ICC-ICA Rules zinaruhusu review ya tuzo na mchakato?

Am sure hapa we have a case and its worth a shot...., hata kama tukishindwa ku-reverse hukumu ya ICC nadhani hapa tuna grounds za kuweza kuishitaki Dowans... whichever the case we need to look at this more deeply

Nakubaliana nawe VOR kwani ikiwa ipo clause inasema hivi kwenye contract, ni vema tukapata mtiririko wa matokeo je ni lini Richmond na Tanesco walikaa na kuwa mutual agreement? Pia je ICC court walifahamu hili ikiwa kama ICC walifahamu ila wakaignore then we can revoke the award.
 
Sema kwa mfano baada ya hukumu na kabla ya malipo new facts zinatokea ambazo ni muhimu katika hukumu na zilifichwa kwa makusudi ili kunufaisha upande mmoja aliyedhuriwa ana recourse gani ya kisheria in light of 'no appeal clause'?

Just thinking outside the box, mfano tumewalipa hao Dowans na baadae "new facts zinatokea ambazo ni muhimu katika hukumu na zilifichwa kwa makusudi ili kunufaisha upande mmoja" au ikathibitika majaji walihongwa. Dowans wataturudishia hela yetu?
 
majibu ya wengi kuwa it doesn't matter.. tutawalipa tu. Kwa sababu kama hakuna nafasi ya kukata rufaa utatengua tuzo kwa msingi gani?
 
Nakubaliana nawe VOR kwani ikiwa ipo clause inasema hivi kwenye contract, ni vema tukapata mtiririko wa matokeo je ni lini Richmond na Tanesco walikaa na kuwa mutual agreement? Pia je ICC court walifahamu hili ikiwa kama ICC walifahamu ila wakaignore then we can revoke the award.

Jamani si usome ripoti ya Mwakyembe imedetails process nzima na kusema wazi ni lini mkataba wa Tanesco ulirithishwa kwa Dowans.
 
Mzee Mwanakijiji, Ni mkataba wa Tanesco na ICC ndio ume relinguish haki zote za Tanesco kwa uamuzi wa ICC, japo mkataba umebainisha wazi, sheria za kutumika ni za Tanzania, vipengele vya mkataba huo vimeifanya ICC ndio final na supreme na kuiamuru High Court yetu kutekeleza maamuzi ya ICC bila kuyahoji. Hili ni kwenda kinyume cha katiba yetu!.

Kwa vile mdaiwa kakubali kulipa kwa roho nyeupe, pesa ni za Tanesco na sio zenu!, nyie wengine unaopinga malipo nikiwemo mimi, swali mnaulizwa, " Pilipili iko shamba, nyie inawawashia nini?.

Waziri wa Fedha wa keshasema, Hazina haina fedha, hilo ni zigo la Tanesco, sasa mnawasiwasi gani wakati fedha zitakazolipwa sio za hazina bali ni za Tanesco, tena Tanesco, imeshawatoa wasiwasi kuwa kupanda kwa umeme hakuna uhusiano na fidia ya Dowans, sasa wasiwasi wa nini?.

Hivi hili suala bado mlipigia kelele mpaka leo, hivi hamjaelewa tuu kinachoendelea?. Wenyewe wanaodaiwa wamekubali kulipa, nyiemsio daiwa mnakatalia nini?.

Wakati wa Rada, walioambiwa kila kitu mpaka Claire Short akaligomea huko Uingereza, wenyewe wanaitaka Rada walishakubali kuilipia na wakailipia, sasa leo mnashanga nini?.

Bei ya Gulf Steam tuliambiwa ni bilioni 42, John Cheyo akaingia kwenye web site yao, akakuta bei ni Bilioni 18!.Akaiambia serikali bei ni nusu ya mliopewa, nunueni straight toka BAE, serikali ilikataa na ikalipa ile Bilioni 42!, sasa leo mnashangaa nini?.

Na ile tenda ya ununuzi wa magari ya jeshi ni hivyo hiyo, tena naomba nisitoe siri ya ununuzi wa silaha za kivita zikiwemo helcopter bomu kwa bei mara mbili ya bei halisi na ajenti ni yule yule, serikali ni ile ile, hivi hamjaelewa tuu?.

Hizo fedha ni zao, ama zenu?.Kama ni zao, wenyewe wamekubali kulipa, nyie kelele za nini?.

