Idrisa abadili mawazo. Hatojiuzulu tena

mie sitazungumzia hii mada moja kwa moja nnaomba nichangie kwa muundo huu

suala la utumiaji umeme kwa njia ya kuiba hivi sasa limefurutu ada kupita kiasi. watu wengi wa binafsi , mashirtika na hata sekta za serikali huiba umeme.


la kusikitisha zaidi mambo haya yanafanyika na wahusika wengi wao wakijua na wengine kusaidia uhal;ifu au sijui niite hujuma hizo.

hii tanga cement ni moja tu, lkn kama kutafanyika utafiti utagundua wako wengi tena sio siku tatu wao muda mwingi au miaka. wanalipa kiduchu na wakati mwingi wanakula bwerere.


hali hii inapelekea shirika kukosa mapato na kuandaa hayo mauaji kwa wachache wanaolipa, bili huwa kubwa kiasi cha kutisha na wale wengine wakiwemo viongozi(utashangaa lkn ni kweli kuna viongozi wanaiba umeme)wanaendelea kubonyoa keki ya taifa kihuni.

nnajua kuna mengi yanayolikosesha shirika mapato ikiwemo uzembe, mikataba mibovu na hili pia limo.

ushauri nnaomba kwanza waliopewa dhamana waelewe wanajukumu la kuwajibika kwa mujibu wa dhamana walizopewa.

wateja wote kwa ujumla wetu tujitahidi kutumia na kulipia umeme kwa kadiri tunavyotumia tena kwa wakati.

shirika kujitahidi kuepuka uzembe kutoingiliana katika maamuzi, kuwa creative na kuzal;isha kwa sana umeme na kurahisisha usambazaji wa umeme.

matumaini yangu makubwa hii itakuwa chachu njema ya kuibua kila uozo na kuushughulikia in right time.

mwisho nnamalizia kwa :

TANZANIA NDIPO KWETU
HAKUNA PENGINE KATU
ASITUDANGANYE MTU

NAIPENDA TANZANIA
 
Back
Top Bottom