Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
- Thread starter
- #21
Mkuu Lunyungu,
Na wewe usijiangushe bure kujifanya hujui maana sahihi ya hicho kipengere.
Mambo kama haya ndio yanatisha Watanzania wengine. Ukiwa na watu kama akina mwanakijiji serikalini, wanaweza kuwa wabaya (last time you said Hatari!) kuliko akina Rweyemamu.
Take your shots all you want.. my argument still stand.
Na unaweza kujaribu tafsiri za kichina, kijerumani, kizaramo na kindegereko ili kuondoa ukweli ambao uko wazi katika lugha ya Kiswahili. Jukumu la "kwanza" la mwanaCCM ni kwa CCM, unaweza kujaribu kuchambua unavyoweza lakini kwa mwana CCM hili halina mjadala.
Kunapotokea mgongano kati ya maslahi ya CCM na ya Taifa mwana CCM achague lipi anapoangalia Katiba yake..? Kwangu hakuna utata lakini kwa mwana CCM kijijini?
Juzi, mtu mmoja alivamiwa na kuwashika wabaya wake na aliwapeleka wapi Polisi? hapana kwa "mwenyekiti wa CCM".