Idara ya Usalama wa Taifa yakanusha tuhuma

Status
Not open for further replies.
Hapana Mkuu,

Inabidi wanunue hiki kifaa na wakipitishe kwa Watanzania wooote....... Neuralyzer flash

Neuralizer_5336.jpg
news-052512b.jpg

Labda watuformat vichwa Kama computer tusahau kila kitu
 
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamaba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visvyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.

Taarifa hii sina uhakika kama imeandikwa na idara ya Usalama wa Taifa maana mpangilio tu wa maandishi inaonekana mwandishi ni kihiyo kabla ya maneno yenyewe, hata hivyo haitatokea kamwe kokote duniani Idara ya usalama wa Taifa ya nchi yoyote ile ikakubali imehusika kufanya chochote kiwe kizuri au kibaya, na hasa kibaya, huwa hawasemi kwa mujibu wa kiapo na kuthibitisha hilo mbona Ramadhani askari mwenzao wa Makole National house hawajamkataa kuwa hawamjui na yeye mbona hajakanusha kutumia simu zile kwa taarifa hii ni wenye MATOPE tu vichwani mwao ndiyo wanaweza kukubali upuuzi huu.
 
mods mna maslahi gani na habari ya Mwanahalisi?
Mnamlinda nani na kwa maslahi ya nani?
Kwanini mnafuta habari ya kubenea wakati gazeti lipo tayari mtaani?

Nashukuru nimeshaisoma habari nzima na nimeicopy

Hata mie wameniudhi sana kuna mdau kajitolea kuiweka wameiondoa bana,bahati mbaya nilikuwa sijacoppy. Hivi inawezekana ni kwann mods JF wanafanya hivi?
 
ni matamko ya kipuuzi,tanzania ipo ktk hatua kubwa katika suala upashanaji habari,tanzania ya leo ni tofauti na ya miaka 5 nyuma,kutuletea ngonjera za kijinga wakati kila mtu anaelewa nini kilifanyika hata kabla ya mwanahalisi kutoa series ya matukio sasa gazeti limekuja kumalizia yote yaliyobaki,bora wanyamaze

jamani acheni lawama. Kaka JZoka kaamua kuja kivingine baada ya kuona Kova anamuangusha. Sasa ameona ni heri kumtumia Gabriel Zacharia kuliko Kova. Anafikiri that is going incognito. Jamani mnara wa babeli upo kuanguka. Tiss mlifanya kosa mtakalolijutia sana kushindwa kumua kabisa Ulimboka. Kwasasa raia wamekuwa ni tiss kuliko nyie. Mpango wenu wowote ule dhidi ya wenye haki utabumbuluka kabla hamjautekeza na utawaumbua na kuwadhalilisha vibaya.
 
Unahitajika kuwa na akili ya mwendawazimu kuamini Tiss hawahusiki ktk matukio mbalimbali likiwamo hili la Ulimboka kwanza wanazidi kujichoresha kwa hili tamko lao ni heri wangekaa kimya.
 
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamaba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visvyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.
Sidhani kama kuna usalama wa Taifa dhaifu kama hii duniani,taarifa imeandikwa kama ya
Mtu aliyejawa na hofu au anayeshtakiwa na nafisi yake kwa kosa la kumwaga damu isiyo
na hatia!!!!!shame on you mnaojiita usalama wa taifa kumbe ni wauaji wa Taifa.
Taarifa
 
Labda watuformat vichwa Kama computer tusahau kila kitu
solokondo hiyo itakuwa kazi kubwa sana! Sijui vichwa vya wengine lakini changu hakina hiyo programme! Kwangu mie idara imeshachafuka na hakuna sabuni ya kuisafisha kuhusu suala la Dr. Ulimboka.
 
Last edited by a moderator:
Yakanusha kuwa haikupanga kumuua Dr. Ulimboka na kwamaba kinachotangazwa na vyombo vya habari ni vipande vya taarifa visvyo na ukweli wowote na wananchi wapuuze.

Sidhani kama kuna usalama wa Taifa dhaifu kama hii duniani,taarifa imeandikwa kama ya Mtu aliyejawa na hofu au anayeshtakiwa na nafisi yake kwa kosa la kumwaga damu isiyo na hatia!!!!!shame on you mnaojiita usalama wa taifa kumbe ni wauaji wa Taifa.

Taarifa yenu imea haaswali kwanini msitwambie alipo Ramadhani,kwanini msiseme km mnamjua na nistaff wenu au siyo,na Kama hamkutuma kwanini msiuambie umma hatua mlizochukua dhidi yake ikiwa ni pampja na kumpeleka polisi ahojiwe??

