Idara ya Uhamiaji kunani? Vipi ucheleweshaji huu wa kutoa paspoti?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
WanaJF:

naomba kuoitia jamvi hili iwapo kuna mtu anafhamu kinachoendelea katika Idara ya Uhamiaji -- sababu ya kuchelewesha kutoa paspoti.

Kuna dada yangu mmoja alioma pasipoti na kila kitu alikamilisha, hatua ya mwisho ilikuwa ni kuchukuliwa alama za vidole ambayo tayari alishachukuliwa, na akapangiwa tarehe ya kwenda kuchukua hiyo pasi ya kusafiria -- yaani aende baada ya wiki mbili.

Inakuwaje hadi leo karibu miezi miwili bado hajapata? kila akienda katika ofisi yao kule Wizara ya Ndani anaambiwa bado haijaletwa. Na hawatoi jibu ni kwa nini uchelewshaji huu.

Naomba Uhamiaji waeleze inakuwaje?
 
Kama angekuwa ni mgeni anaomba vibali vya kuishi angeshamaliziwa ila kwa Wazawa inabidi usumbuliwe kwanza kama humjui mtu hapoa Uhamiaji basi inabidi uwe mvumilivu.
 
WanaJF:

Kuna dada yangu mmoja alioma pasipoti na kila kitu alikamilisha, hatua ya mwisho ilikuwa ni kuchukuliwa alama za vidole na akapangiwa tarehe ya kwenda kuchukua hiyo pasi ya kusafiria -- yaani aende baada ya wiki mbili.

Naomba Uhamiaji waeleze inakuwaje?

Sasa atachukuaje passport wakati hatua ya mwisho ya kuchukua alama za vidole hajafanya, nachojua ukishakamilisha hatua hiyo ya kuchukua vidole ndo unaaambiwa kusubiria wiki mbili lakini kutokana na uharaka wa mtu kuna wengine ndani ya siku mbili unachukua mzigo, so mwambie akamilishe hatua hiyo ya mwisho
 
Sasa atachukuaje passport wakati hatua ya mwisho ya kuchukua alama za vidole hajafanya, nachojua ukishakamilisha hatua hiyo ya kuchukua vidole ndo unaaambiwa kusubiria wiki mbili lakini kutokana na uharaka wa mtu kuna wengine ndani ya siku mbili unachukua mzigo, so mwambie akamilishe hatua hiyo ya mwisho

Mkuu, sorry, nimesharekebisha thread -- tayari alishachukuliwa alama za vidole na kupangiwa siku ya kuchukuwa, lakini sasa ni miezi miwili imepita tangu hiyo siku ya kuchukua.
 
Du sasa kama alama za vidole keshachukuliwa zaidi ya mwezi mzima halafu passport hajapata wala siwezi kusema kuwa eti ni rushwa inahitajika hapo maana rushwa inatolewa wakati wa kuiprocess lakini ikishafika hatua ya kuchukuliwa vidole kunakuwa tena hakuna longo longo ni kuchukua tu.Naomba mhusika aende sehemu passport zinapotolewa baada ya kuwa processed ambapo ni kule ofisi za uhamiaji karibia na TACAIDS maeneo ya stesheni kama hawajabadilisha na wala sio Wizara ya Mambo ya Ndani then aangalie kama jina lake lilishatoka
 
Back
Top Bottom