Acheni walipe tuendelee na maisha ya kila siku, after all mwenye nyumba ameshasema hizi ni kele tuu za mlango, bado mnapiga kelele?.

Mwenye nyumba ana pochi kuliko Rais wa Zamani wa Tunisia??
Tulio mpa ale tukianza songombingo andhani fedha itamsaidia??
Tangu sasa "kuendelea na Maisha ya kila siku" haiwezekani it is too expensive we cant afford it. Anatakiwa kusoma Alama Za Nyakati.
As 2012 approaches the land beneath his feet will keep on shifting.
ni mbele kwa mbele nyuma hapana.
 
Mchakato mzima na tuzo kwa Dowans na Richmond huko nyuma hakika tutazipitia upya lakini kwanza tuhakikishe uchafu wote uliotufikisha hapa tulipo leo hii huopo tena kwenye ofisi zetu hata kidogo.

UFISADI TOKA, wananchi wapate maendeleo!! UFISADI TOKA, ili kila mwananchi utaifa tuuweke mbeeellee kama tai katika haki!!!

Nasema UFISADI TOKA!!!
 
Nishasahu au nimepitiwa sikuliona katika Report we tujuze kama unaweza maana wengine tuko mbali
Mdondoaji, Tanesco waliikataa Richmond since day one.Ni serikali ndio ilishinikiza. Richmond waliposhindwa kudeliver on time, Tanesco wakaandika letter of intent kuvunja mkataba, Richmond wakajibu kwa barua ya kuhuisha mkataba kwa Dowans. Tanesco wakagoma. Waziri Karamagi

Akashinikiza kupitia M/K wa bodi ya Tanesco kukubali, bodi ikakubali. Dr. Rashid agaigomea. Akaandika resignation letter akawabwagia akatimka. Kesho yake akaitwa Ikulu wakayamaliza. Akawithdraw barua wakasaini kuhuishwa kwa mkataba. Je mmepata picha Dowans halisi ni nani?!
 
Akashinikiza kupitia M/K wa bodi ya Tanesco kukubali, bodi ikakubali. Dr. Rashid agaigomea.
Akaandika resignation letter akawabwagia akatimka. Kesho yake akaitwa Ikulu wakayamaliza. Akawithdraw barua wakasaini kuhuishwa kwa mkataba. Je mmepata picha Dowans halisi ni nani?!

Pasco, hiyo stori iliyosimuliwa na ikaaminika tangu wakati ule; uchunguzi wangu mwepesi tu umegundua wakati hayo yanatokea Richmond ilikuwa imekwisha hamisha mkataba kwenda kwa Dowans S.A bila Tanesco kujua! Kule kuhamishwa kwa baadaye ilikuwa ni geresha tu.
 
Mdondoaji, Tanesco waliikataa Richmond since day one.Ni serikali ndio ilishinikiza. Richmond waliposhindwa kudeliver on time, Tanesco wakaandika letter of intent kuvunja mkataba, Richmond wakajibu kwa barua ya kuhuisha mkataba kwa Dowans. Tanesco wakagoma. Waziri Karamagi

Akashinikiza kupitia M/K wa bodi ya Tanesco kukubali, bodi ikakubali. Dr. Rashid agaigomea. Akaandika resignation letter akawabwagia akatimka. Kesho yake akaitwa Ikulu wakayamaliza. Akawithdraw barua wakasaini kuhuishwa kwa mkataba. Je mmepata picha Dowans halisi ni nani?!
Ndugu hapo kwenye mashinikizo ni sababu tosha ya kufanya mkataba kuwa void....., sababu contract kuwa legally binding lazima kuwe na free consent kwa both parties bila shinikizo...., I think this contract is void in so many angles and Dowans have got a case to answear
 
Pasco, hiyo stori iliyosimuliwa na ikaaminika tangu wakati ule; uchunguzi wangu mwepesi tu umegundua wakati hayo yanatokea Richmond ilikuwa imekwisha hamisha mkataba kwenda kwa Dowans S.A bila Tanesco kujua! Kule kuhamishwa kwa baadaye ilikuwa ni geresha tu.

sasa MM naomba utuambie ni lini hayo ya kuhamishwa kwa mkataba yalifanyika bila ya Tanesco kujua? na yalifanyika kwamisingi gani? na ikiwa hivyo ndivyo, hao wanasheria wa Tanesco walienda na utetezi gani mbele ya ICC?
 