Nimeshangaa hamma hata maofisa wenye uwezo wakiingundua taarifa yenu kuwa ni mfu?? Watumieni hata maveterani wawasaidie msifanye mambo ya kitoto km haya.
 
Huu ni uhuni. Tamko la Usalama wa Taifa halina jina la mtu na wadhifa wa aliyelitoa? Kutuambia tu kuwa imetolewa Dar-es-Salaam "Makao Makuu" ndio nini? limetolewa na mfagizi? Lakini kitu pekee ambacho hawakanushi - na ni vigumu kukanusha - ni kama watu wanaotajwa kuhusika ni watu wao au la.
 
Mr Rocky upo? movie inazidi kunoga. Tuko katikati ya episode 5!
 
Last edited by a moderator:

Tiss haina tatizo katika hili, bali tatizo ni uchakavu wa nyaya au kuna nati zilizolegea ndani ya vichwa vya viongozi wao. Hivyo siyo vyema kuilaumu idara nzima kwa upuuzi wa viongozi chakavu, wenye mawazo mgando na wasioenda na wakati. Upuuzi kama huu ndiyo ulipelekeaga KGB ikavunjwa.

Upuuzi wa Tiss

1. Mbali na jaribio la kitoto la kutaka kupata information kutoka kwa ulimboka kwa kum'tocha, hali ya kuwa kuna teknolojia nyepesi ipo mitaani, ya kukamata mawasiliano ya simu, email n.k, inaonyesha udhaifu uliopitiliza wa idara, ama aliyeongoza hiyo operation.

2. Kashfa ya pili ya aibu na fedheha, ni kwa Tiss kuwa exposed dhahiri shahiri kwa ushiriki katika kumteka na kumtesa Ulimboka, tena kwa njia zinazokinzana na haki za binaadamu duniani.

3. Agent wa intelijensia huwa ni vigumu kutambuliwa, hivyo basi, nia aibu kubwa sana kwa Tiss kwa agents wake kutambuliwa na kuanikwa wazi kiasi hiki kwa jamii. Nchi zilizoendelea, mkurugenzi wa intelijensia angekuwa ameshapigwa chini. Hali ambayo ina hatarisha usalama wa familia zao kitaani.....!

4. Kuonnyesha Ukilaza, na hali ya kupeana kazi ndani ya Tiss kwa watu wasio na uwezo wala sifa, inakuwaje agents watumie simu zao binafsi katika operation za idara?!!

5. Ukanushaji wa kitoto usio na mashiko, ukizingatia kauli nyingi za Zoka (Human Resouce) wa TISS za kukimbila mahakamani kila idara inapotajwa, lakini kwa hili zito, idara imetoa SMS tu.....what a shame...?!

6. Na hata andiko lenu linasema tu kuwa MwanaHALISI imeunganisha tu baadhi ya mambo, lakini idara haijatoa kasoro wapi KUBENEA amedanganya kwa majina ya wahusika, ama namba zao za simu, ama mida ya simu hizo zilipoyumika, wala hata kukanusha kuwa hao waliotajwa ni waajiriwa wa Tiss.

Kwa hali hii, tutaibiwa Twiga wote.......!

Kibanga Msese
 
ni taarifa fupi lakini yenye content iliyojitosheleza.hawa mwanahalisi kwa kweli wanakotupeleka ipo siku nchi itaingia vitani hivi hivi.wanapaswa kudhibitiwa mapema sana,maana chuki wanayopandikiza kwa wananchi sio ndogo
 
Wajameni, hii kweli ni taarifa ya TISS??-Kwa jinsi ilivyo, ni kwamba inaweza kutolewa na mtu yeyote. Labda mlioko Tz mmeona ktk vyombo vya habari vingine????
 
Mie nashangaa hawa TISS. Kama hizi habari ni za kutunga kwa nini wasiende mahakamani kufungua mashtaka dhidi ya Mwanahalisi? Kuna wakati fulani walilifungia Mwanahalisi wakisema ooh linahatarisha amani nchini, ooh linaeneza chuki kwa jamii dhidi ya serikali. Sasa tofauti hapa ni nini?? Kwa nini wasiende mahakamani ili tujue mkweli ni nani??

Wakiogopa kwenda mahakamani kama wale fisadiz waliomtishia nyau Dr. Slaa, basi tutaamini kuwa walichosema Mwanahalisi ni UKWELI MTUPU.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom