Idadi ya vifo vilivyotokana na mgomo wa madaktari

Kwanini ishindikane? Tatizo la serikali ya ccm hawa think beyond. Wao wanafikiria usawa wa pua zao na ndomana kila mwaka vyanzo vikuu vya kodi vimekuwa vinywaji wakati vipo vingi sana tumewashauri lakini vichwa vigumu. Nadhani hata wewe uwezo wako wakufikiri ni usawa wa pua yako
Karibu jamvini mdau! Hebu nikuulize kitu,unauhakika JK akitoka madarakani atakaye m-replace atawalipa madaktari mshahara na marupurupu ya Shilingi mil 7.7 kwa mwezi?
Ataweka mazingira mazuri ya hospitali nchini kote ndani ya siku moja ili kesho yake madaktari wafanyekazi?

Tafakari!!!!!! Chukua hatua!!!!! Punguza kiherehere and think critically!!!!
 
Ndugu wanajamvi kufuatia mgomo wa madaktari unaoendelea watu wengi wamepoteza maisha wakiwa hospitalini, njiani kupelekwa Private hospitals na kurudishwa majumbani kutokana na Mgomo. Kulingana na Tathmini niliyoifanya mimi katika hospitali ya rufaa mhimbili na baadhi ya mitaa katika jiji la Dar na Mbeya watu 698 wamepoteza maisha katika wiki hz za mgomo. JK na utawala wako mna kesi ya kujibu na Ifike hatua sasa mshughulikie matatizo kwa dhati na sio kushutumu CHADEMA wakati ninyi ndo vyanzo vya matatizo na vifo hivi kwa utendaji wenu dhaifu. Swalahili la mgoo tusilihusishe kabisa na siasa

Mnakuza tu mambo, mbona huwa hamfanyi tathmini ya vifo vinavyotokea kila mara kutokana na uduni wa huduma za hospitali zetu? Yawezekana huu mgomo ukaleta mabadiliko mengi na kuokoa maisha ya watanzania wa baadae ambao wangekuja kufa kwa wingi kutokana na serikali kupuuzia uboreshaji wa huduma hii
 
Haya yote sababu ni dr.ulimboka na wenzake.tumuombe mungu amponye kisha wapandiswe kizimbani wakajibu hoja kwa hivi vifo watz wasio na htia
 
Ndugu wanajamvi kufuatia mgomo wa madaktari unaoendelea watu wengi wamepoteza maisha wakiwa hospitalini, njiani kupelekwa Private hospitals na kurudishwa majumbani kutokana na Mgomo. Kulingana na Tathmini niliyoifanya mimi katika hospitali ya rufaa mhimbili na baadhi ya mitaa katika jiji la Dar na Mbeya watu 698 wamepoteza maisha katika wiki hz za mgomo. JK na utawala wako mna kesi ya kujibu na Ifike hatua sasa mshughulikie matatizo kwa dhati na sio kushutumu CHADEMA wakati ninyi ndo vyanzo vya matatizo na vifo hivi kwa utendaji wenu dhaifu. Swalahili la mgoo tusilihusishe kabisa na siasa

Toka mgomo huu ulipoanza, nimekua nikijiuliza maswali mengi kadiri siku ziendavyo. Lazima nikiri kwamba na mimi nilitumbukia katika mtego wa kulaumu upande mmoja wapo kabla ya kujiuliza vizuri... Ama baada ya kutafakari kwa kina, nikagundua kwamba kwa vyovyote vila itakavokua, tunaoathirika ni sisi wananchi, bila kujali tunaunga mkono madaktari au serikali.




Nilianza kujiuliza hivi: Hawa wanasiasa wanaotupiana mpira, mara CHADEMA, mara CCM, bila kujali vyama vyao, wanatibiwa wapi kwa kawaida? Hawa kwani hawana madaktari maalum ambao wanawalipa binafsi? Hivyo basi, huyu kiongozi anayesema fukuza, hakutani na daktari wake binafsi ambaye huenda anatugomea sisi wananchi? Mimi mwananchi wa kawaida ambaye sijuani na daktari na wala sina pesa, nani atanitibia?




Je, nikisema serikali ifukuze madaktari wote, nani atanitibia? Nikisema pia wagome, kwani nikienda hospitali wataniuliza kama nawaunga mkono ili wanitibie? Au ndio yale ya "naunga mkono mgomo", lakini kwa sababu mimi sina jamaa daktari, au sio daktari, basi sina wa kunitibia. Lakini wao wanasema wananisaidia, ilihali wananiacha nateseka na wao wakitibia ndugu na marafiki zao!




Baada ya kuangalia hali yangu na hao viongozi wa siasa, bila kujali vyama vyao, nikajiuliza maswali mengine: Je, miongoni mwa madaktari wanaogoma, hawana wateja wao binafsi ambao ndio hao hao mawaziri wanaowatuhumu kufisidi sekta ya afya? Je, mawaziri hawa wakienda katika clinics zao binafsi wanawagomea? Je, ni kweli kwamba madaktari wote wanaoshiriki mgomo, hakuna hata mmoja ambaye aliwahi kwa njia moja au nyingine kushiriki katika kufisidi sekta ya afya, iwe kwa kuiba panadol au vifaa vya malaki au hata mamilioni? Je, na wao wanahaki ya kusema kwamba wanagoma kwa sababu ya ukosefu wa vifaa?




