IBM Yaimarisha ofisi zake Afrika Mashariki

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
DAR ES SALAAM, Tanzania, - 01 June 2011: IBM (NYSE: IBM) inatangaza kuwa imefungua ofisi tawi lake jipya Dar es Salaam, ikiwa ni mwendelezo wa kujitanua kimkakati na kupatikana katika sehemu muhimu zinzokuwa kimasoko na kusaidia mkakati wa ukuaji duniani.

Ofisi mpya tanzu ni sehemu ya mpango mkuu wa programu ya uwekezaji ambao IBM inautekeleza Afrika ikiwa ni pamoja na kutengeneza miundombinu, ofisi, mafunzo na kuajiri, masoko na mauzo.

Taarifa hizi zinakuja siku chache baada ya IBM kufungua ofisi huko Dakar, Senegal and gives IBM na kuifanya kusambaa katika nchi 20 kwa sasa zikiwemo Afrika Kusini, Ghana, Nigeria, Kenya, Morocco, Misri, Tunisia na Algeria.

Uwepo wake Tanzania utaiwezesha IBM kuongeza kiwango chake cha utoaji huduma kwa wateja na washirika katika kanda ya Afrika Mashariki katika ubora wa hali ya juu.

IBM tayari inawahudumia wateja muhimu Afrika Mashariki, sekta mbalimbali zikiwemo za mawasiliano, mafuta na gesi, fedha na serikali. Kwa mfano nchini Tanzania, IBM inafanya kazi na National Microfinance Bank (NMB) kwa ajili ya kuibadilisha mifumo yake ya miundombinu yake mikuu ya teknolojia ya kibenki kwa ajili ya kuendanda na ukuaji wa kibiashara.

Pamoja na muundo mpya wa mashine za IBM katika kuhifadhi umeme kutokana na teknolojia yake, NMB imeweza kuongeza idadi ya akaunti za wateja wake hadi kufikia milioni 1.4, kuongeza idadi ya mashine za kuchukulia fedha (ATM) hadi 400, kutoa kadi za kuchukulia fedha na huduma za kibenki zinazohusu kuwafuata wateja pale walipo nchini kote. Leo benki inatoa mamilioni ya huduma mbalimbali za wateja kwa mwezi na inatoa huduma ya haraka kuliko benki zote nchini.

2yo1vsg.jpg

David Sawe, IBM CGM Tanzania (kushoto) akiwa na John Ncube, CIO wa National Microfinance Bank

“IBM imeweza kutusaidia kubadili mfumo wetu wa kibenki na kutufanya tuweze kutoa huduma za kisasa, kupunguza foleni kwa wateja na kutusaidia kuwa katika nafasi ya ushindani,” alisema John Ncube, Ofisa Habari Mwandamizi wa NMB.

Aidha IBM inafanya kazi kwa ukaribu zaidi na serikali ya Tanzania katika kuiwezesha kuendana na teknolojia ya habari pia katika maeneo yake muhimu ya maendeleo, elimu, utafiti na maendeleo.

“Tunaikaribisha IBM kuwepo Tanzania moja kwa moja,” alisema Mh. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na kuongeza “Tunathamini uhusiano wetu na IBM na tunategemea kufanya kazi pamoja katika kutumia teknolojia katika kuinua maendeleo ya kiuchimi na mifumo ya kijamii”.

"Kwa kuzingatia mpango wetu wa ukuaji, tunaongeza uwezo wetu wa kutoa huduma bora na za thamani kwa wateja wetu katika bara zima," alisema David Sawe, Meneja Mkuu Mkazi wa IBM Tanzania.

“Kwa kufungua ofisi yetu tanzu hapa Tanzania, tunauchukulia uwepo wetu nchini katika hali ya juu kwa kuandaa misingi ya sayari ya kipekee.”

55jqkh.jpg

David Sawe, IBM CGM Tanzania (kushoto) akiwa na John Ncube, CIO wa NMB mbele ya mitambo ya IBM (IBM Power Systems) iliyowekwa katika Benki ya NMB

Kwa ajili ya kuzisaidia huduma zake hapa nchini, IBM inafanya kazi na vyuo mbalimbali lengo likiwa ni kukuza vipaji na kuwezesha kufanyika miradi ya tafiti katika mifumo ya kipekee zaidi.

Kwa mfano, IBM inafanya kazi kwa karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma nchini Tanzania kusaidia kuunda “Silicon Valley” aina ya mazingira katika chuo na kuendeleza utamaduni wa kujasiriamali.

IBM pia imechangia vitabu vya kujisomea 22,000 vya Teknolojia ya Mawasiliano. Katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), IBM imechangia jumla ya vitabu 15,000 pamoja na zawadi ya dola za Kimarekani 15,000 kwa kitivo cha Fizikia kwa ajili ya kusaidia jitihada zake za kufanya utafiti.

IBM pia imejiingiza moja kwa moja katika programu ya ‘uraia’ nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Tangu mwaka 2008 IBM imeweza kuweka timu za waajiriwa wake Tanzania, Kenya, Nigeria, Ghana, Afrika Kusini, Morocco na Misri kwea ajili ya kufanya kazi ya kuboresha hali ya maisha ya wenyeji na kusaidia ukuaji wa fursa za ajira.

Aidha, IBM kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania inaendesha mradi unaojulikana kama ‘SMS for Life’ pamoja wadau wengine kama Novartis, Vodafone na Roll Back Malaria kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi ili kuboresha upatikanaji wa dawa za malaria na kusaidia kuokoa maisha ya watu walioko maeneo yasiyofikika kwa urahisi.

Ofisi ya Dar es Salaam ni sehemu ya shughuli za IBM Afrika Mashariki na itaisaidia ofisi nyingine ya IBM Afrika Mashariki iliyopo Nairobi, Kenya ni kituo kikuu cha biashara katika ukanda huu.IBM imeweza kusambaza huduma zake Afrika Mashariki tangu miaka ya 1950 wakati ilipofungua ofisi yake ya kwanza jijini Nairobi.

Ofisi mpya imefunguliwa wiki hii katika hafla iliyoshirikisha wateja, washirika wa kibiashara na maofisa wa serikali jijini Dar es Salaam.

Taarifa juu ya IBM: Kwa taarifa zaidi juu ya IBM tafadhali tembelea: IBM in Africa | A Smarter Planet Blog
 
Back
Top Bottom