Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Amemteua Ibrahim Mussa Kuwa mkurugenzi wa Idara ya Utalii kwanzia 01 February 2011.Uteuzi Huo Ameufanya kwa Mujibu wa kifungu cha 6 (1) B Cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya Mwaka 2002
Ibrahimu Mussa (53)ni mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwanzia Mwaka 1983 hadi sasa ambapo alifanya kazi kwenye ngazi mbalimbali ,katika idara ya misitu na idara ya utalii.kabla ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa idara ya utalii,Ibrahim Musa alikua mkurugenzi msaidizi anaesimamia utafiti,takwimu namafunzo katika idara ya utalii
Bw ibrahim Mussa Ana Shahada ya Uzamili(international Tourism Management)aliyoipata mwaka 2005 kutoka chuo cha Sheffield nchini uingereza,Bw ibrahim Mussa anachukua nafasi ya Ukurugenzi wa idara ya Utalii kutoka kwa Maria Mmari ambaye amepangiwa kazi nyingine.Habari hii na Tulizo Kilaga -Wizara ya Maliasili na Utalii
Source: Haki Ngowi
udini udini udini udini,hatutafika kabisaaaaaaa,aliyekuwepo awali alikuwa ni maria mmari hatutegemei watu kuhoji juu ya hili,ila wa sasa ni ibrahim mussa najuwa tutahoji kwanini,tunajimaliza wenyewe,natamani wewe bwana ufe na kizazi chako ili hii sumu ya udini ipoteeeeeeeee kabisaaaaaa ktk familia yakoooookhaaaaaa.kateuliwa na nani??? hivi jamani??? mi sielewi ...nikisema ntaonekana mdini..Ibrahimu Mussa huyu ni dini ile ya rais au?
tatizo ukiumwa na nyoka hata jani utalikimbia
Namkubali kwa ajili yako maana najua huwezi kutudanganya hapa! Ole wako aje ki Rost tamu AzizNaomba nianze kwa kupingana tena kwa sauti kubwa na wale wote wanaohoji juu ya Uraia wa Musa. Binafsi namfahamu kwa kiwango cha kumtetea. Musa ni MZALENDO WA KWELI, mwenye UTANZANIA WA ROHONI na si wa kwenye NGOZI. Ni mtu asiyejikweza (extremely social). Nikiwa kama mdau katika wizara husika, kwa miaka kama mitatu mfululizo nahudhuria the Meeting of Executives wa MNRT. Ripoti za utendaji wa Musa zimekuwa hazina mawaha wala uswahili. Hata shauri zake kwenye mikutano hiyo mara zote zinakuwa na mtazamo wa Kizalendo na Kimaendeleo. Binafsi ningefarijika tupate watu wengi wa jinsi ya Musa wanakubali kuingia serikalini na kulitumikia Taifa kwa Uadilifu Mkubwa. Mungu amwongoze vema katika nafasi yake mpya.
Rangi zetu hizi zinatuponza mkuu wanaona bora mtu mweusi hata asiwe mtanzania kuliko mtanzania mwenye asili ya kiasia kushika nyadhifa serikalini. Kuna mada moja niliiona sehem sehemu ilikuwa ikiuliza mbona siku hizi hakuna watu wa aina kama Ibrahim Musa? Watu walitoa michango yao mingi lakini mimi nasema tunaogopa!
Nina amini kuwa wapo waasia kama Prof Shivji ni watu waadilifu na ndio maana watu hawa waadilifu aghalabu kuwa na post kama za AG watawala huwa wanataka "good boys" mtu kama Shivji sidhani kama anaweza kulishwa maneno au vitu ambavyo "ethics" za kisheria hazimruhusu na akakubali kwa ajili ya kutetea unga wake siamini na nitakufa kutoamini hivyo ingekuwa Shivji ni AG wa wakati wa Mkapa nina imani asingefanya ambayo leo yanaigharimu nchi. Na nina amini wapo Watanzania wasiokuwa wazalendo lakini hakuna anaesema kwakuwa ni tu ni mweusi mwenzao. Hii dhana ya huyu ni mwenzetu "mweusi mwenzetu" haitalipeleka taifa popote huyo mweusi mwenzetu akijinufaisha wewe unanufaika na nini? Eleweni kuwa ikiwa kutatokea shida yoyote basi watanzania waasia na watanzania wamatumbi wote wataionja iwe shubiri au mwarubaini! Kwani mgao wa umeme unakatika kwa waasia peke yao? TAFAKARI.
