Idd Azan akana kuomba radhi CCM!

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Imeandikwa na Oscar Job;
Tarehe: 4th June 2011

MBUNGE wa Kinondoni, Idd Azzan, amekanusha kuomba radhi kwa uongozi wa CCM Mkoa kutokana na kauli yake aliyowahi kuitoa, kutaka uongozi huo ujivue gamba kwa ajili ya kulinda maslahi ya chama hicho.

Pia amemtaka Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda, kuthibitisha kama kweli anauza unga, vinginevyo atampeleka mahakamani kwa madai ya kumchafua yeye, familia yake, pamoja na wapiga kura wake.

Azzan alitoa kauli hiyo jana katika ofisi za CCM tawi la Mchangani kata ya Makumbusho, wakati wa sherehe za kuwapongeza vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa wilaya hiyo, walioibuka na ubingwa katika michezo mbalimbali iliyoandaliwa na umoja huo Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa wajivue gamba kwa ajili ya kulinda maslahi ya chama hicho.

Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa pia na baadhi ya vijana wa CCM kutoka wilaya za Temeke na Ilala, Azzan alisema malengo yake si kuleta mgongano wa maneno ndani ya chama hicho, isipokuwa kuna watu wana chuki binafsi na yeye.

Alisema yeye kama mbunge aliyechaguliwa kwa kishindo na wananchi wa Kinondoni, anachokiangalia zaidi ni kujenga mshikamano ndani ya chama hicho ili kuendelea kukipa ushindi.

Mbali na kukanusha taarifa hizo, Azzan pia alitangaza kuwania urais mwaka 2025, huku akiwafananisha watu wanaomchafulia katika nafasi yake kuwa ni sawa na ‘fisi anayesubiria mkono wake udondoke'.

"Nitafuata nyayo za Rais Kikwete, yeye alikaa bungeni vipindi vitatu vya kuchaguliwa, na kingine kimoja cha kuteuliwa na baadaye akagombea urais, hiki ni kipindi changu cha pili, itakapofika 2025 nitawania urais kufuata nyayo zake," alisema Azzan.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Kinondoni, Aron Mwaikambo, aliwataka wanachama wa chama hicho kudumisha mshikamano kwa lengo la kukijengea heshima ya chama hicho tawala.
 
Asijeakachukuliwa na marekani kama alivyochukuliwa Noriega wa Panama!! Marekani wametangaza vita dhidi ya wauza Unga.
 
Urais wa chama cha ndondi au,kwanza aende shule akasome hatuwezi ongozwa na mtu wa kidato cha pili aache utani..
 
Imeandikwa na Oscar Job;
Tarehe: 4th June 2011

MBUNGE wa Kinondoni, Idd Azzan, amekanusha kuomba radhi kwa uongozi wa CCM Mkoa kutokana na kauli yake aliyowahi kuitoa, kutaka uongozi huo ujivue gamba kwa ajili ya kulinda maslahi ya chama hicho.

Pia amemtaka Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda, kuthibitisha kama kweli anauza unga, vinginevyo atampeleka mahakamani kwa madai ya kumchafua yeye, familia yake, pamoja na wapiga kura wake.

Azzan alitoa kauli hiyo jana katika ofisi za CCM tawi la Mchangani kata ya Makumbusho, wakati wa sherehe za kuwapongeza vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa wilaya hiyo, walioibuka na ubingwa katika michezo mbalimbali iliyoandaliwa na umoja huo Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa wajivue gamba kwa ajili ya kulinda maslahi ya chama hicho.

Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa pia na baadhi ya vijana wa CCM kutoka wilaya za Temeke na Ilala, Azzan alisema malengo yake si kuleta mgongano wa maneno ndani ya chama hicho, isipokuwa kuna watu wana chuki binafsi na yeye.

Alisema yeye kama mbunge aliyechaguliwa kwa kishindo na wananchi wa Kinondoni, anachokiangalia zaidi ni kujenga mshikamano ndani ya chama hicho ili kuendelea kukipa ushindi.

Mbali na kukanusha taarifa hizo, Azzan pia alitangaza kuwania urais mwaka 2025, huku akiwafananisha watu wanaomchafulia katika nafasi yake kuwa ni sawa na ‘fisi anayesubiria mkono wake udondoke'.

"Nitafuata nyayo za Rais Kikwete, yeye alikaa bungeni vipindi vitatu vya kuchaguliwa, na kingine kimoja cha kuteuliwa na baadaye akagombea urais, hiki ni kipindi changu cha pili, itakapofika 2025 nitawania urais kufuata nyayo zake," alisema Azzan.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Kinondoni, Aron Mwaikambo, aliwataka wanachama wa chama hicho kudumisha mshikamano kwa lengo la kukijengea heshima ya chama hicho tawala.

Hivi nani kamhakikishia 2025 atakuwa hai??
Hata hili la kukanusha kuomba radhi mbona limechelewa sana?
Sihasa bana . . .
 
idd azam aliambiwa aidha athibitishe matamshi yake la sivyo aombe radhi, baada ya kushindwa kuthibitisha akaomba radhi lakini utaratibu wa kanuni unasema mtenda kosa akishapewa adhabu hata akiomba radhi basi suala hilo linajadiliwa baada ya miezi sita kupita. Hili limemchanganya iddd azam kwani itabidi adhabu aendelee kuitumikia mpaka miezi sita ipite na ndiyo maana ameona ngoja akanushe kwamba aliomba radhi!!!

eti anataka kipindi cha tatu ubunge?? kweli anatania safari hii atastaajabu na nguvu ya umma...pia anadai alishinda kwa kishindo? mgombea wa cdm hakufanya kampeni kabisa na bado alimpelekesha idd azam sana na idd kujitapa kwamba alishinda kwa kishindo ni jambo la kuchekesha sana. Mwaka 2015 chadema wasimamishe mgombea aliyesimama bac jimbo litakuwa la chadema.
 
Back
Top Bottom