Walifanyia mambo yote hapa Dar pale kempsiki. Nani aliefoot gharama zao? Je uraia wa wale waliokuwa wapatanishi je?

naomba niongezee kaswali kengine hapo, je kama Dowans walikua wakijua kua kuna mapungufu katika mchakato mzima wa biashara yao na Tanesco, walitoa wapi jeuri ya kwenda mbele ya mahakama? au na huko nako walikuwa wameshaseti mambo yao? hapa usalama wa taifa wanaweza kutupa majibu hapa!
 
Pasco, hiyo stori iliyosimuliwa na ikaaminika tangu wakati ule; uchunguzi wangu mwepesi tu umegundua wakati hayo yanatokea Richmond ilikuwa imekwisha hamisha mkataba kwenda kwa Dowans S.A bila Tanesco kujua! Kule kuhamishwa kwa baadaye ilikuwa ni geresha tu.
Mzee Mwanakijiji, yako mambo yanayoufanya mkataba kuwa void na voidable. Void contract ni ule ambao haurekebishiki lakini voidable ni ule ambao unarekebishika.

Kutokeleza masharti ya mkataba, yanaufanya mkataba uwe void, kama hayatekelezeki kabisa au kushindwa kuutekeleza.

Hivyo pale tuu richmond waliposhindwa kuutekeleza mkataba, pale pale ulishakuwa void, yaani hautekelezeki na ulipaswa uvunjwe.

Ilitakiwa Tanesco wakauvunjilie mbali mbali na sio kuuuisha.
Kitendo cha Tanesco kutouvunja na kusubiri ule uhuuishaji, ni taarifa kuwa Tanesco wamevumilia udhaifu wa Richmond na wataendelea.

Haijalishi uhuishaji ulianza lini, kama matayarisho, lakini uhuuishaji rasmi ulianza siku pale Tanesco waliposaini kukubali.

Hivyo ule uhuishaji ulianza kabla ya Tanesco kuridhia, uliofanya mkataba ule uwe voidable na sio void mpaka Tanesco waliposaini, ndio wakaurudisha mkataba ule kwenye uhai.

Unless ukithibitisha kuwa Richmond na Dowans walichange hands kabla ya Tanesco kuarifiwa, then kwa kukitumia kipengele hicho pekee, kingeweza kuufanya mkataba kuwa void, only if Tanesco angetaka kuuvunja, as long as Tanesco hakuwahi kutaka kuuvunja kwa sababu hiyo, lakini baadaye akauvunja kwa sababu nyingine, kwa sasa hawezi tena kutaka kurudi nyuma kuwa mkataba ule sio halali.

Hapa wanatumia sheria ya changing hands, kama unapoagiza gari, baada tuu ya kulipia, gari linakuwa ni lako lakini chini ya dhamana ya bima. Jee gari hilo linachange hands wakati gani?, likishapakiwa tuu kwenye meli (FOB), kishasafirishwa mpaka bandarini (CIF), au ikishakabidhiwa rasmi gari lako mkononi?.

The actual changing hands za hilo gari kati yako na muuzaji, ni pale tuu wewe unapopokea bills of landing, kwa muuzaji kulipakia gari lako melini, weather lilifika, liliibiwa, meli ilizama, hizo ni issues zako na bima, mwenye gari aliuza na wewe ulipokea gari makaratasi (bills of Landing)

Richmond alipochange hands na Dowans bila Tanesco kuambiwa ilikuwa ni kuiweka Richmond kwenye FOB ya Dowans, na Tanesco kuendelea kuilipa Richmond ilikuwa ni ku (CIF) hiyo Dowans the actual changing hands imetake place baada ya kusainiwa mkataba (bills of Landing) za Dowans.

Mzee Mwanakijiji, bado tumeshikwa mahali pabaya, ila pabaya zaidi ni wenye mali kuamua kujilipa kwa pesa zetu, unless tuwagomee na kusema to hell with ICC.
 
Naona hili swala watu wanaligeuza kuwa la kisiasa, sheria na siasa ni vitu viwili tofauti ni bora watu tujadili kisheria zaidi badala ya kisiasa kwani hapo ndio utapeli unaweza kugundulika. Mimi nakuunga mkono mwanakijiji kama zipo evidence zitoe jamani JF tujadiliane kihoja zaidi kwa manufaa ya nchi na sio kisiasa kwani ikienda hivyo sidhani kama tutafika sehemu.

