Ibrahim Mussa Ndiye Mkurugenzi Mpya wa Utalii Tanzania

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
PPort_Ibra.jpg

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii amemteua Bw. Ibarahim Mussa kuwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kuanzia tarehe 01 February 2011.

Uteuzi huo ameufanya kwa mujibu wa kifungu cha 6 (1) (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002.

Ibrahim A. Mussa (53) ni mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii tangu mwaka 1982 hadi sasa ambapo alifanya kazi katika ngazi mbalimbali, katika Idara ya Misitu na Idara ya Utalii.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Utalii, Ibrahim A. Mussa alikuwa Mkurugenzi Msaidizi anaesimamia Utafiti, Takwimu na Mafunzo katika Idara ya Utalii.

Bw. Mussa ana Shahada ya Uzamili (International Tourism Management) aliyoipata mwaka 2005 kutoka chuo cha Sheffield nchini Uingereza

Bw. Mussa anachukua nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kutoka kwa Bi. Maria Mmari ambaye amepangiwa kazi nyingine.

TULIZO HENRY KILAGA
INFORMATION OFFICER
MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM
MPINGO HOUSE - NYERERE ROAD
P.O BOX 9372
DSM-TANZANIA

Source:MICHUZI: NEWS ALERT: IBRAHIM MUSSA NDIYE MKURUGENZI MPYA WA IDARA YA UTALII
 
Ni Mtanzania tena mzalendo ndugu yangu . Ana historia ndefu katika utumishi wa Umma . Kwakweli ni mchapakazi sana. Personally namfahamu sana .
 
Historia gani ndefu Mkuu tumegee basi, kabla ya hapo alikuwa na wadhifa gani???? Kipi kafanya hadi mkuu akamkumbuka kwenye ufalme wake???
 
Atakkuwa mwarabu maana nasikia warabu wamenunua sana mbuga. Yuko kulinda mslahi yao

Conspiracy mshaanza yaani watanzania sie matatizo sasa kama yupo kulinda maslahi hebu tuchambulie maelezo haya:-

Ibrahim A. Mussa (53) ni mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii tangu mwaka 1982 hadi sasa na alifanya kazi ngazi mbali mbali katika idara ya misitu na utalii

Source: Michuzi.

Swali langu kama amewekwa je huo mpango ulianza lini? Maana huyu jamaa alianza kazi tangu enzi za nyerere sasa je Nyerere ameshiriki? Na inaelekea alianza tangu ngazi za chini mpaka sasa kaukwaa ukurugenzi je ni vibaya mtu akiwa promoted?
 
kaka rostam nae ni mtumishi mzuuuuri wa umma.....wa siku nyingi
 
Conspiracy mshaanza yaani watanzania sie matatizo sasa kama yupo kulinda maslahi hebu tuchambulie maelezo haya:-
Ibrahim A. Mussa (53) ni mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii tangu mwaka 1982 hadi sasa na alifanya kazi ngazi mbali mbali katika idara ya misitu na utalii

Source: Michuzi.

Swali langu kama amewekwa je huo mpango ulianza lini? Maana huyu jamaa alianza kazi tangu enzi za nyerere sasa je Nyerere ameshiriki? Na inaelekea alianza tangu ngazi za chini mpaka sasa kaukwaa ukurugenzi je ni vibaya mtu akiwa promoted?

Maandalizi huwa yanaanza muda mrefu mkuu
 
Najua Jk aliangalia kigezo kimoja tu.... Hayo mengine sio muhimu sana kwa sisi wakwere
 
Back
Top Bottom