Sikuishia hapo tu... nikajiuiza tena: vipi sisi wenyewe, ambao tunashangiia au kushabikia ama serikali kufukuza madaktari, au madaktari kugoma: Hakuna miongoni mwetu walioshiriki kuziibia hospitali zetu? Je, ni haki, kwa mwananchi mwenzetu, ambaye naye ameshiriki kufisidi hospitali, kunyoosha kidole, au kushabikia akisema serikali ifukuze, au madaktari wagome, wakati huyo naye ni sehemu ya tatizo?




Bado nikajiuliza maswali zaidi: Hivi tunaposikia serikali na madaktari wameshindwa kuafikiana, tunayachukua hivyo hivyo tu, au tunauliza kwa kina ni kwa nini wameshindwa? Tunaposikia serikali au madaktari wanasema wako tayari kwa majadiliano, tunawauliza ni hatua gani wanazichukua kwa ajili ya majadiliano, wakati upande mmoja unaendelea kufukuza na mwingine unaendelea kugoma? Tunapozikosoa taarifa zao, ni kwa sababu tumeamua kuchukua upande mmoja, au tunajua madhara ya mgomo huo kwetu sisi?




Maswali haya mengi yamenileta katika swai moja muhimu... Sisi wananchi, tusio wanasiasa, wala tusio madaktari au walau na ujamaa na daktari - tumekua tunatoa maoni yenye kuleta suluhu, au yenye kuchochea mgogoro? (bila kujali uko upande gani)




Watanzania wenzangu, katika hili, tunahusika wote. Kwa wale wanaosema madaktari wasigome, wasiishie tu hapo, watafakari sababu za matatizo ya sekta ya afya. Na kwa wale wanaosema wagome, wajiulize swai moja tu: Je, sababu kwamba ukosefu wa huduma bora kwa miaka kadhaa umesha sababisha vifo fingi, ni kisingizio haswa cha mgomo ambao na wenyewe pia unasababisha vifo na mateso?




Mimi na wewe tunafanya nini ili kurudishiwa huduma ya afya? Tuendelee kupiga siasa? au tutoe maoni ya suluhu?
 
Doctors are very treak. They argue about hospitals services while hiding there agenda for salary increases shame on them. They are now politician, not proffessional again. This is where we are now. A dr. Doing political, this is not acceptable dr go go to heal. Tanzanians pray for all people who are now on the bed suffering from diseases because of what is so called drs. Shame on them. They are killing us , what have we done for them. We have train them and now they are killing us, this is not fear. Ulimboka shame on you, dr.s that are in the streak shame on you, come back to humanity pse.
 
ndugu wanajamvi kufuatia mgomo wa madaktari unaoendelea watu wengi wamepoteza maisha wakiwa hospitalini, njiani kupelekwa private hospitals na kurudishwa majumbani kutokana na mgomo. Kulingana na tathmini niliyoifanya mimi katika hospitali ya rufaa mhimbili na baadhi ya mitaa katika jiji la dar na mbeya watu 698 wamepoteza maisha katika wiki hz za mgomo. Jk na utawala wako mna kesi ya kujibu na ifike hatua sasa mshughulikie matatizo kwa dhati na sio kushutumu chadema wakati ninyi ndo vyanzo vya matatizo na vifo hivi kwa utendaji wenu dhaifu. Swalahili la mgoo tusilihusishe kabisa na siasa
wewe ni diwani wa ccm??? Hawa ndo hutumia hoja feki. Kweli watu wamekufa ila si kwa hiyo exagaration. Usiwe nkama diwani wa ccm
 
Ndugu zangu nakupeni kisa cha kweli wala sina unafiki kwa hili na imetokea muda si mrefu.
Nina ndugu yangu ambaye alikuwa na matatizo ambayo hayakuweza kutambulika mara moja hapo Muhimbili kwa sababu ya kukosa uchunguzi wa CT scan , kwa hiyo daktari akatushahuri tukampeleke hospital binafsi na tukapewa kipimo hicho na tukamkuta huyu mama ana uvimbe kwenye ubongo na tumewahisha India kwa upasuaji
Nilijiuliza mambo mengi baada ya kuona haya , ni watu wangapi wanakufa sababu ya kukosa vitenda kazi hivi ?
 
Wewe Njiwa ulitarajia nikakusanye taarifa kijiweni? Nimefanya maeneo tajwa! Kama huamini takwimu nenda kafanye utafiti wako uje na criticsm

i have my own reasonable doubts wasema umepata muda wa kutembelea muhimbili na mitaa ya dar mbeya na mitaa ya mbea ukapata idadi kamili watu 698 wamefariki! tuwekee basi hiyo survey yako katika maandishi tupate kuiona kuliko kuja kubwabwaja na mdomo mkavu ..
 
Wagome madaktari ashitakiwe Kikwete? Unaakili sana wewe, hata baada ya mahakama kuamuru madaktari warudi makazini?

Kabla ya mgomo kwa kipindi kama hicho huwa kuna vifo vingapi?
 
Wewe Zomba unafikiri Rais akiwa dhaifu na watendaji wake what happen? Si ndo mamigomo haya yanayoendelea? Huwez kuacha kuhusisha serikal ya ccm na watendaj wake wabov kwenye swala hili. Na nilazima Jk anachakujibu mahakama ya Kimataifa. Kwanza wew Zomba nakufaham ninyi ndo walewale dhaifu.
Wagome madaktari ashitakiwe Kikwete? Unaakili sana wewe, hata baada ya mahakama kuamuru madaktari warudi makazini?

Kabla ya mgomo kwa kipindi kama hicho huwa kuna vifo vingapi?
 
Back
Top Bottom