOJA MPAKA TANO MWISHO

4. KAMA HISA MOJA NI TSH 2000 SO KWA KILA KIKAO MWANACHAMA ANAWEZA NUNUA
HISA 5 ZENYE THAMANI YA SH 10000
HISA 4 ZENYE THAMANI YA SH 8000
AU HISA 1 YENYE THAMANI YA SH 2000

5. KILA MWANACHAMA ANAKUWA ANANUNUA HISA KWA MANUFAA YAKE

MIKOPO

1. KWENYE KUKOPA MWANACHAMA ANAKOPA MPAKA MARA TATU YA THAMANI YA HISA ZAKE SO KAMA HISA ZAKO ZINATHAMANI YA TSH 500,000 UNAWEZA KOPA HADI 1,500,000

RIBA
1. KIKUNDI HUPANGA RIBA YAKE MFANO 10% NDO KIWANGO CHA JUU KABISA

FAIDA

1. KIKUNDI HUTENGENEZA FAIDA KUPITIA NJIA HIZI

- RIBA- hii ndo njia kuu ya kutengeneza faida
- FAINI- faini mbalimbali ambazo wanachama hupigwa nazo ni faida kwa kikundi
- MIRADI YA KIKUNDI
- ZAWADI/MISAADA

HIVYO IKIKUTA KIKUNDI KINA TSH 90,000,000 SI KWAMBA WAMEPEWA NO NI KUPITIA RIBA ZAO NA MIRADI YAO NDO WAMEWEZA KUTENGENEZA HIZO PESA, NA MISAADA HUTOKEA MARA CHACHE SANA ILA MARA NYINGI AU MARA ZOTE NI JUHUDI ZAO WENYEWE

NAZANI UMENIELEWA VIZURI
 
Wakuu, heshima kwenu!

Huu ni Uzi wa siku nyingi, kama mnavyoona. Badala ya kuanzisha Uzi mpya, hata kama ni bure, ninaomba niufufue Uzi huu kwa kupachika maswali yangu kwa mwenye/wenye ufahamu: 1. Ninaomba kueleweshwa jinsi Kikundi cha HISA/VSLA/VICOBA kinavyofanya kazi kwa kutumia Zao la M-Pesa la VODACOM na TIGO PESA la TIGO
2. Ninaomba kufahamishwa faida na athari/hasara kwa Kikundi cha HISA katika kutumia zao hizo
3. Ninafahamu kuwa kuna urasimu, utapeli, ujanja ujanja mwingi, rushwa, wizi, ubabe na kila aina ya michezo michafu katika mchakato wa kupata na kuendesha laini za M-Pesa (sina hakika na laini za TIGO Pesa na AIRTEL Money). Je hali hiyo iko vipi kwa laini za Vikundi vya HISA?
 
Back
Top Bottom