Hpakuwa na mtu mwingine mwenye vigezo zaidi ya huyu? Au ndo vile tena mambo ya ud...i.
kaka rostam nae ni mtumishi mzuuuuri wa umma.....wa siku nyingi
mm cmtaki hata kama ni mtumishi wa siku nyingi,...wanapeleka pesa kwao india hawa....
Yaani nyie sijui tusemeje? Kwani ulidhani alinyanyuliwa tu kutoka mbinguni akawekwa utalii? Ushaambiwa alianza kazi since 1982 na nadhani walikuwa wawili au watatu waliokuwa katika kufikiriwa ndio yeye akafanikiwa but kama kawaida baadhi yenu umelenga katika udini. Nikuulize wewe kule TBC hapakuwa na wengine wa kuteuliwa zile nafasi? au na waislamu nao walenge katika ud....i
udini udini udini udini,hatutafika kabisaaaaaaa,aliyekuwepo awali alikuwa ni maria mmari hatutegemei watu kuhoji juu ya hili,ila wa sasa ni ibrahim mussa najuwa tutahoji kwanini,tunajimaliza wenyewe,natamani wewe bwana ufe na kizazi chako ili hii sumu ya udini ipoteeeeeeeee kabisaaaaaa ktk familia yakooooo
msemaaaaa ukweliiiii hapendwiiii daimaaaaaa:clap2:
Conspiracy mshaanza yaani watanzania sie matatizo sasa kama yupo kulinda maslahi hebu tuchambulie maelezo haya:-
Ibrahim A. Mussa (53) ni mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii tangu mwaka 1982 hadi sasa na alifanya kazi ngazi mbali mbali katika idara ya misitu na utalii
Source: Michuzi.
Swali langu kama amewekwa je huo mpango ulianza lini? Maana huyu jamaa alianza kazi tangu enzi za nyerere sasa je Nyerere ameshiriki? Na inaelekea alianza tangu ngazi za chini mpaka sasa kaukwaa ukurugenzi je ni vibaya mtu akiwa promoted?
Huyu hana elimu na vigezo kuwashinda hao walioachwa. Nawafahamu wako wengi sana hapo tena wenye shahada za uzamivu siyo ya huyu ya uzamili ya kuipata uzeeni.
Kama unahitaji fairness duniani, na wewe nenda India omba uraia uzae watoto huko halafu uone wakikua kama wanaweza kupewa post yoyote serikalini au hata makampuni binafsi licha ya kuwa na vigezo. Sisi tu ndio tumerogwa.
Kuwa na PhD sio kigezo cha kutaka wewe uteuliwe ukurugenzi kama huna experience ya kutosha. Kama lijitu lina PhD ya misitu na kakaa ofisini mwaka mmoja unadhani ni bora zaidi ya yule mwenye Masters na amefanya kazi katika ofisini miaka 25?? Wake up ndugu.
Inawezekana na mchapa kazi. Mimi naamini hivyo. Tatizo ni moja tu kwamba mtu anaweza kuwa na historia iliyotukuka, mwadirifu na mchapa kazi lakini akishaingia kwenye mfumo uliooza naye anaingia kuoza. Kama alizoea kufanya kazi kwa uhuru bila vikwazo wakato akiwa kwenye ngazi za chini asitarajie kuwa mambo yataendelea hivyo hivyo. Lazima sasa akae mkao wa kukabiliana na fedha za mafisadi.
Mkuu kama mtu ana PhD 5 za hisani yaani zile za kupewa kiheshima heshima hata kama hastahili anafaa kuwa raisi?
Mtanzania huyu?