Mdondoaji:

You nailed it home. Nimeangalia hapa Toyota Land Cruiser kwenye wavuti ya Toyota na hayo madude yauzwa dola 65,000.00. CAG et al wote ni majoka ya kibisa!:suspicious:
 
Ndugu hapo kwenye mashinikizo ni sababu tosha ya kufanya mkataba kuwa void....., sababu contract kuwa legally binding lazima kuwe na free consent kwa both parties bila shinikizo...., I think this contract is void in so many angles and Dowans have got a case to answear
VOR nakubaliana na wewe, huu mkataba ulitakiwa kuwa void ab-initio, yaani ni void tangu mwanzo, lakini lilikuwa ni jukumu la Tanesco kuuvunja, hata kama ni void, na ulijua ni void, lakini ukaendelea mpaka kwenye perfomance, then unakuwa umeukubali. Kitendo cha Tanesco kusaini kwa shinikizo la serikali, kunahesabika ndio msimamo wa mwenyemali, kwa vile Tanesco imamilikiwa na serikali aslimia mia 100%. Ili kuufanya mkataba ugeuke void baada ya kusainiwa, ikijengwa hoja, Dr. Rashid was a person of un sond mind ile siku anasaini, ama ikajengwa hoja supported by medical papers kuwa alikuwa insane, then itahesabika kweli mkataba ni void, lakini kama wamekwenda mpaka kwenye performance, hapo bado huwezi kutokea.

Siku zote nasisitiza hii issue inajadiliwa kisiasa zaidi kuliko kisheria. Wanasheria mahiri Sitta na Mwakiembe wanaipigia debe la kisiasa tusilipe huku mkataba halisi wameiona na wanajua hakuna pa kutokea!.

Kwao issue ni hizo pesa analipwa nani. Lile tozo la ICC kwa ajili ya Dowans, sio kuilipa kampuni inayoitwa Dowans, wala kuwalipa wamiliki wa Dowans, Tozo ni kufidia zile genereta pale Ubungo na kuzuiliwa kuziuza, na tangu hukumu itakaposajiliwa, then ni shilingi milioni 25 zinaongezeka kila siku iendayo kwa Mungu.

Kiukweli Richmond/Dowans zote ni kampuni hewa ila zile genereta, sio genereta hewa na wala umeme unaofuliwa pale, sio umeme hewa!.

Ni baada ya tozo hilo kulipwa, ndipo wengi wetu humu tutaanza kumqwelewa vizuri Zitto!.
 
Ripoti ya Mwakyembe inapatikana online wewe andika tu " Richmond Report"

Mzee mwenzangu,

Nimeitafuta hiyo nikaipata taarifa katika website moja inaitwa Tanzania Affairs, nilipoisoma sikuona mahali inaposema mtiririko wa kesi. Dhumuni langu ni kuoanisha mtiririko wa matukio kupata kuona je Tanesco baada ya kuikataa walivunja mkataba? Pia kama wameuvunja mkataba Richmond walikuwa na mkataba nani? Tukishaelewa hilo tutakuja kudebate swala zima la Dowans? Anyway mie sinayo report nzima ya Mwakyembe mkuu nataka mtiririko wa events leading to the dowans case!
 
Pasco.. ur missing the point.. Tanesco hawakujua kabisa kuwa mkataba ulikuwa tayari umehaulishwa kwa Dowans na Richmond; hawakua na jinsi ya kujua isipokuwa kama Richmond na Dowans wangewaambia. Hivyo majadiliano yote ambayo Tanesco iliyafanya kuanzia Novemba 28 waliyafanya wakiamini (in good faith) kuwa bado Richmond na Dowans walikuwa hawageana mkataba hadi wao waridhie. Hivyo, juhudi za tanesco kujaribu kukataa kuhaisha mkataba hazikuwa na nafasi kwani mkataba ulikuwa umeshahamishiwa kwa Dowans na Dowans walikuwa wameshautekeleza kwa kuleta majenereta ya kwanza ya 22MW Oktoba 30, 2006!

Dowans kimataifa haitambui kuhamishiwa kwa mkataba wake Disemba 23, 2006 kama Tanesco inavyotambua au kama Kamati ya mwakyembe ilivyoambiwa. Wao wanatambua walichukua mkataba toka kwa Richmond nyuma kabisa kabla Tanesco hawajauombwa kuhamishiwa mkataba.
 
Back
Top Bottom